Jasusi hatari nyuma ya NGO nchini Burkina Faso.

Jasusi hatari nyuma ya NGO nchini Burkina Faso.

Yani mfaransa amfanyie Burkinabe ujasusi kwenye majeshi yake? Wabongo bana? Ujasusi wa nini? Biashara? Usalama? Tishio lake ni nini? Wana ushindani gani na koloni lake la zamani? Mmama aende vijijini kujasusi nini nchi maskini ya kutupwa ile?😎

Anyway waliosomea security wananielewa, otherwise JF ni burudani muda wote!

Oh ndio maaana makoloni yake yana muengua moja baada ya moja, majeshi yana rejeshwa kwao ufaransa

Jibu Hawa kuweza kujasusi yajayo sababu hakuna wanacho nufaika kwa kuwepo pale na kuwa na ubalozi hapo
 
Jasusi hatari nyuma ya NGO nchini Burkina Faso.

Jasusi Joe Bassey kutoka Perrot Island nchini Cana ameachia nyaraka za siri zinazofichua kwamba Bi Claire Dubois, mwanamke Mfaransa katika miaka 30 iliyopita aliwasili Burkina Faso akijifanya kama mkurugenzi wa NGO ya Magharibi iitwayo Hope Forward, ambayo shughuli zake kuu ilikuwa ni kusaidia elimu ya wasichana na afya ya wanawake.

Bi Claire alijionyesha kama mwanamisaada ya kiutu aliyelenga kusaidia wanawake wa Kiafrika, akitembelea vijiji, shule, na masoko, na kutumia muda mwingi kusifu uongozi wa Burkina Faso kwenye televisheni ya serikali.

Walakini, nyuma ya shuguuli hii ya kibinadamu, Bi Dubois alikuwa akijishughulisha na ujasusi. Alikuwa akikusanya taarifa za kijasusi kwenye tovuti za kijeshi, ikiwa ni pamoja na vituo vya mafunzo ya kijeshi, vituo vya mafuta, na vituo vya uongozaji wa ndege zisizo na rubani, akitumia kivuli cha kazi ya kibinadamu.

Katika kazi zake zilizoonekana ni za kiraia lakini alibeba simu mbili-moja ya kiraia na ya pili ni simu maalumu kwa mawasiliano kijasusu na aliitumia kutuma barua pepe zilizowekwa katika mfumo wa ulinzi imara ambazo ni ramani zilizochakatwa vizuri na picha za setilaiti za maeneo nyeti ya kijeshi, kwenda kwa watu wa NATO na majasusi wemgine wa kigeni.

Shirika la ujasusi la Burkina Faso kwa msaada wa Shirika la Ujasusi la Urusi FSB tayari lilikuwa limetilia shaka shughuli Mama huyu na kufuatilia mawasiliano yake kwa ukaribu sana hasa kuingilia mawasiliano ya simu yake ambayo ilikuwa ikitumia Setelaiti. Baads ya kujiridhisha kwamba Bi Claire anafanya shughuli za kijasusi kweli, Walifanikiwa kuzuia nyaraka hizo zisiwe zinawafikia Nato na washirika kwakuwa tayari mawasiliano hayo ya Bi Claire walikuwa wameyaingilia kila akituma email zilikuwa zinaingia Moscow sio Brusels tena.

Rais Ibrahim Traoré aliwaamuru majasusi wake wamwache aendelee kukusanya nyaraka za misheni yake ili wamkamate akiwa na ushahidi halisi. Na baada ya miezi kadhaa, Hatimaye, alikamatwa na kuwekwa hadharani katika Kongamano la Kitaifa la Mamlaka ya Afrika, ambapo rais aliwasilisha nyaraka zake za siri na barua pepe zote moja kwa moja jukwaani, akifichua shughuli zake za kijasusi kwa ulimwengu. Na baadaye akazuiliwa kimya kimya na serikali licha ya shinikizo la nchi za magharibi kwakutumia mgongo wa azimio la kidiplomasia, Rais Traoré alisisitiza juu ya uwazi na haki, akisisitiza usaliti wa kuaminika ni adui wa Bukinafaso.

Swali la kujiuliza, ni mashirika mangapi ya kigeni yako nchini na yanafanya shughuli wazosema watafanya bila kuwa na agenda nyingine? Wanafuatliwa kwa kiwango gani? Jibu lipo Lumumba!
It is more of propaganda.....The era of cold war again.
 
Yani mfaransa amfanyie Burkinabe ujasusi kwenye majeshi yake? Wabongo bana? Ujasusi wa nini? Biashara? Usalama? Tishio lake ni nini? Wana ushindani gani na koloni lake la zamani? Mmama aende vijijini kujasusi nini nchi maskini ya kutupwa ile?😎

Anyway waliosomea security wananielewa, otherwise JF ni burudani muda wote!
Hii taarifa kama ni kweli ilitolewa ni mwendelezo wa propaganda za uongo za Urusi. Yani Burkinafaso ina nini hadi ifanyiwe upelelezi na Ulaya nzima?. Hii ni ile ya Urusi kutangaza amekata maabara za kibailojia Ukraine na mpaka leo hajataja chochote alichokamata.
 
Ni uongo mkubwa sana. Uko wazi kabisa.😀😀
 
Ushasema lilikua shamba lake sasa kama analijua vema left and right alifanyie ujasusi apate nini kipya sasa? Yani kuku wake mwenyewe amuundie manati! Basics za usalama zinapaswa kufundishwa mashuleni kwa wabongo aisee
Hapo ndo wanapotushida wazungu...Wanaamini strategies zinabadilika so research ni muhimu!
 
Katika kazi zake zilizoonekana ni za kiraia lakini alibeba simu mbili-moja ya kiraia na ya pili ni simu maalumu kwa mawasiliano kijasusu na aliitumia kutuma barua pepe zilizowekwa katika mfumo wa ulinzi imara ambazo ni ramani zilizochakatwa vizuri na picha za setilaiti za maeneo nyeti ya kijeshi, kwenda kwa watu wa NATO na majasusi wemgine wa kigeni.
Hao ni majasusi gani wapumbavu hivyo kupiga picha kwa satellite kisha kuzituma kwa simu?

Yaani satellite ipige picha ikiwa angani, kisha ichakate itume kwenye simu ya mbibi yuko Burkina Faso. Ili huyo mbibi atume picha NATO? Kwanini satellite isitume direct kwenye kituo chake cha kukusanya taarifa?
Shirika la ujasusi la Burkina Faso kwa msaada wa Shirika la Ujasusi la Urusi FSB tayari lilikuwa limetilia shaka shughuli Mama huyu na kufuatilia mawasiliano yake kwa ukaribu sana hasa kuingilia mawasiliano ya simu yake ambayo ilikuwa ikitumia Setelaiti. Baads ya kujiridhisha kwamba Bi Claire anafanya shughuli za kijasusi kweli, Walifanikiwa kuzuia nyaraka hizo zisiwe zinawafikia Nato na washirika kwakuwa tayari mawasiliano hayo ya Bi Claire walikuwa wameyaingilia kila akituma email zilikuwa zinaingia Moscow sio Brusels tena.
Kwamba huyo mmama alikuwa anatuma taarifa blindly na hajui kama imefika au haijafika kwa mlengwa?

Iko hivi kwenye medani, kila agent anakuwa na handler. Wote wanawasiliana na lazima kuwepo mrejesho, handler asipopata taarifa ya agent atatafuta kwanini agent hajatoa taarifa. Agent asipopata feedback, handler atatafuta sababu ni nini.

Shirika la kijasusi likitoa task, handler akaifikisha kwa agent kisha agent akatekeleza, anaiwasilisha. Kitendo cha shirika kukosa report kitachochea waulize kwanini, agent atasema ametuma, watasisitiza hawajapokea na mara moja watachunguza taarifa imeishia wapi.

Huu ujasusi wa kijiweni.
 
Back
Top Bottom