Companero
Platinum Member
- Jul 12, 2008
- 5,606
- 1,711
Wabishi na Wanapropaganda hebu someni huu ushuhuda wa askari aliyekuwepo kwenye hilo seke seke la 1964: allAfrica.com: Tanzania: Col Kashmiri Puts 1964 Army Mutiny in Perspective (Page 1 of 3)
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hivi historia hutengenezwa au hujitengeneza?
Mheshimiwa kama unakijua kitu na kipo akilini mwako huku ukizima wanaotaka kujua kwakuwaita hawajii huo ni uhaini wa fikra huru!
Unadiriki kuzorotesha machipuzi huru bila kusadifu kilicho chema cha kichwani mwako!
Companero,Mkuu give credit where it is due, Kambona ndiye aliyemsaidia Nyerere. Na ndio maana tunasisitiza kuwa hawa walikuwa washikaji hadi Nyerere akawa ndiye aliyemtoa bibi harusi wa Kambona siku ya harusi yake. Picha zipo zimejaa tele kwenye gazeti la Drum mlilolifungia!
Companero.. kuna baadhi ya vitu ambavyo vimekuwa ni sehemu ya 'myths' za Kambona. Kambona ndiye alikuwa Waziri wa Ulinzi wakati maasi yanatokea. Lilikuwa jukumu la nani kuwatuliwa maaskari au kukutana nao? Leo tumeona madaktari wanagoma nani anaenda - Waziri wa Afya; tumeona mgogoro wa raia na polisi nani anaenda - Waziri wa Mambo ya Ndani. Maasi yale (mutiny) yalikuwa ni maasi yaliyohusiana sana na suala la ajira na hali za kazi mambo ambayo yalikuwa ndani ya waziri wa ulinzi - Oscar Kambona.
Lakini kinyume na watu wanavyosema Kambona asingeweza kuchukua urais wakati Nyerere yuko mafichoni. Hakuwa na uwezo wa kuwa Rais na wala hakuwa amejenga ile 'political clout' dhidi ya popular figure like Nyerere. Watu wengi wanachosahau ni kuwa Nyerere alijitokeza siku mbili baadaye na kutembea katikati ya jiji la Dar kukagua hali ilivyokuwa na kuonesha kuwa alikuwa na uwezo dhidi ya jeshi - alilivunja.
Kikwete ajaribu kuvunja sungusungu leo...
Companero,
Nakubali Nyerere na Kambona walikuwa marafiki wa karibu. Hata alipotembelea Uingereza wakati Kambona ni mwanafunzi Mwalimu alilala chumba cha Kambona. Pia nakubalia Mwalimu alimtoa bibi harusi wakati wa ndoa ya Kambona, lakini sikubali kuwa Kambona alimficha Mwalimu. Ninachojua ni kwamba Kambona hakujua Mwalimu amejificha wapi na only person aliyekuwa na habari alikuwa ni Kawawa.


Hapana. Kawawa hakujificha. Lakini aliadimika. Paul Bomani alipigwa makofi na wanajeshi usoni.Kawawa yeye hakujificha?
Lakini pia kuna myths dhidi ya Kambona, aisie pitia tena makala na mapicha ya Drum magazine ya enzi hizo (kumbuka Nyerere alikuja kulifungia Tanzania) - Kambona was way too popular, kuna sehemu nilizipiga picha hizo picha ngoja nizitafute!
Historia ya Kambona bado haijaandikwa. Bintiye naona bado anasuasua. Watanzania tunazembea. Mzungu huyu kaivalia njuga:
unajua kitu cha kwanza ambacho academics wetu wangepigania ni kufunguliwa kwa classified materials ambazo zilikuwa zinazuiwa hadi ipite miaka 30. Karibu nyaraka zote za kati ya 1961 hadi sasa zimeshapita huo muda na zinatakiwa kisheria ziwekwe huru kwa wasomi kupitia. Nyaraka zote kuhusiana na uhuru, mapinduzi, muungano, n.k .. vinatakiwa viwe kwenye public domain sasa. But.. I said our academics.. sijui kama bado wapo...
Hili suala la kutunzwa kwa classified documents mpaka miaka 30 ipite ni la kisheria au ni watawala wameamua kuweka ili kulinda mambo yao???unajua kitu cha kwanza ambacho academics wetu wangepigania ni kufunguliwa kwa classified materials ambazo zilikuwa zinazuiwa hadi ipite miaka 30. Karibu nyaraka zote za kati ya 1961 hadi sasa zimeshapita huo muda na zinatakiwa kisheria ziwekwe huru kwa wasomi kupitia. Nyaraka zote kuhusiana na uhuru, mapinduzi, muungano, n.k .. vinatakiwa viwe kwenye public domain sasa. But.. I said our academics.. sijui kama bado wapo...
Kwa hiyo mkuu Lengo la ule uasi haikua kuchukua nafasi ya urais wa mwalimu ila ilikua kma kamgomo fulani kakudai maslahi mazuri pamoja na vyeo???Saf mkuu, hapa sasa umefunguka vema na kutanua wigo wa mjadala huru!