Jaribio la kutaka kuiangusha serikali ya Nyerere 1982/1983

Informer

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2006
Posts
1,606
Reaction score
6,672
Februari 26, 1982 Tanzania ilitikisika baada ya kutokea taarifa kuwa ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATC) imetekwa. Lilikuwa ni tukio la kwanza la aina yake kuwahi kutokea katika nchi hii na kuzua mijadala kote duniani.

=====
KWA UELEWA, SOMA:

1) Jaribio la kutaka kuiangusha serikali ya Nyerere 1982/1983

2) Nini kilipelekea vijana wa Tanzania kuteka ndege ya ATC 1982 Mwanza?

Aidha, soma hii:

2
3
4
5
6
7
Matukio ya utekaji ndege Tanzania:

Matukio ya kutekwa kwa ndege nchini yalianza mwaka 1972 wakati wakimbizi wa Uganda walioukimbia utawala wa Idi Amin, wakisaidiwa na Watanzania, walijaribu kumrejesha Dk Milton Obote madarakani.

Sehemu ya uvamizi huo, kwa mujibu wa jarida la Africa Contemporary Record, ni kuchukua ndege iliyojaa ‘waasi’ ili itue kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe. Ili mpango huo uwezekano, maofisa wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam waliamriwa kufumba macho wakati rubani wa Uganda “akiiba” ndege ya Shirika la Ndege la Afrika Mashariki kutoka uwanjani hapo.

Alhamisi ya Septemba 14, 1972, kwa mujibu wa ukurasa wa 47 wa kitabu cha Terrorism in Africa (Ugaidi barani Afrika), ndege ya Shirika la Afrika Mashariki iliibwa usiku na rubani asiyejulikana kutoka Dar es Salaam.

Baadaye ndege hiyo ilikutwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro ikiwa imepasuka matairi.

Mpango ulikuwa rubani huyo atue Uwanja wa Kilimanjaro kuwabeba waasi hao, lakini cha kushangaza alipokuwa akitua alisahau breki ya magurudumu ya ndege. Kwa sababu hiyo magurudumu hayo yakapasuka na mpango mzima nao ukaishia hapo. Wakati huo baadhi ya Waganda walioukimbia utawala wa Idi Amin walikuwa wakikutana mjini Moshi, Kilimanjaro kupanga mikakati ya kuuangusha utawala wa Amin. Kufikia mwaka 1979 zaidi ya vikundi 25 vya Waganda vilivyokuwa na lengo la kuikomboa nchi hiyo vilikuwa vimeshaundwa na vilikuwa vikikutana Moshi.

Hatimaye vikaibuka na kile kilichokuja kujulikana kama “Roho ya Moshi”. Utekaji wa ndege hiyo ulikuwa ni sehemu ya mikakati yao wakisaidiwa na Tanzania.

Utekaji wa pili ulifanywa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Na, jarida moja liliandika kuwa huenda huo ulikuwa ni utekaji wa kwanza wa kielektroniki kuwahi kutokea duniani.

Utekaji huo wa kielektroniki uliofanywa na JWTZ ulifanyika mwaka 1979 wakati vita ikiendelea kati ya Tanzania na Uganda. Wakati huo, ndege za mizigo za Libya zilikuwa zikifanya safari zake za usiku kumpelekea silaha Idi Amin. Mpango ulibuniwa jeshini kuziteka ndege hizo.

Usiku wa manane, wanajeshi wa JWTZ wakiwa Mwanza, walisubiri hadi walipoona kwenye rada ndege mojawapo ikielekea Entebbe, upande wa Uganda, karibu na Ziwa Victoria.

Waliwasiliana na rubani wa ndege hiyo na kujitambulisha kwake kwamba wao ni waongozaji wa ndege kwenye Uwanja wa Entebbe na kumuonya kuwa uwanja huo unashambuliwa vikali na wanajeshi na kwa hiyo isingefaa atue huko.

Wasiwasi mkubwa ulimpata rubani huyo kiasi kwamba alilazimika kuomba ushauri. Wanajeshi wa Tanzania wakamshauri kuwa uwanja wa ndege ulio karibu zaidi ni ule wa Mwanza na kwamba kwa sasa ni salama zaidi kutua.

Rubani alijaribu kuuliza maswali kadhaa alijibiwa kwa uangalifu. Majibu hayo, na jinsi yalivyotolewa, yalimridhisha rubani huyo. Kwa hiyo akaachana na uamuzi wake wa kwenda kutua Entebbe na akaamua kwenda Mwanza.

Mara baada ya ndege hiyo kutua Mwanza, ikazingirwa na wanajeshi wa Tanzania. Hata hivyo, walishangazwa kubaini kuwa ilikuwa ni ndege ya mizigo ya Shirika la Ubelgiji, Sabena, badala ya ndege ya Libya na iliyobeba silaha. Ndege hiyo ya Ubelgiji ilikuwa safarini kwenda Entebbe kubeba kahawa ili kuipeleka Djibout.

Kwa jinsi hali ilivyokuwa mbaya kutokana na kile kilichofanywa na Tanzania, Rais Julius Nyerere alilazimika kwenda ubalozi wa Ubelgiji kuomba radhi.

Tanzania na Uganda hawakuwa na uhusiano mzuri tangu Jumatatu ya Januari 25, 1971, siku ambayo Jenerali Idi Amin aliipindua Serikali ya Dk Milton Obote. Tangu wakati huo kulikuwa na harakati nyingi kwa upande wa Tanzania zilizokuwa na lengo la kumrejesha Dk Obote madarakani.

Wakati hayo yaliposhindikana, huku uhusiano kati ya Tanzania na Uganda ukizidi kuzorota, mwaka 1978, Rais Julius Nyerere alitangaza vita dhidi ya “Nduli Idi Amin” baada ya majeshi ya Uganda kuvamia Kagera.

Alhamisi ya Novemba 2, 1978, Mwalimu Julius Nyerere alilitangazia Taifa kuhusu “uvamizi wa Idi Amin na uamuzi wa Tanzania wa kumpiga.” Akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa Diamond Jubilee, Mwalimu Nyerere alielezea uamuzi huo wa Serikali.

“Nimewaombeni mkusanyike tena hapa (ili)niwaelezeni jambo ambalo kwa sasa wote mnalijua. Lakini naona si vibaya nikieleza. Nitajaribu kueleza kwa ufupi,” alisema Rais Nyerere.

“Huyu mtu ameivamia nchi yetu. Sasa hiyo ndiyo hali. Tufanye nini! Tunayo kazi moja tu. Watanzania sasa tunayo kazi moja tu—ni kumpiga.”
 
Kwenye siasa na historia ya nchi hii kumewahi kutokea mapinduzi ya kijeshi katika utawala wa awamu ya kwanza(JK NYERERE regime) yaliyojulikana kama TANGANYIKA RIFFLES ..Japo huwezi kukuta jambo hili likizingumzwa sana au kuwekwa katika historia ya nchi naomba kueleweshwa yafuatayo:

1)Nini kilikua chanzo cha mapinduzi haya na lengo lake lilikua ni nini??
2)Mapinduzi yalivyoshindikana wale wahaini walichukuliwa hatua gani??
3)Kwa nini historia ya hii nchi hailizungumzii suala hili kama inavyo vizungumzia vita vya kagera??
4)Nasikia NYERERE na KAWAWA walijificha kigamboni kwenye moja ya nyumba za raia wa kawaida mambo yalivyokua magumu je ni kweli??

Natanguliza shukrani.
 
ninachofahamu na kuchukia ni histori aya uongo ya hawa mashujaa wa jadi akina mkwawa,mirambo, kinjekitile, abushir and the sort.Hao mahaini ni shemu tuu t ahistoria ya nchi inayohitaji kuwekwa katk kumbukumbu na hata ikibidi wahojiwe rasmi hao watu waliobaki na famila zao ili iandikwe historia kabili kwa angle zote.
 

Ni kweli mkuu maana siku moja nlikua IRINGA cha ajabu ni kuwa historia ya mtemi Mkwawa tunayoisoma kwenye vitabu inaonekana ni ya kupikwa sana si kile ambacho wenyeji wanakifahamu.

Mkwawa anaonekana kuwa alikuwa ni kiongozi aliyetumia diplomasia sana na uchawi sana kutaka kupata suluhu na wajerumani lakini tunaambiwa alikua shujaa aliyepambana na wajerumani mpaka dakika ya mwisho wakati ukweli ni kuwa aliwakimbia wajerumani kwa kutaka kujiokoa baada ya diplomasia na utabiri wa mganga wake wa kienyeji kuwa atawashinda wajerumani kushindwa.

Ninachojiuliza hapa je ni kweli kuwa historia ya nchi hii nyingi ni ya kupika??
kwa nini matukio mazito kama haya ya mapinduzi ya kijeshi hayatajwi katika historia ya hii nchi?
 
Japo historia haisemi wazi juu ya mambo mengi sana Tanganyika na Tanzania ya leo, lakini Mwalimu Nyerere tangu awe kiongozi wa nchi hii amenusurika mapinduzi MATATU,

Moja ni la mwaka 1964, lapili ni la mwaka 1970 na la mwisho ni la mwaka 1980 (Sina uhakika sawa na hiyo miaka)

Jaribio la kwanza ndilo lilipelekea kuundwa kwa JWTZ na lilizimwa kwamsaada wa Malkia wa Uingereza aliyetuma makomandoo maalumu na wakafanikiwa, Jaribio la pili ndilo lililopelekea kuundwa kwa Usalama wa Taifa na kikosi maalumu cha ulinzi wa Rais,

na jaribio la mwisho ndio lilipelekea kubadili sera ya usalama wa Taifa kwa kuwapandikiza kila kwenye sekta na kuwa kila mtu ni mlinzi wa nchi hii (usalama)

Sikumbuki vema lakwanza kama liliongozwa na nani lakini Kambona ndie alimficha Mwalimu, lapili sikumbuki vema, lakini la mwisho liliongozwa na baadhi ya wanajeshi wa kikosi cha Anga cha Ukonga Banana,

Na mipango yao iliharibikia palepale Banana baa baada ya mmoja wao kulewa na kuanza kuongea hovyo hasa akisema yeye anataka cheo cha uwaziri mkuu!

Enzi hizo 1980+ mmoja wa makamanda wa usalama wa taifa aliyeongoza kuwadhibiti waasi hao ni Mabere Marandu,

Na alifanikiwa kuongoza oparesheni za kumsaka na kumuua mmoja wa makomandoo ambae alikuwa ameandaliwa rasmi kumuua Nyerere,

Mapambano yalikuwa ni makubwa kutoka airport hadi kinondoni ulipo ubalozi wa Marekani sasa ndipo walipofanikiwa kumuua!

Jambo la kuwashangaza waasi wale (wanajeshi) wote Mwalimu aliwaita ikulu,

akamwambia kiongozi wa mapinduzi yale (simkumbuki) kuwa

"Shika bunduki uniue wewe mwenyewe kwamkono wako ili uwe rais wa nchi hii"

jamaa aliomba radhi huku akitambaa kisha mwalimu akasema

"nimewasamehe wote"

na aliwapa vyeo na kazi, wengi walikwenda kuwa mabalozi wa Tz nchi za nje!

Sisi hapa tunasema kama porojo tu, lakini yapo mengi sana nyuma ya pazia!

Watawala wanahisi kuyataja ni kama kuharibu sifa ya Tanzania na wengine wanaona kama itaharibu sifa ya Mwalimu.

Mimi binafsi nafikiri kama yatasemwa hadharani yataongeza sifa ya Mwalimu Nyerere na utawala wa ccm ya kale!

Atakuwa ni kiongozi pekee barani afrika na duniani aliyenusurika majaribio matatu ya uasi,

Atakuwa ni kiongozi wa kwanza duniani kuwasamehe waasi kwa mda huohuo wa uasi (baada ya kuwakamata) na kuwapa kazi nyingine za kitaifa

Atakuwa ni kiongozi pekee duniani aliye ng'atuka kwa amani na kwenda kuishi kijiji tena bila hata ulinzi, akitembelea land rover ya shamba miaka mitano tu baada ya jaribio kali la mapinduzi ya Banana Ukonga!

Hizo zote zilikuwa ni sifa zake ambazo watawala wa leo kwa makusudi ama kwakujua au kutojua wamefifisha nyota ya mwana wa Afrika mbele ya uso wa mataifa!

Na kwakuwafahamisha tu ni kuwa mmoja ya wanajeshi hao walioasi ni Meja Gen Hans Popi yule mwenye Sams Super Store pale Mbezi Makonde!

Kwakifupi hayo ndiyo ninayafahamu,
 
wengi wao hao wana anga walikuwa ni makaka wa familia moja iliyokuwa exposed nje na kupat amafunzo haba kipindi hicho ya urubani,mmoja wapo walikuwa rubani wa Mzee mkubwa.

Tetesi aliponea bahati kwa vile naye alikuwa safairini na mzee huku akijidaia kuwa mtiifu sana,ila kaka zake walinyea lupango kwa siku kadhaa,Leaders Club pia ilikuwa ni sehemu mojawapo ya kukutana sijui ndio iliwafanya wagombee uongezi sana.

Siku walikuwa wakilewa walikuwa ndio siku ya mwisho ya kupanda kwa hivyo walikuwa wakifurahia kuwa kesho yake wataitwa majina mapya.

Tetesi pia ni kwamba wake zao nao walikuwa mashushu na laiyebahatika ni ya huyo mpenda sifa na uongozi alipopasua kila alipokuwa akilewa.
 
Yericko Nyerere,

asante sana mkuu kwa kinifungua macho... Huyu MABERE MARANDO aliyeendesha hii operation ndiye huyu huyu wa CHEDEMA?? au majina yamefanana?? Kuna tetesi pia kuwa mwalimu mambo yalipoenda kombo kutokana na kikosi cha anga kumgeuka aliamua kuomba msaada kwa majeshi ya UINGEREZA na within a minitu kuna midege ilikuja na kusafisha wasaliti wote msituni na hakuna hata mabaki yaliyopatikana...je ni keli au ni stori za vijiweni??
 
Imeandikwa sana na inasomwa sana tu. Na kulikuwa na thread hapahapa jamvini si siku nyingi iliyoeleza kwa kirefu sana. Search!
Ilikuwa ni mutiny na si mapinduzi.

Lugha yoyote itakayotumika bado usalama wataifa unahiataji kuwa na mpango wa de classify baadhi ya documents kadiri miaka inavyokwenda ili kueleimisha watu.Kwani baadhi yao wanakuja kuwa wanasiasa,wengine wanakwenda usalama ,jeshini etc sasa wanakwenda wakiwa mbumbuku sana hawana fact za karibu za kuwasaidia kufany aquick analysis ktk shughuli za kila siku au wanapokutana na watu wenye historia fulani na nchi yetu.

Pia hao raia watakuwa kuwa preamble ktk kustage espionage platform kupitia raia.Enzi ya mwalimu tuliweza,watanzania walikuwa wambea sana,hakuingia mgeni bila kipira kuingia mtaani na king`ora kubwa siku hiyo hiyo na huyo mtu kupotea.Nyamisi yale meldan rover+Peugeot 404....israeli wameweza sisi inatushinda nini?

Nilitegemea baad aya mwalimu kipindi ch amwinyi kingewapeleka watanzania mbalia zaidi kuacha kuwa wambea kwa kila mtu ila kupitia channels zilizoweka na mfumo wa nchi.

Sasa hivi pembe za tembe zinaondoka wageni wanapewa urais haraka kuliko hata mama anavyoingia labour na kutoak ana mtoto.
 

Ndio ni Mabere Marandu huyu wa Chadema,

Nigeria walisaidia sana kuja kuleta amani, tulitawaliwa karibu mwaka mmoja!

Wengi wa waasi walisamehewa, lakini makomando na baadhi waliuawa na wengine kupelekwa Gwantanamo ya Afrika, hicho ni kisiwa kidogo kinachomilikiwa na Tanzania kipo kata ya Zanzibar na Tanganyika,

Sina uhakika kama badoo kinatumika ama kinatumika kwa siri zaidi!
 
Kambona ndiye aliyemuokoa Nyerere kwa kumficha kwenye mapinduzi ya 1964.

Mtafiti wa masuala haya anaitwa Nestor Luanda, machapisho yake haya hapa:

nestor luanda mutiny - Google Search

Companero,
Si kweli kwamba Oscar ndiye aliyemwokoa na kumficha Mwalimu katika mapinduzi ya 1964. Huyu mtafiti amekosea. Nadhani Kawawa alikuwa na jukumu kubwa zaidi kumshawishi Mwalimu kujificha kuliko Kambona. Kambona hakujua alipofichwa Mwalimu.
 
Companero,
Si kweli kwamba Oscar ndiye aliyemwokoa na kumficha Mwalimu katika mapinduzi ya 1964. Huyu mtafiti amekosea. Nadhani Kawawa alikuwa na jukumu kubwa zaidi kumshawishi Mwalimu kujificha kuliko Kambona. Kambona hakujua alipofichwa Mwalimu.

Kuasi kule kwa Wanajeshi Januari/20/1964 (Tanganyika Rifles) wala sio jambo la zamani sana kiasi cha kusema kwamba Historia ile imetupwa na hakuna anayesema ukweli,nilikuwa nahisi Viongozi kama Mwalimu,kawawa na Kambona wangeyaweka katika maandishi mambo yale muhimu ktk Historia ya Nchi yetu kabla hawajatutoka.Hakuna mahali mambo haya yameandikwa na ndio maana Vijana wanaotaka kujua historia ya Nchi yao wanakuja na hizi hear/say

Askari wale wa Tanganyika Rifles waliasi...Miongoni mwa mambo waliyokuwa wanadai ni hali nzuri ya maisha ya askari mtanganyika,mshahara ulikuwa mdogo,hawakupandishwa vyeo na hakukuwa na Watanganyika katika vyeo vya juu ndani ya Jeshi lile.Askari waliasi na kuingia mjini,na wengine walikwenda kwenye Makazi ya Maafisa wa kiingereza (Raia) na kuwashikilia.Waziri wa Ulinzi wakati huo alikuwa Oscar Kambona....Mwalimu na Mzee Kawawa kwa usalama wao walitoroshwa na kwenda kujificha,inasemekana Maficho yao yalikuwa Kigamboni.Waziri wa Ulinzi (Kambona) alijaribu kupita ktk Barracks na kuwaomba askari watulie bila mafanikio.

Hali ile iliendelea kuwa mbaya,na Mwalimu kwa ushauri wa Kambona na Kawawa akaomba msaada kwa Uingereza ili waje waokoe hali ile ambayo ilikuwa inaelekea kuwa mbaya,kufuatia kuasi kwa Askari wetu,askari wa Kenya na Uganda nao waliasi kwa sababu sawa kabisa na za UASI wa Tanganyika Rifles.Malkia alituma kikosi maalumu cha Askari wa Uingereza ambao walikuwepo ktk ghuba ya Aden,Askari hao walikuja na Meli kubwa ya kivita HMS Centaur ambayo ilikuwa na Makomandoo (45 RM),askari na helikopta.Walifanikiwa kutuliza maasi yale,na Mwalimu na Kawawa wakatoka mafichoni na kuonekana hadharani wakiwa na Waziri wa Ulinzi,ambaye alifanya kazi kubwa bila mafanikio kuwaomba askari(Waliokuwa wananuheshimu sana) waache uasi na madai yao yatafanyiwa kazi.Ukitaka kupata mambo mengi kuhusu maasi yale pitia kitabu "Dar Mutiny Of 1964" by Christopher MacRae
 
Jamani kama hamjui historia ya nchi yenu msiitengeneze..

Hivi historia hutengenezwa au hujitengeneza?

Mheshimiwa kama unakijua kitu na kipo akilini mwako huku ukizima wanaotaka kujua kwakuwaita hawajii huo ni uhaini wa fikra huru!

Unadiriki kuzorotesha machipuzi huru bila kusadifu kilicho chema cha kichwani mwako!
 
Companero,
Si kweli kwamba Oscar ndiye aliyemwokoa na kumficha Mwalimu katika mapinduzi ya 1964. Huyu mtafiti amekosea. Nadhani Kawawa alikuwa na jukumu kubwa zaidi kumshawishi Mwalimu kujificha kuliko Kambona. Kambona hakujua alipofichwa Mwalimu.

Mkuu give credit where it is due, Kambona ndiye aliyemsaidia Nyerere. Na ndio maana tunasisitiza kuwa hawa walikuwa washikaji hadi Nyerere akawa ndiye aliyemtoa bibi harusi wa Kambona siku ya harusi yake. Picha zipo zimejaa tele kwenye gazeti la Drum mlilolifungia!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…