Jaribio la kugomea Sensa: Mwitikio wa Serikali

Mwanakijiji uko sahihi umefanya vizuri kutoa maoni.
 
Hao wachache unao dhani na ambao mliwapandikiza hiyo dhambi ndio sasa wanaleta madhara!
Hata wasio na vyama wameona pakushika ni hapo kwenye kipengele cha dini kwani ni matokeo ya kilicho pandwa mwaka2010.

Mlitumia propaganda za udini kushawishi leo umeona madhara yake, hata kama unasema ni wachache lakini wameleta madhara makubwa!

Kila mtu atavuna alicho kipanda!

Nani kakwambia udini Tanzania umeanza mwaka 2010 nadhani umri wako mdogo soma historia ya Tanzania vizuri, hivi hunajua Bakwata imeanzishwa na nani? Na kwa madhumuni gani? Sio unakurupuka tu kujibu...halafu hakuna sehemu ambayo nimesema wachache.
 
Kwa mtazamo wangu sioni madhara yake kama kipengele hiki kingekuwepo, na zaidi kingekuwa namafaa kwa vizazi vijavyo, nimejitahidi kuangalia takwimu za mataifa mengi nimeona kunatakwimu za imani za watu, sijajua wataalamu wetu wameakisi kutoka wapi mfumo huu wenye kizungumkuti.

Upande wa sarafu nachelea kuwaunga mkono hasa kwakulifanya suala hili ni LAO, UBINAFSI hata kama linamashiko ila wamesimamia hoja dhaifu na kuimiliki kiasi kwamba mie MUYAHUDI siwezi kupenyeza hoja yangu ikakubalika kwao na tukaungana kupinga utaratibu huu wa sensa.
 
Mzee Mwanakijiji, ningependa kuongelea point yako ya waislamu wanajifikiria/ kujiangalia wenyewe. Mi nasema upo wrong sana, katika jamii ya Tanzania waislamu hawana hayo mambo na ukiona inatokea basi uvumilivu umefikia kikomo. Ngoja nikupe mfano mdogo sana, kipindi serikali ilifuta misamaha ya kodi kwa mashirika ya dini kwa lengo la kuiongezea kipato taifa ingeneral/hazina je akina nani walipinga vikali kwa jazba?? Jibu ni makanisa na taasis zake zoote. Je huu sio ubinafsi/kujifikiria wenyewe na sio nchi ingeneral?? Ulisikia waislamu wanapinga kulipa kodi? Je huoni hizo kodi zingelipwa hata jamii uliyoitaja. Wahazabe etc wangefaidika nao?? Na pia elewa waislamu hawasemi iwekwe kipengele cha uislamu tu bali kiwekwe kipengele cha dini( means dini zote hata ya jadi) sasa ubinafsi/kujiangalia wao inakujaje?? Pia kama uislamu inavyosema siku zote kutii sheria iliyo ya haki inatii sheria/ kanuni za umoja wa mataifa ambapo kipengele cha dini kinaruhusu kuwepo kny sensa, sasa kutii huku kanuni ndio ubinafsi? Si kila siku tunahubiri kutii sheria/kanuni humu jamvini, je leo inajuwaje the same isitumike kisa waislamu wanahoji. Embu tusiwe biased, tuwe na hoja za kujenga nchi yetu sote na sio ujanja ujanja wa kudonyoa hints. US,UK etc wameweka hata jirani zetu Uganda why sisi tu Tanzania ndo kikwazo? Tatizo watawala wamekariri waislamu wakiongea basi wanaleta udini, mambo haya ndo wanapelekea kuamsha jazba/hisia za waumimi wa dini ya kiislamu. Mzee Mwanakijiji huwa naheshimu sana mda zako Lakini hili la leo nina maswali mengi kuliko majibu. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Africa.

QUOTE=Mzee Mwanakijiji;4495728]Hoja pekee ambayo ninakubaliana nao wale wanaopinga sensa ni kuwa sensa ilipaswa kuuliza sifa zote za msingi za kijamii ili kuweza kupata takwimu sahihi za watu waishio Tanzania. Lengo kubwa la sensa ni kutoa picha sahihi ya jamii yetu ilivyo na imeundwa vipi. Hivyo, maswali yanayohusu kabila, dini, rangi na hata tofauzi za chini ya hapo (madhehebu, kuchanganya kabila au rangi, n.k) yalipaswa kuwepo kama sehemu ya dodoso za sensa. Tofauti yangu kubwa hata hivyo kwenye hili ni kuwa maswali ya aina hiyo yalipaswa kuwa ya uchaguzi wa mtu kujibu (OPTIONAL) bila kumlazimisha. Hivyo, Watanzania ambao wamekuwa wakitaka swali la dini liwepo kwenye maswali ya sensa wana hoja inayoishia hapo tu lakini hawana hoja ya kulazimisha watu kujibu.

Kwa mfano, swali la dini kwenye sensa ya Marekani ni 'optional' kama ilivyo kwa maswali mengine kadhaa ya kidemographia. Sheria ya Marekani inakata Idara ya Sensa kuuliza swali la dini huku ikilazimisha mtu kujibu. Hivyo, hata kwetu swali hili lingeweza kabisa kuwekwa na mtu anayetaka kujibu anajibu na asiyetaka hajibu. Kutokana na kanuni hiyo kama nilivyoandika karibu miezi miwili iliyopita mahali pengine kimsingi hakuna hoja ya serikali ya kutetea kukataa kuuliza swali hili. Hii ni kweli hata kwenye maswali ya kabila, rangi au madhehebu. Mtu - kwa mfano - angeweza kuulizwa "je unajitambulisha kama mfuasi wa dini gani?" na akapewa uchaguzi wa "Uislamu", "Ukristu", "Uhindu" na "Za Jadi", "Nyinginezo" na "Hakuna" lakini swali zima likiwa ni la uchaguzi. Mtu akijibu kwa mfano na kusema ni "Mkristu" bado anakuwa na uchaguzi wa kujibu kama ni wa dhehebu gani "Pentekoste", "Kilutheri", "Romani Katoliki" au "SDA" na bado akawa huru kujibu swali hilo zaidi au kuishia tu kwenye kujitambulisha dini yake.

Sasa, hili lingewezekana kabisa na naamini lingeweza kufanywa bila ya kuonesha aina yoyote ya upendeleo au kubania watu. Hata hivyo, serikali yetu ambayo ina tatizo kubwa la hekima iliamua kuondoa kabisa uwezekano wa swali hili kwa sababu moja kubwa tu: Inaogopa matokeo ya majibu ya swali hilo. Tuchukulia mfano ambao unatokana na hoja nzima ya kundi la Waislamu wanaotaka kususia sensa.

Fikiria kuwa matokeo ya sensa ambapo maswali yangekuwa si ya kulazimisha kujibu (mandatory) na ikaja kuonesha kuwa waliojibu sensa nzima Waislamu wanaonekana ni wengi je ina maana kuwa Waislamu ni wengi zaidi Tanzania kuliko Wakristu au ni kuwa tu wengi waliojibu swali hilo ni Waislamu? Je ingekuwa vipi kama ingekuwa kinyume chake? Lakini zaidi ni kuwa kwenye kundi ambalo linaamini kuwa kuna mfumo Kristu ambao unakandamiza Waislamu nchini je kuna uwezekano wowote wa sensa kuonesha matokeo ambayo hayaoneshi Waislamu wakiwa wengi? Jawabu ni kuwa tayari wapo viongozi na wanaharakati wa makundi ya Kiislamu ambao wameshawaaminisha wafuasi wao kuwa Waislamu ni wengi nchini na hivyo matokeo ya sensa ambayo yangeonesha kuwa ni kinyume na hili (kwamba wako wachache) yangepokewa kwa hisia ya kuonewa, kudhulumiwa na madai yale yale ya kutamalaki kwa kile kinachoitwa "mfumo Kristo".

Ni kutokana na hili basi swali la dini limekuwa gumu kuwekwa katika sensa ya sasa ya watu na makazi kwa sababu hakuna namna rahisi ya kuweza kuliweka bila kuwa tayari na matokeo yake. Ni hili basi naamini (sina sababu ya kuamini vinginevyo) serikali iliamua kama ilivyoamua huko nyuma kutokuuliza swali hili la dini au kabila au la tofauti nyingine za kidemographia. Binafsi ninaamini ni uamuzi wa kiwoga, wenye makosa na ambao unaonesha udhaifu wa walio madarakani kutowaamini Watanzania kuwa hakuna matokeo yoyote ya sensa ambayo yangeweza kubadili mahusiano yaliyopo sasa kama propaganda za sasa zote hazikuweza kufanya hivyo.

Sasa, uamuzi wa viongozi wa vikundi hivi vya Kiislamu kudai kuwa wanasusia sensa kwa sababu ati serikali imekataa kuwekwa swali la dini kwenye sensa ni uamuzi wa kibinafsi, wa kujipendelea na kujinyanyua dhidi ya Watanzania wengine. Sababu kubwa ni kwamba katika taifa letu jamii inayodhulumiwa zaidi na mfumo wa kifisadi ambao umetamalaki nchini kwa miaka thelathini sasa SIYO WAISLAMU. Naomba kurudia kauli hiyo ili isije ikapita hivi hivi: katika taifa letu jamii inayodhulumiwa zaidi na mfumo wa kifisadi ambao umetamalaki nchini kwa miaka thelathini sasa SIYO WAISLAMU.

Watu pekee ambao nina uhakika wana haki ya kulalamika na hata kususia sensa hii siyo Waislamu wala Wakristu; siyo Wahindu wala Waarabu! Bali ni watu wa jamii za jadi ambao wametupwa pembezoni mwa mafanikio ya taifa letu, wakiwa ni raia wa daraja la nne (nje ya treni) kwenye taifa lao. Watu ambao maisha yao yamekuwa ni ya kusahauliwa na kutendewa kama wageni. Makabila mawili yanakuja kwa haraka - kwanza ni Wahadzabe na wenzao Watindiga, na Wamang'ati. Makabila haya yana haki ya kutaka kujua idadi yao, wana haki ya kutaka kujua wamefikiwa na maendeleo ya karne ya 21 kwa kiasi gani kulinganisha na makabila mengine. Ikumbukwe kuwa Mchagga Muislamu na Mkristu Muislamu kwa kiasi kikubwa wako katika mafanikio zaidi na nafasi zaidi kufanikiwa kuliko Mtindiga au Mhadzabe Muislamu au Mkristu. Hawa ndio watu ambao kweli wako kwenye pembezoni ya kona za mafanikio ya taifa.

Kwa kundi la Waislamu hawa kuamua kususia sensa kana kwamba wanaonewa sana kuliko jamii nyingine yoyote au hata kuonesha kuwa wanaonewa ni absurd. Ninaamini wangeweza kabisa kudai swali hili na kutumia njia za kawaida ili siku moja liweze kuingizwa kwani lina maslahi makubwa zaidi. Lakini kuamua kususia ati kwa vile hawajasikilizwa ni kujiona kupita kiasi. Na hili ni kweli kwa sababu wanachotaka kujua ni suala la "dini" tu lakini siyo kabila, rangi, madhehebu. Kwanini wanagomea sensa kwa sababu ya kutohusisha dini tu? Yawezekana ni kwa sababu wao HAWAJALI hali za jamii nyingine ambazo nazo zingependa kunufaika na takwimu za sensa.

Ndio maana kwenye hoja yangu ya awali miezi ile miwili iliyopita nilisema kuwa swali la demographia mambo ya dini, kabila, rangi na hata dhehebu nilisema kuwa kujua idadi na mambo mengine yanayohusiana na haya ni muhimu kwa kuweza kupanga maendeleo - ambalo ndilo lengo la sensa. Kujua jamii gani na kwa kiasi gani iko nyuma kwa kuangaliwa takwimu zilizokusanywa kwa sensa kunasaidia taifa.

Kwa vile zoezi hili lengo lake ni kujua hasa 'idadi' ya Watanzania na wakazi wa Tanzania vitambulisho vingine vyao vyovyote siyo vya muhimu kuliko hilo la idadi. Binafsi naamini baada ya serikali kuboronga suala la sensa ipo haja ya kufikiria sensa maalum ya demographia ya wananchi wetu. Ninaamini ili kufanikisha sensa hii ya idadi watawala wetu watoe ofa ya kuamua kufanya sensa ya demographia (kabila, dini, na rangi(race)) Hata hivyo sensa hiyo maalum inapaswa kuwa optional kwa Watanzania watakaotaka kushiriki na isiwe ya lazima. Nje ya hapo serikali itoe ahadi kuwa sensa ijayo (miaka kumi toka sasa) itakuwa ni sensa ya demographia vile vile.

Kususia sensa ya idadi na ambayo miaka yote imekuwa ni ya idadi ni kukosa busara, ni kuonesha kutokujali mahitaji ya wengine lakini zaidi ni kutaka kujipendelea na kujitukuza juu ya wengine. Lakini zaidi ni kuwa wale ambao leo wanahamasisha kususia sensa hii baadhi yao ndio hao hao waliosimama kuipigia debe ilirudi madarakani mwaka 2010. Yaani wale wale ambao waliwacheka wengine walipoona magugu wao waliendelea kulia 'panda mbegu panda mbegu!' Sasa leo yanaota wanaruka na kutaka kukana.

Binafsi ninaamini watakuwa na hoja ya kususia sensa kama kwanza watakuwa tayari kususia na kutaka wananchi wakisusie chama kilichounda serikali hiyo. Kwa sababu uamuzi wa kukataa kuweka maswali ya demographia ni wa kisiasa na umetolewa na viongozi wa kisiasa. Ni uamuzi wa CCM. Badala ya kususia sensa waisusie CCM na wataonesha mfano kweli wa kuchukuizwa kama wataanza kurudisha kadi za CCM. Endapo watafanya hivyo wawe tayari kuunga mkono chama ambacho kitakuja na sera ya kuhakikisha sensa ijayo ya taifa itakuwa ni ya kidemographia.

Nje ya hapo, kususia sensa hakuna tena.

MMM[/QUOTE]
 
Acha kupanic! Mwaka 2010 mlichoche kaa la moto najua utakataa maana ukweli kwenu CCM ni uongo! unaposema kuwa nani kasema waislam wote ni ccm una maanisha sio wote bali kuna baadhi yao na hao ndio mliwatumia kupandikiza mnayo yavuna!

Unapo sema udini ulianza zamani unaweza ukawa sahihi lakini unatakiwa utumie kichwa chako kujiuliza je hisia za kipindi hicho ni sawa na sasa?

Ritz lazima ukubali mnavuna mlicho panda!

Nani kakwambia udini Tanzania umeanza mwaka 2010 nadhani umri wako mdogo soma historia ya Tanzania vizuri, hivi hunajua Bakwata imeanzishwa na nani? Na kwa madhumuni gani? Sio unakurupuka tu kujibu...halafu hakuna sehemu ambayo nimesema wachache.
 
Hoja pekee ambayo ninakubaliana nao wale wanaopinga sensa ni kuwa sensa ilipaswa kuuliza sifa zote za msingi za kijamii ili kuweza kupata takwimu sahihi za watu waishio Tanzania. Lengo kubwa la sensa ni kutoa picha sahihi ya jamii yetu ilivyo na imeundwa vipi. Hivyo, maswali yanayohusu kabila, dini, rangi na hata tofauzi za chini ya hapo (madhehebu, kuchanganya kabila au rangi, n.k) yalipaswa kuwepo kama sehemu ya dodoso za sensa. Tofauti yangu kubwa hata hivyo kwenye hili ni kuwa maswali ya aina hiyo yalipaswa kuwa ya uchaguzi wa mtu kujibu (OPTIONAL) bila kumlazimisha. Hivyo, Watanzania ambao wamekuwa wakitaka swali la dini liwepo kwenye maswali ya sensa wana hoja inayoishia hapo tu lakini hawana hoja ya kulazimisha watu kujibu.

Kwa mfano, swali la dini kwenye sensa ya Marekani ni 'optional' kama ilivyo kwa maswali mengine kadhaa ya kidemographia. Sheria ya Marekani inakata Idara ya Sensa kuuliza swali la dini huku ikilazimisha mtu kujibu. Hivyo, hata kwetu swali hili lingeweza kabisa kuwekwa na mtu anayetaka kujibu anajibu na asiyetaka hajibu. Kutokana na kanuni hiyo kama nilivyoandika karibu miezi miwili iliyopita mahali pengine kimsingi hakuna hoja ya serikali ya kutetea kukataa kuuliza swali hili. Hii ni kweli hata kwenye maswali ya kabila, rangi au madhehebu. Mtu - kwa mfano - angeweza kuulizwa "je unajitambulisha kama mfuasi wa dini gani?" na akapewa uchaguzi wa "Uislamu", "Ukristu", "Uhindu" na "Za Jadi", "Nyinginezo" na "Hakuna" lakini swali zima likiwa ni la uchaguzi. Mtu akijibu kwa mfano na kusema ni "Mkristu" bado anakuwa na uchaguzi wa kujibu kama ni wa dhehebu gani "Pentekoste", "Kilutheri", "Romani Katoliki" au "SDA" na bado akawa huru kujibu swali hilo zaidi au kuishia tu kwenye kujitambulisha dini yake.

Sasa, hili lingewezekana kabisa na naamini lingeweza kufanywa bila ya kuonesha aina yoyote ya upendeleo au kubania watu. Hata hivyo, serikali yetu ambayo ina tatizo kubwa la hekima iliamua kuondoa kabisa uwezekano wa swali hili kwa sababu moja kubwa tu: Inaogopa matokeo ya majibu ya swali hilo. Tuchukulia mfano ambao unatokana na hoja nzima ya kundi la Waislamu wanaotaka kususia sensa.

Fikiria kuwa matokeo ya sensa ambapo maswali yangekuwa si ya kulazimisha kujibu (mandatory) na ikaja kuonesha kuwa waliojibu sensa nzima Waislamu wanaonekana ni wengi je ina maana kuwa Waislamu ni wengi zaidi Tanzania kuliko Wakristu au ni kuwa tu wengi waliojibu swali hilo ni Waislamu? Je ingekuwa vipi kama ingekuwa kinyume chake? Lakini zaidi ni kuwa kwenye kundi ambalo linaamini kuwa kuna mfumo Kristu ambao unakandamiza Waislamu nchini je kuna uwezekano wowote wa sensa kuonesha matokeo ambayo hayaoneshi Waislamu wakiwa wengi? Jawabu ni kuwa tayari wapo viongozi na wanaharakati wa makundi ya Kiislamu ambao wameshawaaminisha wafuasi wao kuwa Waislamu ni wengi nchini na hivyo matokeo ya sensa ambayo yangeonesha kuwa ni kinyume na hili (kwamba wako wachache) yangepokewa kwa hisia ya kuonewa, kudhulumiwa na madai yale yale ya kutamalaki kwa kile kinachoitwa "mfumo Kristo".

Ni kutokana na hili basi swali la dini limekuwa gumu kuwekwa katika sensa ya sasa ya watu na makazi kwa sababu hakuna namna rahisi ya kuweza kuliweka bila kuwa tayari na matokeo yake. Ni hili basi naamini (sina sababu ya kuamini vinginevyo) serikali iliamua kama ilivyoamua huko nyuma kutokuuliza swali hili la dini au kabila au la tofauti nyingine za kidemographia. Binafsi ninaamini ni uamuzi wa kiwoga, wenye makosa na ambao unaonesha udhaifu wa walio madarakani kutowaamini Watanzania kuwa hakuna matokeo yoyote ya sensa ambayo yangeweza kubadili mahusiano yaliyopo sasa kama propaganda za sasa zote hazikuweza kufanya hivyo.

Sasa, uamuzi wa viongozi wa vikundi hivi vya Kiislamu kudai kuwa wanasusia sensa kwa sababu ati serikali imekataa kuwekwa swali la dini kwenye sensa ni uamuzi wa kibinafsi, wa kujipendelea na kujinyanyua dhidi ya Watanzania wengine. Sababu kubwa ni kwamba katika taifa letu jamii inayodhulumiwa zaidi na mfumo wa kifisadi ambao umetamalaki nchini kwa miaka thelathini sasa SIYO WAISLAMU. Naomba kurudia kauli hiyo ili isije ikapita hivi hivi: katika taifa letu jamii inayodhulumiwa zaidi na mfumo wa kifisadi ambao umetamalaki nchini kwa miaka thelathini sasa SIYO WAISLAMU.

Watu pekee ambao nina uhakika wana haki ya kulalamika na hata kususia sensa hii siyo Waislamu wala Wakristu; siyo Wahindu wala Waarabu! Bali ni watu wa jamii za jadi ambao wametupwa pembezoni mwa mafanikio ya taifa letu, wakiwa ni raia wa daraja la nne (nje ya treni) kwenye taifa lao. Watu ambao maisha yao yamekuwa ni ya kusahauliwa na kutendewa kama wageni. Makabila mawili yanakuja kwa haraka - kwanza ni Wahadzabe na wenzao Watindiga, na Wamang'ati. Makabila haya yana haki ya kutaka kujua idadi yao, wana haki ya kutaka kujua wamefikiwa na maendeleo ya karne ya 21 kwa kiasi gani kulinganisha na makabila mengine. Ikumbukwe kuwa Mchagga Muislamu na Mkristu Muislamu kwa kiasi kikubwa wako katika mafanikio zaidi na nafasi zaidi kufanikiwa kuliko Mtindiga au Mhadzabe Muislamu au Mkristu. Hawa ndio watu ambao kweli wako kwenye pembezoni ya kona za mafanikio ya taifa.

Kwa kundi la Waislamu hawa kuamua kususia sensa kana kwamba wanaonewa sana kuliko jamii nyingine yoyote au hata kuonesha kuwa wanaonewa ni absurd. Ninaamini wangeweza kabisa kudai swali hili na kutumia njia za kawaida ili siku moja liweze kuingizwa kwani lina maslahi makubwa zaidi. Lakini kuamua kususia ati kwa vile hawajasikilizwa ni kujiona kupita kiasi. Na hili ni kweli kwa sababu wanachotaka kujua ni suala la "dini" tu lakini siyo kabila, rangi, madhehebu. Kwanini wanagomea sensa kwa sababu ya kutohusisha dini tu? Yawezekana ni kwa sababu wao HAWAJALI hali za jamii nyingine ambazo nazo zingependa kunufaika na takwimu za sensa.

Ndio maana kwenye hoja yangu ya awali miezi ile miwili iliyopita nilisema kuwa swali la demographia mambo ya dini, kabila, rangi na hata dhehebu nilisema kuwa kujua idadi na mambo mengine yanayohusiana na haya ni muhimu kwa kuweza kupanga maendeleo - ambalo ndilo lengo la sensa. Kujua jamii gani na kwa kiasi gani iko nyuma kwa kuangaliwa takwimu zilizokusanywa kwa sensa kunasaidia taifa.

Kwa vile zoezi hili lengo lake ni kujua hasa 'idadi' ya Watanzania na wakazi wa Tanzania vitambulisho vingine vyao vyovyote siyo vya muhimu kuliko hilo la idadi. Binafsi naamini baada ya serikali kuboronga suala la sensa ipo haja ya kufikiria sensa maalum ya demographia ya wananchi wetu. Ninaamini ili kufanikisha sensa hii ya idadi watawala wetu watoe ofa ya kuamua kufanya sensa ya demographia (kabila, dini, na rangi(race)) Hata hivyo sensa hiyo maalum inapaswa kuwa optional kwa Watanzania watakaotaka kushiriki na isiwe ya lazima. Nje ya hapo serikali itoe ahadi kuwa sensa ijayo (miaka kumi toka sasa) itakuwa ni sensa ya demographia vile vile.

Kususia sensa ya idadi na ambayo miaka yote imekuwa ni ya idadi ni kukosa busara, ni kuonesha kutokujali mahitaji ya wengine lakini zaidi ni kutaka kujipendelea na kujitukuza juu ya wengine. Lakini zaidi ni kuwa wale ambao leo wanahamasisha kususia sensa hii baadhi yao ndio hao hao waliosimama kuipigia debe ilirudi madarakani mwaka 2010. Yaani wale wale ambao waliwacheka wengine walipoona magugu wao waliendelea kulia 'panda mbegu panda mbegu!' Sasa leo yanaota wanaruka na kutaka kukana.

Binafsi ninaamini watakuwa na hoja ya kususia sensa kama kwanza watakuwa tayari kususia na kutaka wananchi wakisusie chama kilichounda serikali hiyo. Kwa sababu uamuzi wa kukataa kuweka maswali ya demographia ni wa kisiasa na umetolewa na viongozi wa kisiasa. Ni uamuzi wa CCM. Badala ya kususia sensa waisusie CCM na wataonesha mfano kweli wa kuchukuizwa kama wataanza kurudisha kadi za CCM. Endapo watafanya hivyo wawe tayari kuunga mkono chama ambacho kitakuja na sera ya kuhakikisha sensa ijayo ya taifa itakuwa ni ya kidemographia.

Nje ya hapo, kususia sensa hakuna tena.

MMM

Mkuu, Nimekuelewa!
pia nilichokiona serkali haina hata sababu ya kuweka kipengele cha dini maana wao serkali hawana Pepo ya kuwapa na anaewajua waumini ni Allah tu!
 
Aksante pamoja na mtizamo wako hasi, umeuliza swali zuri kwa nini inaogopa matokeo ya swali la sensa? Historia sahihi inaonesha Waislamu ni wengi katika nchi hii maana walikuwa hivyo sensa ya mwisho ya mkoloni 1957, Lakini pia katika Dunia makadirio ya ongezeko la watu kufuatana na dini zao yalifanywa kati ya mwaka 1935 na 1985 na matokeo kwa dini mbili kuu duniani yalikuwa hivi: Islam 235% increase, and Christianity 78% maana yake kama Tanzania ni subset ya dunia na growth rate ya kidunia ni hivyo na kwamba 1957 waislamu walikuwa wengi then automatically sensa yenye kipengele cha dini itaonesha waislamu ni wengi. HATA hivyo mtoa mada anaweza kunifafanulia zaidi:

  1. Kwa nini taasisi mbalimbali za serikali na binafsi zimekua zikitoa takwimu za watu na dini zao?
Mfano0fisi ya waziri mkuu inadai wakristo ni 45%-waislamu 35%. TBC1, imetangazawakristo ni 52%-waislamu 32%.Bodi ya watalii -Christianity and Islam are the predominantreligions of Tanzania. About 40-45% of the population practice Christianity,about 35-40% practice Islam.,Tovuti kikatoliki (RCNet) waislamu 34%- na wakristo ni 44%

a) kwa nini takwimu zinatofautiana? na b)kwa nini pamoja na kutofautiana zotezinaonesha wakristo ni wengi kuliko waislamu?

Hapo kwenye red tunajuaje hiyo sensa ilikuwa sahihi?
Mkoloni alikuwa na lengo gani au na uchungu gani na nchi hii kwa sisi kuamini sensa yake?
Je kwenye sensa za mwanzo za mkoloni ratio zilikuwa vipi?
 
Kiukweli upofu wa DINI humfanya hata aliye msomi aonekane mjinga. Namashaka sana na USOMI na UELEWA wa huyu mtoa mada. Elimu ya mtu sio kukaa darasani tu. Mungu ikomboe Tanzania maana dalili za mwisho wa Armani yetu umekaribia maana hawa uzao wa Ismail wamepofushwa hata wasinjure iliyo kweli. Kutwa kulalamika tu. Hata wakiwa 100% katika Tanzania yetu; kamwe hawatabakia salama.
Ume qoute lakini hujajibu hata hoja moja katiak kiambatanisho.
Pamekuwa na watu ambao wanaona Waislamu ni wajinga.Nimeambatanisha makala ya msomi wa Kiislamu na hoja alizotoa.
Changia hoja la sivyo kaa kimya.
 
Naona kugomea sensa ni hujuma kwa "mzee wa magogoni"...:A S-baby:
 
Katika kifungu cha 11 cha mkataba huo kinasema:
”Serikali ni lazima itoe nafasi za ajira katika vyuo vyake vya Ualimu (TTC) kwa Wakufunzi wa kikristo kufundisha watu wataofuzu kama Walimu kwa ajili ya shule za Makanisa zilizoanzishwa.”
Je, hii si mipango ya maendeleo kwa kuzingatia dini?

Kutokana na makubaliano hayo baina ya Serikali na kanisa, imelazimika Serikali kuyapa makanisa mabilioni ya fedha za wa-Tanzania kila mwaka katika utekelezaji wa mkataba huu. Mfano mwaka 2008 Serikali iliyapa makanisa jumla shilingi bilioni 170 (Gazeti la Jambo Leo la Jumapili 20/03/2011) liliandika hivi:

“Mwaka 2009 Serikali iliyapa makanisa shilingi bilioni 45. Mwaka 2010 iliyapa shilingi bilioni 61.9.”

Kwa maana hiyo Serikali kuanzia 2008 hadi 2011 imeyapa makanisa na taasisi zake shilingi billioni 331. Jee Waislam na taasisi zake wamepewa nini?

Pia iweleweke kwamba zaidi ya asilimia 54 ya bajeti ya Wizara ya Afya inakwenda kwenye vituo vya Afya, zahanati, mahospitali na taasisi nyingine za afya za kikristo. Je fedha hizi zinaweza kutoka bila ya Serikali kuwa na mipango ya maendeleo?

(Baada ya sensa ni kuibana serikali ya chama cha nyenyere idai marejesho ya haya mabilioni - HUU NI UFISADI MWINGINE).
 
Kitu ambacho natakakuelewa...kuna faida gani katika kuweka kipengele cha dini kwenye sensa?

Hakuna hasara yoyote ndugu yangu ila serikali yetu siku hizi kwa jambo lolote lile inaogopa hata kivuli chake, badala ya kutatua tatizo kama lilivyo wao hujibanza banza mafichoni na kuishia kuwatuma akina Ramadhani Ighondu wa wawakilishe
 
Hahaha Mkuu Mwanakijiji umenena kweli kweli... Leo wanakataa nini na wao ndio walikuwa mstari wa mbele kumtaka aliyeko madarakani.. Vitabu vitakatifu vinasema tutii mamlaka sasa hawa ndugu zetu wasichoelewa ni nini?? kwani sisi nzi mpaka tusihesabiwa au mbu. Huu ni upuuzi uliovuka mpaka eti hutaki kuhesabiwa na liwalo eti liwalo! Hizi njozi za mchana zitawaponza wengi. Acha mimi nihesabiwa wajukuu zangu wapate kujua na pengine kusoma historia ya nchi yao siku za mbeleni.

We mdada/m mama USIJITOE UFAHAMU - NI MASHEKHE NDO WALIOKUWA WANAHUBIRI KUWA KIKWETE CHAGUO LA MUNGU????? Mlipiga kampeni kubwa sana ya kidini mwaka 2005 kuwa JK ni chaguo la Mungu ili CUF iliyokuwa Chama kikuu cha upinzani ( mlikiita chama cha kiislam) kipindi hiko kisipate kura za Wakristo. Na mkampa JK ushindi wa kishindo...... HUYAJUI HAYA/UMEYASAHAU narudia tena USIJITOE UFAHAM ukajiona smart.
 
Katika kifungu cha 11 cha mkataba huo kinasema:
”Serikali ni lazima itoe nafasi za ajira katika vyuo vyake vya Ualimu (TTC) kwa Wakufunzi wa kikristo kufundisha watu wataofuzu kama Walimu kwa ajili ya shule za Makanisa zilizoanzishwa.”
Je, hii si mipango ya maendeleo kwa kuzingatia dini?

Kutokana na makubaliano hayo baina ya Serikali na kanisa, imelazimika Serikali kuyapa makanisa mabilioni ya fedha za wa-Tanzania kila mwaka katika utekelezaji wa mkataba huu. Mfano mwaka 2008 Serikali iliyapa makanisa jumla shilingi bilioni 170 (Gazeti la Jambo Leo la Jumapili 20/03/2011) liliandika hivi:

“Mwaka 2009 Serikali iliyapa makanisa shilingi bilioni 45. Mwaka 2010 iliyapa shilingi bilioni 61.9.”

Kwa maana hiyo Serikali kuanzia 2008 hadi 2011 imeyapa makanisa na taasisi zake shilingi billioni 331. Jee Waislam na taasisi zake wamepewa nini?

Pia iweleweke kwamba zaidi ya asilimia 54 ya bajeti ya Wizara ya Afya inakwenda kwenye vituo vya Afya, zahanati, mahospitali na taasisi nyingine za afya za kikristo. Je fedha hizi zinaweza kutoka bila ya Serikali kuwa na mipango ya maendeleo?

(Baada ya sensa ni kuibana serikali ya chama cha nyenyere idai marejesho ya haya mabilioni - HUU NI UFISADI MWINGINE).

Hapo inachotakiwa ni kuwasukuma wahusika wa taasisi nyingine nao waandike michanganuo na kuipeleka serkalini na kudai hiyo huduma! Ukinyimwa unayo haki ya kulalamika hata juu ya mapaa ya nyumba, la hujafanya hilo fanya leo, ima kalaga baho na ubozi!
 
Mwanakijiji,

I'm afraid now this "sensa thing" is bordering to insanity and beyond logic...hivi hata huyo ambao watu wa dini hizi wanadai wanamuamini, namaanisha waislamu na wakristo, ana haja ya kujua ni wangapi katika dunia hii wanamuamini?
 
Tanga Kunani? Miaka 14 hajaongezeka hata mtu mmoja dah! labda ni wazuri sana katika kutumia contraceptive pills....Maisha magumu hawataki kuongeza familia zao!!!!

WAISLAM KUTOKUWA NA IMANI NA IDARA YA TAKWIMU YA SENSA ILIYOPO HIVI SASA:

Waislam hawana imani na idara ya Takwimu na tume yake ya Sensa kwa kukaa kimya kwake juu ya takwimu zilizotolewa za bandia kwa lengo la kupotosha ulimwengu kwamba Wakristo nchi hii ni wengi kuliko Waislam ni dalili kwamba idara hii inashiriki kueneza propaganda hizo.

Isitoshe matokeo ya Sensa katika baadhi ya mikoa yenye Waislam wengi, kwamba idadi ya watu ni ndogo na haiongezeki. Mikoa yenye Wakristo wengi idadi ya watu ni kubwa sana.

Mfano mzuri ni katika Sensa iliyofanyika mwaka 1988, mkoa wa Tanga idadi ya wakazi wake ilikuwa 1,500,000 (milioni moja lako tano) na Sensa nyingine ilipofanyika mwaka 2002 idadi ya watu mkoani humo ilibaki kuwa hiyo hiyo yaani 1,500,000. (milioni moja laki tano).

Hii ina maana katika kipindi cha miaka 14 kutoka 1988 hadi 2012 hajaongezeka katika mkoa wa Tanga hata mtu mmoja na Serikali hadi leo haijaeleza sababu za kutoongezeka idadi ya watu katika mkoa huo, ni watu wanakufa sana au hawazaani. Hili ndio limeleta mashaka kwamba takwimu zinachakachuliwa kwa makusudi kwa lengo maalum.
BAK Natumaini hata matokeo ya mwaka huu yanaweza yasiwe na tofauti kubwa!
 
Last edited by a moderator:
Hapo inachotakiwa ni kuwasukuma wahusika wa taasisi nyingine nao waandike michanganuo na kuipeleka serkalini na kudai hiyo huduma! Ukinyimwa unayo haki ya kulalamika hata juu ya mapaa ya nyumba, la hujafanya hilo fanya leo, ima kalaga baho na ubozi!
Ili twende sawa ni lazima michanganuo inayopelekwa na waislam ijumlishwe na bilioni 331 mlizogaina hapo awali. na serikali isiyo na dini ijiandae kugawa mabilioni kwa Wahindu/buddha/wapagani/wasio na dini etc.
 
Fikiria kuwa matokeo ya sensa ambapo maswali yangekuwa si ya kulazimisha kujibu (mandatory) na ikaja kuonesha kuwa waliojibu sensa nzima Waislamu wanaonekana ni wengi je ina maana kuwa Waislamu ni wengi zaidi Tanzania kuliko Wakristu au ni kuwa tu wengi waliojibu swali hilo ni Waislamu? Je ingekuwa vipi kama ingekuwa kinyume chake? Lakini zaidi ni kuwa kwenye kundi ambalo linaamini kuwa kuna mfumo Kristu ambao unakandamiza Waislamu nchini je kuna uwezekano wowote wa sensa kuonesha matokeo ambayo hayaoneshi Waislamu wakiwa wengi? Jawabu ni kuwa tayari wapo viongozi na wanaharakati wa makundi ya Kiislamu ambao wameshawaaminisha wafuasi wao kuwa Waislamu ni wengi nchini na hivyo matokeo ya sensa ambayo yangeonesha kuwa ni kinyume na hili (kwamba wako wachache) yangepokewa kwa hisia ya kuonewa, kudhulumiwa na madai yale yale ya kutamalaki kwa kile kinachoitwa "mfumo Kristo".

Ni kutokana na hili basi swali la dini limekuwa gumu kuwekwa katika sensa ya sasa ya watu na makazi kwa sababu hakuna namna rahisi ya kuweza kuliweka bila kuwa tayari na matokeo yake. Ni hili basi naamini (sina sababu ya kuamini vinginevyo) serikali iliamua kama ilivyoamua huko nyuma kutokuuliza swali hili la dini au kabila au la tofauti nyingine za kidemographia. Binafsi ninaamini ni uamuzi wa kiwoga, wenye makosa na ambao unaonesha udhaifu wa walio madarakani kutowaamini Watanzania kuwa hakuna matokeo yoyote ya sensa ambayo yangeweza kubadili mahusiano yaliyopo sasa kama propaganda za sasa zote hazikuweza kufanya hivyo.
Kwa mawazo yangu tu na kwa kutumia mantiki, kipengele cha dini kingewza kuwepo bila ya kutoa taswira za utata kama zingefafanuliwa vizuri. Kwa utaratibu huo, na kama ulivyopendekeza Mzee Mwanakijiji kuwa kipengele cha dini kingewekwa kuwa cha hiyari, lakini zikawekwadini zote, kubwa na ndogo, pamoja na vipengele vya wasio na dini na wanaokataa kujibu, tungeweza kupata idadi halisi. Lakini takwimu zetu mpaka sasa ziwe za kweli au uongo, zinaonesha kama kwamba TZ ina dini mbili tu, waliobakia wote, wa dini ndogo ndogo na wanaokataa kujibu, huwekwa katika kundi la Wapagani.

Lakini nilichotaka kukisemea hasa ni kuwa, "hata kama Waislamu wana madai yao ya halali," lakini kwa kuwa hawaelezei wazi madai hayo, wengi tunashindwa kujua wanataka nini hasa na kwa ajili gani. Badala yake, wale wenye maarifa wanawashawishi maamuma wao ambao wengi wao ni wale wa "Sheikh kasema" kwa hivyo huwa hawafikiri tena hata kama uwezo wanao, hufuata mkumbo tu. Wakiambiwa 'kubali' wanakubali, wakiambiwa 'kataa' wanakataa kama waliofungwa minyororo ya akili.

Laiti angetokea mmoja tu akauliza, "hivi huduma zinazosombazwa kama vile hospitali, dawa, shule, barabara, umeme, huwa zinainishwa kuwa hizi ni za wa dini fulani na hizi za wa dini nyengine?," bila ya shaka wasingekubali kuburuzwa.

Naomba nileweke tu kuwa ninasema haya kama Muislamu, kwa hivyo kama kuna mashambulizi yoyote yaelekezwe upande huo, kwa mimi kama mimi na sio msemaji wao.
 
Back
Top Bottom