Jaribio la kugomea Sensa: Mwitikio wa Serikali

Ni kweli walikuwa wanaenda kwenye sensa, na sensa ya kiyahudi ilikuwa watu wanahesabiwa kwa kufuata yale makabila 12 yanayotokana na watoto wa Yakobo. Mtoa hoja ana hoja. Naona watu mnajaribu kuipotosha, yeye kama alivyosema hana matatizo na zoezi la sensa tatizo lake lipo kwenye mchakato ambapo anahisi kuna wahuni watatumia zoezi hili kukwapua hela hazina, na pili anahoji matumizi ya hizo taarifa zitokanazo na sensa? Kama nimemwelewa vizuri anataka kutuambia kuwa yeye anahisi zoezi la sensa ni kiini macho au tunafanya kwa lengo la kufurahisha umati kuwa Tanzania imefanya sensa na takwimu zake ni hizi, kitu ambacho si mhimu. Na anatoa mifano yake ya kuonesha ni jinsi gani kama taarifa za sensa zingetumika basi baadhi ya maamuzi yasingekuchukuliwa. Binafsi pamoja na kuunga mkono uchambuzi wake sikubaliani nae kuwa suluhisho ni kugomea sensa. Na namuomba akahesabiwe, you never know with tommorrow inaweza ikaingia serikali makini ambayo kwauhakika itatumia matokea ya sensa na huenda hata yeye mwenyewe akajikuta ndani ya hiyo serikali mpya maana anaonekana anauwezo huyu mkatolic. Nawasilisha
 
Na wewe ni mkristu wa wapi? Soma luka 2: 1- 7
.
Mi ni mkristu Mkatoliki. Doubt yangu ilikuwa hapa:

Kwamba kwa kuwa Yesu alizaliwa kipindi cha Sensa, basi ishakuwa IMANI haipingani na zoezi hilo!! Kwamba Yesu angezaliwa kipindi cha Vita basi Kanisa lisingepingana na VITA?
 
Ningepost bila kutaja imani yangu wangefikiri kutoshiriki kwangu ni kwasababu labda mimi ni mwislamu ambaye naungana na wale wanaotaka kipengere cha dini kiingizwe lakini mimi nina sababu tofauti ndio maana nikataja imani yangu
 
Waislamu wanaonewa kweli,Waislamu lazima tuwe wengi kuliko wakristo kwa sababu hz,mtu mmoja ana wake watatu kwa wakati mmoja hvyo uwezekano wa kuwa na watoto wengi ni mkubwa,kwa Dar waislamu wengi wanakaa uswazi,tandika,tandale,manzese,mbagala n.k na huko ndipo wanapozaliana kupita kiasi wakijiaminisha kila mtoto na riziki yake pia tajiri na mali zake masikini na wanawe...nyie wakristo wakati mnahangaika na kitabu,mwenzio nilioishia la 7 nishaanza kuzaa zamani sana,wakati wewe msomi una mtoto m1 mimi nina wa4,sisi waislamu tupo wengi sana ndomana hata ukienda mahakamani kesi nyingi kwa siku ni za waislamu,bdo tu hamuamini tumewazidi?hebu tuacheni tujiunge na OIC yetu lbd na sie tutakuwa na maendeleo hata tukajenga na vyuo vyetu.Mimi muislamu sihesabiwi sensa.TAKBIR
 

Hivi unajielewa kweli wewe?? Mbona umekuja na gia za oh mimi Rc..

Nahc hujitambui
 


Wewe kweli umepagawa kama jina lako,hivi nyie kipindi cha Mkapa na awamu ya kwanza ya JK mlivyokuwa mnaipigia kampeni CCM makanisani kuwa JK ni chaguo la mungu na CUF ni cha waislamu cha kidini huo haukuwa udini? Mimi binafsi sijawahi kupiga kura na wala sitakuja kupiga kura lakini kwa mwenendo wa uchaguzi wa mwaka 2010 hata mimi nisingemchagua Padri awe rais ,nilikuwa na shuhudia kampeni zinavyoenezwa kwenye nyumba zenu za ibada sasa mimi wa imani nyingine unafikiri ningefikiriaje? Kwa ufinyu wako wa kufikiri kwahiyo unadhani tungemchagua Padri Slaa ndiyo angesikiliza maombi ya waislamu?
 
Naamini Waislamu walikuwa na hoja ilitakiwa itafutwe namna ya kuboresha hilo swali, na kiukweli huwa naamini kuwa Waislamu wengi wanafahamu kudai haki zao kuliko sisi wakristo, ingawa wakati flani wanavuka mipaka lakini katika hili Serikali haijawatendea haki, walitakiwa kusikilizwa na kama wakiamua kutoshirki binafsi naona waachwe huru tu.

Kitu kingine hata sisi tutakaohesabiwa je kwa nchi hii na huu ufisadi ulivyojikita hata tukihesabiwa na hizo ahadi wanazotueleza je kuna mabadiliko ya maana yatakayotokana na hiyo sensa?
Je hadi sasa idadi ya walimu na madaktari haijulikani? je idadi ya hospitali na shule za kata Tz hazijulikani mbona ni shida tupu, ndiyo maana nasema tukahesabiwe tu lakini sitegemei lolote la maana kwenye hii sensa iliyoko chini ya serikali inayokumbatia mafisadi
 
Yale yale ya kwenye kitabu cha NGOSWE PENZI KITOVU CHA UZEMBE.kweli mwandishi ni sawa na NABII nimeamini.
 
Kuna watu humu wanabwata tu kuwa hawatahesabiwa, lakini kwenye makazi yao hao ndo watakuwa watoaji wakuu wa taarifa kuhusu wenzao, kama wewe hutaki kuhesabiwa si ukae kimya kwani sisi yanatuhusu nini, najua kwa wale watakaohesabiwa kesho wapo kimya na sio nyinyi mnaopiga kelele hapa
 
Nashangaa sana watu mnashambulia mleta uzi kama vile anachosema sis sahihi, acheni kukimbilia tu kutoa hukumu kama vile ni nyie mliojaliwa ubongo hapa kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni yake. Je walimu na madaktari kuboreshewa mazingira ya kazi bado kunahitaji sensa hawajulikani? Tukihesabiwa baada ya sensa nchi itabadilika kwa maendeleo.
Acheni kukurupuka na kurusha maneno mambo mengine lazima tuwe na ubongo wa kufikiri, hivi tumefika hapa tulipo kwa kuwa sensa haijafanyika? Tusiende kama makasuku tu, na kukariri eti sensa inaenda kuleta maendeleo, kwangu mimi kushiriki au kutoshiriki ni sawa tu
 
Hakuna hasara yoyote ndugu yangu ila serikali yetu siku hizi kwa jambo lolote lile inaogopa hata kivuli chake, badala ya kutatua tatizo kama lilivyo wao hujibanza banza mafichoni na kuishia kuwatuma akina Ramadhani Ighondu wa wawakilishe

Sasa kama hakuna hasara wala faida, basi kila mtu ashiriki sensa watu waache maelezo yasiyo na miguu wala kichwa
 
R.C inahusianaje na sensa pamoja na madai yako?Ungesema mimi mtz!
 
MMM,Mimi concern yangu sio kwenye dini lakini nikwa sababu za kidemographia zaidi na ninafikiri wataalam wa sosholojia watakubaliana na mimi. Kipengele cha Biodata ni muhimu sana katika tafiti za kijamii na ukosefu wa takwimu sahihi zimesababisha usumbufu mkubwa kwa wasomi wa kitanzania na hata wale wa nje ambao wamekuja kufanya utafiti Tanzania. Hii ni kwa sababu wanapopitia machapisho tofauti(in literature review) wanakuja na takwimu tofauti tofauti na hii inasababisha iwe vigumu kuamini kwamba nani ana takwimu sahihi.Na imani iliyojengeka kwa baadhi ya watu kwamba ''waafrika katika tafiti zao wanapika sana data'' inaanzia hapo au inazidi kupata mashiko.
Kwa mfano, mtaalam ambaye anafanya utafiti juu ya ''matumizi na perception ya watu juu ya matumizi ya kondomu'' ni vema ajue religious affiliation ya mahali anapokwenda kufanyia utafiti ili hata maswali yake na approach kwa jamii husika isimpe tabu. je'takwimu kama hizi atazipata wapi? katika majarida na ofisi ambapo kila sehemu ina data tofauti?Let us think of the possibility the data you have about religious affiliation in a certain community shows 20% muslims lakini in reality unakutana na 70% ni muslims. Unafikiri utapata ulichotarajia?
Secondly, kumekuwa na sweeping statements kwamba baadhi ya lugha na makabila yanapotea na mengine yameishapotea hapa Tanzania. kwa mfano wasandawe,na hayo ulotaja MMM wamang'ati na wahadzabe. Tunaambiwa wahadzabe wapo 5000tu!A clear justification can only be achieve through National Census. Sioni ubaya wa kuuliza kabila la mtu katk sensa ili kufanikisha hilo.Na hata pia tunapopanga mipango ya maendeleo,ni vema kujua kabila ili uweze ku-plan approach ipi itumike kufikisha ujumbe uliokusudiwa.Implementation ya Mipango mingi ya maendeleo ina-fail kwa sababu tuna-assume tunawajua watu ambao tunawapelekea maendeleo, na hata kujifanya kwamba data za dini,kabila,etc hazina umuhimu!
So to me hii ni baadhi ya mifano inayonifanya niamini kwamba maelezo ya kidemografia kama dini na kabila ni muhimu sana.
Tatizo ninaloliona mimi ni moja, ''Ni nini madhumuni ya sensa inayofanyika?''. kama jibu ni ''Maendeleo'' basi hivyo vipengele ni muhimu sana. I stand to be corrected!
 
Mods mngeonesha uzalendo kama mleta uzi angepigwa ban walau ya wiki nzima.Msicheze na maslahi ya taifa bana.
 
Hata mie nahisi hivyo kwa kusoma hapo red. Yesu alizaliwa wakati wa sensa? Over My Dead Body! Sijui ni biblia gani ameisoma asee!!

Duh! Jamaa ana uwelewa kiasi chake. Nikweli yesu alizaliwa kipindi cha sensa lakini ninachojua R.C wanabiblia yao! Tehe tehe! Liwalo na liwe
 
Mie na familia yangu hatuhesabiwi. Ina faida gani hii sensa?
 
Mimi kama muislamu tena baba yangu sheikh hapa Tabata tutahesabiwa na nawaomba waislamu wenzangu tujitokeze
Mie na familia yangu hatuhesabiwi. Ina faida gani hii sensa?
 
Mze Mwanajiji kimsingi hawa watu hawana hoja ya msingi hata 1. Hata ile hoja dhaifu inafia katika ukweli kuwa anayetaka sensa ni serikali na ndio iliyoainisha nini inataka kujua kwa watanzania wote. Kama mlipa kodi, nakubariana na mawazao ya kamanda wetu mku wa oparesheni kuwa wanaopinga wapigwe balaabalaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…