Jasusi hatari nyuma ya NGO nchini Burkina Faso.

Jasusi hatari nyuma ya NGO nchini Burkina Faso.

Mkuu
Jasusi wao amekamatwa EU Wana bweka. Milio inasikika kutokea nchi za mbali.

Vipi bado yupo katika mgomo wa kula? Wanasheria wake waje waseme yupo NOVENA ya ngapi?
Huyo hana ujasusi wo wote! Lakini fikiria ni wazungu wangapi wako nchi hii ambao wamekuwa wakiingia na kutoka?
 
Yani mfaransa amfanyie Burkinabe ujasusi kwenye majeshi yake? Wabongo bana? Ujasusi wa nini? Biashara? Usalama? Tishio lake ni nini? Wana ushindani gani na koloni lake la zamani? Mmama aende vijijini kujasusi nini nchi maskini ya kutupwa ile?😎

Anyway waliosomea security wananielewa, otherwise JF ni burudani muda wote!
Lile lilikuwa shamba la mfaransa la kuvuna rasilimali za bwerere kabla ya kutimuliwa na Rais Ibrahim, Kwa nini asilifanyie ujasusi?
 
Lile lilikuwa shamba la mfaransa la kuvuna rasilimali za bwerere kabla ya kutimuliwa na Rais Ibrahim, Kwa nini asilifanyie ujasusi?

Ushasema lilikua shamba lake sasa kama analijua vema left and right alifanyie ujasusi apate nini kipya sasa? Yani kuku wake mwenyewe amuundie manati! Basics za usalama zinapaswa kufundishwa mashuleni kwa wabongo aisee
 
Sisi urafiki na mataifa makubwa kama China ni kuletewa Yeboyebo na fake items tu
Ujasusi na sisi wapi na wapi
Kuna wasiliti kibao waswahili
Mswahili akimuona Mzungu airport anamshobokea mpaka masanduku atabeba

Kuna magari ukienda mikoani utaona ina picha ya ndege anaepatikana tz
Eti wanafanya utafiti na kumchunguza
Na serikali imetoa kibali kabisa waendelee na utafiti daaa masikini nchi yangu
 
Yani mfaransa amfanyie Burkinabe ujasusi kwenye majeshi yake? Wabongo bana? Ujasusi wa nini? Biashara? Usalama? Tishio lake ni nini? Wana ushindani gani na koloni lake la zamani? Mmama aende vijijini kujasusi nini nchi maskini ya kutupwa ile?😎

Anyway waliosomea security wananielewa, otherwise JF ni burudani muda wote!
Hiyo habari IPO twitter imepostiwa na Yericko Nyerere huyu Fala anajiita jasusi na vitabu vyake vya mchongo
 
Ushasema lilikua shamba lake sasa kama analijua vema left and right alifanyie ujasusi apate nini kipya sasa? Yani kuku wake mwenyewe amuundie manati! Basics za usalama zinapaswa kufundishwa mashuleni kwa wabongo aisee
Mbona kafukuzwa kwenye hilo shamba?..unadhani ameondoka Kwa kupenda? na unaelewa ni Kwa nini TRAORE ameopt kuside na Russia? hauoni kwamba kulikuwa na kila ulazima wa mfaransa kupeleleza military intelligence ya Burkinabe na kujua ni kitu gani wanakipanga? Mbona unaonekana unashindwa kuelewa mambo madogo yasiyohitaji hata elimu!
 
Yani mfaransa hajui military capacity ya Burkinables? You're joking brother, ungesema wanamfanyia ujasusi Traore binafsi ingeleta maana kidogo sio intelligence wala capacity ya jeshi, wakati makamanda wote wakubwa wanapatia training zao France. Yani kimsingi Burkina faso atapanga intelligence ya kujilinda na majirani zake (sio France) wanaolingana naye! So huyo mama kusema anafanya intelligence vijijini ni overreaction tu ya kiafrika na kama wamemfukuza ni kama tu jiwe alivyokua anawazushia asiowapenda kuwa sio watanzania, kutengeneza panic status! Kwa taifa kama Burkinafso kwa wakati huu wa utawala wa kijeshi ni moja ya mbinu ya utawala, so kumfukuza haimaanishi lazima iwe kweli watawala wanavyosema! Ni common sense na njia mojawapo ya kujenga uungwaji mkono!
 
Jasusi hatari nyuma ya NGO nchini Burkina Faso.

Jasusi Joe Bassey kutoka Perrot Island nchini Cana ameachia nyaraka za siri zinazofichua kwamba Bi Claire Dubois, mwanamke Mfaransa katika miaka 30 iliyopita aliwasili Burkina Faso akijifanya kama mkurugenzi wa NGO ya Magharibi iitwayo Hope Forward, ambayo shughuli zake kuu ilikuwa ni kusaidia elimu ya wasichana na afya ya wanawake.

Bi Claire alijionyesha kama mwanamisaada ya kiutu aliyelenga kusaidia wanawake wa Kiafrika, akitembelea vijiji, shule, na masoko, na kutumia muda mwingi kusifu uongozi wa Burkina Faso kwenye televisheni ya serikali.

Walakini, nyuma ya shuguuli hii ya kibinadamu, Bi Dubois alikuwa akijishughulisha na ujasusi. Alikuwa akikusanya taarifa za kijasusi kwenye tovuti za kijeshi, ikiwa ni pamoja na vituo vya mafunzo ya kijeshi, vituo vya mafuta, na vituo vya uongozaji wa ndege zisizo na rubani, akitumia kivuli cha kazi ya kibinadamu.

Katika kazi zake zilizoonekana ni za kiraia lakini alibeba simu mbili-moja ya kiraia na ya pili ni simu maalumu kwa mawasiliano kijasusu na aliitumia kutuma barua pepe zilizowekwa katika mfumo wa ulinzi imara ambazo ni ramani zilizochakatwa vizuri na picha za setilaiti za maeneo nyeti ya kijeshi, kwenda kwa watu wa NATO na majasusi wemgine wa kigeni.

Shirika la ujasusi la Burkina Faso kwa msaada wa Shirika la Ujasusi la Urusi FSB tayari lilikuwa limetilia shaka shughuli Mama huyu na kufuatilia mawasiliano yake kwa ukaribu sana hasa kuingilia mawasiliano ya simu yake ambayo ilikuwa ikitumia Setelaiti. Baads ya kujiridhisha kwamba Bi Claire anafanya shughuli za kijasusi kweli, Walifanikiwa kuzuia nyaraka hizo zisiwe zinawafikia Nato na washirika kwakuwa tayari mawasiliano hayo ya Bi Claire walikuwa wameyaingilia kila akituma email zilikuwa zinaingia Moscow sio Brusels tena.

Rais Ibrahim Traoré aliwaamuru majasusi wake wamwache aendelee kukusanya nyaraka za misheni yake ili wamkamate akiwa na ushahidi halisi. Na baada ya miezi kadhaa, Hatimaye, alikamatwa na kuwekwa hadharani katika Kongamano la Kitaifa la Mamlaka ya Afrika, ambapo rais aliwasilisha nyaraka zake za siri na barua pepe zote moja kwa moja jukwaani, akifichua shughuli zake za kijasusi kwa ulimwengu. Na baadaye akazuiliwa kimya kimya na serikali licha ya shinikizo la nchi za magharibi kwakutumia mgongo wa azimio la kidiplomasia, Rais Traoré alisisitiza juu ya uwazi na haki, akisisitiza usaliti wa kuaminika ni adui wa Bukinafaso.

Swali la kujiuliza, ni mashirika mangapi ya kigeni yako nchini na yanafanya shughuli wazosema watafanya bila kuwa na agenda nyingine? Wanafuatliwa kwa kiwango gani? Jibu lipo Lumumba!
hata haya makampuni ya kubet kutoka nje sio ya kuyaamini japo tushakuwa addicted ila yanatujasusi
 
Mzungu na mwarabu ukizinduka na kumnyima rasilimali na maliasili ndio utamjuwa ana roho gani!
JPM aliminya korodani zao kidogo ikawa issue!
Mzungu shetani kabisa......
 
Back
Top Bottom