Jasmine anywa sumu na kujinyonga baada ya kunyimwa nauli ya kwenda Singida na mumewe.

Jasmine anywa sumu na kujinyonga baada ya kunyimwa nauli ya kwenda Singida na mumewe.

Frank Wanjiru

Platinum Member
Joined
Apr 12, 2012
Posts
25,686
Reaction score
46,842
Jasmini Hamisi, mkazi wa mtaa wa Murieti, kata ya Murieti jijini Arusha, amefariki dunia baada ya kudaiwa kunywa sumu na kisha kujinyonga, siku moja baada ya maelezo kuwa aliwahi kumwomba mumewe nauli ya kwenda Singida kuwasalimia wazazi wake.

Inaelezwa kuwa Jasmini alimwomba mumewe, Hamisi Maulidi, nauli ya kwenda Singida, lakini akaambiwa asubiri hadi hali ya kifedha itakapokuwa nzuri. Mumewe pia alieleza kuwa angeweza kupitia nyumbani kwao, ambako nako ni mkoani Singida.

Tukio hilo limetokea Oktoba 18, 2026, ndani ya nyumba aliyokuwa akiishi na mumewe. Inadaiwa kuwa Hamisi aliondoka nyumbani asubuhi kwenda site, na aliporejea aligonga mlango bila kufunguliwa, ndipo alipomwita jirani kumsaidia.

Jirani huyo alizunguka nyuma ya nyumba na kufungua dirisha. Alipochungulia ndani, alimwona Jasmini akiwa amejinyonga kwa kutumia mtandio aliokuwa ameufunga kwenye chuma cha kutundikia pazia kilichokuwa mlangoni.

Mtoto mdogo aliingizwa ndani kupitia dirishani ili kufungua mlango. Walipoingia, walimkuta Jasmini akiwa bado anapumua kwa shida na kufanya jitihada za kumpeleka hospitalini, lakini alifariki dunia.

Majirani wanasema walikata mtandio huo haraka wakijaribu kumuokoa. Ndani ya nyumba hiyo pia kulionekana kikombe chenye kimiminika kisichofahamika, huku soda ikiwa pembeni. Hata hivyo, haijathibitishwa iwapo kimiminika hicho kilikuwa sumu.

Haijathibitishwa iwapo ombi la nauli ya kwenda Singida lilikuwa na uhusiano wowote na tukio hilo, na chanzo cha kifo chake bado hakijafahamika rasmi.

<<<<

Aisee jamani
 
Ila jamaa selfish sana mtu kaombwa ruhusa mke aende kwa wazazi wake yeye anapeleka mada ya mke apitie na ukweni kufanya nini sasa. Labda kuna mabalaa huko ukweni akaona bora ajiondoe tu
 
Kifo cha kujitakia...
Huyo alikua na safari zake za kushinikizwa kwamba usipokuja mimi na wewe basi...


Cc: Mahondaw
 
Back
Top Bottom