Jaribio la kutaka kuiangusha serikali ya Nyerere 1982/1983

Kuna s
Kuna somo linaitwa HIstoriography ikiwa na maana ya history of history writing. Ilivo ni kuwa uandishi wa historia hauwezi kuwa objective ikiwa utaachiwa kundi fulani. mathalani kundi la watawala. kwa vyovyote hao watajipendelea na kutakuwa na biase tele. kwa hivi inapaswa tuwajue hawa waandishi na mfumo uliowazaa. in fact wanazuoni na watafiti wanaakiwa wawe huru katika kuandika historia ya nchi
 
Nakuelewaga saana Yeriko
 
Duuuh!!!!! Yericko nakuheshimu sana lakini kwa hili umechapia sana kupotosha kwa kiwango kikubwa, upo karibu na kamanda Mabere Marando, hebu tafuta muda ufanye nae mahojiano utapata kile ulichotaka kuwapa wana jf ni jambo zuri kuandika historia lakini isiwe ya kuchapia kama ilivyo ya kwako, na wakati kumbuka huyo unaesema Major General Hans Pope hakuwahi kuwa na cheo hicho mpaka wakati wa jaribio la mapinduzi alikua na cheo cha Captain,
 

Ile bar yao ya kujinafasi sijui bado ipo!!!?????
 
Salamu kwenu wanabodi!

leo nataka niwasogezee kisa hiki cha kesi ya uhaini ya miaka ya 1980.ilikuwa ni kesi ya kihistoria na kielelezo tosha cha uhuru wa mahakama.kwanini nimeleta kwenu leo? ni kwamba kisa chote kilionesha ustadi wa wahusika kila mhusika kwa upande wake.Nitaanza upande mmoja baada ya mwingine na mwisho nitatoa majumuisho.

wahusika wa mipango ya kumpindua mwalimu nNyerere kwa upande wao ilionesha walijipanga vizuri na kwa mtazamo wao walikuwa na uhakika kufanikiwa kutekeleza azima yao.Lakini kwanini walishindwa?Ni kwasababu ya ustadi na mbinu za hali ya juu ya utendaji wa usalama wa Taifa.walimuonesha Nyerere kilele cha ustadi wao.

kamatakama ya wote walio panga kutekeleza uhalifu ule ilikuwa fantastic, kama senema vile lakini ilikuwa ni tukio la kweli.Mmoja baada ya mwingine alitiwa mbaroni na hatimaye kufikishwa mbele ya sheria.

Kilicho nivutia mimi ni jinsi kesi yenyewe ilivyo endeshwa kwa ustadi mkubwa kwa Lugha ya kiingereza, wale mawakili wa pande zote walipiga kiingereza kizuri hatari utadhani walifanya majaribio kabla ya kufika mbele ya jaji.Kwangu mimi nilifurahi sana na nikajivunia elimu bora waliyo kuwa nayo vijana wetu wakati ule. Maswahili mtu anahojiwa lakini jibu litakalo toka nalo lilikuwa fantastic !usinge bashiri upande gani ungeibuka mshindi.

Hayo yalikuwa ya zamani, na watuhumiwa baada ya kesi kuendeshwa muda mrefu walitiwa hatiani kwa ushahidi usio na mashaka hata kidogo.

Baada ya kesi ile , Mwandishi wa habari mmoja alisema ukiacha unyeti wa kesi yenyewe, hakika Nchi ina vijana walio pikwa wakapikika achilia mbali kile kiingereza mujaarabu lakini ujuzi walio uonesha ulitoa matumaini makubwa kuwa huko tuendako tutatisha sana na wataalamu wetu.

Najiuliza nini kimekwenda kombo siku hizi vijana hawa muda kuongea kiswahili sanifu seuzi kiingereza.tatizo limetokea wapi? Kuna rafiki yangu Hakimu mfawidhi mstaafu alisema ukitaka ucheke mpaka uzimie mpe kijana aliye hitimu chuo miaka ya hivi karibumu hukumu ya kesi kwa kiingereza.ukiweza kuielewa alikuwa anamaanisha nini utakuwa na bahati sana.Ni mmoja kati ya watano. Sijui fani zingine hali ikoje? Siyo tu lugha bali na maarifa yenyewe.
 
Mkuu unaweza kutukumbusha hao mawakili walikuwa wanaitwa kina nani majina yao maana umeturudisha mbali kiduchu.
 
Wakati wingine terminologies za fani husika huwa ni kikwwzo kwenye kuelewa... mfano ukisema...File... Wa Engineering atajuwa hiyo mi tupa na wa secretarial kozi atajuwa hilo ji folder....
 
Wakati wingine terminologies za fani husika huwa ni kikwwzo kwenye kuelewa... mfano ukisema...File... Wa Engineering atajuwa hiyo mi tupa na wa secretarial kozi atajuwa hilo ji folder....
mmh hapo unataka kunichekesha tu! siku hizi kiswahili watu watu hawawezi kukiongea kwa ufasaha.fuatilia utaona mtu msomi tu anasema husiniambie, husije, habali, bizaa, inshu yaani ni shida tupu.watangazaji wengi wa radio ni majanga wako half cooked.
 
Nachingia kidogo nawakumbuka alikuwepo Murtaza Lakha, Issa shirvji
Kwa kweli Huyo Murtaza Lakha hata mie alikuwa ana nikosha kwa umahiri wake. Na bahati nzuri ndiye alikuwa kiongozi wa wale mawakili wa upande wa utetezi. Baada ya Keisha kwa kesi ile habari zinasema alihwmishia shughuli zake Uingereza.
Ule ulikuwa mfano dhahiri wa mawakili bora, anaweza kutumia muda wa kutosha kufanya research ya kesi yake na kuipigania bila kuchoka.
Kwa hawa waendesha mashtaka na mawakili wa serikali wa aina hii tuliyonao sasa hivi ingekuwa kesi nyingi hata za kweli wangepoteza
 
al
ponesha ustadi wa hali ya juu sana.
 
Kwenye hiyo kamatakamata ya watuhumiwa komondoo mmoja wa Jwtz aliuwawa na makomandoo wenzake wa Jwtz wakati wakitaka kumkamata, nakumbuka pia kuna kitabu kilitolewa kinachoelezea jaribio hilo la mapindunzi ambacho baadaye kilikuja kupigwa marufuku, mimi nilikuwa nacho ila sikumbuki nilikificha wapi
 
Hii stori mbona ina imperfection nyingi sana ,kama akina nani walishitakiwa?ilikuaje?kesi hukumu yake ilitolowaje and proceedings za kesi zilikuaje
 
Komando kapten Tamim hakuuwawa na makomandoo wenzake bali na maafisa usalama baada ya zoezi la kumkamata mchana kweupe barabarani kuonekana linaelekea kushindwa na jamaa anaweza kutoweka
 

Kama kumbukumbu zangu ziko sahihi yule wakili mwenye asili ya Asia, LAKHA, alikuwa wakili wa utetezi...sina hakika sana, ila yule wakili kwa hakika alikuwa ni noma. Nasikia alikwenda Canada, hivi jamani ni nani ana habari za yule wakili?
 
Komando kapten Tamim hakuuwawa na makomandoo wenzake bali na maafisa usalama baada ya zoezi la kumkamata mchana kweupe barabarani kuonekana linaelekea kushindwa na jamaa anaweza kutoweka

Tamim, nadhani aliuawa pale KINONDONI, au siyo?
 
mmh hapo unataka kunichekesha tu! siku hizi kiswahili watu watu hawawezi kukiongea kwa ufasaha.fuatilia utaona mtu msomi tu anasema husiniambie, husije, habali, bizaa, inshu yaani ni shida tupu.watangazaji wengi wa radio ni majanga wako half cooked.

Nimecheka sana...Mwingine anasema 'gharama za masomo' kuwa ni 'bei za masomo'; wengine 'suala' kwa maana ya 'issue' wanasema 'swala'; 'afadhali' wanasema 'afadhari' au 'hafadhali'. 'kwenda' wanasema 'kwendaga'
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…