Mentality hizo za kudhgarau dini za wengine zinawaletea wote wanaoziendekeza ugonjwa wa mtindio wa ubongo...achana nazo bwana wewe.Hazijawahi kumlipa yeyete anayezifanya na hazitakaa kufanya hivyo. Don't waste your precious time!
Watawala wengi wa kiafrika walipewa utawala,na kurithi mifumo na wat;umishi waliokuwa wanafanya kazi serikali za Wazungu.kwa hiyo wafanyakazi walikuwa wanawadharau watawala wapya wa kiafrika ambao walikuwa ni wanasiasa waliozungukwa na watu wasio wasomi.
1961;unakabidhiwa nchi,majeshi,wafanyakazi na wizara kama ilivyokuwa chini ya mkoloni.:
1964;wanajeshi walikuwa wanataka vilevile na wao wajikomboe na amri na makamanda wakigeni waliokuwa bado wapo nadani ya majeshi,hali hii ilikuwa inasumbu nchi nyingi za afrika,na baadhi ya wafrika walikuwa baado wanawatukuza wakoloni.
Kipindi hiki J.K.Nyerere,akaamuwa kuwapa madaraka makada wa TANU,chama tawala nafasi zote muhimu na wanajeshi wapewa madaraka ya juu ili kutuliza manung'uniko;lakini kuanzia hapo mpaka leo Tz imeporomoka kwa kila kitu.!!!!!
1967;Nyerere akafikiri akitaifisha biashara na mashamba ndipo serikali itawea kudhibiti na kusimamia uchumi,kumbe uchumi ukazidi kuporomoka.
Mpaka kufikia mwaka 1975,nchi ilikuwa taabani,mpaka akataka kung'atuka lakini,makada ndani ya chama wakamshawishi Nyerere aendelee.
kipindi chote hiki alikuwa anawafadhilli wapigania uhuru na wakimbizi wa kisiasa kutoka nchi majirani,pamoja na kufanya jitihada za kumrudisha Obote madarakani,kwa bahati mbaya vita vya Uganda vikadhoofisha uchumi wa Tz+sera zilizoshindwa kusimamia uchumi.Miaka ya 80,hali ya uchumi ikawa ngumu sana,mashirika mengi yakawa taabani na upungufu wa bidhaa ukawa mkubwa.!!!
Serikali ya Nyerere ilikuwa imewapeleka wanajeshi vijana kusoma nje ya nchi( Kanada na U.K) ,na unavyojua msomi yeyote anapenda kufanyia kazi alichokisomea;ukizingatia kule walikuwa wanakutana na WaNIGERIA ambao walikuwa classmates wenzao walikuwa wakirudi kwao wanafanya Mapinduzi pindi serikali inapokuwa imeshindwa kulinda katiba na kusimamia Utawala bora.
Wengi walioshiriki ktk jaribio lile la mapinduzi mwaka 1982 walikuwa ni wale waliokuwa wamesoma nje,kwani ipo Mapinduzi ya kijeshi ipo kwenye syllabus ya msomo ya jeshi.Kipindi hiki na hapo Kenya vilevile Moi alikumbana na jaribo la Mapinduzi.!!!
Jaribio hili,lilimfanya Nyerere ajitathimini upya(uamuzi wa kung'atuka) na ukizingatia kwa wakati huo alikuwa ametoka katika vita,takwimu za uchumi zilikuwa zinaporomoka,fedha ya kigeni ilikuwa imepungua.!!!
Mara madogo wakateka ndege ya ATC.!!!,yaaani ilikuwa kama,kiongozi wa nchi hakuna kilichokuwa kinakwenda sawa.
Nafikiri utakuwa umepata baadhi ya sababu ya kutaka kufanyika kwa Jaribio la Mapinduzi.!!!!!!Kuna habari nimewahi kusoma sikumbuki chanzo chake kwa sasa, inazungumzia kuhusu kuporomoka kwa uchumi kwa sababu kama vita ulivyoelezea hapo juu,kuangushwa kwa ucommunist ikapelekea kuwa sehemu ambapo nchi ingeweza kupata msaada ni IMF NA WB.
Kwa maana hiyo ingempasa Nyerere kufuata masharti ya IMF na WB kitu ambacho kilikuwa kinyume kabisa na sera zake.... na isingekuwa rahisi kwake kuanza kuimba wimbo mpya hivyo akaamua kung'atuka.
Na kwa mtazamo wangu kinachonifanya niamini hiki ni kwamba alipotoka madarakani aliweka kautaratibu ka kuingilia utendaji pamoja na kuchagua viongozi anaowataka yeye ikiimanisha kuna mambo bado alitaka yawe anavyotaka yeye kitu ambacho kama angeweza angefanya akiwa bado madarakani.Haikusemwa wazi wazi lakini inaonekana kuna hiden pressure nyuma ya kung'atuka kwake.
Ningekuelewa ulichokisema hapa kama Mwalimu Nyerere angeachia madaraka 1980. Lakini aliondoka madarakani 1985 (na alimkemea bwana mmoja alietaka aendelee - and with what later happened I wish he did). Sasa kama aliondoka madarakani kipindi hicho, conspiracy ya WB na IMF inatokea wapi?
Kwanini watu hawazungumzii jaribio la Mwaka 1982 wanajadili lisilokuwepo kwenye mada?
Mwaka huo nilikuwa nyoka,nikiona kipira cha polisi nilikuwa sina amani kabisa walikuwa wakiibuka na maswali yao lazima utoe ushirikiano kujibu maswali na muda si mrefu wanaondoka na watu,ingawa njaa yanga miaka michache baadaye nilikuwa nikiuza unga kwa kopo babake.Watu walikuwa akigombea kama daladala dar leo au foleni za maji ubungo.Mafisadi wa enzi walikuwa lupango wakati familia zao zikiunga mstari kununua unga.Mafuta ya Amarica walinunua wakati baba zao walikuwa wamefukia Ardhini,na kwenye mapango mtoni.
Ndahani,JokaKuu, you must be of the same generation...inawezekana natakiwa kusema shikamoo maana hizo details, mhhh!
Sio kama alikwenda Msumbiji kama Mwambata wa Jeshi?NB:
..Musuguri na Mwakalindile waliendelea kuongoza JWTZ mpaka wakati wa Raisi Ali Hassan Mwinyi.
..nadhani[sina uhakika] baada ya kutoka jeshini Mwakalindile aliteuliwa kuwa balozi Msumbiji.
Hivi historia hutengenezwa au hujitengeneza?
Mheshimiwa kama unakijua kitu na kipo akilini mwako huku ukizima wanaotaka kujua kwakuwaita hawajii huo ni uhaini wa fikra huru!
Unadiriki kuzorotesha machipuzi huru bila kusadifu kilicho chema cha kichwani mwako!
inafaa kuandika kitabu cha matukio haya. Kwani kuna sheria inakataza
Duuh, hizi twist and turns za hii debate,unaweza jistukia umerun mentoKunaUfisadi zaidi ya kabla kuondoka kwake madarakani akachoma moto na kuiteketeza kabisa benki kuu? au hulijui hilo?
Sasa unanilaumu mimi wakati Mwingereza ndio aliweka hiyo sheria! Unasikitisha sana kama hutaki kujuwa ulikotoka, wewe utakuwa ni zao lilelile la Wabaguzi wa Ujinga.
Ni wapi dini ya mtu ilidharauliwa?
Ndahani,
..LOL!!
..of which generation?? Hingo Ilogi's generation, or Zacharia Hans Pope's generation?
..kuna kitabu kinachoongelea maasi ya Tanganyika Rifles. it is a very interesting book, na kinajibu maswali yote yaliyoulizwa hapa.
..pia nilifuatilia kesi ya uhaini miaka ya 80. waandishi waliokuwa wakiripoti kesi ile walifanya kazi nzuri sana.
Mwl wa genius than all muslims put together
teh teh teh...zomba, imagine I move around busy feeding my mind and brain those issues which you are so busy trying to portray as the sources of your own problems.... Do you know what you do to your own mind, especially subconscious mind? white and Arab boys used to rule us back then...what a waste of energy and time!!!
Kuasi kule kwa Wanajeshi Januari/20/1964 (Tanganyika Rifles) wala sio jambo la zamani sana kiasi cha kusema kwamba Historia ile imetupwa na hakuna anayesema ukweli,nilikuwa nahisi Viongozi kama Mwalimu,kawawa na Kambona wangeyaweka katika maandishi mambo yale muhimu ktk Historia ya Nchi yetu kabla hawajatutoka.Hakuna mahali mambo haya yameandikwa na ndio maana Vijana wanaotaka kujua historia ya Nchi yao wanakuja na hizi hear/say
Askari wale wa Tanganyika Rifles waliasi...Miongoni mwa mambo waliyokuwa wanadai ni hali nzuri ya maisha ya askari mtanganyika,mshahara ulikuwa mdogo,hawakupandishwa vyeo na hakukuwa na Watanganyika katika vyeo vya juu ndani ya Jeshi lile.Askari waliasi na kuingia mjini,na wengine walikwenda kwenye Makazi ya Maafisa wa kiingereza (Raia) na kuwashikilia.Waziri wa Ulinzi wakati huo alikuwa Oscar Kambona....Mwalimu na Mzee Kawawa kwa usalama wao walitoroshwa na kwenda kujificha,inasemekana Maficho yao yalikuwa Kigamboni.Waziri wa Ulinzi (Kambona) alijaribu kupita ktk Barracks na kuwaomba askari watulie bila mafanikio.
Hali ile iliendelea kuwa mbaya,na Mwalimu kwa ushauri wa Kambona na Kawawa akaomba msaada kwa Uingereza ili waje waokoe hali ile ambayo ilikuwa inaelekea kuwa mbaya,kufuatia kuasi kwa Askari wetu,askari wa Kenya na Uganda nao waliasi kwa sababu sawa kabisa na za UASI wa Tanganyika Rifles.Malkia alituma kikosi maalumu cha Askari wa Uingereza ambao walikuwepo ktk ghuba ya Aden,Askari hao walikuja na Meli kubwa ya kivita HMS Centaur ambayo ilikuwa na Makomandoo (45 RM),askari na helikopta.Walifanikiwa kutuliza maasi yale,na Mwalimu na Kawawa wakatoka mafichoni na kuonekana hadharani wakiwa na Waziri wa Ulinzi,ambaye alifanya kazi kubwa bila mafanikio kuwaomba askari(Waliokuwa wananuheshimu sana) waache uasi na madai yao yatafanyiwa kazi.Ukitaka kupata mambo mengi kuhusu maasi yale pitia kitabu "Dar Mutiny Of 1964" by Christopher MacRae