Mpitagwa
JF-Expert Member
- Feb 10, 2012
- 2,339
- 1,123
Ni kweli walikuwa wanaenda kwenye sensa, na sensa ya kiyahudi ilikuwa watu wanahesabiwa kwa kufuata yale makabila 12 yanayotokana na watoto wa Yakobo. Mtoa hoja ana hoja. Naona watu mnajaribu kuipotosha, yeye kama alivyosema hana matatizo na zoezi la sensa tatizo lake lipo kwenye mchakato ambapo anahisi kuna wahuni watatumia zoezi hili kukwapua hela hazina, na pili anahoji matumizi ya hizo taarifa zitokanazo na sensa? Kama nimemwelewa vizuri anataka kutuambia kuwa yeye anahisi zoezi la sensa ni kiini macho au tunafanya kwa lengo la kufurahisha umati kuwa Tanzania imefanya sensa na takwimu zake ni hizi, kitu ambacho si mhimu. Na anatoa mifano yake ya kuonesha ni jinsi gani kama taarifa za sensa zingetumika basi baadhi ya maamuzi yasingekuchukuliwa. Binafsi pamoja na kuunga mkono uchambuzi wake sikubaliani nae kuwa suluhisho ni kugomea sensa. Na namuomba akahesabiwe, you never know with tommorrow inaweza ikaingia serikali makini ambayo kwauhakika itatumia matokea ya sensa na huenda hata yeye mwenyewe akajikuta ndani ya hiyo serikali mpya maana anaonekana anauwezo huyu mkatolic. Nawasilisha