Habari
stormryder
Japo sikuzungumzia kuhusu Ibrahimu Kufika Makka/Bakka ila ninaweza kuwa nina majibu ya Huenda alifika Makka au Bakka..
Kwanza
nitadeclare Interest:- Mimi sio Muislamu,Muarabu wala Mkristo..
Ila ni Mtu wa kuchunguza na Kuweka Fact mezani...
Kwanza kabisa katika Mapito ya Ibrahimu Alizaliwa
Ur of the Chaldeans (Uru wa Wakaldayo) ambayo ilipatikana Mesopotamia..Ambayo kwa sasa inaitwa
modern town of Tell el-Muqayyar in southern Iraq..
So naweza kusema Kuwa Ibrahimu Alizaliwa Iraq ambapo Ni Uarabuni..
(Soma Mwanzo 11:31-32)
Tuendelee.. Abrahimu Aliishi Shuri (
Ambayo kwa Sasa Huitwa saudi Arabia au Macca na medina)
Mwanzo 20:1
"Ibrahimu akaondoka huko kwenda nchi ya kusini, akakaa kati ya Kadeshi na Shuri, naye akatembea katika Gerari."
Na Je Hajari na Mwanaye walikimbilia Wapi?
Mwanzo 16:7
"Malaika wa BWANA akamwona kwenye chemchemi ya maji katika jangwa, chemchemi iliyoko katika njia ya kuendea Shuri"
Je Hiyo Shuri Iko wapi kwa Sasa?
Jaribu kusoma Historia Utajua..
Wote Tunafahamu kuwa Shuri Ipo karibu na Bahari ya Shamu Humo ndyo Mlima sinai ulipo..(Kutoka 15:22)
Sasa Mlima sinai Upo wapi?
Wagalatia 4:25
"Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa anatumika pamoja na watoto."
Sasa kwakuwa Sasa Tunajua kuwa Ibrahimu alikaa Shuri yaani Uarabuni....
Kwanini Sasa Tutaje makka.. Nifuatishe hapa Chini..
Zaburi 84:6-8 (Psalms)
"As they pass through the Valley of Baca, they make it a place of springs; the autumn rains also cover it with pools.
They go from strength to strength, every one of them in Zion appeareth before God.
O LORD God of hosts, hear my prayer: give ear, O God of Jacob. Selah."
Umeona valley of Baca/Bakka/Makka?
Sasa hao wanaoenda Makka/Bakka ni kina nani?
Najua unaweza ukashangaa ila Jina Jingine la Maca ni baca..
View attachment 3021297
Kama una swali Unaweza kuniuliza nitakujib