Japo Wakristo na Waislamu ni Watoto wa Baba Mmoja, Nabii Ibrahim na Mungu ni Mmoja, Kati ya Ismail na Isaka ni nani aliyetolewa Sadaka ya Kuchinja?

Japo Wakristo na Waislamu ni Watoto wa Baba Mmoja, Nabii Ibrahim na Mungu ni Mmoja, Kati ya Ismail na Isaka ni nani aliyetolewa Sadaka ya Kuchinja?

Ni kati ya somo nililokuwa nikilifaulu sana, ilikuwa nikipata B ni kama nimefeli.
Basi ulikuwa unakiriri tu. Kwa habari yako hadi Betlehemu alikozaliwa Yesu kuko Palestine. Hamna nchi inaitwa Israel kabla Mwaka 1948. Mwaka 1948 baada uvamizi wa Wayahudi bandia ndo Hilo Taifa feki la Wayahudi feki lilikuja kubuniwa.
 
Naomba someni tena hapa kwa umakini.

Mwanzo 22:1
Ikawa baada ya mambo hayo Mungu alimjaribu Ibrahimu, akamwambia, Ee Ibrahimu! Naye akasema, Mimi hapa.

2 Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia.

3 Ibrahimu akaondoka alfajiri, akatandika punda wake, akachukua vijana wawili pamoja naye, na Isaka mwanawe, akachanja kuni kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, akaondoka, akaenda mpaka mahali alipoambiwa na Mungu.

4 Siku ya tatu Ibrahimu akainua macho yake, akapaona mahali pakali mbali.

5 Ibrahimu akawaambia vijana wake, Kaeni ninyi hapa pamoja na punda, na mimi na kijana tutakwenda kule, tukaabudu, na kuwarudia tena.

6 Basi Ibrahimu akazitwaa kuni za hiyo sadaka, akamtwika Isaka mwanawe; akatwaa moto na kisu mkononi mwake, wakaenda wote wawili pamoja.

7 Isaka akasema na Ibrahimu baba yake, akinena, Babangu! Naye akasema, Mimi hapa, mwanangu. Akasema, Tazama! Moto upo, na kuni zipo, lakini yuko wapi mwana-kondoo kwa sadaka ya kuteketezwa?

8 Ibrahimu akasema, Mungu atajipatia mwana-kondoo kwa hiyo sadaka, mwanangu. Basi wakaendelea wote wawili pamoja.

9 Wakafika mahali pale alipoambiwa na Mungu, Ibrahimu akajenga madhabahu huko, akaziweka tayari kuni, kisha akamfunga Isaka mwanawe, akamweka juu ya madhabahu, juu ya zile kuni.

10 Ibrahimu akanyosha mkono wake, akakitwaa kisu ili amchinje mwanawe.

11 Ndipo malaika wa Bwana akamwita kutoka mbinguni, akasema, Ibrahimu! Ibrahimu! Naye akasema, Mimi hapa.

12 Akasema, Usimnyoshee kijana mkono wako, wala usimtendee neno; kwa maana sasa ninajua ya kuwa unamcha Mungu, iwapo hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee.

13 Ibrahimu akainua macho yake, akaangalia, na tazama, kondoo mume yuko nyuma yake, amenaswa pembe zake katika kichaka. Basi Ibrahimu akaenda akamtwaa huyo kondoo, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe.

14 Ibrahimu akapaita mahali hapo Yehova-yire,kama watu wasemavyo hata leo,Katika mlima wa BWANA itapatikana.

15 Malaika wa Bwana akamwita Ibrahimu mara ya pili kutoka mbinguni

16 akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema Bwana, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee,

17 katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao;

18 na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu.

19 Basi Ibrahimu akawarudia vijana wake, wakaondoka, wakaenda zao pamoja mpaka Beer-sheba; Ibrahimu akakaa huko Beer-sheba.
........
Naomba andiko lingine tulilinganishe na hili.

Hivi mtoto wa miezi kadhaa anaitwa Kijana?
 
Quran nayo inamakosa mengi Mkuu Tunaweza tukayataja ila sio kwa leo
ALLAH ameshawa challenge wewe na babu zako waliokutangulia katika ukafiri mlete walau kosa moja tu ndani ya Quran au hata mfano wa sura moja tu ila hakuna aliyeleta na atakayeleta mpaka dunia inatamatika
 
Hajir unajua alifukuzwa mara mbili? alipokuwa mjamzito na alipokuwa na mtoto, na wewe unazungumzia ugomvi mkubwa ulitokea ambao ndio uliomwondoa Hajir moja kwa moja, lakini pia ukisoma mistari hiyo ni Sarah alitoa oda ya Hajiri kufukuzwa na likawa jambo baya kwa Ibrahimu sijui hapo umesema, na Mungu alikuwa upande wa Sarah hapo umejiuliza kwa nini?

Lakini mwanzoni Sarah alimfukuza Hajir akiwa mjamzito haya labda tujadiliane ilikuwaje Ibrahimu alimruhusu Sarah kumfukuza Hajiri? Je inawezekana bimkubwa wako kumfukuza bimdogo wako?
Nikianza na Kuwa sara alitoa Oda nakataa kuwa Hapana Sara hakutoa Order ya Kufukuzwa kwa Hajiri..
Alienda Kushitaki kama Mke mwingine anavyoweza kwenda Kushtaki mfano tuseme alisema "Huyu Mke mdogo amenidharau nataka Umfukuze"

Ibrahimu akakasirika kuona sara anataka Mke mwingine afukuzwe..

"Ila kabla hajatoa maamuzi mabaya kwa Sara mungu akamwambia aha ahaa Msikilize mkeo na Umfukuze Huyo mwanamke kwakuwa kama yeye ndo aliyekupa ndyo anajua Bora kwako" (Nimeongeza maneno)..

Unajua Mila za Kiebrania Kuhusu Mamlaka ya Mke Mkubwa????

MKe mkubwa ndyo mwamuzi Wa Pili baada ya Mume
 
Mwanzo 16:1

[1]Basi Sarai mkewe Abramu hakumzalia mwana, naye alikuwa na mjakazi, Mmisri, jina lake Hajiri.

Now Sarai Abram's wife bare him no children: and she had an handmaid, an Egyptian, whose name was Hagar.
Je kilugha itakuwa ni sawa wasaidizi wa nyumbani kwa sasa tukiwaita wajakazi?
 
Km Biblia ilitangulia kabla ya Qur'an na yule Jamaa alipoingizwa pangoni kule kwenda kumezeshwa aya za Bible katika muonekano mwingine alipofika pale pa Isaka na Ishmael kwamba Ibrahim aliambiwa amchukue Isaka Jamaa akafuta Isaka akaweka Ishmael itoshe kusema aliekosea ni yule aliesema ameshushiwa Qur'an kisha akamfuta Isaka akamweka Ishmael kwa sababu zake mwenyewe Ila mtoto alietolewa dhabiu na Ibrahim ni Mtoto wake wa Ahadi anaetambulika km Isaka kwa hio upande wa Pili wamlaumu yule Jamaa yao aliesema ameshushiwa Qur'an

Mboni Yesu amemtaja vizuri tu bila shida na ametambua vizuri tu bila shida yoyote mpaka waislamu wote wanamtambua km Nabii Issa Bin Maryam ingawa ukija kwa wakristu wanakwambia huyo Issa Bin Maryam wa kwenye Qur'an wao hawamtambui maana sio Yesu wa kwenye Bible Ila Bwana yule alimtambua Nabii Issa Bin Maryam kwamba ndio kabisa Ila alipofika kwa Isaka akamfuta akamweka Ishmael kwamba ndie aliekwenda kule Magharibi na Baba yake Ibrahim

Hata mwanae wa karibu Fatima alipofariki alisema mwanae huyo amelala pahala takatifu pa patakatifu na akitoka Bikra Maryam anaefuatia kwa utakatifu ni huyo mwanae

Unaelewa vizuri sijui hapo?

Itoshe kusema wa upande Pili wamlaumu Jamaa yao aliesema ameshushiwa Qur'an kule mapangoni kwa udhamini wa Bibi Hadija na kumuondoa Isaka na kumweka Ishmael km mtoto wa Ibrahim alietolewa dhabiu
 
Sasa Nataka uniambia Ibrahimu kwanin alitaka Kuchinja Mtoto wa Miezi kadhaa?
Wakati mtoto wa Miaka 14 yupo??

Maana ibrahimu kajaribiwa akiwa na miaka 100...
Kipindi hicho Isaka ana miezi kadhaa tu na ishamaeli alikuwa na miaka 14
Waandishi wa bublia kwenye eneo hili walidanganya halafu wakashindwa kuficha ushahidi wa uwongo wao. Bublia hiyo hiyo inasema kijana alikuwa akimuuliza baba yake kwamba Kuni wanazo na kisu wanachuo ila mbona hawana kondoo wa kumchinja kama sadaka. Tunaona baba yake anamjibu kuwa kondoo watamkuta huko. Hili linathibisha wazi kuwa aliyekuwa anaenda kutolewa sadaka ni kijana aliyekuwa akitembea Kwa miguu yake na ana umri wa kumsaidia baba yake baadhi ya shughuli. Ni wazi kabisa ni Ishmaeli.
 
Nikianza na Kuwa sara alitoa Oda nakataa kuwa Hapana Sara hakutoa Order ya Kufukuzwa kwa Hajiri..
Alienda Kushitaki kama Mke mwingine anavyoweza kwenda Kushtaki mfano tuseme alisema "Huyu Mke mdogo amenidharau nataka Umfukuze"

Ibrahimu akakasirika kuona sara anataka Mke mwingine afukuzwe..

"Ila kabla hajatoa maamuzi mabaya kwa Sara mungu akamwambia aha ahaa Msikilize mkeo na Umfukuze Huyo mwanamke kwakuwa kama yeye ndo aliyekupa ndyo anajua Bora kwako" (Nimeongeza maneno)..

Unajua Mila za Kiebrania Kuhusu Mamlaka ya Mke Mkubwa????

MKe mkubwa ndyo mwamuzi Wa Pili baada ya Mume
Bado haujajibu kwenye kisa cha kwanza?

Mwanzo 16:5-6
[5]Sarai akamwambia Abramu, Ubaya ulionipata na uwe juu yako; nimekupa mjakazi wangu kifuani mwako, naye alipoona kwamba amepata mimba, mimi nimekuwa duni machoni pake. BWANA na ahukumu kati ya mimi na wewe.

[6]Naye Abramu akamwambia Sarai, Tazama, mjakazi wako yu mkononi mwako, mtendee lililo jema machoni pako. Sarai akamtesa, naye akakimbia kutoka mbele yake.

Ilikuaje Ibrahimu akamruhusu mkewe amfukuze Hajir?

Hoja 2 kuhusu utamaduni wa waebrania

-Umesoma kisa cha lea na Rahel wake zake Yakobo?

- Umesoma kisa cha Hana na Penina wake zake Elkana?
 
ALLAH ameshawa challenge wewe na babu zako waliokutangulia katika ukafiri mlete walau kosa moja tu ndani ya Quran au hata mfano wa sura moja tu ila hakuna aliyeleta na atakayeleta mpaka dunia inatamatika
Wewe ni mfia dini tu na sio mchambuzi huru.
Hivyo vitabu viliandikwa na watu na vina makosa ya kibinadamu mengi tu.
Ila mfia dini kama wewe huwezi kuyaona.
 
ALLAH ameshawa challenge wewe na babu zako waliokutangulia katika ukafiri mlete walau kosa moja tu ndani ya Quran au hata mfano wa sura moja tu ila hakuna aliyeleta na atakayeleta mpaka dunia inatamatika
Kwanza kabisa Mkuu Mimi sio Kafiri maana Hakuna Sehemu Nilipokufuru..

Pili Tuanze na Aya moja tu Unipe majibu

Surah Maryam aya ya 28

يَٰٓأُخْتَ هَٰرُونَ مَا كَانَ أَبُوكِ ٱمْرَأَ سَوْءٍۢ وَمَا كَانَتْ أُمُّكِ بَغِيًّۭا

inatamkwa hivi

Ya ukhta haruuna ma kana abuuki imraa sawin wama kanat ummuki baghiyyan

Maana Yake!

Ewe dada yake Harun! Baba yako hakuwa mtu muovu, wala mama yako hakuwa kahaba.

Concern Yangu:-
Kuna mchanganyo kati ya Miriam na Mariam kwenye Hiyo Aya..

Mariam hakuwahi kuwa Dada wa Haruni (Kama unafahamu utakuwa unajua kuwa mariam alizaliwa Peke yake na Huku akiwa na Mtoto wa Pekee)..

Dada wa Haruni alikuwa Miriam na ndiyo alikuwa Dada Yake Na Musa Pia..

Una cha kusema kuhusu hilo
 
Waandishi wa bublia kwenye eneo hili walidanganya halafu wakashindwa kuficha ushahidi wa uwongo wao. Bublia hiyo hiyo inasema kijana alikuwa akimuuliza baba yake kwamba Kuni wanazo na kisu wanachuo ila mbona hawana kondoo wa kumchinja kama sadaka. Tunaona baba yake anamjibu kuwa kondoo watamkuta huko. Hili linathibisha wazi kuwa aliyekuwa anaenda kutolewa sadaka ni kijana aliyekuwa akitembea Kwa miguu yake na ana umri wa kumsaidia baba yake baadhi ya shughuli. Ni wazi kabisa ni Ishmaeli.
Mnaongea sana bila kuweka Maandiko.
Hebu weka hilo andiko tuone miaka ya Isaka na Ishmaeli.
 
Kumbuka Ibrahim hakuwa mgumba?

Ungeanza kuuliza tamaduni na sheria za Kale za kiebrània zilikuwa zinasemaje.

Mtoto wa kijakazi nd Suria hahesabiki kama mtoto wa pekee yaani astahiliye urithi.
Mtoto wa mke halali wa ndoa ndiye mtoto anayetambulika

Alafu waislamu haohao sio kwamba hawajui hi,o sheria kwa sababu wanazitumia mpaka hivi leo.
Mtoto haramu haitwi kwa jina la Baba na wala hastahili urithi

Hizo ni sheria za zamani huko mashariki ya kati
Sheria aliyotumia Ibrahim ndiyo sheria ipo kwenye Quran,vijakazi ni ruksa kuwafanya wake kwa kuwaingilia na inahesabika halali mbele za Mungu,kumbuka kijakazi siyo house girl Bali palikua na utaratibu wa kununua watumwa anakua Mali yako totally,hayo ya kwenye biblia ni kawaida ya waisrael kubadili maandiko na vile bifu na dharau kwa waarabu tangu kale, ndiyo wakatia mikononi maandiko,mwana wa pekee hawezi kuwa wa pili
 
Nimesikiliza "qari" yaani msomaji, kasoma Surat Saffat aya ya 100 mpaka aya ya 105. Nimesikiliza na aliyepewa kutafsiri, hapo ndipo aliporonga. Na yeye kwa kuwa anajuwa anahokisema akamsukumia mtafsiri mwengine aitwae Ibn kathir, akasema huyo mtafsiri ndiye kasema huyo ni mtoto ni "Ismail".Hayo Yanabaki kuwa ni maneno ya mtafsiri (commentator) na siyo ya Qur'an.

Maana yake nini hiyo? Maana yake hakuna katika hiyo aya alipotajwa Ismail.

Ndiyto maana post ya juu huko nikasema yamepachikwa maneno kutoka nje ya Qur'an. Hata wewe ukiisikiliza aya inaposomwa hutosikia jina la Ismail, hilo utalisikia kutoka kwa "mtafsiri (commentator). Kayatowa wapi hayo aliyoongezea kama hayapo kwenye Qur'an? Hilo ndilo swali la kujiuliza.
Asante sana, kwa kauli hii, umeufunga huu mjadala. Asante.
P
 
Bado haujajibu kwenye kisa cha kwanza?

Mwanzo 16:5-6
[5]Sarai akamwambia Abramu, Ubaya ulionipata na uwe juu yako; nimekupa mjakazi wangu kifuani mwako, naye alipoona kwamba amepata mimba, mimi nimekuwa duni machoni pake. BWANA na ahukumu kati ya mimi na wewe.

[6]Naye Abramu akamwambia Sarai, Tazama, mjakazi wako yu mkononi mwako, mtendee lililo jema machoni pako. Sarai akamtesa, naye akakimbia kutoka mbele yake.

Ilikuaje Ibrahimu akamruhusu mkewe amfukuze Hajir?

Hoja 2 kuhusu utamaduni wa waebrania

-Umesoma kisa cha lea na Rahel wake zake Yakobo?

- Umesoma kisa cha Hana na Penina wake zake Elkana?
Mkuu naomba nikuulize kitu una Mke??
UMewahi kupitia Kipindi ambacho mke anakuchosha lets say anakushitakia sana kuhusu Mtoto ambaye yuko chini Yake (Yaani naye pia ni mwanae)..

Ndyo tukio lililotokea Hapo Ibrahimu alichoshwa na lawama ma Minung'uniko ya Sara na ndo maana alimjibu kuwa Amfanyie mema tu..

Hakurusu mkewe afukuzwe na Ndo maana mungu alimrudisha kwa sababu Hajiri naye Tangu alipoolewa alianza kupata kiburi na kumdharau sara..

Ibahimu baada ya Kushtakiwa alijibu nini?

Mwanzo 16:6

"Naye Abramu akamwambia Sarai, Tazama, mjakazi wako yu mkononi mwako, mtendee lililo jema machoni pako. Sarai akamtesa, naye akakimbia kutoka mbele yake."

ukiangalia Hilo Jibu unahisi ni la Furaha..
Alimwambia Mfanye unachoona wewe ni sawa kwako yaani kitakachokufurahisha wewe..

Na Mind you kwamba Hajiri hakufukuzwa..

Hajiri aliondoka baada ya kuteswa na hakuomba msamaha ila akaondoka nyumbani na ndo maana malaika akaMrudisha tena nyumbani na akamwambia akaombe msamaha...
 
Kwa vile mtoto aliyetolewa sadaka ni mmoja, hivyo kati ya vitabu hivi viwili, kuna kimoja ni ukweli na kingine ni uongo
Swali hapa ni kubaini ukweli ni upi na uongo ni upi.
P
Kike kinachodai kwamba Mungu alishuka usiku akapigana mieleka na yakobo na akashindwa Hadi kulalamika kwa yakobo amuachie binaadam wasije muona pakipambazuka,na kutakiwa kumbariki kwanza yakobo na kuwa Israel,hakiwezi kuwa kitabu kisemacho kweli
 
Siyo sawa,kisheria kijakazi ni mtumwa uliyemnunua,Tena kauzwa na wazazi wake
ununuzi ulikuwa na time limit, na time ikiisha alikuwa na uhuru wa kuondoka ama kuendelea kubaki, maana malipo yake si wanakuwa wamepewa wazazi wake, housegirl wa sasa hela wanapewa wenyewe
 
Waandishi wa bublia kwenye eneo hili walidanganya halafu wakashindwa kuficha ushahidi wa uwongo wao. Bublia hiyo hiyo inasema kijana alikuwa akimuuliza baba yake kwamba Kuni wanazo na kisu wanachuo ila mbona hawana kondoo wa kumchinja kama sadaka. Tunaona baba yake anamjibu kuwa kondoo watamkuta huko. Hili linathibisha wazi kuwa aliyekuwa anaenda kutolewa sadaka ni kijana aliyekuwa akitembea Kwa miguu yake na ana umri wa kumsaidia baba yake baadhi ya shughuli. Ni wazi kabisa ni Ishmaeli.
Ukifatilia kwa umakini Ndo utagundua ila ukisoma bila reasoning utaona ni sawa 🤣🤣
Ila mtoto wa Miezi michache tu anaongea na anatembea Kilometer 300
 
Back
Top Bottom