Jaribio la kutaka kuiangusha serikali ya Nyerere 1982/1983

Jaribio la kutaka kuiangusha serikali ya Nyerere 1982/1983

Mentality hizo za kudhgarau dini za wengine zinawaletea wote wanaoziendekeza ugonjwa wa mtindio wa ubongo...achana nazo bwana wewe.Hazijawahi kumlipa yeyete anayezifanya na hazitakaa kufanya hivyo. Don't waste your precious time!

Sasa unanilaumu mimi wakati Mwingereza ndio aliweka hiyo sheria! Unasikitisha sana kama hutaki kujuwa ulikotoka, wewe utakuwa ni zao lilelile la Wabaguzi wa Ujinga.

Ni wapi dini ya mtu ilidharauliwa?
 
Watawala wengi wa kiafrika walipewa utawala,na kurithi mifumo na wat;umishi waliokuwa wanafanya kazi serikali za Wazungu.kwa hiyo wafanyakazi walikuwa wanawadharau watawala wapya wa kiafrika ambao walikuwa ni wanasiasa waliozungukwa na watu wasio wasomi.

1961;unakabidhiwa nchi,majeshi,wafanyakazi na wizara kama ilivyokuwa chini ya mkoloni.:
1964;wanajeshi walikuwa wanataka vilevile na wao wajikomboe na amri na makamanda wakigeni waliokuwa bado wapo nadani ya majeshi,hali hii ilikuwa inasumbu nchi nyingi za afrika,na baadhi ya wafrika walikuwa baado wanawatukuza wakoloni.

Kipindi hiki J.K.Nyerere,akaamuwa kuwapa madaraka makada wa TANU,chama tawala nafasi zote muhimu na wanajeshi wapewa madaraka ya juu ili kutuliza manung'uniko;lakini kuanzia hapo mpaka leo Tz imeporomoka kwa kila kitu.!!!!!
1967;Nyerere akafikiri akitaifisha biashara na mashamba ndipo serikali itawea kudhibiti na kusimamia uchumi,kumbe uchumi ukazidi kuporomoka.

Mpaka kufikia mwaka 1975,nchi ilikuwa taabani,mpaka akataka kung'atuka lakini,makada ndani ya chama wakamshawishi Nyerere aendelee.

kipindi chote hiki alikuwa anawafadhilli wapigania uhuru na wakimbizi wa kisiasa kutoka nchi majirani,pamoja na kufanya jitihada za kumrudisha Obote madarakani,kwa bahati mbaya vita vya Uganda vikadhoofisha uchumi wa Tz+sera zilizoshindwa kusimamia uchumi.Miaka ya 80,hali ya uchumi ikawa ngumu sana,mashirika mengi yakawa taabani na upungufu wa bidhaa ukawa mkubwa.!!!

Serikali ya Nyerere ilikuwa imewapeleka wanajeshi vijana kusoma nje ya nchi( Kanada na U.K) ,na unavyojua msomi yeyote anapenda kufanyia kazi alichokisomea;ukizingatia kule walikuwa wanakutana na WaNIGERIA ambao walikuwa classmates wenzao walikuwa wakirudi kwao wanafanya Mapinduzi pindi serikali inapokuwa imeshindwa kulinda katiba na kusimamia Utawala bora.

Wengi walioshiriki ktk jaribio lile la mapinduzi mwaka 1982 walikuwa ni wale waliokuwa wamesoma nje,kwani ipo Mapinduzi ya kijeshi ipo kwenye syllabus ya msomo ya jeshi.Kipindi hiki na hapo Kenya vilevile Moi alikumbana na jaribo la Mapinduzi.!!!

Jaribio hili,lilimfanya Nyerere ajitathimini upya(uamuzi wa kung'atuka) na ukizingatia kwa wakati huo alikuwa ametoka katika vita,takwimu za uchumi zilikuwa zinaporomoka,fedha ya kigeni ilikuwa imepungua.!!!

Mara madogo wakateka ndege ya ATC.!!!,yaaani ilikuwa kama,kiongozi wa nchi hakuna kilichokuwa kinakwenda sawa.

Nafikiri utakuwa umepata baadhi ya sababu ya kutaka kufanyika kwa Jaribio la Mapinduzi.!!!!!!
Kuna habari nimewahi kusoma sikumbuki chanzo chake kwa sasa, inazungumzia kuhusu kuporomoka kwa uchumi kwa sababu kama vita ulivyoelezea hapo juu,kuangushwa kwa ucommunist ikapelekea kuwa sehemu ambapo nchi ingeweza kupata msaada ni IMF NA WB.

Kwa maana hiyo ingempasa Nyerere kufuata masharti ya IMF na WB kitu ambacho kilikuwa kinyume kabisa na sera zake.... na isingekuwa rahisi kwake kuanza kuimba wimbo mpya hivyo akaamua kung'atuka.

Na kwa mtazamo wangu kinachonifanya niamini hiki ni kwamba alipotoka madarakani aliweka kautaratibu ka kuingilia utendaji pamoja na kuchagua viongozi anaowataka yeye ikiimanisha kuna mambo bado alitaka yawe anavyotaka yeye kitu ambacho kama angeweza angefanya akiwa bado madarakani.Haikusemwa wazi wazi lakini inaonekana kuna hiden pressure nyuma ya kung'atuka kwake.

Ningekuelewa ulichokisema hapa kama Mwalimu Nyerere angeachia madaraka 1980. Lakini aliondoka madarakani 1985 (na alimkemea bwana mmoja alietaka aendelee - and with what later happened I wish he did). Sasa kama aliondoka madarakani kipindi hicho, conspiracy ya WB na IMF inatokea wapi?
 
Kwanini watu hawazungumzii jaribio la Mwaka 1982 wanajadili lisilokuwepo kwenye mada?
 
Ahsante mkuu marcos kwa post hii #157 :
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...serikali-ya-nyerere-1982-a-8.html#post4971387

Kwa haraka between line na ufahamu wa mambo mengine yanayomzunguka Nyerere na waingereza na sababu ya wao kumuamini ktk suala la uongozi ni wazi waingereza walimsaidia mwalimu haraka kwa sababu hizi:

1.Ili kuwaokoa raia wake wakiokuwa wakifanya kazi ya hand over na espionage.Ila haikuwa rahisi kuwaokoa bila kuzima uasi.

2.Hawakuwa wamekabidhi taifa rasmi likiwa linajitegemea,na hivyo walikuwa liable kwa hayo.

3.pamoja na kwamba walikuwa a shida na Mitizamo ya Nyerere bado hawakua na mtu anayeaminika kwa kauli na maetndo kama Nyerere.Nyerere hakuwa threat kwa mtu kwa vile hakuna mchokozi kwa ustaarabu wa magharibi au hata mashariki,


Pia mwalimu kuamua meza jeuri yake mbele ya mabeberu huku akijifanyia mzaha,inaonyesha jinsi gani alikuwa kiongozi safi,jasiri na clever.hakuona ni kitu kigumu ingawa bado alikuwa na jeuri ya kusem abila bila jinyenyekeza(au kujipendekeza).

Pia kinachoonekana ni Mgogoro mkubwa uliopo kati ya agha khan na tanzania kwa ujumla, alichohofia Nyerere kuhusu Agha khan,kunaonekana pia kuwa Hilo gazeti lilishaonyesha kuwa silaha baada ya hawa jamaa kushidnwa kupitia Jumuia ya Kiislam ya Africa mashariki,na pengine pia nao walishiriki kwa hilo.

Kwa mwenendo uliopo ni wazi agha khan wana agenda ya siri na hii nchi kwani tayari wameshashika vitu vingi sana hapa nchini,kuanzia ktk korosho,kahawa, mahoteli, hospital na vituo vya afya, shule, na universities, wana NGOs chingi sana na miradi yake chini AKDN na wameshika kasi sana kipindi cha awamu hii.Sasa wanachukua mashamba yao waliyoachia watu enzi hizo wamiliki kwa niaba yao.

Picture inakuwa clear taratibu.
 
Kwanini watu hawazungumzii jaribio la Mwaka 1982 wanajadili lisilokuwepo kwenye mada?

Mwaka huo nilikuwa nyoka,nikiona kipira cha polisi nilikuwa sina amani kabisa walikuwa wakiibuka na maswali yao lazima utoe ushirikiano kujibu maswali na muda si mrefu wanaondoka na watu,ingawa njaa yanga miaka michache baadaye nilikuwa nikiuza unga kwa kopo babake.Watu walikuwa akigombea kama daladala dar leo au foleni za maji ubungo.Mafisadi wa enzi walikuwa lupango wakati familia zao zikiunga mstari kununua unga.Mafuta ya Amarica walinunua wakati baba zao walikuwa wamefukia Ardhini,na kwenye mapango mtoni.
 
Mwaka huo nilikuwa nyoka,nikiona kipira cha polisi nilikuwa sina amani kabisa walikuwa wakiibuka na maswali yao lazima utoe ushirikiano kujibu maswali na muda si mrefu wanaondoka na watu,ingawa njaa yanga miaka michache baadaye nilikuwa nikiuza unga kwa kopo babake.Watu walikuwa akigombea kama daladala dar leo au foleni za maji ubungo.Mafisadi wa enzi walikuwa lupango wakati familia zao zikiunga mstari kununua unga.Mafuta ya Amarica walinunua wakati baba zao walikuwa wamefukia Ardhini,na kwenye mapango mtoni.

Umenikumbusha historia za unga wa yanga!

Unajua nchi ilikuwa ndio inatoka bitani hivyo uchumi ulidhoofu ilihali!
 
Mzawa Halisi, Kibunango,

..nadhani wakati wa jaribio la mwaka 80, Maj.Gen.Mwakalindile alikuwa Chief of Staff.

..mimi hii kesi niliifuatilia kupitia magazeti yaliyokuwa yanaripoti kesi hiyo ilipofika mahakama kuu.

..inasemekana hawa jamaa walijaribu kum-rectruit Maj.Gen.Silas Mayunga kwa kumtumia askari mmoja aliyekuwa karibu naye ambaye alikuwa stationed Zanzibar.

..it is a long time now kukumbuka kila kitu, lakini nadhani huyo jamaa wa Zanzibar ni mmoja kati wa watu walioripoti mpango mzima kwenye vyombo vya usalama.

..kuna ushahidi ulitolewa na Brig.Gen Juma Pongwe[r.i.p], na askari mmoja anaitwa Balarti. I wish ningepata nafasi kuusoma tena.


NB:

..Musuguri na Mwakalindile waliendelea kuongoza JWTZ mpaka wakati wa Raisi Ali Hassan Mwinyi.

..nadhani[sina uhakika] baada ya kutoka jeshini Mwakalindile aliteuliwa kuwa balozi Msumbiji.
 
JokaKuu, you must be of the same generation...inawezekana natakiwa kusema shikamoo maana hizo details, mhhh!
Ndahani,

..LOL!!

..of which generation?? Hingo Ilogi's generation, or Zacharia Hans Pope's generation?

..kuna kitabu kinachoongelea maasi ya Tanganyika Rifles. it is a very interesting book, na kinajibu maswali yote yaliyoulizwa hapa.

..pia nilifuatilia kesi ya uhaini miaka ya 80. waandishi waliokuwa wakiripoti kesi ile walifanya kazi nzuri sana.
 
Last edited by a moderator:
NB:

..Musuguri na Mwakalindile waliendelea kuongoza JWTZ mpaka wakati wa Raisi Ali Hassan Mwinyi.

..nadhani[sina uhakika] baada ya kutoka jeshini Mwakalindile aliteuliwa kuwa balozi Msumbiji.
Sio kama alikwenda Msumbiji kama Mwambata wa Jeshi?
 
Hivi historia hutengenezwa au hujitengeneza?

Mheshimiwa kama unakijua kitu na kipo akilini mwako huku ukizima wanaotaka kujua kwakuwaita hawajii huo ni uhaini wa fikra huru!

Unadiriki kuzorotesha machipuzi huru bila kusadifu kilicho chema cha kichwani mwako!

inafaa kuandika kitabu cha matukio haya. Kwani kuna sheria inakataza
 
Kuna kitabu fulani kinaitwa uhaini kinaelezea kesi ilivyokuwa kwa watu hawa miaka ya 80 sidhani kama kitabu hicho kipo sokoni!
 
Hii mada ni jaribio la miaka 80 lakini watu wanaongelea jaribio la miaka ya 60.
 
Sasa unanilaumu mimi wakati Mwingereza ndio aliweka hiyo sheria! Unasikitisha sana kama hutaki kujuwa ulikotoka, wewe utakuwa ni zao lilelile la Wabaguzi wa Ujinga.

Ni wapi dini ya mtu ilidharauliwa?

teh teh teh...zomba, imagine I move around busy feeding my mind and brain those issues which you are so busy trying to portray as the sources of your own problems.... Do you know what you do to your own mind, especially subconscious mind? white and Arab boys used to rule us back then...what a waste of energy and time!!!
 
Ndahani,

..LOL!!

..of which generation?? Hingo Ilogi's generation, or Zacharia Hans Pope's generation?

..kuna kitabu kinachoongelea maasi ya Tanganyika Rifles. it is a very interesting book, na kinajibu maswali yote yaliyoulizwa hapa.

..pia nilifuatilia kesi ya uhaini miaka ya 80. waandishi waliokuwa wakiripoti kesi ile walifanya kazi nzuri sana.


I was too young to remember everything...but worth sharing the story maana siku hizi longo longo zimezidi utafikiri kuna watu watakaa milele kwenye ofiosi za umma walizopo.
 
teh teh teh...zomba, imagine I move around busy feeding my mind and brain those issues which you are so busy trying to portray as the sources of your own problems.... Do you know what you do to your own mind, especially subconscious mind? white and Arab boys used to rule us back then...what a waste of energy and time!!!

Never a problem of mine could be depicted to others. We had a problematic leader, highly. Believe you me, he was insane. Family heritage.
Who can deny that? not even Andrew
 
Last edited by a moderator:
Kuasi kule kwa Wanajeshi Januari/20/1964 (Tanganyika Rifles) wala sio jambo la zamani sana kiasi cha kusema kwamba Historia ile imetupwa na hakuna anayesema ukweli,nilikuwa nahisi Viongozi kama Mwalimu,kawawa na Kambona wangeyaweka katika maandishi mambo yale muhimu ktk Historia ya Nchi yetu kabla hawajatutoka.Hakuna mahali mambo haya yameandikwa na ndio maana Vijana wanaotaka kujua historia ya Nchi yao wanakuja na hizi hear/say

Askari wale wa Tanganyika Rifles waliasi...Miongoni mwa mambo waliyokuwa wanadai ni hali nzuri ya maisha ya askari mtanganyika,mshahara ulikuwa mdogo,hawakupandishwa vyeo na hakukuwa na Watanganyika katika vyeo vya juu ndani ya Jeshi lile.Askari waliasi na kuingia mjini,na wengine walikwenda kwenye Makazi ya Maafisa wa kiingereza (Raia) na kuwashikilia.Waziri wa Ulinzi wakati huo alikuwa Oscar Kambona....Mwalimu na Mzee Kawawa kwa usalama wao walitoroshwa na kwenda kujificha,inasemekana Maficho yao yalikuwa Kigamboni.Waziri wa Ulinzi (Kambona) alijaribu kupita ktk Barracks na kuwaomba askari watulie bila mafanikio.

Hali ile iliendelea kuwa mbaya,na Mwalimu kwa ushauri wa Kambona na Kawawa akaomba msaada kwa Uingereza ili waje waokoe hali ile ambayo ilikuwa inaelekea kuwa mbaya,kufuatia kuasi kwa Askari wetu,askari wa Kenya na Uganda nao waliasi kwa sababu sawa kabisa na za UASI wa Tanganyika Rifles.Malkia alituma kikosi maalumu cha Askari wa Uingereza ambao walikuwepo ktk ghuba ya Aden,Askari hao walikuja na Meli kubwa ya kivita HMS Centaur ambayo ilikuwa na Makomandoo (45 RM),askari na helikopta.Walifanikiwa kutuliza maasi yale,na Mwalimu na Kawawa wakatoka mafichoni na kuonekana hadharani wakiwa na Waziri wa Ulinzi,ambaye alifanya kazi kubwa bila mafanikio kuwaomba askari(Waliokuwa wananuheshimu sana) waache uasi na madai yao yatafanyiwa kazi.Ukitaka kupata mambo mengi kuhusu maasi yale pitia kitabu "Dar Mutiny Of 1964" by Christopher MacRae

Mkuu mimi huwa siamini kama askali waasi walikuwa na nia ya kumdhulu Mwalimu, shida yao ilikuwa ni maslahi tu na vyeo - lakini wabaya wa Kambona walimgeuzia kibao na kutaka kumuhushisha na na ghasia hizo, alafu si kweli kusema Kambona alikuwa hajuhi kwamba Kawawa na Mwalimu walikuwa wamejificha kwa mzee mmoja huko Kigamboni; mtu aliye wapeleka huko ni the late Mzena ambaye alikuwa mkuu wa Usalama wa Taifa kama sikosei.

Kambona ali-play a pivotal role kujaribu ku-contain wanajeshi hao at his own risk, nikisikia watu wana muhusisha na mutiny hiyo, basi huwa nasema kwamba kumbe fitina katika Taifa letu haijahanza leo - kama Kambona angekuwa na nia ya kumugehuka Mwalimu basi angetumia mwanya huo kufanya lolote maana Wanajeshi walikuwa wana msikiliza sana Kambona lakini alibakia kuwa royal kwa Mwalimu mpaka alipo toka mafichoni.
 
Mkuu Yericko,huyu Meja Gen Hans Popi ndiye yule Zakariah Hans Pope ambaye ni kiongozi wa lile kundi la Friend of Simba na mwnyekiti wa kamati ya usajili ya Simba Sports Club?
 
Back
Top Bottom