Jasusi Honda ndani ya mpango wa Congo

Remi angenyoosha moja kwa moja hadi Mhandu secondary tu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
RIWAYA : MPANGO WA CONGO

SEHEMU YA 21


Taa za gari lile ziliendelea kumulika na punde wakashuka watu watatu waliokuwa wamevaa mavazi ya Polisi!!

"Dadeki!!" alijisemea Remi.

Askari wale walipomfikia Remi wala hawakujihqngaisha kuuliza linalomkimbiza wao moja kwa moja wakamdaka!

"Nyie ndo wazururaji tunawatafuta twende...!!" alisema askari mmoja huku akianza kumsukuma bila utaratibu.

Remi akataka kujitete lakini askari mmoja akamkatisha huku akitishia kumtandika makofi.

Remi aliwatizama vijana wale ambao walizidi kusogea huku wakijifanya kama hawana habari na lile lililokuwa linaendelea kwa Remi.

Remi akanyoosha mkono ili aseme kuhusu vijana wale.

"Nitakutia mikwenzi sasa hivi nyau wewe!!" alikoroma askari mmoja huku sasa akimsukuma kwa jaziba.

Remi alipandishwa kwenye karandinga kisha safari ikaanza na ndani ya karandinga kulikuwa na vijana wengine watatu ambao nao inaonekana walikutwa na masaibu kama ya Remi.

Waliitwa wazururaji.

Vijana waliokuwa wakimkimbiza Remi wao walipitiliza na kushuhudia Remi akiwa ndani ya gari la Polisi.

Hilo lingewagarimu na hawakutaka Remi atue mikononi mwa jeshi la Polisi.
Mmoja wao akanyanyua simu yake na kumpigia mtu waliekuwa wamehifadhi jina lake ELCHAPO!!

walitoa taarifa kama ilivyo kisha wakaambiwa wao kazi yao imeishia pale hivyo waendelee na majukumu mengine.

Vijana wakatokemea wanakokujua.

Gari lile la Polisi likiwa na watuhumiwa wa uzururaji,liliendelea kuikata mitaa na kurudi barabara ya Musoma.
Wakiwa wamefika njia panda ya kiwanda cha maji cha AquarRock na Tanesco; ikatokea pikipiki kubwa ambayo hakuna alieitilia shaka na safari ikaendelea huku kukiwa hakuna askari alieitilia shaka pikipiki ile.

Ni hadi gari lilipofika karibu na kiwanda cha samaki cha Nile perch hatua kadhaa kabla ya kuifikia barabara kuu ya Musoma road.
Ni kitendo kilichofanyika kwa weledi wa hali ya juu kutoka kwa mtu aliekuwa juu ya pikipiki.

Kwanza aliongeza mwendo wa pikipiki kama anaehitaji kulipita gari lile,lakini haikuwa hivyo badala yake alipofika karibu na upande waliokuwa askari na watuhumiwa wao akatoa kitu kama kibomu kidogo ambacho aliking'ata na kukitupia nyuma ya gari ambapo kilianza kutoa moshi mzito na kupelekea waliokuwamo kuanza kukohoa mfululizo.
Baada ya yule jamaa kufanya vile aliongeza mwendo zaidi hadi usawa wa dereva ambapo nae alimtupia kibomu kile jambo lilklofanya dereva kukosa mwelekeo huku akiongeza mwendo badala ya kusimama kisha akaenda kuyapamia magari yaliokuwa yamepaki kwa ajili ya kushusha na kupakia samaki.

Kilichofuatia ni ajali mbaya sana.

Gari la Polisi lilinyanyuka juu kisha likajipigiza chini na kurudi tena juu kisha kuanguka na kubiringita mara mbili kisha likatulia huku moshi wa vile vibomu ukitanda angani ukiwa umechanganyikana na vumbi.

Watu walishika vichwa wengine vinywa vyao kwa kutokujua kama kuna aliesalimika kwenye ajali ile.

Jamaa aliekuwa kwenye pikipiki akageuza haraka kurudi ilipokuwa imedondokea gari ile na alipofika akapaki haraka na kuwa kama anataka kutoa msaada kwa watu waliokuwa nyuma ya karandinga ile.

Ila lengo lake halikuwa hilo,lengo lake lilikuwa ni Remi.

Akiwa mzima ama mfu ni lazima ampate!!


******

Mtega nyoka alikuwa ameshazunguka kila kona akijaribu kutazama wapi anaweza kuona ilipo Club D ila hadi inapata kuwa saa tano usiku bado hakuwa amefanikiwa kuiona..

Alichoka na alihitaji kupumzika!!

Alimwelekeza dereva wa bajaji ampeleke Meko darajani kulipokuwa na baa ya Tesha.


Alishuka na kuingia ndani ya baa ile iliokuwa imejaza watu wa kila aina,wengine walikuwa wanaserebuka na wengine walikuwa wamebambiana ili mradi tu kila mtu na furaha yake usiku ule.

Akachagua kiti kimoja kilichokuwa kipo wazi bila kukaliwa na mtu.

Mtega nyoka alipenda sana wanawake ila si wanawake wa kutongoza. Alipenda wahudumu wa baa ama makahaba kwa sababu wanawake wa kawaida huwa haamini usalama wake mana wengine hutumiwa kumfuatilia nyendo zake.

Makahaba ni nadra mana haingekuwa rahisi kujua ni lini na wapi angeingia kuchukua ili ajistareheshe.

Alihisi anakuwa salama zaidi akiishi bila kupenda.
.

Akiwa bado anapepesa macho ili kupata yule ambae angemfaa,mhudumu akamfikia na hakuwa na budi kuagiza kinywaji alichokipenda.

Kuna kitu aligundua!!
.
Tofauti na siku zote ambazo huwa kuna makahaba wengi ndani ya baa ile,ila siku hii hakuona kabisa wingi ule na kila aliekuwepo alikuwa yupo bize na mambo yake huku wengine wakiwa wamekaa watatu ama wawili wawili.

Hakushobokewa kabisa siku hiyo.

Alizidi kuukata tu huku wanawake wakitoka mafungu mafungu na kutokomea huko nje!!


Akaona si vibaya akiuliza.

Akamwita binti mmoja aliekuwa amekaa karibu na yeye!!

"Samahani tunaweza kuwa wote usiku huu?" alihoji Mtega nyoka.

"Unataka kuchetua ama unataka kulala?" alihoji binti yule huku macho yakiwa juu juu kama mkojoa stendi.

"Kulala!!" alijibu Mtega nyoka.

"Babu wee utanikosesha Dolali bure wewe!!" alisema kishambenga yule binti huku akichezesha vidole vyake kwa kuvigusanisha akiashiria pesa.

Mtega nyoka akashituka kidogo kisha akahoji.

"Nakukosesha vipi hizo Dolali wakati nami nakupa pesa utakayo?"

"Aah wee leo kuna midolali haiwezi kuwa kama hivyo visenti vyako labda nikuchetue dakika mbili hapo utoe vinyege vyako hivyo!!" alisema Yule dada huku akitikisa makalio yake kwa kuhamasisha kingono.


"Ooh sawa, vipi hizo Dolali mwazichukua wapi?" alihoji tena Mtega nyoka huku akiwa hajatilia mkazo swali lake.

"Aaah wa wapi wewe!!! Yani hujui huu mwisho wa mwezi Club Dekuku kunakuwa hivi yani..." alisema yule binti huku akimshangaa Mtega nyoka kwa kutokujua kinachoendelea huko Dekuku ambapo alionesha ishara ya kimbea yani kunakuwa moto.

"Dekuku!?" alishangaa Mtega nyoka huku akikaa vyema kwenye kiti chake.

"Ndio!; afu wanipotezea muda mi najiandaa bwana!" alisema yule binti huku akianza kuondoka.

Mtega nyoka akamdaka mkono yule binti ambae aligeuka kwa mshangao wa kitendo kile.

Mtega nyoka ili kumtoa wasiwasi akamwonyesha shilingi elfu kumi na binti akatabasamu kama chatu alieona windo.

"Aaah!! Kitu gani huko kinachowapeleka?!" alihoji Mtega nyoka huku akimpa ile pesa.

"Tunaenda kulala na vijana, ambao hutupa pesa nyingi sana kulingana na huduma utakayompa na vile ataridhika!" alisema yule binti.

"Huwa wanatoka wapi vijana hao"


"hakuna anaejua ila huwa tunafuatwa hapa na gari na kupelekwa huko kila mwisho wa mwezi!"


"unajua ilipo hiyo Dekuku?"

"Hapana huwa tunafungwa vitambaa tukishaingia ndani ya gari!!"

Mtega nyoka alizubaa kidogo huku neno Club D na Dekuku yakipita kichwani mwake kama upepo na asijue kama ni aina moja.

Akakumbuka maneno ya Zana bwana mdogo aliemteka kwenye msiba wakati akimfuatilia Malima.

Mtega nyoka alitoka nje ya Club ile kisha akatafuta sehemu nzuri na kutulia huku lengo likiwa ni kusubiri aone hilo gari.


Haikupita nusu saa gari aina ya kosta likapaki nje ya ile baa na dakika tatu baadae wakatoka mabinti kama saba hivi na kuingia ndani na haikupita dakika wakatoka kule baa wadada wengine kumi akiwemo yule aliekuwa anaongea na Mtega nyoka.

Punde ile gari ikaondoka!

Mtega nyoka haraka akadandia pikipiki na kumwelekeza dereva wake aifuatilie ile gari ambayo ilikuwa inaenda taratibu bila papara.

Ile gari ikawa inazunguka mitaa tofauti tofauti bila kuonesha ni wapi inapoenda.

"Big; mbona tunazunguka tu.." alihoji dereva wa pikipiki.

"Usiogope nitakulipa!!" alidakia Mtega nyoka.


"Sio kunilipa hapa mafuta yanaenda kukata broo!!" alisema dereva huku akiegesha pembeni.

Mtega nyoka akafyonza huku akishuhudia gari ile ikiongeza kasi na kupotea yani ni kama dereva alijua wanafuatiliwa na alitumia nafasi hiyo kutokomea.

Mtega nyoka alibaki akitoa matusi tu bila msaada na eneo walilokuwapo ni eneo pweke ambalo halikuwa na pilika za watu.

Wakageuza na kurudi ili kuokoa mafuta yaliokuwa yamesalia.

Mtega nyoka alilaani sana siku hiyo.

Akaenda kupumzika huku akingoja ahsubuh iliokuja na mambo mengi licha ya kuwa na muda kidogo!!

*****

Shusha utabiri wako tujue kinachofuata!!
 
patamu hapo, kitendawili cha club D, Dekuku kinaelekea kuteguliwa..
shukrani Kudo
 
Wamemteka kizembe sana...

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Kwa majasusi kutekwa au kukutana na maadui ni faida kubwa sana kwani ndio inamrahisishia kujua ukubwa Wa kazi yake,kupata majibu ya maswali yake nk.
Tena apo usikute Jasusi Honda kachukia kukutana na hao wazembe tena labda labda atataka kujua tu wamejuaje lile Chimbo lake LA siri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtega nyoka angekuwa anabadilisha piki piki Kila baada ya hatua kadhaa, wacha tusubiri itakavyokuwa
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…