Jaribio la kutaka kuiangusha serikali ya Nyerere 1982/1983

Jaribio la kutaka kuiangusha serikali ya Nyerere 1982/1983

Heshima juu mkuu, ngoja na mimi niweke input zangu kidogo kwa zile ninazoweza

Ni kweli mzee Hans Pope alikua RPC na alikwenda kupigana vita ya kagera akaishia mikononi mwa Idd Amin na alikufa kifo kibaya sana, baadaye recovering ya mwili wake ilikua priority namba moja ndio akaja kuzikwa Tz, nakumbuka ilikua ni baada ya TPDF kuteka wale askari wa Gadafi ndio Idd Amin nae akawa anadai kuwa na Mwalimu kakodisha mamluki wa kizungu( Alikua mzungu kabisa huyu jamaa masalia ya wajerumani) kwa hiyo sidhani kama ilikua 1972 na pia kama kumbukumbu zangu ziko sawa nadhani alikuaga RPC wa Iringa sio Kagera

Vijana wa Hans Pope walioshiriki walikua wawili Zakaria na Harry, nakumbuka Harry ndo aliyekua rubani pale 613KJ naye walikua wanamuita Capt kwa sababu hiyo ila sidhani kama alifikia cheo cha uCaptain, aliyekua Captain for sure ni Zakaria ambaye ni mkubwa kwa Harry.

Kuna mdau hapo juu ameongelea namna mipango ilivuja SIO kweli kwamba walilewa huko Ukonga ila aliyeharibu ni Hatty McGhee ndo alipiga stori na mwenzake mmoja kwenye Taxi akiwa anaenda airport kupanda ndege to Zanzibar( Nadhani mnajua coCabs wakati ule zilikua zinamilikiwa na watu gani) basi jamaa waliwapandikizia Agent kirahisi kwa kutumia njia ya Dereva Taxi na wakawa wanawaangalia wote kwa muda mrefu mpaka waliporidhika ndo wakaanza kuwakamata

Kwa sasa niishie hapa.
Mkuu Hans Poppe hakwenda kupigana kwenye vita bali alitekwa na askari wa Idd Amin. Actually kifo chake pamoja na wahaya waliomwagika midomo kilichangia sana Tanzania uivamia Uganda na kumfukuza nduli idd amin.
 
Ni kweli mkuu maana siku moja nlikua IRINGA cha ajabu ni kuwa historia ya mtemi Mkwawa tunayoisoma kwenye vitabu inaonekana ni ya kupikwa sana si kile ambacho wenyeji wanakifahamu.

Mkwawa anaonekana kuwa alikuwa ni kiongozi aliyetumia diplomasia sana na uchawi sana kutaka kupata suluhu na wajerumani lakini tunaambiwa alikua shujaa aliyepambana na wajerumani mpaka dakika ya mwisho wakati ukweli ni kuwa aliwakimbia wajerumani kwa kutaka kujiokoa baada ya diplomasia na utabiri wa mganga wake wa kienyeji kuwa atawashinda wajerumani kushindwa.

Ninachojiuliza hapa je ni kweli kuwa historia ya nchi hii nyingi ni ya kupika??
kwa nini matukio mazito kama haya ya mapinduzi ya kijeshi hayatajwi katika historia ya hii nchi?
Hakuna kitu kama hicho, aliyekusimulia huo uongo lazima alikuwa na umri na akili kama zako! Hakuna mhehe aliyekuwepo wakati huo ambaye alikuwa akikusimulia. Utakuwa ulisimuliwa na vibaka wenzio!
 
Japo historia haisemi wazi juu ya mambo mengi sana Tanganyika na Tanzania ya leo, lakini Mwalimu Nyerere tangu awe kiongozi wa nchi hii amenusurika mapinduzi MATATU,

Moja ni la mwaka 1964, lapili ni la mwaka 1970 na la mwisho ni la mwaka 1980 (Sina uhakika sawa na hiyo miaka)

Jaribio la kwanza ndilo lilipelekea kuundwa kwa JWTZ na lilizimwa kwamsaada wa Malkia wa Uingereza aliyetuma makomandoo maalumu na wakafanikiwa, Jaribio la pili ndilo lililopelekea kuundwa kwa Usalama wa Taifa na kikosi maalumu cha ulinzi wa Rais,

na jaribio la mwisho ndio lilipelekea kubadili sera ya usalama wa Taifa kwa kuwapandikiza kila kwenye sekta na kuwa kila mtu ni mlinzi wa nchi hii (usalama)

Sikumbuki vema lakwanza kama liliongozwa na nani lakini Kambona ndie alimficha Mwalimu, lapili sikumbuki vema, lakini la mwisho liliongozwa na baadhi ya wanajeshi wa kikosi cha Anga cha Ukonga Banana,

Na mipango yao iliharibikia palepale Banana baa baada ya mmoja wao kulewa na kuanza kuongea hovyo hasa akisema yeye anataka cheo cha uwaziri mkuu!

Enzi hizo 1980+ mmoja wa makamanda wa usalama wa taifa aliyeongoza kuwadhibiti waasi hao ni Mabere Marandu,

Na alifanikiwa kuongoza oparesheni za kumsaka na kumuua mmoja wa makomandoo ambae alikuwa ameandaliwa rasmi kumuua Nyerere,

Mapambano yalikuwa ni makubwa kutoka airport hadi kinondoni ulipo ubalozi wa Marekani sasa ndipo walipofanikiwa kumuua!

Jambo la kuwashangaza waasi wale (wanajeshi) wote Mwalimu aliwaita ikulu,

akamwambia kiongozi wa mapinduzi yale (simkumbuki) kuwa

"Shika bunduki uniue wewe mwenyewe kwamkono wako ili uwe rais wa nchi hii"

jamaa aliomba radhi huku akitambaa kisha mwalimu akasema

"nimewasamehe wote"

na aliwapa vyeo na kazi, wengi walikwenda kuwa mabalozi wa Tz nchi za nje!

Sisi hapa tunasema kama porojo tu, lakini yapo mengi sana nyuma ya pazia!

Watawala wanahisi kuyataja ni kama kuharibu sifa ya Tanzania na wengine wanaona kama itaharibu sifa ya Mwalimu.

Mimi binafsi nafikiri kama yatasemwa hadharani yataongeza sifa ya Mwalimu Nyerere na utawala wa ccm ya kale!

Atakuwa ni kiongozi pekee barani afrika na duniani aliyenusurika majaribio matatu ya uasi,

Atakuwa ni kiongozi wa kwanza duniani kuwasamehe waasi kwa mda huohuo wa uasi (baada ya kuwakamata) na kuwapa kazi nyingine za kitaifa

Atakuwa ni kiongozi pekee duniani aliye ng'atuka kwa amani na kwenda kuishi kijiji tena bila hata ulinzi, akitembelea land rover ya shamba miaka mitano tu baada ya jaribio kali la mapinduzi ya Banana Ukonga!

Hizo zote zilikuwa ni sifa zake ambazo watawala wa leo kwa makusudi ama kwakujua au kutojua wamefifisha nyota ya mwana wa Afrika mbele ya uso wa mataifa!

Na kwakuwafahamisha tu ni kuwa mmoja ya wanajeshi hao walioasi ni Meja Gen Hans Popi yule mwenye Sams Super Store pale Mbezi Makonde!

Kwakifupi hayo ndiyo ninayafahamu,
Tamim ndio alikuwa comandoo aliyeandaliwa kumuua Nyerere. Unasema tukio lilitokea pale ubalozi wa Marekani lakini nasikia lilitokea pale Kinondoni Mkwajuni.

Wanasema aliruka ukuta kujiokoa halafu akadandia lori la bia akawa anawarushia chupa jamaa wa usalama waliotumwa kumkamata, ndio wakampiga risasi akafariki hapo hapo.
 
wengi wao hao wana anga walikuwa ni makaka wa familia moja iliyokuwa exposed nje na kupat amafunzo haba kipindi hicho ya urubani,mmoja wapo walikuwa rubani wa Mzee mkubwa.

Tetesi aliponea bahati kwa vile naye alikuwa safairini na mzee huku akijidaia kuwa mtiifu sana,ila kaka zake walinyea lupango kwa siku kadhaa,Leaders Club pia ilikuwa ni sehemu mojawapo ya kukutana sijui ndio iliwafanya wagombee uongezi sana.

Siku walikuwa wakilewa walikuwa ndio siku ya mwisho ya kupanda kwa hivyo walikuwa wakifurahia kuwa kesho yake wataitwa majina mapya.

Tetesi pia ni kwamba wake zao nao walikuwa mashushu na laiyebahatika ni ya huyo mpenda sifa na uongozi alipopasua kila alipokuwa akilewa.
Umenikumbusha mbali mkuu. Wengi walikuwa ni jamaa wa kanda ya ziwa, walidakwa mmoja baada ya mwingine.
 
Kuna mtu kuandika imani yake na matamanio yake na kuyafanya yawe historia. Katika Tanzania hayajawahi kutokea Mapinduzi ya kijeshi. Hilo la kwanza.

La pili kile ambacho tunakiita kwa Kiswahili "maasi ya jeshi" kwa kweli hayakuwa maasi ya "jeshi" kwa maana ya "armed rebellion". Wanajeshi wetu hawakuinua silaha zao dhidi ya watawala wa kisiasa ili kuwaondoa madarakani. Kilichotokea (na Kwa Kiingereza kinatumia neno zuri la kitalaamu" kinaitwa "mutiny". Utaona karibu maandishi yote ya kihistoria hayaelezei kile kilichotokea kuwa ni "military rebellion" bali "army mutiny". Mutiny ni aina ya uasi ambapo kikundi cha watu waliokuwa kwenye amri au chini ya mtu fulani wanaamua kukataa kutii amri hiyo na hata kureplace. Hii inatumiwa sana kwa mfano kwenye meli, au jeshini ambapo maaskari wanakataa kutii amri za mkubwa wao kijeshi.

Sasa "mutiny" inaweza kabisa kufikisha kwenye rebellion ambapo kundi kubwa zaidi la wanajeshi linaamua kuchukua silaha na kuanza harakati za kupinga serikali. Lakini kama mutiny inatokea mara moja na uasi wa kijeshi unatokea mara moja na kuharakisha kuwaondoa watawala walioko madarakani kinachotokea ni mapinduzi. Mapinduzi hata hivyo si lazima yafanywe na wanajeshi. Na kwa kawaida sana "mutiny" inazungumzia mambo ya kijeshi kwa mfano raia hawawezi kudaiwa kufanya "mutiny" japo wanaweza kuanzisha uasi dhidi ya watawala.

Uhaini kwa upande mwingine siyo mutiny (japo kosa la mutiny linaweza kuingizwa kwenye uhaini). Uhaini ni ile kula njama ya kutaka kuiondoa serikali halali madarakani kwa kutumia njia zisizo za kidemokrasia au kwa hata kutumia nguvu. Yaliyotokea katika kesi mbili za uhaini (ya kina Bi. Titi na baadaye ya miaka 1980s) ni uhaini kwa maana ya kwamba kulikuwa na madai ya watu waliokuwa wanajaribu kula njama. Sasa uhaini unaweza kufanywa na raia si lazima awe askari. Na katika nchi yetu kosa kubwa zaidi dhidi ya Jamhuri ni uhaini na huu unaweza kufanyika dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa TAnzania na si dhidi ya Zanzibar.

Narudia hakujawahi kuwepo Mapinduzi dhidi ya serikali ya Nyerere. Kumewahi kuwepo uasi (mutiny) ya kikundi cha wanajeshi dhidi ya maafisa wao (siyo dhidi ya Nyerere - of course wakitumwa ujumbe kwa wanasiasa kuwa mambo hayakuwa sawa jeshini) na kumewahi kuwepo na njama za uhaini (kumpindua).

Lakini watu wengine wanafikiria kwenda kumficha Nyerere wakati nchi ina utata lilikuwa jambo la ajabu. NI labda kutttokujua tu. Wakati Marekani inashambuliwa Septemba 11, 2001 Rais Bush aliondoka Florida na kwenda "kusikojulikana" akifichwa angani kwa muda hadi wajue nini kinaendelea hasa kwa vile kulikuwa na tuhuma za ndege kuelekea Ikulu ya DC. Sasa kama taifa kubwa na tena mwaka 2001 linamficha Rais wake "at undisclosed location' sisi ka nchi ka Tanganyika mlitaka Nyerere ajitokeze au akae Ikulu pale anakunywa chai kwa ajili ya nini?

Hata leo hii ikitokea kuna watu wanatishia Ikulu msidhani Kikwete ataenda kupiga nao soga na kuanza "ndugu zangu..." watamkimbiza kwenda kumficha (na mipango hiyo ipo na mahali pa kumpeleka papo).
Umenikumbusha utotoni miaka ile ya 1980 mwanzoni wakati kesi ikiwa inaendelea pale mahakamu kuu. Tulikuwa tunajifanya kama vile tunaangalia meli zinavyoingia kumbe nia yetu tuwaone wahaini wakipandishwa ndani ya karandinga.

Namkumbuka wakili Lakha, mhindi mmoja mfupi akiwa anavaa miwani yake. Miaka inakwenda kasi sana.
 
Nyerere kisha taka kupinduliwa mara nyingi tu.

Ni watu walikuwa hawampendi, kadhulumu mali za watu, kuanzia majumba, mashamba, biashara. Akawa hajui kuongoza nchi, aliongoza kidikteta, atakacho yeye ndio hicho hicho, watu wakawa masikini wa kutupwa, kila mtu mnyonge na kadhoofika, kasoro watu wa mduara wake tu.

Kuna kupendwa hapo? Watu waliompenda ni wa kanisa katoliki tu kwani wao ndio aliwatumikia kwanza kuliko nchi, na hilo kalisema mwenyewe si maneno yangu hayo, anaebisha namwekea nukuu. Anza.
Nyerere alifanya makubwa kuliko haya unayoyazungumza kwa chuki zako binafsi. Nyerere aliua uchifu sidhani kama unayaelewa madhara yake kama angeamua kuwaacha machifu waendelee kuwepo Tanzania.

Lugha ya kiswahili kusambaa nchi nzima usidhani ni kazi nyepesi, alijenga umoja ambao unaifanya Tanzania iwe kama ilivyo miaka 60 baada ya uhuru.

Alikuwa mwanadamu aliyeumbwa na udhaifu kama mimi na wewe na mwingine yoyote yule, haimuondolei uwezo wake wa kuiongozi uliounganisha nchi nzima.
 
Nani aliokudanganya kuwa Aga-Khan ni Asians?

Kwanza kabisa uelewe kuwa hao wanaitwa Ismailia, Ismaili ni mji mmoja uliopo Afrika, huko Misr(Egypt). Sasaa u Egyption na u Asia wapi na wapi? kipi kilichokufanya uwaone ma Aga Khan kuwa ni wa Asia?

Kama unakumbuka hata hapa Tanzania timu ya mpira ya kutoka Ismailia imeshawahi kuja na kupambana na Mnyama Mkali, SSC.
Ismailia 2 Yanga 0 uwanja wa taifa 1992.
 
Tamim ndio alikuwa comandoo aliyeandaliwa kumuua Nyerere. Unasema tukio lilitokea pale ubalozi wa Marekani lakini nasikia lilitokea pale Kinondoni Mkwajuni.

Wanasema aliruka ukuta kujiokoa halafu akadandia lori la bia akawa anawarushia chupa jamaa wa usalama waliotumwa kumkamata, ndio wakampiga risasi akafariki hapo hapo.
Nimeona maandiko kadhaa na mahojiano lakini hii issue ya kumuua Nyerere haikuwepo. Sasa wewe umeipata wapi historia hiyo?

Mmoja kati wa wanamapinduzi alisema katika mjadala wao issue ya kumuua Nyerere waliona ingeleta vurugu kubwa sana kitaifa na kimataifa.
 
Malcolm alimkejeli Kiongozi wa Nation of Islam akawaudhi waislam na ndio wakamuua.
Malcom X Aka Maliki Shaabaz,alikuja kufahamu uislamu wa kweli ndo akaanza kumkosoa muhuni Elijah Mohammed wa Nation of Islam.Hapa ndo mwanzo wa kifo chake.Elijah was a hooligan.
 
Tamim ndio alikuwa comandoo aliyeandaliwa kumuua Nyerere. Unasema tukio lilitokea pale ubalozi wa Marekani lakini nasikia lilitokea pale Kinondoni Mkwajuni.

Wanasema aliruka ukuta kujiokoa halafu akadandia lori la bia akawa anawarushia chupa jamaa wa usalama waliotumwa kumkamata, ndio wakampiga risasi akafariki hapo hapo.
Marando anatakiwa kuandika kitabu kuhusu hili sakata kwani inasemekana yeye alikuwa muhusika mkuu upande wa usalama wa taifa.

Alitendee haki taifa hili kwa kuandika historia yake kama anavyoikumbuka yeye.
 
Malcom X Aka Maliki Shaabaz,alikuja kufahamu uislu wa kweli ndo akaanza kkosoa muhuni Elijah Mohammed wa Nation of Islam.Hapa ndo mwanzo wa kifo chake.Elijah was a hooligan.
Malcom X walimuita hypocrite yaani mnafiki. Kuitwa mnafiki katika uislam inatosha kabisa kuwa sababu ya kifo cha mtu.
 
Halikuwa suala la dini au udini. Ilikuwa ni "damu." Damu yao iliwaunganisha. Walikuwa ni Waislamu na Wakristo, pia kutoka pande zote mbili za Muungano. Huo ndiyo ukweli na inatubidi tuseme ukweli. Mimi ni Mkristo mweusi mwenye asili ya Kiafrika kutoka moja ya makabila ya hapa nchini Tanzania.

Kwa wale waliompinga na kumchafua, Salim Ahmed Salim hakuwa "damu" yao ingawa ana damu hiyo kutoka upande wa mama yake. Lakini waliona damu hiyo haitoshi, ni kidogo sana, kutoka upande wa mama yake. Pamoja na damu ya kigeni kabisa kutoka upande wa baba yake, waliona hakuwa "mmoja wetu." Kwa mfano, wazazi wa Salim Ahmed Salim wengekuwa Wamanyema au Wanyamwezi au wa kabila lingine lolote, au kutokana na mchanganyiko wa makabila, asingekuwa na tatizo kuchaguliwa kuwa mgombea wa uraisi kutoka Chama Cha Mapinduzi na angeshinda uchaguzi kuwa raisi wa Tanzania.

Miongoni mwa waliompinga walikuwa viongozi kadhaa. Lakini kulikuwa na viongozi wa taifa, hasa kutoka upande wetu wa bara, waliomuunga mkono. Kwa wale waliompinga, walimpinga kwa sababu hakuwa na "damu yetu."

Bila shaka bado kuna ambao wana msimamo huo. Akija mwingine kama Salim kugombea uraisi, au mwingine kama Amir Jamal (ambaye hakuwahi kugombea uraisi lakini alikuwa karibu sana na Mwalimu Nyerere kuliko mawaziri wote tangu tupate uhuru), atakumbana na tatizo hilo.

Kuna Watanzania ambao bado hawajajifunza chochote kutokana na athari za ukabila au ubaguzi wa aina yoyote ingawa wanajua matokeo na madhara yake katika nchi jirani: Rwanda, Burundi na Kenya. Matokeo ya siasa na sera za ukabila na ukanda nchini Nigeria, na katika nchi zingine katika bara letu, siyo ya kujivunia. Siyo msingi wa amani na umoja wa nchi yoyote.

Enzi ya Mwalimu Nyerere, msingi wa umoja wetu nchini Tanzania na katika bara letu ulikuwa ni: "Afrika ni moja. Binadamu wote ni ndugu zangu." Halafu sasa tunaulizana makabila, na kadhalika, na asili yetu "kuhakikisha" ni raia au "ni ndugu yangu kwa sababu anatakoka kwetu." Kwenu wapi? Kwenu si Tanzania yote?

Kuna hata wenzetu ambao ni raia wanaoambiwa, "rudi kwenu," "mkimbizi we," "Mnyasa huyo," "Karundi hako," na kadhalika, kwa sababu mbalimbali (pamoja na kutofautiana kimawazo na viongozi) hata kama wana uthibitisho kwamba ni raia.

Tukianza kufukuzana, na kuambiana wewe siyo Mtanzania, nani atabaki hapa? Wagogo tu? Na Watindiga, Wanyaturu na wengineo wenye "asili" ya mikoa ya kati? Wao pia walitoka mahali pengine, katika bara letu, nje ya eneo ambalo sasa linaitwa Tanzania.

Ni dhambi ukitoka sehemu za mpakani na nchi jirani? Ni kosa gani hata ukiwa na asili nje ya bara letu lakini ni raia wa Tanzania?

Kuna hata ambao walisema Nyerere ni Mtusi (kwahiyo siyo Mtanzania na haipendi nchi yetu kwa sababu ya Utusi wake kama Christopher Mtikila alivyosema) ingawa pia inasemekana alikuwa na asili ya Kijaluo kutoka Kenya au visiwa vya Ssese ziwani Nyanza.

Lakini hata kama ni kweli alikuwa na asili ya Kitusi pia, labda upande wa mama yake (ni mfano tu), kuna kosa gani? Hakuna watu wa asili ya Kitusi ambao ni raia wa Tanzania? Hakuna Watusi wanaoweza, na wanaostahili, kuwa raia wa Tanzania? Kwa nini yawe makabila fulani tu? Na kwa sababu gani?

Hata kama ulizaliwa nchi nyingine, unaweza kuwa raia wa Tanzania ukitaka kuwa raia wa nchi yetu; kwa mfano, Derek Bryceson, Shirley Graham Du Bois, na wengineo waliozaliwa nje ya nchi yetu, na nje ya bara letu, bila kujali "sina kundi langu au la watu wa asili yangu watakao nitetea kupata haki zangu au watakaopigania haki zetu" kama Wazungu, Afro-Americans, Waha, Wagogo, Wahindi, Wasafwa, Wakurya, Wasomali, Wazanaki, Waarabu, Wapogoro, Wafipa, Wameru, Wamatumbi na kadhalika. "Haki zangu na haki zetu" ni haki ambazo ni haki za wananchi wote kama watu binafsi na siyo kwa sababu ni watu au wananchi wa makundi fulani.

Raia wote wa nchi yetu, waliozaliwa nchini na waliozaliwa nje ya nchi yetu, wote ni sawa. Hakuna ambaye ana haki zaidi kuliko mwingine, hakuna ambaye ni bora kuliko raia mwenzake. Ni uraia wa mtu binafsi bila kujali alikotoka. Huo ndiyo msingi wa haki na umoja wa nchi yetu.

Ndiyo maana Nyerere alipoanza rasmi kudai uhuru kutoka kwa wakoloni miaka ya hamsini, alisema tutajenga nchi yetu ya Tanganyika, na taifa letu la Tanganyika, kutokana na haki na uraia wa watu binafsi (individuals), siyo haki na uraia kutokana na msingi wa makundi ya makabila au makundi ya watu wenye asili mbalimbali (Wazungu, Wahindi, Waarabu) na kadhalika.

Hakutakuwa na sehemu itakayotengwa kuwa ni ya Wazungu tu, ni ya Wahindi, Waarabu, Wasomali, Wahehe, Wanyamwezi, Waluguru, Wamakonde, Machotara, Wasukuma, Wayao, Wachaga, Wazaramo, Wamasai, Wandengereko, Wanyakyusa, Wadigo, Wangoni, Wanyasa, Wahaya, na kadhalika. Sehemu zote za Tanganyika zitakuwa ni za Watanganyika wote. Huo ndiyo moyo wa umoja wetu, si Tanzania tu, bali bara zima. Ndiyo maana Nkrumah aliwahi kusema kila nchi na mji katika bara la Afrika ni nyumbani kwake: "Every country and town in Africa is my home."

Nyerere aliwahi kusema: it is shame for Africans to be refugees in Africa - Waafrika kuwa wakimbizi nyumbani kwao Afrika. Kila nchi wanakokimbilia iwe ni nyumbani kwao.

Tumekuwa Watanganyika tangu tupate uhuru, na Watanzania baada ya kuungana na ndugu zetu wa visiwani Unguja na Pemba, na tumekuwa tunajisifu kuwa tuna umoja bila kujali kabila la mtu au rangi yake na asili yake. Tumekuwa na sifa hiyo, ya umoja na amani, karibu kuliko nchi zote katika bara letu.

Halafu sasa hata askari wetu wameanza kuuliza "wewe kabila gani?"

Tumerudi nyuma miaka mingi sana.

Enzi ya Nyerere, kulikuwa na ukabila hapa na pale, lakini ulikuwa hauvumiliwi.

Hatuna ukabila kama nchini Kenya, kwa mfano kati ya Wakikuyu na Wajaluo, au nchini Rwanda na Burundi ambako Wahutu na Watusi wamechinjana kwa miaka mingi sana. Lakini tusipojiangalia, tukiendelea kuvumilia ubaguzi wa aina yoyote mpaka watu wanajisifu na wanajiona ni bora kuliko Watanzania wengine kwa sababu wanatoka makabila fulani, na mikoa au ukanda fulani - "bila sisi, msingekuwa na wasomi nchi hii," "hamna akili nyie," "ukanda wetu una maendeleo ya pekee kuliko sehemu zote nchini kwa sababu tumewazidi akili, sisi ni vichwa" "watu wa kabila lenu, mbona mko nyuma sana?" - tutakuwa na matatizo sana kama taifa.

Kuna hata vyama vya siasa ambavyo vinasemekana ni vya makabila fulani, au vinaongozwa na watu wa kabila fulani au wa makabila fulani tu kwa sababu wanachama wa makabila mengine wanabaguliwa. Kuna wengine wanaosema watu kutoka makabila fulani hawastahili kuwa viongozi wa nchi yetu kwa sababu wana ubaguzi sana, wanawabagua watu wa makabila mengine.

Pia kuna ubaguzi kazini. Unavumiliwa hata kama kuna ushahidi watu wa makabila fulani wanapendeleana kupeana kazi.

Tusivumilie ubaguzi wa aina yoyote. Nani anakemea ubaguzi huo, na anamaanisha anachosema, kama Nyerere?

Bado tuna safari ndefu sana.

I weep for my country.
Mkuu Shwari asante sana kwa haya 'madini' unayoandika humu Jukwaani. Watu leo wanambagua Samia kwa kumuita Mzanzibari na wengi wao ni wadogo kiumri.

Hawayajui madhara ya ubaguzi wanaoukuza kwa maandishi yao. Mungu na alisaidie taifa hili.
 
Kapten Kadego anajiita mwanachama was Soldiers without boarders.Alinambia walikuwa na support ya Roanald Reagan wa Marekani ila mengine akasema ni top secret.Huyu mtu sijawasiliana naye miaka mingi lakini akili yake haikuwa sawa.Kapten Maganga yeye alifariki mwaka 2010 ndugu Bagyem yeye alifariki mwaka juzi na mwenzao aliyetoboa ni Zakharia Hanspope wa Simba.
Mcghee chotara fulani, bado yupo?.
 
Marekebisho:

Huyo komandoo aliyeuawa hakuuwawa jirani na ubalozi wa Marekani sijui kwa nini watu wanapotosha.Na hii habari ilikuwa wazi kabisa.

Mimi nikuwa naishi O/bay jirani sana na huo ubalozi wa USA wa zamani kwa nyuma.

Huyo Kamandoo aliuawa kinondoni pale inapoanza down ya kwenda magomeni , alidandia pickup ya wazi baada ya kuwatoroka ghafla waliomkamata..

Nakumbuka kama alikuwa anaitwa Tammim
Wanasema alidandia lori la bia akawa anawarushia chupa za bia waliokuwa wanamfuatia kwa nyuma, ndipo wakampiga risasi akafa.
 
Sahihi kabisa, naikumbuka vema siku hiyo. Nilikuwa nimempiga uncle wangu mmoja mzinga kidogo ili kuongezea nguvu nikirudi shule kesho yake niwe na nguvu ya ziada.
Sasa kwa vile yeye alikuwa anaishi Mwananyamala habari zikawa zimeenea kuwa maeneo hayo sio salama kwenda na mie kesho yake narudi shule Moshi.
Ikala kwangu
1983 nipo forodhani shule ya msingi. Nakumbuka kusoma gazetini mwenendo mzima wa kesi.
 
Salamu kwenu wanabodi!

leo nataka niwasogezee kisa hiki cha kesi ya uhaini ya miaka ya 1980.ilikuwa ni kesi ya kihistoria na kielelezo tosha cha uhuru wa mahakama.kwanini nimeleta kwenu leo? ni kwamba kisa chote kilionesha ustadi wa wahusika kila mhusika kwa upande wake.Nitaanza upande mmoja baada ya mwingine na mwisho nitatoa majumuisho.

wahusika wa mipango ya kumpindua mwalimu nNyerere kwa upande wao ilionesha walijipanga vizuri na kwa mtazamo wao walikuwa na uhakika kufanikiwa kutekeleza azima yao.Lakini kwanini walishindwa?Ni kwasababu ya ustadi na mbinu za hali ya juu ya utendaji wa usalama wa Taifa.walimuonesha Nyerere kilele cha ustadi wao.

kamatakama ya wote walio panga kutekeleza uhalifu ule ilikuwa fantastic, kama senema vile lakini ilikuwa ni tukio la kweli.Mmoja baada ya mwingine alitiwa mbaroni na hatimaye kufikishwa mbele ya sheria.

Kilicho nivutia mimi ni jinsi kesi yenyewe ilivyo endeshwa kwa ustadi mkubwa kwa Lugha ya kiingereza, wale mawakili wa pande zote walipiga kiingereza kizuri hatari utadhani walifanya majaribio kabla ya kufika mbele ya jaji.Kwangu mimi nilifurahi sana na nikajivunia elimu bora waliyo kuwa nayo vijana wetu wakati ule. Maswahili mtu anahojiwa lakini jibu litakalo toka nalo lilikuwa fantastic !usinge bashiri upande gani ungeibuka mshindi.

Hayo yalikuwa ya zamani, na watuhumiwa baada ya kesi kuendeshwa muda mrefu walitiwa hatiani kwa ushahidi usio na mashaka hata kidogo.

Baada ya kesi ile , Mwandishi wa habari mmoja alisema ukiacha unyeti wa kesi yenyewe, hakika Nchi ina vijana walio pikwa wakapikika achilia mbali kile kiingereza mujaarabu lakini ujuzi walio uonesha ulitoa matumaini makubwa kuwa huko tuendako tutatisha sana na wataalamu wetu.

Najiuliza nini kimekwenda kombo siku hizi vijana hawa muda kuongea kiswahili sanifu seuzi kiingereza.tatizo limetokea wapi? Kuna rafiki yangu Hakimu mfawidhi mstaafu alisema ukitaka ucheke mpaka uzimie mpe kijana aliye hitimu chuo miaka ya hivi karibumu hukumu ya kesi kwa kiingereza.ukiweza kuielewa alikuwa anamaanisha nini utakuwa na bahati sana.Ni mmoja kati ya watano. Sijui fani zingine hali ikoje? Siyo tu lugha bali na maarifa yenyewe.
Alikuwepo wakili Lakha, mhindi mmoja anavaa miwani. Kama sijakosea vikao vya kupanga mapinduzi karibu vyote vilifanyikia kwa RIP Banyikwa karibu na iliyokuwa Drive Inn Cinema.
 
Uhaini ulipangwa 1982, home kwetu ni Drive-in Estate, nyumba yetu na nyumba ya Banyikwa ziliuwa zimeungana tukitenganishwa na ukuta. Hapo ndipo ilipokuwa ikifanyika mikutano ya kupanga mambo!. PW No. 1 ni Hope Banyikwa, ambaye ndie binti mkubwa wa familia ya Banyikwa, hawa walikuwa ni Wahangaza, hao mabinti!, usipime!.

Kesi ilivyoanza, ilikuwa na washtakiwa 46. Wote walishikiliwa Ukonga Maximum Prison, Kiongozi mkuu wa mpango huo ni komandoo wa JWTZ aliyeasi, Martin Tamimu aliyeelezewa kuwa ni mtu hatari sana na hashikiki kirahisi, hivyo wakati wa arrest vijana walipewa special instructions, hivyo askari 8 na magari 4 yalimzingira nyumba aliyokuwepo kwa kimada wake Kinondoni Mkwajuni, walipojiririsha yuko ndani ya "game", waliivamia nyumba!, alichomoka bila shati na kuchumpa darini!, jamaa kuingia ndani hayupo!. Huyo demu akawaelekeza askari kwa ishara, wakaizunguka nyumba, ile wanaanza tuu kumpandia, alitobokea kwenye siling board ya bafu la nje na kuruka ukuta hadi upande wa pili, kumbe nako kuna gari la "jamaa", wakamkimbiza, akarukia pick up iliyokuwa inakwenda race,"jamaa" wakaifuata ile pick -up ay very close range, wakamiminia za kutosha na kumaliza kazi!.

Baada ya sterling kuuwawa, Thomas Lugangira "Father Tom" au "Uncle Tom" ndiye alikuwa mshatakiwa wa kwanza Hatibu Macghee wa pili na wenzao 19.

Nitaendelea.

Pasco.
Banyikwa Baba na Mama walishafariki. Kam sijakosea alianza kufa Mama miaka ya 2000 mwanzoni akafuata Baba. Msiba wa Mama mimi na Mzee wangu tulikuwepo hapo Drive inn.

Ni wahangaza kweli, wenyeji wa Bugufyi Ngara.
 
Bobuk Balozi Ngaiza,Zera Banyikwa na mumewe mahakama iliwaachia huru na Aden Rage alikata rufaa mahakama kuu ilimsafisha na tuhuma japo aliishatoka gerezani akawa mtu huru ndio maana wakapata wasaa wa kugombea.
Kesi ya Rage ni nyingine inahusiana na masuala ya TFF, kulifanyika wizi ndio akafungwa jela. Alipotoka akaenda mahakama kuu ili imfutie hatia yake. Alifanikiwa ndipo akagombea ubunge wa Tabora.
 
Back
Top Bottom