Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Mleta mada umenikumbusha utotoni, wakati kesi ikiungurama pale mahakama kuu, sisi tukiwa watoto wa shule ya msingi, tulikuwa tunavizia ifike saa tisa ili tuwaone wale wahaini wakipandishwa kwenye karandinga baada ya siku moja ya kesi kumalizika. Tulikuwa tunakaa upande wa pili wa mahakama kuu, tunavunga kama vile tunaifaidi ile view ya bahari pamoja na kuangalia meli zinavyoingia kumbe lengo letu tuwaone wahaini.
Wakishaingizwa kwenye karandinga ndio sisi taratibu tunarudi nyumbani. Usalama wa nchi ulikuwa kazini enzi zile, ulikuwa huwezi kuongeongea hovyo kama watu wanavyofanya siku hizi.
Huyo wakili Lakha alikuwa mhindi, kichwa fulani cha ukweli.