Jasusi Honda ndani ya mpango wa Congo

Kumbe ni riwaya NNE nazisubiri mkuu maana nimeiona moja tu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
RIWAYA: MPANGO WA CONGO

SEHEMU YA 24

Na Bahati Mwamba


Kitambulisho kile alikigeuza huku na huko bila kupata maana ya kile alichokiona.
Kitambulisho kilikuwa kina picha ya Makanisa yaliojengwa pamoja huku milango ikiwa inajitegemea na kila mlango ulikuwa na msalaba juu yake!

"Ina maana gani hii!!" Mtega nyoka alijiuliza bila kupata majibu sahihi.

Haraka akatoka ndani ya ofisi ile na kuelekea mapokezi kisha akatimka kutoka ndani ya Kasuku Contractors.

Haraka akadandia pikipiki iliokuwa inashusha abiria ndani ya buzuruga plaza.

Lengo lilikuwa ni kuwahi ilipo Kanisa ya wokovu kama ananuani ya Mwasu ilivyoonesha.
.

Alipanga kumuwahi Remi.

*****

Mwasu na Remi walifika salama ndani ya makazi ya Remi. Hii ilikuwa ni tofauti na maelezo aliyopewa ya kuwa anaenda kutibiwa kwenye kituo kikubwa cha matibabu.

"Usijali mdogo wangu,nitakupeleka hospitali kisha tutarudi tena hapa na utakuwa ukitibiwa hapa hapa." Mwasu alimtoa wasiwasi Remi.

Remi hakuwa na usemi alibaki mtazamaji.

Ndani ya nyumba ya Mwasu kulikuwa kuna mtu mwingine na walipoonana na Remi wote hawakutambuana.

Alikuwa ni Malima.

Malima alifika nyumbani kwa Mwasu ili atafute nyaraka alizopoteza kwa kuhisi huenda aliwahi kuziacha pale.

Na sasa ilikuwa imepita saa nzima huku akiwa amepekua kila pahali bila kuona alichokihitaji.

Malima hakumtabua Remi kabisa licha ya kuongea usiku wa siku iliopita.

Malima alishangaa kidogo kisha akahoji.

"Kabla hata sijajua mnaendeleaje,nadhani huyu mgeni hakustahili kuwapo hapa, alitakiwa awe anapewa matibabu sasa hivi"

Mwasu hakumjibu badala yake alikuwa anafanya jitihada za kumkaliza Remi kwenye sofa.

"Hauna pesa ya matibabu nikupe?" aliendelea kuhoji Malima.

"Pesa ninayo ila nina sababu zangu za kumleta hapa kwanza." alijibu Mwasu.

"Sababu gani kwa mtu alieumia kiasi hiki?" alimaka Malima.

"Unataka kuijua?!" alihoji Mwasu huku akimtizama Malima usoni bila kupepesa macho yake.

"Sina shida ya kuijua Mwasu; zaidi ya afya ya huyu binti kuzingatiwa, akifia hapa je!!" alisema Malima huku akitanabaisha wasiwasi wake.

Mwasu akitikisa kichwa tu huku akielelea chumbani kwake ambako alikuta kumevurugwa vya kutosha.

Mwasu alitabasamu!!

Alijua nini Malima alitafuta.

Dakika tatu badae Mwasu aliungana na Remi sebuleni huku wakimwomba Malima awapishe kidogo.

Hakuuliza akatoka kwenda kibalazani.

"Ni nini kimekukuta Remi!!" alisema Mwasu huku akikaa kwenye sofa lililokuwa kando ya sofa alilokalia Remi.

Remi alikaa kimya kidogo kisha akasema;

"Tangu tulipoachana pale kambini, kulitokea sintofahamu kadhaa hivi ambazo inasemekana zilianza kuwapo hata wakati upo..." alinyamaza Remi baada ya kujikuta roho yake inakuwa nzito kuendelea kuzungumza.

Hata yeye mwenyewe hakujua ni kwanini.

"Aah nitakweleza siku nyingine Dada!!" alisema Remi huku akishika kichwa kuashiria hajisikii vizuri.

"Ooh pole sana!!" alisema Mwasu huku akinyanyuka na kwenda kumshika kichwa Remi kwa kutumia mgongo wa kiganja chake.

***

Malima aliendelea kuwaza ni vipi atamwambia mkurugenzi wake kuhusu upotevu wa nyaraka za jengo muhimu sana.

Alijikuna kichwa akiwa haelewi ni lipi afanye.

Malima kila alipofikiria bado akili yake ilimpa kumbukumbu ya mwisho ni Mwasu alieondoka na gari huku kukiwa na nyaraka.

"Ziko wapi!!" Malima alijigonga kichwa huku akishindwa kabisa kuchanganua mambo yalivyo kuhusu nyaraka zile.

Kama ni akili kugoma,basi za Malima ziliamua kusimama kabisa kutatua kitendawili kile.

Alihofu!!

Alihofia kazi yake kupotea.

****

Mwasu bado walikuwa wamekaa wanazungumza mambo mbalimbali ya huko nyuma na jinsi walivyotokea kushibana pindi walipokuwa pamoja.

"Dada hakuna aliekushitukia kwamba wewe ni mgeni hapa jijini?" alihoji Remi.

"unajua mdogo wangu, Tanzania sio kama nchi zingine. Ni ngumu sana mgeni kuulizwa ukazi wake, hivyo nilipofika hapa wala hakuna aliehangaika kujua ubini wangu,hivyo nami sasa ni Mtanzania." alijibu Mwasu.

"Mh!! vipi sasa ukishitukiwa?" alihoji tena Remi.

Mwasu aliachia cheko dogo huku akijifuta midomo kwa kiganja cha mkono wa kulia.

"Ni ngumu sana mdogo wangu,nimeshakuwa Mtanzania kabisa sasa,najua lugha yao na ninajua tamaduni zao,hivyo si rahisi kabisa" alijibu Mwasu.

Remi aliguna tu.

"kwanini hujiulizi kuhusu wewe Remi!!" alihoji Mwasu.

"Basi tu imenibidi na ni bora nikamatwe!" alijibu bila shaka yoyote Remi.

Mwasu akatafakari kwa kauli ile kisha akahoji tena.

"Kwanini ulikuja huku?"

Remi alibabaika kidogo kujibu huku akijiuliza kama ni sahihi kwake kumwambia yaliomsibu dada yake huyo wa hiyari.

"Mmh nadhani kwa sasa ningepona kwanza halafu tutazungumza kwa kina kabisa hili suala." alisema Remi.

Mwasu akapandisha mabega kisha akatazama saa yake na kutaka kunyanyuka ila Remi akauliza swali.

"Hivi Amokachi nae nilisikia kalowea huku,mliwahi onana?"

Lilikuwa swali la mtego ambao Mwasu hakujua autegue vipi. Akababaika kidogo kisha akageuka na kumjibu.


"Nadhani hana hata mawasiliano yangu,hivyo ni ngumu kuonana. Mwanza kubwa hii!!"

Remi akatikisa kichwa kukubali bila kuongeza neno.

"aah hujala bado,ngoja niandae chakula ule na shemeji yako!!" alisema Mwasu huku akielekea upande wa jiko lililokuwa ndani ya nyumba ile.

Remi alibaki na maswali kadhaa baada ya kubaki peke yake.

Siku anaingia Mwanza na kuelekea Igoma alikoambiwa ni ofisini kwa Mwasu; macho yake mwenyewe yalimuona Amokachi na Mwasu wakiteta jambo na ndio sababu yeye akatimua mbio ili asiingie mikononi mwa Amokachi anaemtafuta kwa udi na Uvumba.

Sasa alishangaa Mwasu kumwambia hawajawahi kuonana.

Utata!!

Jambo lingine ni vile alivyoona maisha safi ya Mwasu ambayo ni tofauti na kazi anayofanya ya umama ntilie hadi watu wakamwita Mama Ujazo.

Hapo akamfikilia Malima ambae anaeza kuwa ndie mtu aliempangia Mwasu.

Hapo napo akabaki njia panda.

Remi akabaki na fumbo.

***

Nje bado mawazo yalimzonga Malima akabaki amejiinamia tu bila kufanya lolote huku mara kwa mara akichorachora chini bila kujua alichokichora.

Mara akaona kiatu kikubwa(Buti) kikisimama miguuni pake.

Malima akanyanyua uso wake ili aone mmiliki wa buti ile ya jeshi.

Alishuhudia mwanaume mwembamba mrefu aliejenga kimazoezi akiwa amesimama akimtizama yeye.

Kwa utazamaji ule; Malima akagwaya.

"Simama!!" Malima aliamriwa kwa sauti kavu.

Akatii!!

"Haya geuka rudi ndani!!" aliamrisha tena yule mtu.

"Kiongozi tungetambuana kwa..." Malima alitaka kujitetea akaishia njiani baada ya kuona bastola ikimwangalia.

Malima alishikwa na tumbo la kuhara gafla huku akishindwa hata kupiga kelele.

Akajikuta akinyanyua mikono juu kusalimu amri huku akigeuka na kuelekea ndani.

Kule ndani Remi alipitisha wazo moja tu.

Alihitaji kutoroka pale!!

Akajaribu kusimama bado hakuwa na utimamu sawia.

Akajaribu tena.

Mara hii akaweza kusimama na akaanza kupiga hatua ili afike mlangoni.

Wala hakumalizia hatua zote mbili akajikuta akiingiwa na ubaridi wa gafla baada ya kuona Malima akiingia huku akiwa amenyoosha mikono na nyuma yake kukiwa na mtu alieshika bastola.

"Amokachi!!?" alijikuta akitamka bila kupenda..

"Ulidhani unaweza kukimbia kuliko mimi Remi!!?" alihoji amokachi huku akimalizikia kuingia ndani.

Muda huohuo Remi alimshuhudia Mwasu akitokea kule jikoni akiwa hana wasiwasi na kile alichokiona pale sebuleni.

"Kazi nzuri Mwasu; Pimbi wote wamenaswa" alisema Amokachi huku akitabasamu.

Mwasu nae alitabasamu huku akienda haraka na kuuchukua mkoba aliokuwa nao Remi na kuufungua.

Hola!!

Haukuwa na kitu ndani yake! Ulikuwa tupu.

"Viko wapi ulivyochukua?" alikoroma Mwasu huku akiukunguta mkoba ule bila mafanikio zaidi ilidondoka pedi moja tu.

Amokachi na Mwasu walibaki wamepigwa na butwaa.

"Hii ndio sababu ya kumleta mgonjwa hapa!?" alihoji Malima huku akitetemeka.

Mwasu alicheka kidogo.

"Ningeshangaa kama usingeikumbuka hii sababu!!" alijibu Mwasu.

"Niacheni mana nadhani sihusiki!!" alijitetea Malima.

Amokachi alicheka kwa kebehi.

"Yani ungejua wala usingejisumbua kujitetea kunguni wewe!!" alisema Amokachi.

Malima akapigwa na butwaa. Anaingiaje kwenye mkasa asiojua?

Jibu halikukawia!!

"Ramani sahihi iko wapi?" alihoji tena Amokachi.

Malima alitoa macho kwa mshangao kama changudoa aliedondosha simu yenye namba muhimu.

"Hata mimi naitafuta,tena wewe unai..." Malima alikatishwa na mluzi uliopigwa na Mwasu.

Punde wakaingia vijana wengine wawili ambao waliwaziba midomo kwa vitambaa fulani na punde Remi na Malima walijikuta hawana fahamu.

Walibebwa kama mizoga.

Majibu wangeenda kuyatoa huko huko wanakopelekwa.


*****



Bado unaweza kupata riwaya hii na nyingine tatu kwa Tsh 3000/=

Namba ya malipo ni, 0758573660 jina Bahati Mwamba.
 
Barikiwa mkuu kudo

The Unknown
 
Hii namba uliyoweka haipatikani na ikipatikana haiko active Sana.mtu anataka kununua simulizi anakusms hajibiwi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio kweli mkuu ipo hewani kila dakika na kila sms inayoingia najibu. Hakuna alieboeka na aina yangu ya ujibuji on time.

Kama huipati basi piga hapa 0624155629 ila malipo fany hapa 0758573660 nipo hewani hata saa nane usiku
 
Sio kweli mkuu ipo hewani kila dakika na kila sms inayoingia najibu. Hakuna alieboeka na aina yangu ya ujibuji on time.

Kama huipati basi piga hapa 0624155629 ila malipo fany hapa 0758573660 nipo hewani hata saa nane usiku
Nishamaliza Mambo na Sasa hivi nimekuja ku- unsubscribe kwenye huu uzi. Ila sijavutiwa na mwisho wake yule jamaa kujifia kabla hajalipa mabaya aliyotenda.

Ila uko safiiiii safiiiii Sana.

Ukiwa na simulizi nyingine mpya nitag please mr KUDO.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaa ilikuwa lazima afe kwa kihoro sio kwa timu ile ilioingia
 
RIWAYA : MPANGO WA CONGO.

SEHEMU YA 25

****

Solomoni Bukaba alibaki akiwa hana la kufanya licha ya kuzidi kuzibana pumzi ili asiendelee kuvuta hewa nzito ya moshi.

Alijikakamua licha ya mwili wake kutokuwa na nguvu za kutosha kufanya vile ila ilikuwa ni lazima ajiokoe la sivyo maisha yake yangelifika tamati siku hiyo.

Akarudi kulala tena baada ya kugongwa na ubao uliotoka juu ya paa la nyumba.

Kuna sehemu alihitaji kuifikia na ilikuwa mita mbili tu kutoka alipo.

Alijivuta tena licha ya kuwa na udhaifu uliokithiri.
Akajivuta hadi alipopafikia alipopahitaji.

Akalala na kutulia eneo lile na taratibu akaanza kuzama kwenda chini na upande wa zulia aliokuwa amelalia juu yake.

Alizama kabisa hadi alipoikuta chemba ya maji machafu iliokuwa inatiririsha maji yake bondeni mabatini.

Akatulia bila kufanya jitihada zozote kujiokoa ndani ya maji yale yaliokuwa yanatiririka kwa kasi ya ajabu.

Solomoni alijua ni wapi maji yale yangemfikisha.

Akabana pumzi ili zimsaidie kufika salama huku moyoni akishukuru idara yake kumweka kwenye nyumba kama ile.

Haikuchua dakika tano mdomo wa bomba la maji machafu ulimtupa binadamu kwenye mto uliokuwa unatiririsha maji kuelekea ziwa Victoria(Zamani Nyanza).

Alipondondoka hakutaka kusombwa na maji hadi ziwani ila alifanya jitihada kidogo kujinasua kutoka kwenye mkondo wa maji na kujitupa pembeni kidogo.

Alijua watesi wake walitaka afie ndani ya nyumba yake ila mungu alikuwa upande wake.

Alisimama kwa tabu kidogo huku jeraha la risasi likimuuma na kichwa pia kilimuuma kwa kutokwa na damu nyingi.

Alijiinua na kujikokota akatoka bondeni huku akili yake ikimuwaza mwanamke wa kinyarwanda akietokea kumpenda sana.

Sundi!!

Aliwaza sehemu pekee yenye usalama kwake ni nyumbani kwa mpenzi wake Sundi.

Makazi yake hayakuwa mbali sana na kwake.

Sundi aliishi karibu na kiwanda cha kusaga mifupa.

***

Sundi hakuwa amepata usingizi,kuna kitu kiliisumbua roho yake usiku ule na kila alipojaribu kulala alijikuta akijiwa na ndoto za ajabu ajabu.

Sundi alikuwa na taaluma ya utabibu hivyo ndani kwake hakukosekana dawa na baadhi ya vifaa kwa ajili ya kazi yake hiyo endapo kungelitokea dharura yoyote.

Alinyanyuka kutoka kitandani alipokuwa amejilaza na kuelekea kwenye chumba alichokifanya kama ni stoo ya vifaa tiba vyake.

Huko akachukua dawa za usingizi na kumeza kisha akatulia kwenye kiti kilichokuwamo mle.

Bado mawazo yalimwandama.

"Yeye hakutarajia! Hata mimi sikutarajia ni bahati mbaya tu" alijisemea huku akijifunga kanga yake vizuri kuzungushia kifuani.

Akapiga hatua kadhaa na kuelekea chumbani kwake.

Hakika Sundi hakuwa sawa kabisa.

Kwanini!!

Hakuna aliejua!!

Akiwa anakaribia kusombwa na usingizi wa dawa,kengele ya mlangoni ikalia.

Akashituka kisha akatazama ukutani.

Ilisomeka saa ni saa tisa na nusu alfajiri.

Nani tena!! Alijiuliza bila kupata jibu.

Kengele ikalia tena.

Akasita kunyanyuka mana alikuwa na miadi na mtu saa kumi na moja ila si saa tisa usiku.

Alijiwazia kama kuna mpenzi wake yeyote aliewahi kumgongea usiku mkubwa kama huo.

Hakupata kuwapo!!

Akanyanyuka akavaa suruali harakaharaka bila hata kuvaa chupi kisha akaokota fulana nyeusi iliokuwa imedondoka chini akaivaa.

Akajitizama baada ya kuivaa fulana ile.

Ilimjia sura ya mahabuba wake Solomoni Bukaba.

Akatabasamu!!

Akavaa raba zake harakaharaka na kuelekea mlangoni ambapo alifungua na kuelekea geti la nje ambalo ndiko kengele ilitokea.

Alifungua!

Kwanza aliruka nyuma kwa uwoga huku akitoa kilio cha woga kwa kile alichokiona.

Alikutana na sura ya Solomoni iliochakaa na kuchafuka huku akiwa na majeraha hapa na pale mwilini mwake.

Solomoni Bukaba alibaki akiwa amezubaa mlangoni huku akishindwa kuelewa mshituko ule uliompata Sundi ni kwa kumuona alivyo ama kuna lingine.

Hakuwa na nguvu za kuwaza zaidi!

"Nipe msaada tafadhali" alisema Solomoni huku akijiegemeza kwenye geti lililoshindwa kuhimili uzito wake na kurudi nae ndani kisha likambwaga chini baada ya kukosa mhimili katika mwili wake na geti kuteleza.

Sundi alibaki akiwa amesimama huku amejishika mdomo kwa mshangao.

Kuna mawazo fulani yalikuwa yanakinzana kichwani kwake na hakujua afuate lipi kwa wakati huo.

Nguvu ya mapenzi ikamwelemea!!

Akamvaa Solomoni pale chini kisha akamnyanyua na kumkokota hadi kwenye chumba maalumu kilichokuwa kinatumika kama stoo ya vifaa tiba vyake.

Huko harakaharaka akamlaza kwenye kitanda na kumvua nguo zote ambazo zilikuwa zinanuka sana kisha akawasha taa maalumu na kuanza kumsafisha mwili kwa dawa maalumu kisha akaanza jitihada za kumtoa risasi na alipomaliza alimsafisha sehemu aliokuwa amechomwa kisu na kupashona.

Pale ndani alikuwa na akiba ya chupa tatu za damu salama.

Akachukua moja na kumtundikia Solomoni ambae hadi wakati huo alikuwa yu hoi sana na kichwa kilimgonga sana.

Licha ya udhaifu wa mwili ila kichwani bado swali lilibaki moja kuhusu Sundi.

Ni kweli yeye ni tabibu wa hospital kubwa tu jijini Mwanza ila haimaanishi ndio awe na hospital yake ndogo hapo nyumbani. Lakini pia alijiuliza kuhusu chumba walichokuwamo ambacho hakuwahi kuingia licha ya kuwa na mahusiano kwa muda murefu sana na Sundi.

Sawa vifaa tiba kwa tabibu ni muhimu kwa dharura ila sio kuwa hadi na damu ya akiba.

Huwa anamtibu nani sasa!?

Majambazi yanamtumia!!?

Hakukuwa na wa kumjibu maswali yake.

Solomoni alipitiwa na usingizi baada ya kuchomwa sindano ya usingizi na tabibu wake Sundi.

Sundi alibaki akimtizama Somolomon huku akitikisa kichwa.

Akachukua simu akatafuta jina fulani akataka kulipiga ila wazo lingine lilikataa!!.

Alijikuta chozi la huruma linamdondoka.

Alitamani kufanya vitu viwili kwa wakati mmoja.

Sundi akajikuta njia panda.

Akatazama saa yake kwenye simu ilionesha ni saa kumi na moja na dakika ishirini zilisalia dakika chache tu kabla hajaonana na mtu mwingine pale ndani.

Kizungumkuti!!


****

Riwaya hii bado inapatikana kwa bei ya 3000/= na bonus ya riwaya tatu zingine.
Malipo fanya hapa 0758573660
 
Mkuu kongole sana " hii kitu sio mchezo Usaliti kila mahali naona hapo kuwa sundi na yeye ni Mafia .. So huyo jamaa aliye kikimbia Kifo nyumbani kwake " naona amekifuata mikononi kwa sundi " ..... labda itokee sundi amuonee huruma " nahisi sundi ndiye mdada aliyehusika na kwenda kuzichoma zile nyaraka ... Ila kwakuwa alikuwa amevaa kininja Jamaa alishindwa kujua kwamba aliye mvamia nimpenzi Wake "
 
Uko sawa mkuu, nilikua sijawaza hili, ila Sundi atafanya mistake kubwa ya kumuacha hai jamaa, tusubiri.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…