Jaribio la kutaka kuiangusha serikali ya Nyerere 1982/1983

Mkuu Hans Poppe hakwenda kupigana kwenye vita bali alitekwa na askari wa Idd Amin. Actually kifo chake pamoja na wahaya waliomwagika midomo kilichangia sana Tanzania uivamia Uganda na kumfukuza nduli idd amin.
 
Hakuna kitu kama hicho, aliyekusimulia huo uongo lazima alikuwa na umri na akili kama zako! Hakuna mhehe aliyekuwepo wakati huo ambaye alikuwa akikusimulia. Utakuwa ulisimuliwa na vibaka wenzio!
 
Tamim ndio alikuwa comandoo aliyeandaliwa kumuua Nyerere. Unasema tukio lilitokea pale ubalozi wa Marekani lakini nasikia lilitokea pale Kinondoni Mkwajuni.

Wanasema aliruka ukuta kujiokoa halafu akadandia lori la bia akawa anawarushia chupa jamaa wa usalama waliotumwa kumkamata, ndio wakampiga risasi akafariki hapo hapo.
 
Umenikumbusha mbali mkuu. Wengi walikuwa ni jamaa wa kanda ya ziwa, walidakwa mmoja baada ya mwingine.
 
Umenikumbusha utotoni miaka ile ya 1980 mwanzoni wakati kesi ikiwa inaendelea pale mahakamu kuu. Tulikuwa tunajifanya kama vile tunaangalia meli zinavyoingia kumbe nia yetu tuwaone wahaini wakipandishwa ndani ya karandinga.

Namkumbuka wakili Lakha, mhindi mmoja mfupi akiwa anavaa miwani yake. Miaka inakwenda kasi sana.
 
Nyerere alifanya makubwa kuliko haya unayoyazungumza kwa chuki zako binafsi. Nyerere aliua uchifu sidhani kama unayaelewa madhara yake kama angeamua kuwaacha machifu waendelee kuwepo Tanzania.

Lugha ya kiswahili kusambaa nchi nzima usidhani ni kazi nyepesi, alijenga umoja ambao unaifanya Tanzania iwe kama ilivyo miaka 60 baada ya uhuru.

Alikuwa mwanadamu aliyeumbwa na udhaifu kama mimi na wewe na mwingine yoyote yule, haimuondolei uwezo wake wa kuiongozi uliounganisha nchi nzima.
 
Ismailia 2 Yanga 0 uwanja wa taifa 1992.
 
Nimeona maandiko kadhaa na mahojiano lakini hii issue ya kumuua Nyerere haikuwepo. Sasa wewe umeipata wapi historia hiyo?

Mmoja kati wa wanamapinduzi alisema katika mjadala wao issue ya kumuua Nyerere waliona ingeleta vurugu kubwa sana kitaifa na kimataifa.
 
Malcolm alimkejeli Kiongozi wa Nation of Islam akawaudhi waislam na ndio wakamuua.
Malcom X Aka Maliki Shaabaz,alikuja kufahamu uislamu wa kweli ndo akaanza kumkosoa muhuni Elijah Mohammed wa Nation of Islam.Hapa ndo mwanzo wa kifo chake.Elijah was a hooligan.
 
Marando anatakiwa kuandika kitabu kuhusu hili sakata kwani inasemekana yeye alikuwa muhusika mkuu upande wa usalama wa taifa.

Alitendee haki taifa hili kwa kuandika historia yake kama anavyoikumbuka yeye.
 
Malcom X Aka Maliki Shaabaz,alikuja kufahamu uislu wa kweli ndo akaanza kkosoa muhuni Elijah Mohammed wa Nation of Islam.Hapa ndo mwanzo wa kifo chake.Elijah was a hooligan.
Malcom X walimuita hypocrite yaani mnafiki. Kuitwa mnafiki katika uislam inatosha kabisa kuwa sababu ya kifo cha mtu.
 
Mkuu Shwari asante sana kwa haya 'madini' unayoandika humu Jukwaani. Watu leo wanambagua Samia kwa kumuita Mzanzibari na wengi wao ni wadogo kiumri.

Hawayajui madhara ya ubaguzi wanaoukuza kwa maandishi yao. Mungu na alisaidie taifa hili.
 
Mcghee chotara fulani, bado yupo?.
 
Wanasema alidandia lori la bia akawa anawarushia chupa za bia waliokuwa wanamfuatia kwa nyuma, ndipo wakampiga risasi akafa.
 
1983 nipo forodhani shule ya msingi. Nakumbuka kusoma gazetini mwenendo mzima wa kesi.
 
Alikuwepo wakili Lakha, mhindi mmoja anavaa miwani. Kama sijakosea vikao vya kupanga mapinduzi karibu vyote vilifanyikia kwa RIP Banyikwa karibu na iliyokuwa Drive Inn Cinema.
 
Banyikwa Baba na Mama walishafariki. Kam sijakosea alianza kufa Mama miaka ya 2000 mwanzoni akafuata Baba. Msiba wa Mama mimi na Mzee wangu tulikuwepo hapo Drive inn.

Ni wahangaza kweli, wenyeji wa Bugufyi Ngara.
 
Bobuk Balozi Ngaiza,Zera Banyikwa na mumewe mahakama iliwaachia huru na Aden Rage alikata rufaa mahakama kuu ilimsafisha na tuhuma japo aliishatoka gerezani akawa mtu huru ndio maana wakapata wasaa wa kugombea.
Kesi ya Rage ni nyingine inahusiana na masuala ya TFF, kulifanyika wizi ndio akafungwa jela. Alipotoka akaenda mahakama kuu ili imfutie hatia yake. Alifanikiwa ndipo akagombea ubunge wa Tabora.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…