Jaribio la kutaka kuiangusha serikali ya Nyerere 1982/1983

Mataifa mengi yana sheria baada yq miaka fulani basi classifieds info zinakuwa declassified mfano marekani wao ni Miaka 50 ndio mana Mwanzoni mwa mwaka huu trump ali saini na Kuruhusu files haswa za Jf Kennedy assassination kuwa released public lakini sio files zote ni zile ambazo wanaona ziko safe kujulikana na Raia wao pia Kufahamu history hizi katika credibility sources basi Huongeza Capacity ya Juniors na Seniors ndani ya field hizo Za Civilian au millitary intelligence community pia hata kwa wanasiasa na Raia wote wanaopenda kusoma
 
Shukran sana mkuu Shwari, Mzee Mwanakijiji na Gobore kwa kutupa facts za nguvu.
Binanfsi mmenipa somo kubwa sana hapa baada ya kusikia porojo za kijiweni kwa miaka mingi kuhusi hii issue nzima. Kumbe Martin Tamim hakufa kama story za vijiweni zinavyosema.

Paschal Mayalla: Hivi kweli hakuna hata mwandishi mmoja wa Tanzania anayeweza kuandika kitabu ama documentary kuhusu kisa hiki muhimu cha akina Hans Pope brothers, Martin Tamim et el?! Maggid Mjengwa & Co. What are you guys doing?
Hii ni fursa kwenu wote ambao mko kwenye tasnia ya uandishi (investigative journalism).
Hata rais wetu kichaa atapata cha kujifunza hapa kama ambapo Nyerere alivyojifunza
Mbarikiwe wote
 
Salute to these 21 army men!!!
At least they had balls and guts
Rest in peace Hatty McGhee, Father Tom, Harry Hans Pope, Martin Tamim and Eugene Maganga
 
Aaahaa, eeh bwana, acha kuwataja watu bwana, mambo yale yalikwisha,siyo vizuri mnavyofanya

acha utoto wewe, ubaya wake ni upi sasa??

this is history, kwani anavyotajwa A. H. Mwinyi kua alijiuzulu ni vibaya??
hivi tuna matatizo gani lakini?
 
Mimi ni kijana Wa 1990's lakini hii kesi ya uhaini nilikuwa naifuatilia nikiwa mdogo, ilikuwa very interesting na Komandoo Tamim alikuwa Noma sana.!

kwahyo ulikua unaifwatilia kesi ukiwa tumboni kwa mama au kiunoni mwa baba?

sio lazima kuchangia, soma nondo km sie ujifunze
 
Kuna mwingine alieshitakiwa nao, anaitwa Rashian Roberts I think, yeye aliamua ku settle Songea na kulea familia yake. I think he is still alive. Nae ni chotara kama akina Hans Pope.

Roberts ameshafariki yeye aliweka makazi yake mbele kidogo ya Kijiji cha Sisi Kwa Sisia
 
Kumbe mmefukua historia ya zamani! Nilizani imetokea Leo nianze kutabasamu
 
Kweli baada ya Maalkia kuokoa jahazi Mwalimu alipiga U-turn kwenda uchina? Kumekucha upepo na mawimbi hadi forbidden city.
Suti za kichina zinapendeza.
 
"Maganga anakumbuka kushuhudia wafungwa vijana kulawitiwa . Kulikuwa na ndoa za jinsia moja, wachuuzi wa madawa ya kulevya na baadhi ya wafungwa waliweza hata kuandaa ‘mashindano ya urembo’ ambapo wanaume walionyeza mambo yao."

Jela sio mchezo

Salalee !
 
Noma sana
 
Duuh,shukran sana kwa story hii, Yerico, Mwanakijiji, Pascal & wengineo.

Binafsi niliwahi pata kusimuliwa kisa hiki cha akina Tamimu kwa kiasi kwa kuwa aliyekuwa ananisimulia alinieleza zaidi yale aliyoshuhudia na nikajikuta natamani sana kuijua hii story, ila hapa nimepata mwanga japo kiasi pia;

Ila nilisikia pia kuwa Baba wa Taifa hayati Mwl. JK Nyerere aliumia sana kupewa taarifa kuwa Comandoo Tamimu alikuwemo kwenye huo mpango na alitaka akamatwe akiwa hai ili apate mengi toka kwake.

Pia nilisikia kuwa Mh. Mrema alikuwepo kwenye kikosi kazi na ni yeye aliyetoa amri Comandoo Tamim apigwe shaba kwa kuwa alikuwa anapiga na chupa za beer wale wote walikuwa wakimfuatilia na moja ya chupa alizokuwa akirusha ilimpiga Mh. Mrema kichwani ndio maana hadi leo ana alama (kovu) kichwani.

Kwa ajuaye ukweli juu ya hili atujuze kwa undani jaman, mimi nilipata kuambiwa tuu na natamani sana kuujua ukweli kamili
 
Pia nasikia aliyempiga shaba Commando Tamimu aliuwawa huko Arusha akidhaniwa kuwa ni jambazi. Je, hili nalo pia lina ukweli ndani yake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…