Thad
JF-Expert Member
- Mar 14, 2017
- 13,380
- 31,566
Starring hauwawi, usihofu Honda atabaki salama japo cha moto atakiona!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndiye kamponza na ndiye atakayemwokoa, hiyo ndo nguvu ya mwanamkeKwahiyo demu ndo kamponza Honda
Sent from my iPhone using JamiiForums
Hahahaha hujawahi iona hyo unatafuta hela pekee yako ila mnakula wengiHahahahaha yaani Mimi nijitolee kugombana na mwandishi mpaka nipate kitabu halafu nikupe kirahisi???
[emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]
Sent using Jamii Forums mobile app
Naona bado, ngoja nile kwanza niwe fresh.Starring hauwawi, usihofu Honda atabaki salama japo cha moto atakiona!
Dah umenizidi ujanja. haya ngoja nitakushtua.Hahahaha hujawahi iona hyo unatafuta hela pekee yako ila mnakula wengi
Kweli mijitu mingine mipopoma. Kama anataka burudani yake ya moja kwa moja si alipie. Umewawekea namba ya simu hapo. Akufuate hewani,anunue yakeUnanilipa sh ngapi ili nifanye unavyotaka wewe? Familia yangu utailisha wewe?
Acha upopoma aisee afu jaribu kuheshimu mawazo ya mtu, na pia ukiona naringa basi acha kufuatilia kwani uliitwa kuja kusoma?
Yani niliemjibu kanielewa afu wewe ambae hata koment ulikuwa hutoi unatoa povu si ukorofi huo ni nini?
Ukiona nakuchelewesha nunua kitabu kipo sokoni.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]MUNGU anawaonaaa. Muda mwingine utajua anakupenda kumbe kuna kitu anafuata tu kwako,kama anavyofuata hela kwa sajini. Halafu kwa chi baby anafuata ile kitu inaitwa mkuye....Sajini kala mzigo Kwa dakika Tatu alafu chibaby ni zaidi ya masaa matatu....wanawake Mungu anawaona!!
Sent using Jamii Forums mobile app
Acha kutukana wewe.unaniita Mimi popoma wakati hunijui??Kweli mijitu mingine mipopoma. Kama anataka burudani yake ya moja kwa moja si alipie. Umewawekea namba ya simu hapo. Akufuate hewani,anunue yake
Sent using Jamii Forums mobile app
Na wewe umo kwenye hiyo mijitu mingine? Itakuwa una bahati kuwemo humo
Na wewe umo kwenye hiyo mijitu mingine? Itakuwa una bahati kuwemo humo
Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee duuhRIWAYA: MPANGO WA CONGO.
SEHEMU YA 18
Kojo akainama kisha akakiweka vyema kivuli cha Honda na kuachia risasi ambayo ilimnyanyua juu na kumbwaga chini kama kiroba cha mirungi.
Kojo akatabasamu huku akitoka kule alipokuwa amejikinga kwenda kule alipoangukia Honda.
Alienda kumalizia kazi alioianzisha na alipanga kumshushia risasi zote zilizokuwa zimebaki kwenye bastola yake aina ya Revolver colt ya kipolisi.
Honda alinyemelewa na umauti….
Kojo alizidi kumsogelea Honda huku akiwa na imani kabisa ya kuwa adui yake ameipata tamu yake.
Ni hadi alipofika karibu na alipokuwa Honda ndipo alipogundua hesabu zake zilikuwa batili.
Alishangaa Honda akinyanyuka chini kwa mtindo wa sukusi,kisha akamvaa mzima mzima na wakaenda chini wote huku Kojo akitoa kilio cha kuhamanika na uvamizi ule wa gafla.
Honda akadondoka juu ya mwili wa Kojo kisha akaachia makonde manne mfulululizo ambayo mawili yalimwingia Kojo na mawili yalipanguliwa.
Honda alijua mlio wa risasi utakuwa umewasitua mabaradhuli waliokuwa ndani.
Na alikuwa amejeruhiwa juu kidogo ya bega baada ya risasi ya Kojo kumpata eneo hilo.
Hivyo wakati yupo chini akavuta subira ili adui yake asishambulie tena na kumuumiza zaidi na hilo alifanikiwa kwani Kojo hakushambulia akamfuata na kilichomkuta atawasimulia wenzie.
Balaa gani hili Kojo.
Honda akamshindilia teke la tumbo kisha akatokomea kizani huku akilaani kukutana na wale jamaa kila alipoenda.
********
Kizibo na Sajini walitoka mkuku huku wakitazama huku na huko na kitu pekee walichokiona ni Kojo akinyanyuka chini kwa taabu kutoka chini.
Kojo alijilaani kwa kuwa na bahati mbaya ya kukutana na Honda na kilichomuuma zaidi ni kuona Kizibo na Sajini Kebu aliodhani wamepata balaa huko ndani na imekuwa tofauti wanakuja wakiwa wanakimbia kuonesha ni risasi aliopiga ndio imewakurupusha huko ndani.
Akaingiwa na fadhaa huku aibu ikimwelemea kwa kuona anapigika kila mara tofauti na walivyozoea katika kazi zao.
Wa kwanza kufika alipokuwa Kojo ni swahiba wake Kizibo.
“Balaa gani tena komredi!!” alihoji Kizibo huku akifanya jitihada za kumnyanyua kutoka chini.
Sajini Kube alibaki akiangaza huku na huko ili kuhakikisha usalama.
Kojo aliona aibu kusema kapigwa tena na Honda na aliogopa kuonekana mdebwedo mbele ya wenzake.
Akaamua kudanganya bila kujua madhara ya uongo ni makubwa kuliko ukweli wenye kupatiwa ufumbuzi.
“Kuna vibaka hapa wamenivia bana wakataka kunipora ndo nikajitetea aisee”
Jibu hilo likamtia mashaka Kizibo lakini hakutaka kuweka mashaka yake hadharani mana alijua atamkera rafiki yake ama la basi ungezuka ugomvi Kati yake na Sajini.
Nae akabaki na mashaka yake huku akiomba moyoni mjadala wa kufumwa akila chabo chumbani kwa Simbi usianze tena.
Walipanda ndani ya gari na kuondoka huku wakimwacha Simbi asiamini kama ametoka salama kwenye dhahama ile huku akimsifu Honda kwa kutokomea bila kuleta fujo.
Aliwasifu wanaume wa Kitanzania bila kujua limetokea kwa mikakati tu.
****
Honda alirejea nyumbani kwa marehemu Bulembo ambako aliamua kupafanya makazi yake ya muda.
Kama kawaida aliingia kwa njia za panya huku bado akiona utepe wa polisi ukiwa bado upo umezungushwa kwenye nyumba ile.
Alikuwa amejeruhiwa na damu bado ilikuwa ikimtoka hivyo alihitaji kuzuia.
Nyumba ya jasusi siku zote huwa haikosi vifaa vya huduma ya kwanza.
Nyumba ya swahiba wake aliijua,hivyo hakupata tabu kukifikia chumba kilichokuwa na vifaa hivyo.
Alifungua na kuingia ndani yake ambapo alikuta vifaa mbalimbali vya huduma alioihitaji.
Akatumia muda wa saa nzima kuhakikisha jeraha alilopata linapata tiba sahihi kisha akajichoma sindano ya kuondoa maumivu kwa muda wa saa kumi na mbili.
Bado alihitaji kujua ilipo Club X na alijua wa kumpa majibu ni mateka aliemwacha humo ama mwanadada Simbi.
Akatoka kwenye kile chumba na kuelekea kule alikomwacha mateka wake.
Alipoufikia mlango wa chumba alichokuwamo mateka, akashangaa kuona upo wazi wakati aliufunga wakati anatoka.
Akachukua tahadhari.
Akaufungua mlango kisha akasimama pembeni ili kuona kama kuna kitu au mtu atatoka au kushambulia.
Haikuwa hivyo.
Akaamua kuingia kwa mtindo wa aina yake ili kumpoteza yeyote ambae angekuwamo.
Alipofika ndani akajikuta akichunguliana na maiti ya mateka wake aliekuwa amechinjwa bila huruma.
Ni nani mwingine aliejua kuna mtu mle ndani tofauti na Mkurugenzi Papi Mndewa?
Hakupata jibu licha ya kujiuliza maswali mengi sana bila mpangilio.
Honda akiamiani anahujumiwa ila ilikuwa bado mapema kujua anaemhujumu.
Ndani ya nyumba ile hapakuwa mahali salama kwake kuendelea kupaishi,hivyo akaamua kuondoka na kutafuta makazi mengine tena.
Tangu alipomkamata mateka yule hakuwa amemmkagua wala kutaka kujua alibeba nini hivyo akaamua kumpekua harakaharaka.
Punde akakutana na kikaratasi kidogo kilichokuwa na maneno machache tu.
“HOTEL DEKUKU:8:0(88)”
Kikaratasi kile kilikuwa kimeandikwa kwa fumbo maalumu. Hivyo Honda alihitaji kufafanua fumbo lile.
Akatoka ndani ya chumba kile na kuanza kutoka huku akili ikicheza kujua hiyo Hotel Dekuku.
Kuhusu namba haikumsumbua mana 8:0 alijua ni badala ya saa mbili na pia 88 alijua ni chumba cha hotel hiyo ya Dekuku.
Akatoka hadi nje kabisa ya uzio wa nyumba ile ya Bulembo huku akili yake ikicheza kujua lilipo hilo jina la Dekuku ndani ya Kinshasa.
Tangu awe ndani ya Congo hakuwahi kusikia hilo jina la Dekuku.
Akili ikamzunguka,akakumbuka kitu.
Haraka akajipekua ndani ya mifuko yake na kutoka na simu yake aina ya simujanja.
Akafungua sehemu ya kuruhusu kutumia mawasiliano ya mawimbi.
Akaingia kwenye ramani iliokuwa ni moja ya kablasha liloko kwenye simujanja Ile kisha akaingiza neno Dekuku.
Bado haikumletea majibu alioyatarajia.
Akaamua kuacha kupoteza muda zaidi.
Akaendelea na safari huku akijaribu kuvuta kumbukumbu ni wapi amewahi kuliona jina lile.
Akakumbuka!!
Aliwahi kuona kitu kimeandikwa Dekuku na zilikuwa ni sahani za mgahawa ulioko kwenye jengo SAI PLAZA.
Jengo hilo ni lile lililopakana na ofisi za ubalozini ni lile jengo refu lenye hotel kadhaa na migahawa ya kutosha.
Akatabasamu kivivu baada ya kujipongeza kwa hisia zake tangu mwanzo kuhusu jengo lile.
Likabaki swali moja tu ambalo ni muda huo aliotakiwa kuwapo pale ni usiku ama ahsubuhi ama ni muda gani alietakiwa kuwapo awepo?.
Akajiahidi kujua huko huko cha msingi afike chumba namba 88 ndani ya gorofa ya SAI Investment.
Tayari mapambazuko yalikuwa yameanza kuchukua sura ya Dunia.
Kitu ambacho Honda hakujua ni kuwa ahsubuhi ile ilikuwa imaeamka na sura yake kwenye kila gazeti lililotoka siku hiyo tena akituhumiwa kumuua Balozi Ally Sapi na dau nono lilitangazwa kwa atakaesaidia kupatikana kwake.
Mida ya saa tatu na nusu hivi ilimkuta Honda akiingia ndani ya viunga vya SAI PLAZA.
Hakujali macho ya watu yaliokuwa yakimtizama,akafika hadi apokezi na hakwenda kwenye mgahawa wa Dekuku bali alienda kuulizia chumba cha karibu na namba 88 ambapo aliambiwa hakina mtu hivyo akalipia na kupewa kadi ya kufungulia kisha akaelekea huko juu.
Wakati akiwa kwenye chumba cha msaada kinachosafiri kuelekea gorofa ya tatu kuliko chumba hicho alichotaka kupanga,akajiwa na wazo.
“Vipi kama huu ni mtego” alijiwazia baada ya kujiuliza ni vipi kama karatasi ile iliwekwa baada ya kuuwawa yule mtu.
Akapanga kujipa tahadhari.
Alifika hadi kilipokuwa chumba namba 88 na hakujali tena kuhusu chumba alichokuwa amepanga.
Akakuta mlango ukiwa wazi. Akatazama kushoto na kulia hakuona mtu,taratibu na kwa tahadhari kubwa akausukuma mlango na kunyanta huku akiwa na tahadhari ya hali ya juu.
Macho yake yakawa makini upande wa dirishani alikoona kumewekwa bunduki kubwa ya kudungulia aina ya Lapua Magnum rifle.
Akajiuliza.
“Ni imeachwa makusudi au ni mtego?” akazidi kuingiza kiwiliwili ndani.
Mara akajikuta akidakwa na mikono imara iliomvutia kwa kasi ndani na kumbwaga chini ila nae kwa utalamu wake akawahi kusimama.
Ila kwa alichokikuta sicho alichokitegemea.
Wanaume watatu walikuwa wamesimama wakiwa wamenyoosha bastola kumwelekea na mmoja akaupiga mlango teke kwa nyuma ukajifunga.
Wote aliwajua!
Alikuwa ni Kizibo;Kojo na Sajini Kebu.
Kojo alitoa tabasamu baya usoni pake.
Alifurahi kumtia Honda mikononi mwake tena akiwa na usaidizi.
Huko nje nako raia wenye uchu na zawadi walikuwa wamewaarifu polisi uwepo wa Honda eneo lile.
Polisi nao wakawa njiani kumuwahi muuaji Honda.
Pagumu!!