.....Kama zinavyosema sheria za nchi, mtu aliyehukumiwa kifungo, hana haki ya kugombea wadhifa wowote au kuajiriwa tena, Zacharia naye hakuweza kurejea kazini, badala yake akaamua kujiajiri, kwa kuanzisha miradi yake mwenyewe, ambayo leo ikiwa ni miaka 17 baadaye, miradi hiyo imesimama imara........
Huwa nikisoma/nikisikia mpango huo wa kutaka kuipindua Serikali ya Nyerere mwaka 1983 mwili huwa UNANISISIMUKA, sijui ni kwanini, I'm clueless.
Tatizo la Watanzania huwa hatuwezi ku-document mambo wether mazuri au mabaya ili KWANZA kuweka kumbukumbu na PILI ili tuweze kujifunza kutokana na matukio hayo.
Waadishi wa habari wengi wa Tanzania wamezoea kuandika LIGHT TOUCH NEWS au kutafasiri maandishi ya watu wengine kwa lugha ya kiswahili.
Hivi kweli hakuna hata mwandishi mmoja wa Tanzania anayeweza kuandika kitabu kuhusu kisa hiki cha akina Hans Pope?! Maggid Mjengwa & Co. What are you doing?. Nakumbuka Maggid Mjengwa aliwahi kuandika simulizi ya Mwamwidi(?) jinsi alivyomua Dr. Kreluu (?) RC wa Iringa wakati huo katika gazeti ya RAIA MWEMA. Tulipo mu-challenge Maggid andika kitabu kuhusu hicho kisa cha kusisimua akaingia mitini. Haya ndiyo mambo yanayosababisha baadaye historia kupotoshwa kama sasa hivi tunavyoshuhidia ulimwengu ukipotoshwa kwamba kiongozi wa mapinduzi ya Zanzibar alikuwa Amani Karume. Kumbe hata siku ya mapinduzi hakuwepo huko Unguja.
Mkuu hapo nilipo bold kwenye RED. Katika kundi hilo la waliotaka kumpundua Nyerere alikuwemo pia Balozi Ngaiza. Sasa hivi ni Marehemu. Huyu ana Hotel yake Muleba inaitwa KAMACHUMU INN. Kwa standard za Muleba na Kagera naye alikuwa a successfull business man.
Mwaka 2000 aligombea ubunge wa Muleba Kusini (?) kupitia CCM akaongoza kwenye kura za maoni. Lakini akaja kuenguliwa na NEC ya CCM kwa shinikizo la akina Kingunge Ngombale Mwilu kwamba mtu aliyetaka kupindua serikali ya Nyerere hawezi kugombea uongozi kwa tiketi ya CCM.
Balozi Ngaizi akahamia CUF na kugombea kwenye uchaguzi mkuu dhidi ya Lucy Msafiri wa CCM. Balozi Ngaiza akashindwa kwa kura chache (ingawa kulikuwa na tetesi kwamba NEC walichakachua matokeo).
Baadaye Balozi Ngaiai akahamia CDM baada ya CUF kukosa mvuto. Nakumbuka mwaka 2010 alikuwa anajiandaa kugombea ubunge kwa tiketi ya CDM. Lakini kabla ya kutimiza hiyo ndoto yake mauti ikamfika. Nakumbuka M/kiti wa CDM Freeman Mbowe alihudhuria mazishi yake huko Kamachumu Muleba.
Kama uliyoandika hapo juu ni kweli kwamba sheria za nchi haziruhusu mtu aliyepatika na kosa na kufungwa jela, ilikuwaje basi Balozi Ngaiza akagombea ubunge kwa tiketi ya CCM kwenye kura za maoni na baadaye kwenye uchaguzi mkuu kwa tiketi ya CUF?!
For those who have short memory, Ismail Aden Rage alishawahi kupatikana na kosa mbele ya mahakama na akafungwa jela. Je, imekuwaje Ismail Aden Rage amegombea ubunge na sasa ni Mbunge wa Tabora mjini?.
Naomba tu wanasheria/wana JF wanaofahamu sheria wanijibu haya maswali yangu.