MLUGURU
JF-Expert Member
- Mar 30, 2012
- 2,929
- 3,710
Naaam Kudo nashushia Pepsi baridi hapa.....Leo ujaninywesha PEPS ya moto kabisa.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu angalia usije ukatuponza wote kwa kauli yakoHongera Sana kudo naona kelele zangu zimeanza kuzaa matunda hatimae nimesoma vipande viwili Leo.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hongera Sana kudo naona kelele zangu zimeanza kuzaa matunda hatimae nimesoma vipande viwili Leo.
Sent using Jamii Forums mobile app
MPANGO WA CONGO..
SEHEMU YA 20
Vijana wale walimsogelea Remi.
"Tafadhali binti tulia usifanye ujanja wowote!!" alionya mmoja wa vijana wale huku akimsogelea Remi akiwa na bastola mkononi.
Remi akili yake ilifanya kazi harakaharaka bila kupata la kufanya kutoka mikononi mwa vijana wale walioonesha hawana mzaha endapo akiwabugudhi.
Remi akabaki akijiuliza alipo mtu wa tatu ambae alimkoromea na kumfanya asimame na hapo ndipo akafanya akili yake ivute subira kufanya lolote mana hakujua alieamrisha ni upande gani yupo na yupo kwa niaba ipi.
"Huwezi kutukimbia Remi yani wajisumbua tu" alisema kijana mwingine huku akifanya jitihada kuikwepa meza moja ya matunda iliokuwa imewatenganisha.
Remi akapiga hatua moja nyuma ili kujiweka mbali na watu wale lakini jamaa mmoja akamwonya ya kuwa asiendelee kusogea.
"Tulia hivyo hivyo,hatua nyingine nakupasua ubongo wako!!" alikoroma jamaa.
Remi akatulia!!
Jamaa mmoja akamkaribia zaidi huku akiweka simu sikioni kuashiria alihitaji kumpigia mtu wakati huo.
"Tupo nae...ndio..eeh!!" alisema jamaa huku Remi akishindwa kujua walichozungumza.
Punde yule jamaa akampa simu Remi.
Remi akaipokea na kuweka sikioni na kubaki kimya.
"Hatuna shida na wewe endapo ukiwapa hao vijana mzigo wetu na watakwacha uende zako" iliunguruma sauti iliojaa upole wa hali ya juu kana kwamba ni tabibu akisema na mgonjwa wake.
"Najua mtaniua nikiwapa ila.." alikatishwa Remi..
"Kukuua hata sasa vijana wangu wanaweza kukuua ila hatuna nia hiyo kabisa binti!!" ilisihi sauti ile ambayo Remi aliitambua vilivyo.
Remi alijuwa hawawezi kumwacha salama na usalama wake pekee ni kuendelea kuwa na alichonacho mana hata akiwapa bado alishuhudia mengi hivyo ni lazima azibwe mdomo.
Hata!!..
Remi alijakatilia nafsini mwake.
"Haiwezekani niueni tu!" alisema Remi.
Upande wa pili ulikaa kimya kwa muda bila kusema lolote.
"Una hakika unataka kufa Remi!!?" ilihoji sauti upande wa pili.
"Ndio!!" alijibu kimkato Remi.
"Wewe unakufa! Tabibu wako Santina je!?"
Eeh bana eeh!!
Remi alistuka manusura adondoshe simu.
Lilikuwa ni jambo jipya kwake hasa kutajiwa jina la tabibu Santina.
Ndipo alipoamini watu wale kweli wanamkono mrefu.
Akaamua kucheza pata potea!!
"Muueni nae, ila hautakuwa mwisho wa haya mambo" alisema Remi kwa sauti ya kitetemeshi.
Alicheka mtu wa upande wa pili,kisha akasema.
"Chaguo ni la..." sauti haikumalizia likatokea tukio la kustukiza ambapo mlinzi wa soko lile alitokea gafla na kuanza kuita kelele za mwizi huku akipiga filimbi na Remi hakutaka kuipoteza nafasi ile nae akairusha juu simu ile aliokuwa nayo.
Wakati jamaa mwingine akigeuka kumkabili mlinzi, jamaa aliekuwa karibu na Remi akatoa sauti ya hamaniko kwa kitendo kile alichokifanya Remi.
Akajitia mjuzi wa kutaka kuidaka simu yake mpya na ya garama, wakati yupo katikati ya jitihada zake hizo za kuokoa simu ndipo Remi akaachia kifuti kilichompata jamaa yule katikati ya kifua na kumbwaga chini yule jamaa ambae alibaki akitoa miguno kama kahaba aliedhulumiwa haki yake ya kifedhuli.
Jamaa mwingine akashindwa cha kufanya,iwapo amsaidie mwenzie ama amdhibiti mlinzi ambae bado alikuwa anapiga filimbi na kelele za mwizi.
Remi alimsoma vizuri bwana yule wakati anajinyanyua akiwa amepiga magoti.
Remi akamuwahi kwa teke safi lililoenda moja kwa moja kwenye shingo ya jamaa na kumrudisha chini asiamini kama ni Remi aliemtwanga teke lile.
Remi alijua yeye si mjuzi wa ngumi hivyo kuendelea kuwa pale ni kujiweka hatarini zaidi hivyo akaamua kuumwaga huku akijishangaa namna alivyoweza kumdhibiti yule jamaa.
Jamaa mwingine alipoona Remi ameumwaga akaamua nae kumaliza kelele za Mlinzi.
Ambapo alimtandika teke moja la kifua lililokata kelele zote na kumwacha mlinzi akibweka chini kama mbwa koko jalalani.
Akaenda kumnyanyua mwenzie aliekuwa amekaukwa na koo baada ya teke la Remi kumpata sawasawa.
Ikazuka tafrani ndani ya soko huku panya na paka shume wakishindwa kujua Dunia yao imeingiliwa na nini.
Remi alitokomea kwa kupita Mashi hotel kisha akatokezea shule ya Nyakato na kushika njia ya machinjioni.
Kama alidhani vijana wale walimwacha alikosea bado walikuwa nyuma yake haihai.
Kila kichochoro alichopita Remi na wao walipita huku wakiwa makini asiwapotee.
Remi akiwa anakaribia kufikia kiwanda cha pamba mara mbele yake likatokea gari lililowasha taa kali na kummlika usoni.
Akainama chini ili asiumie macho yake na bila kusema lolote kwa kitendo kile japo alijua si salama kwake na alipogeuka nyuma bado vijana wale walikuwa wanamnyemelea huku wakionekana kutokujali kabisa uwepo wa gari lile liliwamulika makusudi.
Remi matatani tena!!
Mkuu Kwa majasusi kutekwa au kukutana na maadui ni faida kubwa sana kwani ndio inamrahisishia kujua ukubwa Wa kazi yake,kupata majibu ya maswali yake nk.
RIWAYA : MPANGO WA CONGO
SEHEMU YA 21
Taa za gari lile ziliendelea kumulika na punde wakashuka watu watatu waliokuwa wamevaa mavazi ya Polisi!!
"Dadeki!!" alijisemea Remi.
Askari wale walipomfikia Remi wala hawakujihqngaisha kuuliza linalomkimbiza wao moja kwa moja wakamdaka!
"Nyie ndo wazururaji tunawatafuta twende...!!" alisema askari mmoja huku akianza kumsukuma bila utaratibu.
Remi akataka kujitete lakini askari mmoja akamkatisha huku akitishia kumtandika makofi.
Remi aliwatizama vijana wale ambao walizidi kusogea huku wakijifanya kama hawana habari na lile lililokuwa linaendelea kwa Remi.
Remi akanyoosha mkono ili aseme kuhusu vijana wale.
"Nitakutia mikwenzi sasa hivi nyau wewe!!" alikoroma askari mmoja huku sasa akimsukuma kwa jaziba.
Remi alipandishwa kwenye karandinga kisha safari ikaanza na ndani ya karandinga kulikuwa na vijana wengine watatu ambao nao inaonekana walikutwa na masaibu kama ya Remi.
Waliitwa wazururaji.
Vijana waliokuwa wakimkimbiza Remi wao walipitiliza na kushuhudia Remi akiwa ndani ya gari la Polisi.
Hilo lingewagarimu na hawakutaka Remi atue mikononi mwa jeshi la Polisi.
Mmoja wao akanyanyua simu yake na kumpigia mtu waliekuwa wamehifadhi jina lake ELCHAPO!!
walitoa taarifa kama ilivyo kisha wakaambiwa wao kazi yao imeishia pale hivyo waendelee na majukumu mengine.
Vijana wakatokemea wanakokujua.
Gari lile la Polisi likiwa na watuhumiwa wa uzururaji,liliendelea kuikata mitaa na kurudi barabara ya Musoma.
Wakiwa wamefika njia panda ya kiwanda cha maji cha AquarRock na Tanesco; ikatokea pikipiki kubwa ambayo hakuna alieitilia shaka na safari ikaendelea huku kukiwa hakuna askari alieitilia shaka pikipiki ile.
Ni hadi gari lilipofika karibu na kiwanda cha samaki cha Nile perch hatua kadhaa kabla ya kuifikia barabara kuu ya Musoma road.
Ni kitendo kilichofanyika kwa weledi wa hali ya juu kutoka kwa mtu aliekuwa juu ya pikipiki.
Kwanza aliongeza mwendo wa pikipiki kama anaehitaji kulipita gari lile,lakini haikuwa hivyo badala yake alipofika karibu na upande waliokuwa askari na watuhumiwa wao akatoa kitu kama kibomu kidogo ambacho aliking'ata na kukitupia nyuma ya gari ambapo kilianza kutoa moshi mzito na kupelekea waliokuwamo kuanza kukohoa mfululizo.
Baada ya yule jamaa kufanya vile aliongeza mwendo zaidi hadi usawa wa dereva ambapo nae alimtupia kibomu kile jambo lilklofanya dereva kukosa mwelekeo huku akiongeza mwendo badala ya kusimama kisha akaenda kuyapamia magari yaliokuwa yamepaki kwa ajili ya kushusha na kupakia samaki.
Kilichofuatia ni ajali mbaya sana.
Gari la Polisi lilinyanyuka juu kisha likajipigiza chini na kurudi tena juu kisha kuanguka na kubiringita mara mbili kisha likatulia huku moshi wa vile vibomu ukitanda angani ukiwa umechanganyikana na vumbi.
Watu walishika vichwa wengine vinywa vyao kwa kutokujua kama kuna aliesalimika kwenye ajali ile.
Jamaa aliekuwa kwenye pikipiki akageuza haraka kurudi ilipokuwa imedondokea gari ile na alipofika akapaki haraka na kuwa kama anataka kutoa msaada kwa watu waliokuwa nyuma ya karandinga ile.
Ila lengo lake halikuwa hilo,lengo lake lilikuwa ni Remi.
Akiwa mzima ama mfu ni lazima ampate!!
******
Mtega nyoka alikuwa ameshazunguka kila kona akijaribu kutazama wapi anaweza kuona ilipo Club D ila hadi inapata kuwa saa tano usiku bado hakuwa amefanikiwa kuiona..
Alichoka na alihitaji kupumzika!!
Alimwelekeza dereva wa bajaji ampeleke Meko darajani kulipokuwa na baa ya Tesha.
Alishuka na kuingia ndani ya baa ile iliokuwa imejaza watu wa kila aina,wengine walikuwa wanaserebuka na wengine walikuwa wamebambiana ili mradi tu kila mtu na furaha yake usiku ule.
Akachagua kiti kimoja kilichokuwa kipo wazi bila kukaliwa na mtu.
Mtega nyoka alipenda sana wanawake ila si wanawake wa kutongoza. Alipenda wahudumu wa baa ama makahaba kwa sababu wanawake wa kawaida huwa haamini usalama wake mana wengine hutumiwa kumfuatilia nyendo zake.
Makahaba ni nadra mana haingekuwa rahisi kujua ni lini na wapi angeingia kuchukua ili ajistareheshe.
Alihisi anakuwa salama zaidi akiishi bila kupenda.
.
Akiwa bado anapepesa macho ili kupata yule ambae angemfaa,mhudumu akamfikia na hakuwa na budi kuagiza kinywaji alichokipenda.
Kuna kitu aligundua!!
.
Tofauti na siku zote ambazo huwa kuna makahaba wengi ndani ya baa ile,ila siku hii hakuona kabisa wingi ule na kila aliekuwepo alikuwa yupo bize na mambo yake huku wengine wakiwa wamekaa watatu ama wawili wawili.
Hakushobokewa kabisa siku hiyo.
Alizidi kuukata tu huku wanawake wakitoka mafungu mafungu na kutokomea huko nje!!
Akaona si vibaya akiuliza.
Akamwita binti mmoja aliekuwa amekaa karibu na yeye!!
"Samahani tunaweza kuwa wote usiku huu?" alihoji Mtega nyoka.
"Unataka kuchetua ama unataka kulala?" alihoji binti yule huku macho yakiwa juu juu kama mkojoa stendi.
"Kulala!!" alijibu Mtega nyoka.
"Babu wee utanikosesha Dolali bure wewe!!" alisema kishambenga yule binti huku akichezesha vidole vyake kwa kuvigusanisha akiashiria pesa.
Mtega nyoka akashituka kidogo kisha akahoji.
"Nakukosesha vipi hizo Dolali wakati nami nakupa pesa utakayo?"
"Aah wee leo kuna midolali haiwezi kuwa kama hivyo visenti vyako labda nikuchetue dakika mbili hapo utoe vinyege vyako hivyo!!" alisema Yule dada huku akitikisa makalio yake kwa kuhamasisha kingono.
"Ooh sawa, vipi hizo Dolali mwazichukua wapi?" alihoji tena Mtega nyoka huku akiwa hajatilia mkazo swali lake.
"Aaah wa wapi wewe!!! Yani hujui huu mwisho wa mwezi Club Dekuku kunakuwa hivi yani..." alisema yule binti huku akimshangaa Mtega nyoka kwa kutokujua kinachoendelea huko Dekuku ambapo alionesha ishara ya kimbea yani kunakuwa moto.
"Dekuku!?" alishangaa Mtega nyoka huku akikaa vyema kwenye kiti chake.
"Ndio!; afu wanipotezea muda mi najiandaa bwana!" alisema yule binti huku akianza kuondoka.
Mtega nyoka akamdaka mkono yule binti ambae aligeuka kwa mshangao wa kitendo kile.
Mtega nyoka ili kumtoa wasiwasi akamwonyesha shilingi elfu kumi na binti akatabasamu kama chatu alieona windo.
"Aaah!! Kitu gani huko kinachowapeleka?!" alihoji Mtega nyoka huku akimpa ile pesa.
"Tunaenda kulala na vijana, ambao hutupa pesa nyingi sana kulingana na huduma utakayompa na vile ataridhika!" alisema yule binti.
"Huwa wanatoka wapi vijana hao"
"hakuna anaejua ila huwa tunafuatwa hapa na gari na kupelekwa huko kila mwisho wa mwezi!"
"unajua ilipo hiyo Dekuku?"
"Hapana huwa tunafungwa vitambaa tukishaingia ndani ya gari!!"
Mtega nyoka alizubaa kidogo huku neno Club D na Dekuku yakipita kichwani mwake kama upepo na asijue kama ni aina moja.
Akakumbuka maneno ya Zana bwana mdogo aliemteka kwenye msiba wakati akimfuatilia Malima.
Mtega nyoka alitoka nje ya Club ile kisha akatafuta sehemu nzuri na kutulia huku lengo likiwa ni kusubiri aone hilo gari.
Haikupita nusu saa gari aina ya kosta likapaki nje ya ile baa na dakika tatu baadae wakatoka mabinti kama saba hivi na kuingia ndani na haikupita dakika wakatoka kule baa wadada wengine kumi akiwemo yule aliekuwa anaongea na Mtega nyoka.
Punde ile gari ikaondoka!
Mtega nyoka haraka akadandia pikipiki na kumwelekeza dereva wake aifuatilie ile gari ambayo ilikuwa inaenda taratibu bila papara.
Ile gari ikawa inazunguka mitaa tofauti tofauti bila kuonesha ni wapi inapoenda.
"Big; mbona tunazunguka tu.." alihoji dereva wa pikipiki.
"Usiogope nitakulipa!!" alidakia Mtega nyoka.
"Sio kunilipa hapa mafuta yanaenda kukata broo!!" alisema dereva huku akiegesha pembeni.
Mtega nyoka akafyonza huku akishuhudia gari ile ikiongeza kasi na kupotea yani ni kama dereva alijua wanafuatiliwa na alitumia nafasi hiyo kutokomea.
Mtega nyoka alibaki akitoa matusi tu bila msaada na eneo walilokuwapo ni eneo pweke ambalo halikuwa na pilika za watu.
Wakageuza na kurudi ili kuokoa mafuta yaliokuwa yamesalia.
Mtega nyoka alilaani sana siku hiyo.
Akaenda kupumzika huku akingoja ahsubuh iliokuja na mambo mengi licha ya kuwa na muda kidogo!!
*****
Shusha utabiri wako tujue kinachofuata!!