Jasusi Honda ndani ya mpango wa Congo

Jasusi Honda ndani ya mpango wa Congo

Ahahahaha mambo ya mtega nyoka
Riwaya : Mpango wa Congo

Sehemu ya 26

Simu : 0758573660

***

Sundi alikaa karibu na Solomoni ambae alikuwa ametopea kwenye usingizi mzito.

Sundi alikuwa bado anaitazama simu yake huku akiwa hana maamuzi sahihi ya nini anatakiwa kufanya wakati ule.

Kuna jambo lilikuwa linamsumbua moyoni mwake hasa alipomtizama Solomoni na majeraha yake mwilini.

Sundi akiwa bado ametopea kwenye lindi la mawazo,kengele ya mlangoni ikalia.

Sundi akavuta pumzi ndefu na kuzishusha kwa mkupuo kisha akasimama na kuzishusha pazia kuzunguka kitanda alichokuwa amelalia Solomoni.

Sundi akaenda kufungua mlango huku akihakikisha hakuna ambae angeweza kujua kama kuna mtu kalala kwenye kitanda kile.

Baada ya dakika kadhaa Sundi akarejea ndani ya chumba kile kile akiwa na mtu mmoja mrefu mwembamba aliejengeka vyema kimazoezi na kuelekea kuficha wembamba wake!!

"Tena kimetokea mbona jeraha!!" alihoji Sundi bada ya mtu aliekuwa akimtegemea kuingia akiwa na jeraha kubwa karibu na mguu!!

"aah ni harakati tu si wajua!!" alijibu yule mtu.

Ulipita ukimya wa dakika kadhaa huku Sundi akishika hiki na kile kuhakikisha anapata vifaa tiba sahihi kwa kumtibu yule bwana jeraha lake.

"inabidi ujikaze sitatumia ganzi!!" alisema Sundi huku akiinama ili kulitazama vyema jeraha.

"Ohoo kwa hiyo ndo kunikomoa au!!" alihoji yule bwana.

"Nope!!" alijibu Sundi huku akimwaga dawa ya kutoa wadudu nyemelezi kwenye vidonda..

Bwana yule akagumia kwa uchungu.

Dakika thelathini badae; Sundi alikuwa anamalizia kufunga bandeji kwenye jeraha la bwana yule.


Muda wote kulikuwa kimya kabisa.


"Kwa hapa hali ilivyo tunahitaji msaada wako wa hali na mali Sundi!!" alisema yule bwana.

Sundi akatazama kule kulipokuwa na mapazia meupe!

Alimwonesha ishara mtu yule ya kuwa watoke wakaongelee sebuleni.

Bwana yule wala hakuwa mbishi,alimwamini Sundi.

Walitoka na kuelekea sebuleni.

"Kuna nini tena!!" akihoji Sundi baada ya wote wawili kukaa kwenye sofa za kutazamana.

"X anaumwa sana na anahitaji matibabu zaidi ili kuokoa uhai wake." alisema yule bwana.
.

Sundi akaguna.

"sasa msaada wangu ni nini ikiwa sura tu ni ngumu kumuona?" alihoji Sundi.

"Kwa ilipofika ni ngumu tena kukwepa kuonekana ni lazima aonekane ili asaidiwe" alisema yule bwana.

"Sawa!! Lakini tatizo ni nini?" alihoji tena Sundi..

"Anakansa ya ngozi,inaonekana upasuaji wa ngozi aliofanya mara ya mwisho ndio umemharibu kiasi kile" alifafanua yule bwana.

Sundi aliguna tena.

"Sasa mpango utakuwaje kama yupo koma huyo bwana!" alihoji tena Sundi..


"Mpango ni mrefu!! Na umechukua watu warefu pia hivyo upo pale pale na ni lazima ufanikiwe japo bado tunakwamishwa na jambo moja tu!!" alisema yule bwana.


"Jambo gani tena!!" alihoji Sundi huku akikaa vyema sofani.

"Ramani haijapatikana bado na ili mambo yaende sawa ni lazima ramani ipatikane ili tuwe sawa siku husika!!" alisema yule bwana.


"ooh ok sawa,sasa mimi msaada wangu zaidi ni upi?" Sundi alihoji.

"ni kumpa huduma ya haraka zaidi ili tupange utaratibu wa kumsafirisha kwa matibabu zaidi" alijibu yule bwana.
.
"Sawa" alijibu Sundi.

"Vipi jana mlimaliza ule mwanya?" alihoji yule bwana.

Sundi akibabaika kidogo kisha akajibu.

"Yah! Kwani hujasoma hata gazeti?"

"Mambo mengi muda kidogo" alijibu yule bwana.

Sundi akanyanyuka kisha akaelekea chumbani kwake na baada ya dakika kumi alitoka akiwa amevaa vyema suruali nyeusi na fulana nyeusi na raba nyeusi.

Alipendeza kumtazama!!

Alipokwisha kufika sebuleni akamuomba yule mtu waongozane kutoka nje!!

Walitoka pamoja huku nyuma waliacha nyumba ikiwa na mtu ambae alimjua Sundi pekee.

***

Yawezekana Sundi hakuona vyema aina ya dawa ya usingizi aliomchoma Solomoni.

Alikuwa na hakika asilimia mia ya kuwa alimchoma Solomoni dawa ya kulala zaidi ya saa tatu.

Sivyo!

Alikuwa amechukua kichupa chenye dawa ya kumlaza usingizi mgonjwa dakika arobaini na tano tu!

Ilikuwa ni bahati mbaya iliomgarimu yeye na wenzie wote.

Lakini Pia ilikuwa bahati mbaya ile imebebwa na nguvu ya mapenzi ndani yake.

Solomoni alikuwa ameamka bado wakiwa wako ndani ya chumba kile cha kitabibu na maongezi aliyasikia.

Hata wakati wanatoka kwenda kuongelea sebuleni, bado yeye alinyata hadi mlangoni na kutega sikio lake vyema na kuyasikia maongezi ya Sundi na mtu yule.

Japo maongezi yao yalitawaliwa na mafumbo mengi ila yalimwachia alama ya kiulizo kichwani mwake.

X!
Ninani mtu huyo? Mgonjwa! Kwanini haendi hospitali anatibiwa kienyeji uchochoroni?

Yalikuwa ni maswali bila majibu.

Lakini Sundi ni nani hasa!!

Solomoni alianza kuingiwa na wasiwasi na mienendo ya Sundi.

Akapanga kufanya jambo.

Wakati Sundi na yule bwana wanaondoka kuelekea huko kusiko julikana,huku nyuma Solomoni hakujali maumivu alionayo.

Haraka akafungua mlango na kutoka hadi sebuleni,akaangaza huku na huko akaona nguo zikiwa zimetundikwa kwenye enga.

Zilikuww ni za kike! Akaziendea ila akasita baada ya kuona vile zimewekwa kimitego afu akaona ajabu nguo kuwekwa sebuleni.

Hakuzichukua!!.
.
Akaelekea chumbani kwa Sundi huko akaingia kwenye kapu la nguo chafu na kuchagua hijabu jeusi akalitinga kisha akajitazama kwenye kioo.

"*****! Leo naeza tongozwa huko!" kisha akacheka peke yake na kuondoka kuharakisha kuwahi Sundi na mtu wake wasije wakampotea!!


Bahati ilikuwa upande wake kwani wakati anaruka uzio na kudondoka nje na hijabu lake ni wakati huo aliliona gari likitoka mitaa ile.

Hakuwa na usafiri ila alijua barabarani atakuta usafiri hivyo haraka sana akawahi kukata uchochoro ambao alijua utawahi kumfikisha barabarani kabla ya gari ile haijafika.

Ndivyo ilivyokuwa.

Akasimamisha pikipiki na kumwomba dereva asubiri kidogo.

Dakika chache badae ile gari ikapita kwa mwendo wa kawaida tu.

Solomoni akaagiza dereva wa pikipiki aipite gari ile awe mbele yake.

Dereva akatii bila kushitukia sauti nzito ya kike ya abiria wake!

Ulikuwa ni mwendo wa dakika arobaini na tano hadi Solomoni alipoona lile gari likisimama yalipokuwa makanisa manne.

Eneo hili la makanisa manne ni eneo maarufu sana kulingana na aina ya makanisa yaliopo.

Lakini eneo hilo lilipewa umaarufu zaidi na kanisa la Efather!
Huku makinisa mengine matatu yaliojengwa kama jengo moja yakiwa hayajulikani ni dhehebu gani licha ya watu kusali kila jumapili kwenye mlango wa kanisa moja huku milango miwili ikiwa haijawahi kutumika kabisa kuingiza waumini.

Siku hiyo hakukuwa na ibada ila kulikuwa kuna magari mengi kidogo yaliongia na kutoka, mengine yakishusha na mengine yakipakia.

Kama ungeliona basi ungejua pale kuna kikao cha viongozi wa makanisa mana wakishuka watu waliovaa mavazi kama ya makasisi na wengine kama mapadiri wengine kama watawa wa kike na kiume.

Kilichokuwa kikiendelea huko hakuna aliejua!!

Sundi alishuka kwenye gari na mtu yule aliemfuata!.

Wakaongozana kuingia huko ndani.

Solomoni kutoka alipokuwa alijifanya kuendelea na shuguli zake kwa kumfuata muuza genge na kununu ndizi kisha akaondoka eneo lile. Huku akitizama kwa makini mambo yaliokuwa yakiendelea pale.

Solomoni alielekea karibu na kanisa la Efather ambalo wakati huo lilikuwa limefungwa!

Alienda sehemu kulikokuwa na makazi ya watu akatulia na kuangalia kilichokuwa kikiendelea kule.

Wakati akiwa bado anashangaa hili na lile akaona kuna mtu mwingine nae akiingia pale huku mbele yake kukiwa na gari jeupe kama la kubebea wagonjwa.

Gari lile halikusimama mbele kama mengine ila lilielekea upande wa pili kulikokuwa na geti na kuingia huko.

Yule mtu aliekuwa nyuma ya gari lile la wagonjwa hakuigia na gari lile badala yake alipitiliza na kwenda usawa wa geti la kuingilia nyumbani kwa mchungaji wa kanisa la Efather.

Macho ya solomoni yaliona yote yale.

Solomoni alimtilia shaka bwana yule alieelekea nyumbani kwa mchungaji.

Alitabasamu!!

Kumbukumbu zilimwambia aliwahi kumuona mtu yule akitoka ofisini kwa OCD siku alipopewa karatasi za ajabu ambazo nusura zimtoe roho.

Alimwona mtega nyoka!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jioni nitaiendeleza mimi mwenyewe hapa mr honda so worry out

Sent using my iPhone using jamiiforum app
 
Back
Top Bottom