Jaribu fanya haya ukipoteza breki kwenye gari yako likiwa kwenye mwendo

Jaribu fanya haya ukipoteza breki kwenye gari yako likiwa kwenye mwendo

Wick

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2012
Posts
8,313
Reaction score
12,170
Tukielekea sherehe za Christmass na Mwaka mpya, kuna madereva wapya na wale wa zamani watakaokuwa safarini sehemu mbalimbali, Iwapo ikatokea upo kwenye mwendo na breki kwenye gari zimefeli, jaribu kufanya haya!. Kumbuka kila moja linajitegemea katika kulifanya!.

1. USIPANIC, ikiwezekana hata abiria wako wasijue tatizo unalohangaika nalo (kuepusha kukuchanganya zaidi).
2. Washa taa za double hazard kuwajulisha madereva wenzio una tatizo. Wenye akili watakaa mbali nawe.
3. Endelea kupump brake inawezekana zikashika au kusaidia punguza mwendo wa gari.
4. Vuta taratibu hand brake, usijaribu kuivuta yote kwa mara moja, ukivuta kwa mara moja utasababisha gari kugeuka ghafla. Kumbuka tumia hand brake iwapo upo chini ya speed 50km/h tu.
4. Iwapo unaendesha Automatic weka gari yako kwenye gia ndogo (L), au kama gari ni Manual shusha gia mpaka 1 hakikisha unadownshift kwenda gia 2 kabla ya 1, usiitoe 4-1 moja kwa moja, hii inaitwa 'engine breaking'.
5. Muda mwingine kuipeleka gari kwenye Neutral (N) itaweza kukusaidia ingawa si salama sana.
6. Washa air conditioning, ipeleke AC ya gari yako mpaka mwisho kwenye ubaridi wake, itaipa uzito mkubwa engine na kukusaidia punguza mwendo wa gari yako. Pia washa taa zote na kila kitu kwenye gari itafanya umeme mwingi zaidi utumike na kuipunguzia nguvu gari.
7. Hii ni hatari lakini inaweza kukusaidia, switch funguo kama unataka zima engine lakini weka kwenye 'Ignition On' sio kwenye 'Engine OFF' juwa kuzitofautisha!.
8. Tafuta eneo salama kugongesha gari yako (unapogongesha lenga upande wa kushoto kwenye kona ili kuzuia dereva usije banwa na steering).

PS: Iwapo upo eneo baya, tegesha gari yako kufunga barabara nzima (utasaidika haraka zaidi).
 
Kwa hyo yule dereva wa bas LA harambee Kule arusha unamshauri nn
 
Hii inanikumbusha kwenye miaka ya nyuma sana nikiwa ni napenda sana racing
Ukiwa kijana unafanya mambo ya hatari sana mpaka sasa najishangaa

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
4. Iwapo unaendesha Automatic weka gari yako kwenye gia ndogo (L), au kama gari ni Manual shusha gia mpaka 1 hakikisha unadownshift kwenda gia 2 kabla ya 1, usiitoe 4-1 moja kwa moja, hii inaitwa 'engine breaking'.

Hii tunaita "Pistoni zinachomokea mbavuni"

Na inabidi kuwa makini kweli kweli haswa kwa gari za Auto. Ukipitiliza tu mpaka R

"Unaichota/unaikata mtama gari"
Kifuatacho ITV........RIP maturubai ma ubweche
 
Hii inanikumbusha kwenye miaka ya nyuma sana nikiwa ni napenda sana racing
Ukiwa kijana unafanya mambo ya hatari sana mpaka sasa najishangaa

Sent from my iPhone using Tapatalk
mambo ya hand brake na kudrift sio!..🙂
 
Hii tunaita "Pistoni zinachomokea mbavuni"

Na inabidi kuwa makini kweli kweli haswa kwa gari za Auto. Ukipitiliza tu mpaka R

"Unaichota/unaikata mtama gari"
Kifuatacho ITV........RIP maturubai ma ubweche
Kwa gari za kisasa kuifikia Reverse (R) kuna kona lazima uikate, inasaidia kutopitiliza.
 
Mengine nskubaliana kasoro namba 5.
Neutral kwenye mteremko ni hatari zaidi, la mzingi ni kushift to "L"

Sent using Jamii Forums mobile app
Unaweza tumia Neutral kuitetemesha gari ikasaidia kuipunguza kasi!. Jaribu ukiwa mwendo mdogo ingiza Neutral then rudisha Drive uone kinachotokea!. Sio hatari kivile!.

Hatari ni kuipeleka funguo kwenda Ignition On ukipitiliza ukaipeleka Engine Off utasababisha Steering Lock, kifuatacho Parapanda zitaliaaa!..
 
Tatizo brake huwa zinazingua eneo ambalo haya yote yanakua hayana msaada.

Imagine zinazingua kitonga.

Sent using Jamii Forums mobile app
hahahaa unaiburuza ukutani mpaka isimame!..
Kipindi hiko tukienda shy town ilikuwa ukipita Sekenke lazima ukutane na scania imeburuzwa kwenye ukuta mlimani!.
 
Back
Top Bottom