Jaribio la kutaka kuiangusha serikali ya Nyerere 1982/1983

Jaribio la kutaka kuiangusha serikali ya Nyerere 1982/1983

nimewahi kusikia kama ishu ya kambona ilikuwa ya kupika?????? sijui ukweli anyway!

Hii ya 1982 ndio leo nimejuzwa! tatizo lilikuwa nini???

Mix with yours
 
Lingine: Kila Uchaguzi ukifanyika wakati huo japo alikuwa mgombea Pekee lakin idadi ya kura alizokuwa akipata zilikuwa Chahche kuliko chaguz zilizofata 1962 kabla ya kufuta Vyama vingi aligombea na Abbas Mtemvu (Baba wa Mbunge wa Temeke) akapata 97% ya kura, Lakin uchaguz wa Mwisho 1980 alipata 75% japo aligombea na kivuli cha dirisha na kura zilihesabiwa na Makada wake wa TANU. Angesimama na Oscar Kambona pengine zisingetosha!
 
Mbona mnarudia mada ambazo tayari tulishazijadili sana hapa?

Kabla huanzisha uwe unajaribu kupekua pekua hapa jf mkuu
 
nimewahi kusikia kama ishu ya kambona ilikuwa ya kupika?????? sijui ukweli anyway!

Hii ya 1982 ndio leo nimejuzwa! tatizo lilikuwa nini???

Mix with yours

watu walichoshwa na Ukosefu wa Bidhaa muhimu kama vile unga,sabuni,sukari ili upate lazima uwe na nguvu nyingi kuliko za kugombea daladala za mbagala kwa kukimbizana na magai ya 'Ugawaji' kutwa nzima kisa Bwana Mkubwa kaleta Protectionism policy kuzuia bidhaa za nje wakati ndan vyama vya ushirika kawapa makada wake kina Bomani wakaviua, Makampuni na mashirika aliyopora kwenye Azimio la Arusha akashindwa kuyasimamia halafu Kwenye Media za Serikal chini ya Mkurugenzi wake Paul Sozwiga wanaimba Ujamaa na 'kujitegemea'. Baada ya hili jaribio ikabidi aanze kujiandaa kurudi Butiama akakabidh nchi kwa Rais wa karatasi Mwinyi 1985 kipindi ambacho hata fedha za kugombelea meli ya mafuta ilitia Nanga Taifa lililojiita la kujitegemea haikuwa nayo, Juhudi za Cleopa Msuya akiwa Wazir wa Fedha, Warioba PM ndio ziliokoa kwa kumuomba fedha Rober Mugabe akaipa fedha hard cash ili tusiadhirike! Sifa kubwa ambayo namkubali sana aliyokuwa nayo ni kutokuwa mbadhirifu ila kwenye uchumi misingi mibovu aliyoweka kutokana na ubishi na kutokupokea ushauri wa kitaalam ndio ulioua nchi na kupelekea kukoswa koswa kupigwa Risas mara kadhaa!
 
nimewahi kusikia kama ishu ya kambona ilikuwa ya kupika?????? sijui ukweli anyway!

Hii ya 1982 ndio leo nimejuzwa! tatizo lilikuwa nini???

Mix with yours
Kambona alikuwa hakukubaliana na Azimio la Arusha hivyo alikimbia uhamishoni Uingereza kama mkimbizi wa kisiasa hivyo akiwa nje alianza mipango ya kufanya mapinduzi. Lakini pia baada ya maasi ya 1964 picha zilikuwa haziendi kati ya Mwalimu na Kambona.

 
Katika kumkumbuka Baba wa Taifa pamoja na mazuri yaliyofanya lakini pia tukumbuke na misukosuko aliyowahi kuipata ikiwemo majaribio ya kutaka kupinduliwa Serikali yake yaliyotaka kufanywa na wakorofi wachache kwenye kipindi cha utawala wake.
- Jaribio la kwanza: Mwaka 1964 Jeshi la wakati huo la Tanganyika Rifles lilipofanya maasi
- Jaribio la pili: Mwaka 1972 hayati Kambona alishirikiana na Kapteni Lifa Chipaka, Bi Titi Mohamed, na Michael
Kamaliza.

- Jaribio la tatu: Mwaka 1982 maafisa wa jeshi wakiongozwa na Komandoo Mohamed Tamimu.
Pamoja na majaribio hayo ya mapinduzi lakini pia mara kadhaa alinusurika kuuwawa kabla uhuru na baada ya wakati akitawala.

kambona aliondoka Tanzania kabla ya 1972
 
duh! kumbe nyerere katoka mbali. mpaka alifikia kujificha kigamboni ili wasimshekhe ponda.
 
duh! kumbe nyerere katoka mbali. mpaka alifikia kujificha kigamboni ili wasimshekhe ponda.
Kawawa alimshauri akimbie akajifiche Kigomboni asikubali kuonana na waasi kufanya nao mazungumzo wangemuua.

 
duh! kumbe nyerere katoka mbali. mpaka alifikia kujificha kigamboni ili wasimshekhe ponda.
Wanajeshi walifanya maasi wakati huo, walitokea kwenye kambi kuu ya kijeshi wakati huo alikua inaitwa Colito barracks(Lugalo) sababu kubwa walitaka maafisa wa kijeshi wa kizungu waondoshwe.
 
Sijui kwanini Kambona amezumgumza na Wanajeshi hao maana bora wangelimuondoa Mungu Mtu wa Tanganyika
 
Hawa CHADEMA ni janga,yani kumbe walianza zamani kuitaka nchi hii kwa mabavu aiseeeee!
Cc Baba V
 
Last edited by a moderator:


Zacharia Hans Poppe, ambaye alizaliwa mwaka 1956 mjini Dar es Salaam na kukulia mkoani Iringa.


Baada ya kumaliza elimu ya sekondari, Zacharia alijiunga na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) ambako alifikia cheo cha Kapteni, kabla ya kuachishwa kazi na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela, kwa tuhuma za uhaini, dhidi ya serikali ya awamu ya kwanza, ya hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, mwaka 1983.

Lakini mwaka 1995, Zacharia aliachiwa huru kwa msamaha wa rais wa awamu ya pili, Alhaj Ally Hassan Mwinyi, mwezi mmoja kabla hajamuachia Ikulu ya Tanzania, Benjamin William Mkapa, rais wa awamu ya tatu.

Kama zinavyosema sheria za nchi, mtu aliyehukumiwa kifungo, hana haki ya kugombea wadhifa wowote au kuajiriwa tena, Zacharia naye hakuweza kurejea kazini, badala yake akaamua kujiajiri, kwa kuanzisha miradi yake mwenyewe, ambayo leo ikiwa ni miaka 17 baadaye, miradi hiyo imesimama imara.

Kwangu mimi namuona shujaa si kwasababu ya kutaka kumpindua nyerere bali pamoja na kupotezewa muda mwingi akiwa gerezani lakini ameibuka na kuwa mmoja wa matajiri na mfanya biashara mkubwa nchini,ikumbukwe baba yake mzazi aliuwa na iddi amini kipindi kile cha vita ya kagera
.
 
Namsikiaga huyu jamaa sijui ni kwenye michezo..
Hivi anafanya au anamiliki kampuni zinazojihusisha na biashara gani?

Ni transporter mkubwa na anafanya vizuri,kwa tunaoshughulikia magari huyu ana heshima yake; ENGEN utapata habari zake vizuri sana!!!!!
Soka anafanyia hobby tu kama sio kurudisha faida kwa jamii!!!!
 
Back
Top Bottom