Ni Januari 9 , 1982 siku ya Mapinduzi ambayo kamwe hayakufanikiwa matokeo yake. Akiwa katika gereza la Butimba lenye ulinzi wa hali ya juu, utaratibu wa mahabusu na wafungwa akiwemo Eugene Maganga kwa miaka miwili ulikuwa ni kuamka mapema mwishoni mwa wiki. Kwa sababu fulani hata hivyo, Jumamosi asubuhi ya Oktoba 22, 1995 aliamkamapema na alipowasha radio yake ndogo ulikuwa wakati muafaka kwake kupata taarifa fupi zikisema kwamba Rais Ali Hassan Mwinyi alitoa msamaha kwa wafungwa akiwemo yeye pamoja na wafungwa wengine wengi. Huu ni wakati ambapo kundi la watu wanane walikuwa wakiusubiri, kwa miaka kumi ambayo wamekuwa kifungoni wakitumikia kifungo cha maisha kwa uhaini.Kamwe hawakuweza kupoteza matumaini. " Wafungwa katika jela mbalimbali ambao pia walisikia habari hizi walianza kushangilia ,"anasimulia Maganga." Cha kushangaza sikufurahia kwa sababu nilikuwa naisubiri siku kama hii kwa muda mrefu. Mara zote ilikuwa inatisha kufikiria kuwa ningeweza kutumia maisha yangu yote gerezani. "
Maganga na watu wengine saba - Suleiman Kamando , Zakaria Aspopo , Vitalis Mapunda, Mbogolo, Kajaji Badru, Hatty MacGhee na Christopher Kadego walitiwa hatiani mwaka 1985 kwa ajili ya mpango uliopangwa miaka miwili iliyopita kuipindua serikali ya Rais wa kwanza nchini Julius Nyerere. mtu wa tisa, Mohamed Tamimu aliuwawa katika mapambano ya risasi na polisi wakati wa kukamatwa kwao.
Siku ya Jumatatu Oktoba 24, 1995, siku mbili baada ya habari kufika kwenye redio, Maganga alitangazwa kuwa mtu huru. Anakumbuka vizuri siku hiyo alipovuka milango ya gereza kwa uhuru. Ilikuwa ni majira ya saa saba mchama. "Tulikaribishwa nje ya gereza na ndugu zangu wenye furaha pamoja na wale wa mfungwa mwenzangu Hatty MacGhee . Hisia zangu zilikuwa juu kiasi kwamba ni vigumu sana kuelezea kwa sasa ," anasema Maganga. Wafungwa wengine sita wa uhaini waliachiwa siku mbili baadae kutoka Gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam. Wakati wa kutolewa kwao, Maganga alikuwa amezungushwa katika magereza kadhaa ikiwa ni pamoja na Ukonga jijini Dar es Salaam na sehemu yake ya mwisho ilikuwa Butimba jijini Mwanza. Licha ya matatizo waliyovumilia gerezani, Maganga anasema hakuna hata mmoja wao aliyewahi kujuta kwa kujaribu kuipindua serikali. "Tunajutia tu kushindwa mapinduzi lakini hatujutii kupanga mapinduzi".
Kabla ya wao kuja na wazo la kuipindua serikali, Maganga na Kadego walifanya kazi katika jeshi kwenye kikosi cha mizinga . Maganga alikuwa Luteni wakati Kadego alikuwa kapteni. Maganga alikuwa na umri wa miaka 26 na alikuwa ndio kwanza amerudi kutoka London ambapo alitumia miezi minne kuongeza ujuzi wake wa kijeshi kabla ya kuitwa kwenda kupambana katika vita vya Uganda mwaka 1978. Kama mmojawapo wa askari waliokuwa mstari wa mbele, Maganga anaamini Tanzania ilishinda vita kwa sababu Uganda ilikuwa na jeshi dhaifu. Lakini hawezi kusamehe misingi ambayo vita ilijengwa . "Rais Nyerere alitumia vibaya rasilimali za nchi kupigania maslahi ya rafiki yake wa karibu Milton Obote ili aweze kurudi madarakani". Endapo sababu za kutoelewana zilizosababisha vita zilikuwa za msingi, Maganga anasema diplomasia ingesaidia kutatua tatizo kirafiki. Badala yake walipendelea kampeni ya kijeshi. Mara baada ya vita hii , Mei 1980, Maganga alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kujifunza Uhusiano wa Kimataifa na Utawala wa Umma . Kamwe hakuwa na furaha kutokana na aina ya maisha ambayo Watanzania walikuwa wakiishi, anasema walikuwa maskini na walikuwa wakilazimishwa kuishi katika vijiji vya Ujamaa .
Kundi hili lilijenga hoja kwamba vita kati ya nchi hizo mbili ilikuwa si lazima na ilisababisha matumizi mabaya ya fedha za umma. "Vita haikuwa kati ya nchi mbili bali ilikuwa ni kati ya Nyerere na Idi Amin".
Maganga anaeleza zaidi kuwa pia walilichukulia suala la hali ya hamasa katika jeshi ambayo ilikuwa imeshuka hasa baada ya Meja Jenerali Mrisho Sarakikya Mkuu wa kwanza wa Majeshi ya Ulinzi (1964-1974) na timu yake kujiuzulu. Wapangaji wa mapinduzi pia walihisi kuwa Rais alikosa imani kwa watu wa kaskazini kwasababu walikuwa wame elimika nje ya nchi hivyo aliogopa kuwa wangejaribu kumpindua.“ Watu ambao walikuwa na elimu ndogo walichukua nafasi za juu na hapo ndipo mambo yalipoenda vibaya,”, anasema Maganga. Askari hawakupandishwa vyeo kutokana na sifa kwa kuwa Rais alikuwa na nia ya kujenga jeshi lenye watu ambao hawakuweza kuleta changamoto yoyote dhidi yake. Anasema baadhi ya maafisa walipandishwa mara mbili kwa juma moja. “Sisi tulitaka kuleta mabadiliko lakini aina ya watu tuliotaka kufanya nao kazi hawakuwa tayari kujitolea . Hata hivyo, sisi hatukukata tamaa juu ya nia yetu ya kuleta mabadiliko”. Wakiwa bado wanajadili jinsi ya kukamilisha mipango yao, Maganga na wenzake, walikutana na marehemu Pius Rugangira (Uncle Tom) ambaye alikuwa mfanyabiashara wa Tanzania aliyejiimarisha nchini Kenya.
Baba yake Rugangira hakuwa na uhusiano mzuri na Rais Nyerere, kwamujibu wa Maganga, naye alikuwa amekwenda kuishi na kufanyakazi nchini Uganda. Na kwasababu yakuwa Uganda, Rugangira alishtakiwa kuwampelele zitoka Uganda, shutuma ambazo zilisababisha mtafaruku na serikali. Kwaujumla, yeye pia aliona kuwa Watanzania hawakustahili kulipa bei ya vita iliyopangwa na ndio sababu aliamua kuwasikiliza wapangamapinduzi. Rugangira alijitolea kugharamia shughuli zao, Maganga na maafisa wengine wa jeshi ambao waliokubaliana kufanya kazi pamoja, walianza kupata matumaini. "Sisi wote tulikuwa vijana na hatukuwa na imani yeyote na afisa wa cheo cha juu jeshini kwa sababu walikuwa wameridhika na jinsi mambo yalivyokuwa". Ingawa kuna ukimya kuhusu mipango yao ya mapinduzi ya kijeshi, Maganga anasita kuonyesha wazi jinsi walivyokuwa wamepanga kutekeleza mpango wao. Anasema tu kuwa bado hiyo "ni siri" ingawa walitarajia kutumia uzembe uliokuwepo jeshini ili kufikia malengo yao .
Mpanga mapinduzi mwingine ambaye alikuwa katika kundi la Maganga wakati wa mahojiano lakini hakutaka jina lake litajwe, anasema watu wengi wanaamini kundi lilipewa fedha nyingi kufanya mapinduzi lakini kwa kweli fedha kidogo walizopata kutoka kwa Rugangira zilikuwa kwa maana tu ya kushughulikia dharura ndogo. Anasisitiza haikuwa fidia kwa ajili ya kufanya mapinduzi . "Kama sisi tulililipwa fedha , hakuna hata mmoja wetu ambaye angekuwa maskini leo". anasema. Askari mmoja mstaafu anaongeza kwamba walitaka kujenga demokrasia ya vyama vingi ambayo watu wangekuwa na uhuru wa kutoa maoni yao na kuchagua rais wao wenyewe . "Tulitoa mapendekezo kwamba Rugangira angekuwa Waziri Mkuu lakini kwa sharti kwamba asingegombea urais katika uchaguzi ambao ungefanyika baada ya miaka mitano baadaye". Siku tatu kabla ya mapinduzi yaliyopangwa hayajafanyika , Rugangira aliripotiwa kuwauliza kuwa walitaka wapewe nafasi gani katika serikali mpya lakini walijibu kuwa hawataki chochote.
Wakati mipango yote ilipokuwa tayari ,walisubiri kuwasili kwa rais ambaye alikuwa katika ziara nje ya nchi. Kwa mujibu wa Maganga, rais alirudi Januari 1982 baada ya kukaa miezi miwili nje na akaenda kijiji nyumbani kwake Butiama ."Sababu ya kutaka kuipindua serikali wakati yeye akiwa nchini ni kwamba tulikuwa na nia ya kumuua". Maganga anasema. Alikuwa Rugangira aliyepinga mpango huo na badala yake alipendekeza kumkamata rais. Nyerere bila kutarajia alitumia muda mwingi akiwa Butiama na alikuwa bado kurudi Dar es Salaam siku mbili kabla ya siku mapinduzi yalipopangwa ilikuwa siku ya Jumatatu Januari 9, 1982. Ijumaa kabla yake Januari 6, waalikuwa wamepanga kukutana kwa mara ya mwisho kabla ya mapinduzi kufanyika lakini baadhi ya wenzao hawakutokea kwenye mkutano. Mohamed Tamimu alikuwa miongoni mwa wale ambao hawakuja . "Tulikuwa na wasiwasi na tuliamua kutuma mmoja wetu Kinondoni Mkwajuni kuuliza lakini tulishtuka kuona kwamba polisi walikuwa wamevamia nyumba yake na aliuawa katika mapambano yaliyodumu saa mbili akifukuzwa kutoka uwanja wa Leaders, alipofika Kinondoni eneo maarufu la sinema (ubalozi wa Marekani leo) alizidiwa nguvu na kuuawa na kikosi cha majasusi kilichokuwa kikiongozwa na jasusi na mwanasheria nguli Mabere Nyaucho Marandu". anasema Maganga. Katika hatua hiyo, walijua utambulisho wao na mipango yao haikuwa siri tena. Tamimu, kwa mujibu wa wenzake, alikuwa na utamaduni wa kutunza kumbukumbu za mikutano na majina ya washirika. Ilikuwa ni suala la muda tu kabla hawajakamatwa.Tamimu alipangwa kuwa mdunguaji maalumu kwaajili ya kumuua rais Nyerere aliyekuwa akirejea toka nje ya nchi.
Hisia zao zilikuwasa hihi. Polisi walikuwa kila mahali kusaka kikundi. Kadego na Maganga waliamua kutoroka kupitia Tanga na Mombasa hadi Nairobi ambako walikaa kwa miezi kumi kama wakimbizi wa kisiasa. "Hatujui nini kilichotokea kwa watu wengine ambao tuliwaacha Dar es Salaam lakini hatukukata tamaa tulipofika Nairobi. Tulitaka kujipanga tena na kurudi kuipindua serikali , "anasema Maganga .
Kamwe hawakuweza kulaumiana wao kwa wao kwa kushindwa kufanya mapinduzi ingawa Maganga anaamini bahati yao iliondoka kwa sababu MacGhee alikuwa raia wa kawaida na hakujua jinsi ya kutunza siri . Anamtuhumu MacGhee kwa kuvujisha taarifa kwani karibu watu wote walijua kabla ya kukakimilka kwa mpango. Maganga pia anahisi kuwa Tamimu alijua kwamba MacGhee hakuwahi kuwa askari wa Marekani kama alivyokuwa akidai lakini hakuwaambia . " Tuligundua baadaye kwamba jina lake halisi alikuwa Hatibu Hassan Gandhi na alikuwa rubani wa Tanzania " Mjini Nairobi , hawakuwa na ajira na walikuwa wanaishi chini ya msaada wa Tume ya Umoja wa Mataifa kwa Wakimbizi. Maganga anasema walikuwa na baadhi ya mawasiliano na ubalozi wa Marekani mjini Nairobi ambako waliomba udhamini na kuanza msingi upya jijini Nairobi ambapo wangeweza kujipanga vizuri na kupanga kwa ajili ya mapinduzi mengine ."Walisema walikuwa na shughuli nyingi zinazofanana na wasingeweza kutuunga mkono". anasema.
Siku chache baadaye Maganga na Kadego wakizunguka katika mitaa ya Nairobi, ghafla waliingia kwa mpanga mapinduzi mwenzao Uncle Tom na MacGhee waliyekuwa wamemwacha Dar es Salaam . Wawili hao walikuwa wamekimbia toka gereza la Keko jijini Dar es Salaam ambako walikuwa wamewekwa baada ya kukamatwa kwao.
Ingawa walikuwa huru na maisha yao mjini Nairobi Rugangira aliamua kusafiri kwenda London kuangalia namna ya kuingia Malawi. Alikuwa na mashaka kuwa serikali jijini Nairobi na Dar es Salaam zinaweza kula njama na kuwakamata. Wote nane walikuwa kwa namna fulani wameweza kutoroka kwenda Nairobi.
Hakika, kabla Rugangira kurudi kutoka London, kundi hili lilikamatwa na mamlaka jijini Nairobi na kubadilishana na Senior Lance Koplo Ochuka na Sergeant Pancras Oteyo ambaye pia alifanya majaribio ya kuipindua serikali ya Rais Daniel Arap Moi mwaka 1982 na walikimbilia Tanzania .
"Tulifungwa sana pingu na kufunikwa macho na kupelekwa gereza la Isaka lenye ulinzi wa hali ya juu mjini Dodoma ambako tulikaa kuanzia Novemba 1983 hadi Oktoba 1984", anasema Maganga .
Juu ya kuwasili huko, walikuta kuta za mahabusu gerezani zimepakwa kinyesi. Walifungwa minyororo kwenye ardhi, walitumia siku tatu bila kuoga. Mkuu wa gereza aliagiza walinzi gerezani wasizungumze na wafungwa au hata kuwa karibu nao kwa kuogopa kwamba wafungwa wangejaribu kuwashawishi wasimamizi wa sheria na usala wa jela kujiunga pamoja nao na kutoroka. Maganga anasema hata hivyo watu waliokuwa wanawalinda hawakuwa wote wabaya na kuna wakati mmoja wao alisaidia wafungwa kusafirisha barua kwenda Ubalozi wa Marekani. Walitaka dunia ijue kwamba walikuwa jela kwa sababu hakuna mtu alikuwa anafahamu hili kwa wakati huo. Barua waliyokuwa wameandika, Maganga anasema, ilisababisha Kamishna wa Umoja wa Mataifa kwa Wakimbizi kutembelea Tanzania na kushinikizwa serikali kupeleka kesi mahakamani. Kesi ilianza Januari 1985 na Desemba ya mwaka huo na walihukumiwa kifungo cha maisha .
Wanasisitiza kwamba kimsingi hawajutii kuhusu kupanga njama ya mapinduzi, lakini Maganga anasema anakatishwa tamaa tu ni kwa namna maisha yao yalivyogeuka. Baada ya kuwekwa huru, waligundua kuwa baadhi ya marafiki na jamaa walikuwa wamegeuka kuwa maadui wao na hata kutotaka kuonekana karibu au pamoja nao. Wote Kadego na Maganga hawakuwahi kuoa na Maganga anasema sehemu ngumu sana labda si miaka kumi waliyotumikia jela lakini kuanza tena upya wakati hawana chochote. "Serikali ilihakikisha kwamba hatuwezi kupata ajira mahali popote na baadhi yetu walibaki bila ajira hadi leo hii, " anasema. Baadhi yao ambao familia zao zilikuwa bora wameweza kujipenyeza katika biashara. " Kadego na mimi tunaishi mkono kwa mdomo . Kwa kweli Kadego ni mmachinga , " Maganga anasema. MacGhee alikufa wiki moja baada ya kutolewa wakati baadhi wao walijaribu kujiunga na vyama vya upinzani lakini waliamua kuacha. Waliona vyama vilikuwa havijajipanga na watu ambao waliwaongoza walionekana wabinafsi. "Katika uchaguzi wa mwaka 1995, mimi niligombea kiti cha ubunge katika jimbo la uchaguzi Tabora lakini nilipoteza . Sitaki kujihusisha katika siasa tena, " Maganga anasema.
Maganga ana watoto wawili kutoka kwa mama tofauti na anasema hakuna mtu aliyejali kuwapeleka katika shule nzuri wakati alipokuwa jela. Yeye bado ana matumaini ya kuwapatia elimu nzuri lakini hana mapato, mipango yake imeanza kuonekana kama ndoto. Alijaribu kujiunga na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kujifunza Sheria mwaka 1999 lakini alishindwa kuendelea katika mwaka wake wa pili kutokana na ukosefu wa ada. "Si marafiki zangu wote wanajali kuhusu matatizo yangu. Baadhi hujaribu kunifikiria mimi wakiwa na kitu cha kunipa , "anasema. Pamoja namna mambo yalivyokwenda hivi sasa, yuko tayari kufanya kazi yoyotte anayoweza kupewa. Hata hivyo, maisha yake binafsi hayamsumbui kabisa kama vile kile anachokiita' mawazo ya Watanzania. "Wanalalamika karibu kila kitu lakini hakuna hata mmoja wao aliyewahi kuchukua hatua yoyote. Wanatoa lawama kwetu kwa kujaribu kuipindua serikali wakati wengi wao bila hata kuthubutu," anasema. Akasema alikuwa anaenda kulala usiku bila chakula chochote lakini hakuwa mnyonge, isingekuwa mara ya kwanza. Ni wakati yeye anasema, "Nchi hii ... Nyerere kapotosha mawazo ya watu . Watu wachache sana wanaweza kufikiri na kuchukua hatua, " kwa hiyo hujikatia tamaa, Maisha ya mbwa.
Wakiwa gerezani walipata taabu sana hasa kwa wafungwa wa kisiasa kama wao. Walikuwa hawaruhusiwi baadhi ya marupurupu ambayo walikuwa na haki kuyapata, na waliweza kushuhudia maovu kadhaa ambayo yaliishia chini ya paa za magereza . Maganga anakumbuka kushuhudia wafungwa vijana kulawitiwa . Kulikuwa na ndoa za jinsia moja, wachuuzi wa madawa ya kulevya na baadhi ya wafungwa waliweza hata kuandaa ‘mashindano ya urembo’ ambapo wanaume walionyeza mambo yao.
"Wafungwa waliosimamia wengine walilala na wale ambao walishinda mashindano ya urembo na wakawapa neema kidogo kama zawadi, kwa mfano, kuwatetea kutofanya kazi ngumu na kuruhusu kwao anasa ya kuoga kwa sabuni. Ilikuwa ni uzoefu mbaya na unaochukiza machukizo ambayo bado yanaendelea katika mawazo yangu , "anasema Maganga . Kabla ya kupelekwa gerezani Maganga anasema alidhani kuwa jela zilisimamiwa na maafisa ustawi lakini kwa mshangao wake hakukuwa na mtu yoyote katika magereza ambayo yeye aliwahi kutumikia adhabu yake.
Aidha, maafisa magereza waliwezesha uuzaji wa madawa ya kulevya katika magereza na hata walishiriki katika kuuzia wafungwa vijana wafungwa wengine. walinzi hawa pia walishuhudia wafungwa dhaifu wakibakwa na wafungwa wenye nguvu bila kujaribu kuingilia kwa namna yoyote .
Maganga hata hivyo ana furaha kwa mabadiliko madogo yeye na wenzake waliyoweza kuleta katika magereza yote waliowahi kutumikia . Pamoja na James Christopher mshirika wa karibu wa Kadego , walikuwa muhimu katika kuimarisha shughuli za michezo na kutetea haki za wafungwa wengine katika gereza la Ukonga . "Hatukuweza kamwe kumvumilia mtu yeyote ambaye alijaribu kukiuka haki za wengine” Kwa sababu ya jitihada zao za kuwatetea, baadhi ya wafungwa wenzao hawakusherehekea kutolewa kwao, kwani sasa wangeachwa na kujilinda wao wenyewe .
....................................................................
Makala hii inapatikana katika kitabu kiitwacho Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi kilichoandikwa na member mwenzetu hapa jf
Yericko Nyerere