Japo Wakristo na Waislamu ni Watoto wa Baba Mmoja, Nabii Ibrahim na Mungu ni Mmoja, Kati ya Ismail na Isaka ni nani aliyetolewa Sadaka ya Kuchinja?

Japo Wakristo na Waislamu ni Watoto wa Baba Mmoja, Nabii Ibrahim na Mungu ni Mmoja, Kati ya Ismail na Isaka ni nani aliyetolewa Sadaka ya Kuchinja?

itakuwa sawa tu, maana kile walichokifanya wajakazi ndicho wanachokifanya house girls
1718883928366.png
 
Sheria aliyotumia Ibrahim ndiyo sheria ipo kwenye Quran,vijakazi ni ruksa kuwafanya wake kwa kuwaingilia na inahesabika halali mbele za Mungu,kumbuka kijakazi siyo house girl Bali palikua na utaratibu wa kununua watumwa anakua Mali yako totally,hayo ya kwenye biblia ni kawaida ya waisrael kubadili maandiko na vile bifu na dharau kwa waarabu tangu kale, ndiyo wakatia mikononi maandiko,mwana wa pekee hawezi kuwa wa pili

Kwa nini Ishmael alifukuzwa kama ni kweli unachoongea?

Kwa nini Ishmael hakurithi mali ikiwa ni mzaliwa wa kwanza?
 
Mkuu naomba nikuulize kitu una Mke??
UMewahi kupitia Kipindi ambacho mke anakuchosha lets say anakushitakia sana kuhusu Mtoto ambaye yuko chini Yake (Yaani naye pia ni mwanae)..

Ndyo tukio lililotokea Hapo Ibrahimu alichoshwa na lawama ma Minung'uniko ya Sara na ndo maana alimjibu kuwa Amfanyie mema tu..

Hakurusu mkewe afukuzwe na Ndo maana mungu alimrudisha kwa sababu Hajiri naye Tangu alipoolewa alianza kupata kiburi na kumdharau sara..

Ibahimu baada ya Kushtakiwa alijibu nini?

Mwanzo 16:6

"Naye Abramu akamwambia Sarai, Tazama, mjakazi wako yu mkononi mwako, mtendee lililo jema machoni pako. Sarai akamtesa, naye akakimbia kutoka mbele yake."

ukiangalia Hilo Jibu unahisi ni la Furaha..
Alimwambia Mfanye unachoona wewe ni sawa kwako yaani kitakachokufurahisha wewe..

Na Mind you kwamba Hajiri hakufukuzwa..

Hajiri aliondoka baada ya kuteswa na hakuomba msamaha ila akaondoka nyumbani na ndo maana malaika akaMrudisha tena nyumbani na akamwambia akaombe msamaha...
Hebu soma kisa cha Penina na Hana, Hana akiwa mke mkubwa na Penina mke mdogo

1samwel 1:1-21 halafu uje tena tuelewane
 
Katika dini zote mbili, Ukristo na Uislamu, imani kuhusu mtoto aliyetakiwa kutolewa sadaka na Nabii Ibrahim kama ishara ya utiifu kwa Mungu hutofautiana.

Katika Uislamu:

Waislamu wanaamini mtoto aliyetakiwa kutolewa sadaka alikuwa Ismail, mtoto wa Ibrahim na mjakazi wake Hajar.

Quran Tukufu inasimulia tukio hili katika Sura 37: 100-107, ikionyesha nia ya Ibrahim kumtoa mwanawe Ismail kama sadaka na kuingiliwa kwa Mungu kwa kumpa kondoo kuchukua nafasi ya Ismail.

Tukio hili linaonekana kama mfano wa utiifu wa hali ya juu kwa Mungu na imani thabiti.

Katika Ukristo:

Wakristo wanaamini mtoto aliyetakiwa kutolewa sadaka alikuwa Isaka, mtoto wa Ibrahim na mkewe Sara.

Biblia Takatifu inasimulia tukio hili katika Mwanzo 22: 1-18, ikionyesha nia ya Ibrahim kumtoa mwanawe Isaka kama sadaka na kuingiliwa kwa Mungu kwa kumpa kondoo kuchukua nafasi ya Isaka.

Japo hadithi ni moja ila napingana kwamba Mungu wa wakristo na Waislamu ni mmoja.

Nawasilisha mkuu
Ibrahim hahusiani chochote na ukiristo,hakuwa mkiristo, wakiristo wao Imani yao inatoka na yesu ambaye kwao ni Mungu na mwana wa Mungu pia, Mungu wa Ibrahim alikua mmoja tu,Hana mwana Wala hakuzaliwa Kama ilivyo Imani ya kiyahudi
 
ununuzi ulikuwa na time limit, na time ikiisha alikuwa na uhuru wa kuondoka ama kuendelea kubaki, maana malipo yake si wanakuwa wamepewa wazazi wake, housegirl wa sasa hela wanapewa wenyewe
Usilazimishe utakavyo wewe,huyo kijakazi anaingia kwenye kundi la 'inayomiliki mikononi yenu ya kuume' katika Quran,ambapo ni vijakazi na mateka wa Vita,Hawa huhitaji process za ndoa ya kawaida,wakikuvutia ni kupiga mbuzi na huhesabiki Kama umezini, kijakazi ilikua mpaka ajikomboe/akombolewe kwa kulipiwa gharama atakazotaja mmiliki
 
Mkuu
Kitu muhimu ni tuutafute ukweli, Mungu hakuleta dini wale Yesu hakuleta dini!. Hoja hapa ni nani mkweli na nani muongo?. Mtoto aliyetaka kutolewa sadaka ya kuchinja ni nani?.
P
Mkuu, jikite kwenye Meditation tu, hizi dini mbili ni pasua kichwa.
 
Kwa nini Ishmael alifukuzwa kama ni kweli unachoongea?

Kwa nini Ishmael hakurithi mali ikiwa ni mzaliwa wa kwanza?
Ishmaeli alimzika Baba yake wakiwa na Isaka baba yao akiwa na miaka 175..

Kingine nani alisema Ishmael hakupewa Urithi??
Mwanzo 17:20
Screenshot_20240620_144826_Biblia Takatifu.jpg

Vizazi kwenye Biblia huanza mkubwa kwenda mdogo na ndivyo ilivyofanyika..
Screenshot_20240620_145236_Biblia Takatifu.jpg
 
Na
Ibrahim hahusiani chochote na ukiristo,hakuwa mkiristo, wakiristo wao Imani yao inatoka na yesu ambaye kwao ni Mungu na mwana wa Mungu pia, Mungu wa Ibrahim alikua mmoja tu,Hana mwana Wala hakuzaliwa Kama ilivyo Imani ya kiyahudi
Nani kasema Ibrahimu alikuwa Mkristo ?
Wewe inamanksweke ?
Naona leo unamkubali Mwanaharamu.
 
Kwa nini Ishmael alifukuzwa kama ni kweli unachoongea?

Kwa nini Ishmael hakurithi mali ikiwa ni mzaliwa wa kwanza?
Bado unataka tutumie kitabu kilichoandikwa na wayahudi wasiompenda mwarabu Ishmael,ndugu yao ambaye upendeleo ungehamia kwake baadae.
Katika ahadi zinazodaiwa ni kuwa za Mungu kwa Wana wa Ibrahim imeandikwa kwamba uzao wa isaka utazidi maradufu na kuwa mkubwa,Sasa kati ya waarabu/Ishmael na waisraeli/wepi wamezidi maradufu?!..ndiyo uanng'amua uhuni wa kubadili majina na story kwenye vitabu vya kiyahudi ambapo QUR'AN huita kutia mikononi,mchezo kongwe wa waisrael
 
Ibrahim hahusiani chochote na ukiristo,hakuwa mkiristo, wakiristo wao Imani yao inatoka na yesu ambaye kwao ni Mungu na mwana wa Mungu pia, Mungu wa Ibrahim alikua mmoja tu,Hana mwana Wala hakuzaliwa Kama ilivyo Imani ya kiyahudi
kwahiyo Ibrahimu alikuwa Muislamu?
 
Bado unataka tutumie kitabu kilichoandikwa na wayahudi wasiompenda mwarabu Ishmael,ndugu yao ambaye upendeleo ungehamia kwake baadae.
Katika ahadi zinazodaiwa ni kuwa za Mungu kwa Wana wa Ibrahim imeandikwa kwamba uzao wa isaka utazidi maradufu na kuwa mkubwa,Sasa kati ya waarabu/Ishmael na waisraeli/wepi wamezidi maradufu?!..ndiyo uanng'amua uhuni wa kubadili majina na story kwenye vitabu vya kiyahudi ambapo QUR'AN huita kutia mikononi,mchezo kongwe wa waisrael
mbona swali ni jepesi tu, kwa ushahidi wa maandiko ni nani alitakiwa kuchinjwa kati ya Isaka na Ishmael?
 
Ikiwa tutaegemea kwenye maandiko tu tukubaliane kutokukubaliana kwa kuwa kila imani imendika kikiwa kinatofautiana na kingine. Tunachopaswa ni kujadili content ya kilichoandikwa hapo ndo tutaelewa kipi kinasema ukweli na kipi ndani yake ukweli umepindishwa.

Kauli ya kusema mtoto wa pekee, Isaac ... hii unai-reconcile vipi na fact ya kuwa Isaac ni mtoto wa pili baada ya kuwa Ibrahim tayari alishakuwa na mtoto mwengine Ismail?
Sijaona kwenye Qur'an kuwa Ibrahim alikuwa na mtoto anitwa Ismail, au hayo ni mafundisho nje ya Qur'an?
 
Cc. DK Mambo Jambo. 🤣🤣💪
Nop Kumbe Hujanielewa Mimi Mkuu!
Am Just Reasoning Na sipo kumtetea Ishmael wala Isaka ninachosema ni kuwa..

Kote kote Ukiangalia Bado hii storry Doesnt add up bado ina lack audacity ya Kusema fulani au ni Nani hasa ndo alitolewa,.. Factually speaking..

Katika Quran story doesnt Cite a name na kwa wakristo story cite a name but Factually wrong..
 
kwahiyo Ibrahimu alikuwa Muislamu?
Kwa mujibu wa Quran yeah, uislam maana yake unyenyekevu kwa Mungu'
kwahiyo Ibrahimu alikuwa Muislamu?
Kuna pahala kwenye bible pameandikwa Ibrahim alikua mnyenyekevu kwa Mungu',Kama kumbukumbu zangu si chakavu,ambapo bible ya kiarabu itakua imeandika Ibrahim alikua muislam
 
Back
Top Bottom