Tumsifu Yesu Kristu wanaJF!
Kwa wakatoliki wenzangu kuna hawa Jamaa wanajiita Charismatic Catholics, au Karismatiki Katoliki.. hawa Jamaa wamekaa muundo fulani wa kilokole.. Hili Jambo binafsi linanikwaza (Japo sio Big deal).. kwa mfano siku Mkarismatiki akiwa mtoa neno utasikia maneno ya kilokole kama Mpendwa, Bwana asifiwe na Mengine Kadhaa.. sasa mimi binafsi nakuwa mvivu kuwa atentive kwa staili yao Hii..
Juzi kuna sala za Novena (sala za siku 9) nilikuwa nazipitia tukiwa tunajiandaa kwa Novena ya Kushukuru.. Kilichonivunja moyo Niliona mstari umeandikwa Tunasema Asante Baba.. Jambo ambalo wakatoliki awali hatujalizoea..
Sasa wakatoliki wenzangu Nafanyeje ili niweze kudeal vyema na hawa Jamaa..? ili niwe comfortable..
Asanteni!
Divine Khan!
Ndugu yangu umesababisha kanisa kutukanwa bure kwenye hii mada yako.
Pole kwa makwazo ila ninaamini wewe ni muumini mlei na sidhani kama akili yako inamapana kuliko maaskofu na mapadre na hata makadnal ambao ndio wazee wakanisa tunaweza kusema ndio wenye kanisa, kwa utashi wao wameruhusu uwepo wa karismatiki na taratibu zao.
Nime kushangaa sana kukosoa wana karismatiki namna wanavyo fanya majukum yao lakini legio maria,moyo wa Yesu , mt yoseph nk haujawakosoa maana wao utaratibu wao na sala zao nje ya mapokeo hazijulikani Kibiblia .
Mimi binafsi nimehudumu karsmatiki kwa miaka 5 nimeona tofouti ya mkrsmatiki na asie karismatiki ndani ya kanisa katoliki.
Karsmatik hufuata mwongozo ambao ni kama katiba ambayo imetungwa na wataalam dini wakiwepo mapadre maaskofu na wanateilojia na kisha kupiwa na baraza la maaskofu kisha kuupitsha uwe mwongozo rasmi wa karsmatiki katoliki.
Ndio nikasema sina hakika kama wewe ni mtaalam sana wa kanisa katoliki za maaskofu kuona mapungufu ya karsmatiki.
Kama karsmatiki wangekua wako nje ya biblia tusinge itetea lakini kwa kua waamini wajikita katika msingi wa liturgia na Biblia kua ya pili ndio maana watu kama nyie hamkosekani.
Ukweli ni kwamba karsmatiki imekua ikimjenga muumini katika msingi wa neno la Mung, karama za Roho Mtakatifu, na kuikimbia dhambi.
Sasa kwa vile waamini wengi pamoja na mapdre ni washirika wa dhambi ni lazima muichukie karsmatiki
Yote ya yote pole sana kwa kukwazika maana Yesu alitahadharisha kwamba mkwazo yapo lakini ole wake ayasabishae.
Pia jua sote wana wa Mungu kwa sababu tumeamini katika Kristo kwa hio haina haja ya mafarakano. Nyumba tunayojenga ni moja na kila mtu anajenga kwa material yake, wengine nyasi wengine fito wengine mawe wengine udongo lakini mwisho wakazi kila kazi itapimwa kwa moto itakayosimama mwenye kujenga atalipwa , kwa hio sote tunajenga katika msingi mmoja nao ni Kristo.