mzamifu
JF-Expert Member
- Mar 10, 2010
- 6,400
- 3,853
Kuna s
Kuna somo linaitwa HIstoriography ikiwa na maana ya history of history writing. Ilivo ni kuwa uandishi wa historia hauwezi kuwa objective ikiwa utaachiwa kundi fulani. mathalani kundi la watawala. kwa vyovyote hao watajipendelea na kutakuwa na biase tele. kwa hivi inapaswa tuwajue hawa waandishi na mfumo uliowazaa. in fact wanazuoni na watafiti wanaakiwa wawe huru katika kuandika historia ya nchiJapo historia haisemi wazi juu ya mambo mengi sana Tanganyika na Tanzania ya leo, lakini Mwalimu Nyerere tangu awe kiongozi wa nchi hii amenusurika mapinduzi MATATU,
Moja ni la mwaka 1964, lapili ni la mwaka 1970 na la mwisho ni la mwaka 1980 (Sina uhakika sawa na hiyo miaka)
Jaribio la kwanza ndilo lilipelekea kuundwa kwa JWTZ na lilizimwa kwamsaada wa Malkia wa Uingereza aliyetuma makomandoo maalumu na wakafanikiwa, Jaribio la pili ndilo lililopelekea kuundwa kwa Usalama wa Taifa na kikosi maalumu cha ulinzi wa Rais,
na jaribio la mwisho ndio lilipelekea kubadili sera ya usalama wa Taifa kwa kuwapandikiza kila kwenye sekta na kuwa kila mtu ni mlinzi wa nchi hii (usalama)
Sikumbuki vema lakwanza kama liliongozwa na nani lakini Kambona ndie alimficha Mwalimu, lapili sikumbuki vema, lakini la mwisho liliongozwa na baadhi ya wanajeshi wa kikosi cha Anga cha Ukonga Banana,
Na mipango yao iliharibikia palepale Banana baa baada ya mmoja wao kulewa na kuanza kuongea hovyo hasa akisema yeye anataka cheo cha uwaziri mkuu!
Enzi hizo 1980+ mmoja wa makamanda wa usalama wa taifa aliyeongoza kuwadhibiti waasi hao ni Mabere Marandu,
Na alifanikiwa kuongoza oparesheni za kumsaka na kumuua mmoja wa makomandoo ambae alikuwa ameandaliwa rasmi kumuua Nyerere,
Mapambano yalikuwa ni makubwa kutoka airport hadi kinondoni ulipo ubalozi wa Marekani sasa ndipo walipofanikiwa kumuua!
Jambo la kuwashangaza waasi wale (wanajeshi) wote Mwalimu aliwaita ikulu,
akamwambia kiongozi wa mapinduzi yale (simkumbuki) kuwa
"Shika bunduki uniue wewe mwenyewe kwamkono wako ili uwe rais wa nchi hii"
jamaa aliomba radhi huku akitambaa kisha mwalimu akasema
"nimewasamehe wote"
na aliwapa vyeo na kazi, wengi walikwenda kuwa mabalozi wa Tz nchi za nje!
Sisi hapa tunasema kama porojo tu, lakini yapo mengi sana nyuma ya pazia!
Watawala wanahisi kuyataja ni kama kuharibu sifa ya Tanzania na wengine wanaona kama itaharibu sifa ya Mwalimu.
Mimi binafsi nafikiri kama yatasemwa hadharani yataongeza sifa ya Mwalimu Nyerere na utawala wa ccm ya kale!
Kwakifupi hayo ndiyo ninayafahamu,