Jaribio la kutaka kuiangusha serikali ya Nyerere 1982/1983

Jaribio la kutaka kuiangusha serikali ya Nyerere 1982/1983

Hivi historia hutengenezwa au hujitengeneza?

Mheshimiwa kama unakijua kitu na kipo akilini mwako huku ukizima wanaotaka kujua kwakuwaita hawajii huo ni uhaini wa fikra huru!

Unadiriki kuzorotesha machipuzi huru bila kusadifu kilicho chema cha kichwani mwako!

Mimi nahisi kuna mtu ame hack Id ya Mzee Mwanakijiji maana michango inayotoka kwa huyu mzee haindani na haiba yake ninayoijua
 
Last edited by a moderator:
Kwa hiyo mkuu Lengo la ule uasi haikua kuchukua nafasi ya urais wa mwalimu ila ilikua kma kamgomo fulani kakudai maslahi mazuri pamoja na vyeo???
Kwa nini sasa wa nigeria waje kulinda amani kwa almost one year kama hali haikua tete kihivyo mpaka mwalimu aliweza kuzunguka mitaani dar es salaam kabla ya officially kutokea publicly??

Hapa wengi wanajadili uasi wa miaka ya 1964 lakini maada inazungumzia jaribio la 1980+

Ukweli usiosemwa nikuwa majaribio yote yalikuwa na lengo la kumtoa Nyerere madarakani,

Tena kuna makomandoo walifanikiwa kupenya mpaka ikulu lakini hawakumkuta mwalimu, Nyerere alishayeyuka mapema kupitia handaki maalumu lilipo ikulu na kutokea baharini kule feri!
 
Did you know Hans Poppe spent more than 10 years behind bars? Nafikiri aliachiwa baada ya kuanza kwa vyama vingi. Hata hivyo ni mmoja ya watu wenye uwezo mkubwa kiakili na kwa jinsi anavyopeleka mambo, he was not a soldier by accident! ndio maana ameweza kujibadili na kuwa mfanyabiashara mkubwa kwa kipindi kifupi baada ya kutoka lupango.
 
ni kweli mkuu unachokisema kuna mtu kanipa tahadhari kuwa uzi huu unaweza kufungiwa ...cha ajabu jina la uzi limebadilishwa ghafla na kuwa jaribio la 1980 na sio la 1964...inavyoonekana kuna kitu kikubwa sana hapa kinafichwa
 
Nchi za Tanzania, Kenya na Uganda zote tawala zao za kwanza baada ya Uhuru zilinusurika kwa majaribio ya mapinduzi, lakini historia zimefichwa bila sababu maalumu!
 
Companero.. kuna baadhi ya vitu ambavyo vimekuwa ni sehemu ya 'myths' za Kambona. Kambona ndiye alikuwa Waziri wa Ulinzi wakati maasi yanatokea. Lilikuwa jukumu la nani kuwatuliwa maaskari au kukutana nao? Leo tumeona madaktari wanagoma nani anaenda - Waziri wa Afya; tumeona mgogoro wa raia na polisi nani anaenda - Waziri wa Mambo ya Ndani. Maasi yale (mutiny) yalikuwa ni maasi yaliyohusiana sana na suala la ajira na hali za kazi mambo ambayo yalikuwa ndani ya waziri wa ulinzi - Oscar Kambona.

Lakini kinyume na watu wanavyosema Kambona asingeweza kuchukua urais wakati Nyerere yuko mafichoni. Hakuwa na uwezo wa kuwa Rais na wala hakuwa amejenga ile 'political clout' dhidi ya popular figure like Nyerere. Watu wengi wanachosahau ni kuwa Nyerere alijitokeza siku mbili baadaye na kutembea katikati ya jiji la Dar kukagua hali ilivyokuwa na kuonesha kuwa alikuwa na uwezo dhidi ya jeshi - alilivunja.

Kikwete ajaribu kuvunja sungusungu leo...

Ati nini?
 
Did you know Hans Poppe spent more than 10 years behind bars? Nafikiri aliachiwa baada ya kuanza kwa vyama vingi. Hata hivyo ni mmoja ya watu wenye uwezo mkubwa kiakili na kwa jinsi anavyopeleka mambo, he was not a soldier by accident! ndio maana ameweza kujibadili na kuwa mfanyabiashara mkubwa kwa kipindi kifupi baada ya kutoka lupango.

Namsifu sana bwana Hans Poppe, amerejea kutoka kifungoni na kuwa mmoja ya raia wema na wachapakazi sana,

Hans Poppe ukikaa nae kwamda mfupi utamtambua kuwa ana uwezo mkubwa kiakili na nimcheshi mwenye kupenda kusimulia yaliyotokea enzi hizo huku akikuasa kufanya kazi kwa uadilifu wa mfano wa Nyerere!

Anamtaja Mwalimu Nyerere kama alama ya mfano kwake na anamshukuru sana kwa kumuokoa na kifo!
 
ni kweli mkuu unachokisema kuna mtu kanipa tahadhari kuwa uzi huu unaweza kufungiwa ...cha ajabu jina la uzi limebadilishwa ghafla na kuwa jaribio la 1980 na sio la 1964...inavyoonekana kuna kitu kikubwa sana hapa kinafichwa

Sisi hapa tunasema kama porojo tu, lakini yapo mengi sana nyuma ya pazia!

Watawala wanahisi kuyataja ni kama kuharibu sifa ya Tanzania na wengine wanaona kama itaharibu sifa ya Mwalimu.

Mimi binafsi nafikiri kama yatasemwa hadharani yataongeza sifa ya Mwalimu Nyerere na utawala wa ccm ya kale!

Atakuwa ni kiongozi pekee barani afrika na duniani aliyenusurika majaribio matatu ya uasi,

Atakuwa ni kiongozi wa kwanza duniani kuwasamehe waasi kwa mda huohuo wa uasi (baada ya kuwakamata) na kuwapa kazi nyingine za kitaifa

Atakuwa ni kiongozi pekee duniani aliye ng'atuka kwa amani na kwenda kuishi kijiji tena bila hata ulinzi, akitembelea land rover ya shamba miaka mitano tu baada ya jaribio kali la mapinduzi ya Banana Ukonga!

Hizo zote zilikuwa ni sifa zake ambazo watawala wa leo kwa makusudi ama kwakujua au kutojua wamefifisha nyota ya mwana wa Afrika mbele ya uso wa mataifa!
 
Kwa hiyo mkuu Lengo la ule uasi haikua kuchukua nafasi ya urais wa mwalimu ila ilikua kma kamgomo fulani kakudai maslahi mazuri pamoja na vyeo???
Kwa nini sasa wa nigeria waje kulinda amani kwa almost one year kama hali haikua tete kihivyo mpaka mwalimu aliweza kuzunguka mitaani dar es salaam kabla ya officially kutokea publicly??
Sababu kubwa ya Nigeria kuja kulinda amani ni kwamba Nyerere aliamua kuvunja jeshi la KAR na kujenga JWT. Ilikuwa ni aibu kwake kwa Uingereza kuzima yale maasi. Waingereza walitaka kubaki waongoze jeshi letu Nyerere akakataa akawaita Wanigeria waje kusaidia kujenga na kutoa mafunzo kwa jeshi jipya la wananchi wa Tanzania.
 
Yericko Nyerere, unaweza kututajia baadhi ya waasi waliosamehewa na kupewa nyadhifa nyingine za kitaifa? I know for sure Captain Hans Poppe was locked behind the bars with some of friends kile Eugene Maganga. Waliopewa nyadhifa ni nani kwa interest ya kuelewa vizuri historia.
 
Ngoja niangalie mafaili yangu hapa, lakini kwa haraka ni kuwa mmoja alikwenda kuwa balozi wa Tanzania kule Nigeria, mwingine akaenda Uganda nk!
 
Hii kitu nzuri sana, Mkuu Yericko Nyerere unaonekana unajua mengi sana

Kwanini haya hayopo kwenye historia ya nchi yetu?
 
Hili suala la kutunzwa kwa classified documents mpaka miaka 30 ipite ni la kisheria au ni watawala wameamua kuweka ili kulinda mambo yao???
Je nchi nyingine zina utaratibu huu au ni hapa hapa BONGO tuu

Hili ni suala la kisheria na nchi zote duniani I presume zinazo. Nafahamu Marekani kwa mfano wanayo.. ndio maana nyaraka zao za ujasusi wa miaka ya 1960 sasa hivi ziko hadharani kwani muda wake wa kuwa classified umepita.
 
Kwa hiyo mkuu Lengo la ule uasi haikua kuchukua nafasi ya urais wa mwalimu ila ilikua kma kamgomo fulani kakudai maslahi mazuri pamoja na vyeo???
Kwa nini sasa wa nigeria waje kulinda amani kwa almost one year kama hali haikua tete kihivyo mpaka mwalimu aliweza kuzunguka mitaani dar es salaam kabla ya officially kutokea publicly??

Nigeria hawakuja kulinda amani; walikuwa kureplace jeshi lililovunjwa. NI lazima ujue kuwa kinachoitwa "Tanganyika Rifles" ndilo ilikuwa mrithi wa jeshi la Muingereza "Royal African Rifles" lililojulikana pia kama "King's African Rifle". Tulipopata uhuru jeshi lile la kikoloni ndilo likawaja jeshi la Tanganyika huru. Maasi ya 1964 yalionesha tu tatizo lililokuwepo la kurithi jeshi la kikoloni. Maafisa wake wa juu bado wengi (kama siyo wote) walikuwa ni Waingereza! Hivyo, baada ya maasi Nyerere alilivunja jeshi na kuanza kuliunda upya kufuatana na mahitaji yetu na kulijenga kuwa one of the most well regulated, highly politicized military. Upande mwingine Polisi haikuvunjwa na matatizo yake tunayaona hadi leo hii kwani tumerithi jeshi la kikoloni na lenye fikra za kikoloni bado.
 
Hili ni suala la kisheria na nchi zote duniani I presume zinazo. Nafahamu Marekani kwa mfano wanayo.. ndio maana nyaraka zao za ujasusi wa miaka ya 1960 sasa hivi ziko hadharani kwani muda wake wa kuwa classified umepita.

Hata huko ambapo sheria hiyo ipo, sio kila nyaraka automatically inaikuwa chini ya sheria hiyo.

Ndio maana hadi sasa kuna nyaraka za wakati wa JFK hazijawekwa wazi.
 
Mkuu binafsi nakushukuru sana kwa maelezo uliyoyatoa hapa,nimejifunza mengi sana
 
Hata huko ambapo sheria hiyo ipo, sio kila nyaraka automatically inaikuwa chini ya sheria hiyo.

Ndio maana hadi sasa kuna nyaraka za wakati wa JFK hazijawekwa wazi.

Ni kweli ila nadhani kuna tatizo kidogo kwenye usimamiaji wa sheria hii!
 
Back
Top Bottom