Watawala wengi wa kiafrika walipewa utawala,na kurithi mifumo na wat;umishi waliokuwa wanafanya kazi serikali za Wazungu.kwa hiyo wafanyakazi walikuwa wanawadharau watawala wapya wa kiafrika ambao walikuwa ni wanasiasa waliozungukwa na watu wasio wasomi.
1961;unakabidhiwa nchi,majeshi,wafanyakazi na wizara kama ilivyokuwa chini ya mkoloni.:
1964;wanajeshi walikuwa wanataka vilevile na wao wajikomboe na amri na makamanda wakigeni waliokuwa bado wapo nadani ya majeshi,hali hii ilikuwa inasumbu nchi nyingi za afrika,na baadhi ya wafrika walikuwa baado wanawatukuza wakoloni.
Kipindi hiki J.K.Nyerere,akaamuwa kuwapa madaraka makada wa TANU,chama tawala nafasi zote muhimu na wanajeshi wapewa madaraka ya juu ili kutuliza manung'uniko;lakini kuanzia hapo mpaka leo Tz imeporomoka kwa kila kitu.!!!!!
1967;Nyerere akafikiri akitaifisha biashara na mashamba ndipo serikali itawea kudhibiti na kusimamia uchumi,kumbe uchumi ukazidi kuporomoka.
Mpaka kufikia mwaka 1975,nchi ilikuwa taabani,mpaka akataka kung'atuka lakini,makada ndani ya chama wakamshawishi Nyerere aendelee.
kipindi chote hiki alikuwa anawafadhilli wapigania uhuru na wakimbizi wa kisiasa kutoka nchi majirani,pamoja na kufanya jitihada za kumrudisha Obote madarakani,kwa bahati mbaya vita vya Uganda vikadhoofisha uchumi wa Tz+sera zilizoshindwa kusimamia uchumi.Miaka ya 80,hali ya uchumi ikawa ngumu sana,mashirika mengi yakawa taabani na upungufu wa bidhaa ukawa mkubwa.!!!
Serikali ya Nyerere ilikuwa imewapeleka wanajeshi vijana kusoma nje ya nchi( Kanada na U.K) ,na unavyojua msomi yeyote anapenda kufanyia kazi alichokisomea;ukizingatia kule walikuwa wanakutana na WaNIGERIA ambao walikuwa classmates wenzao walikuwa wakirudi kwao wanafanya Mapinduzi pindi serikali inapokuwa imeshindwa kulinda katiba na kusimamia Utawala bora.
Wengi walioshiriki ktk jaribio lile la mapinduzi mwaka 1982 walikuwa ni wale waliokuwa wamesoma nje,kwani ipo Mapinduzi ya kijeshi ipo kwenye syllabus ya msomo ya jeshi.Kipindi hiki na hapo Kenya vilevile Moi alikumbana na jaribo la Mapinduzi.!!!
Jaribio hili,lilimfanya Nyerere ajitathimini upya(uamuzi wa kung'atuka) na ukizingatia kwa wakati huo alikuwa ametoka katika vita,takwimu za uchumi zilikuwa zinaporomoka,fedha ya kigeni ilikuwa imepungua.!!!
Mara madogo wakateka ndege ya ATC.!!!,yaaani ilikuwa kama,kiongozi wa nchi hakuna kilichokuwa kinakwenda sawa.
Nafikiri utakuwa umepata baadhi ya sababu ya kutaka kufanyika kwa Jaribio la Mapinduzi.!!!!!!
Kuna habari nimewahi kusoma sikumbuki chanzo chake kwa sasa, inazungumzia kuhusu kuporomoka kwa uchumi kwa sababu kama vita ulivyoelezea hapo juu,kuangushwa kwa ucommunist ikapelekea kuwa sehemu ambapo nchi ingeweza kupata msaada ni IMF NA WB.
Kwa maana hiyo ingempasa Nyerere kufuata masharti ya IMF na WB kitu ambacho kilikuwa kinyume kabisa na sera zake.... na isingekuwa rahisi kwake kuanza kuimba wimbo mpya hivyo akaamua kung'atuka.
Na kwa mtazamo wangu kinachonifanya niamini hiki ni kwamba alipotoka madarakani aliweka kautaratibu ka kuingilia utendaji pamoja na kuchagua viongozi anaowataka yeye ikiimanisha kuna mambo bado alitaka yawe anavyotaka yeye kitu ambacho kama angeweza angefanya akiwa bado madarakani.Haikusemwa wazi wazi lakini inaonekana kuna hiden pressure nyuma ya kung'atuka kwake.