Jasusi Honda ndani ya mpango wa Congo

RIWAYA : MPANGO WA CONGO

SEHEMU YA 27

SIMU 0758573660


***

Mtega nyoka hakuwa mbali na nyumba ya Mwasu ila alishindwa kuingia baada ya kuona tukio fulani akiwa hatua chache kutoka ilipokuwa nyumba ile.

Alikuwa na mwenyeji wake aliemwongoza pale.

Mwenyeji alimwonesha tu wakiwa mbali nyumba ya Mwasu.

Ni wakati akipiga hatua fupifupi ndipo alipoona watu wawili kibalazani.

Mmoja alikuwa amesimama na mwingine amekaa.

Aliekuwa amesimama alikuwa na wajihi sawa na mtu aliepambana nae Buzuruga Plaza siku kadhaa nyuma.

Mtu aliekuwa amesimama alimwona alivyochomoa bastola yake kutoka kiunoni kwa kasi ya ajabu na kumwelekeza jambo mtu aliekuwa amekaa.

Mtu aliekuwa amekaa wakati anasimama ndipo mtega nyoka alipomuona vyema.

Alikuwa ni Malima.

"Kumekucha!!" alijisemea Mtega nyoka..

Alijibanza nyuma ya nyumba iliokuwa jirani.


Haukupita muda mrefu aliona wakitokea vijana wengine wawili na kuingia ndani.

Zilipita dakika tatu ndipo alipoona watu watano wakitoka ndani huku wawili wakiwa ni Malima na Remi.
Na wengine ni mtu mrefu waliepambana Buzuruga Plaza na vijana wengine wawili.

Nyuma yao alitokea Binti mmoja mrembo sana ambae aliishia mlangoni tu na kuwasindikiza kwa macho.

Watu wale ambao walitembea ki kawaida tu bila kuonesha kama kuna mateka kati yao,walipita nyuma ya nyumba walimokuwamo na kutokea kwenye uwanja wa kanisa la Wokovu.

Huko walikuta gari ikiwa imenawangojea!

Wakapanda na kuelekea barabara kubwa kwa kupitia Nyakato shule ya msingi kisha wakakamata barabara kubwa na kuwa kama wanaelekea buzuruga.

Walipofika kona ya Nyakato sokoni,walikunja na kuelekea Meko,walipita karibu na baa ya ShaTemba na kuelekea njia ya vumbi ya Meko majanini.

Nyuma yao alikuwapo Mtega nyoka safari hii akiwa na pikipiki alioendesha mwenyewe huku abiria akiwa ni mwenye pikipiki.

Kwa msaada wa mwenye pikipiki, alimwelekeza kama wenye gari wamepitia njia ya Meko majanini basi wataenda kutokea njia ya Meko shule ya msingi hivyo wao waelekee shuleni na wangoje hapo.

Baada ya dakika kadhaa ilipita gari ya wagonjwa ikitokea Meko majanini.

Mtega nyoka aliona mtu aliekuwa amekaa kushoto mwa dereva.

Alijua wamebadilisha gari!

Akaifuata gari ile ya wagonjwa.

Safari yao ilikuwa ya uangalifu sana ili wasije wakashitukiwa.

Gari ile ilienda kuishia makanisa matatu na ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Mtega nyoka kufika eneo lile.

Hapo ndipo Mtega nyoka alipoona majengo sawa na yale yalioko kwenye kadi alioichukua mifukoni mwa mvamizi aliemuua bwana Kindo Seleman; Mkurugenzi wa Kasuku Contractors.

"Sasa kama ni kanisa ile kadi ya nini?" alijisemea Mtega nyoka huku akielekea kwenye makazi ya mchungaji wa kanisa la Efather.

Bado Mtega nyoka nae alikuwa anashangaa harakati zilizokuwa pale.


Akili yake ilishindwa kabisa kupata walau lililokuwa likiendelea pale.

Kama ni kikao basi ilitakiwa watu waingie na kutulia! Ila watu walikuwa wanaingia na kutoka.

Lakini pia yalikuwa ni mavazi yao.

Mavazi waliovaa ilitakiwa yavaliwe na waumini wa madhehebu ya Roman Catholic ama KKKT na si vinginevyo!!

Kwa mtazamo kanisa lile lilikuwa sawa na kanisa la kakobe ama Mzee wa upako ama wachungaji wenye sifa za utajiri kuliko uwezo wa waumini wao.

Sasa tangu lini makanisa ya aina hiyo yakawa na watawa?

Ajabu hii.


Ilikuwa ni wakati akitoka huko kwa mchungaji ndipo alipomuona mwanamke alievaa hijabu jeusi na kufunika uso wake wote na kubakiza macho tu.

Mwendo!!.

Aliutazama mwendo wa mwanamke yule.

Hata!!

Mwanamke gani huyu anatemebea kama kakanyaga moto!!

Aliachana nae akapanda pikipiki iliomleta pale na kutokomea.

Mwanamke wa hijabu nae akapanda pikipiki iliomfikisha pale na kuondoka.

Huku malipo ya dereva akimwandikia kwenye karatasi na kumuomba dereva afike kituo cha polisi atapewa pesa yake yote endapo akimwonyesha karatasi ile OCCID.

Dereva wa pikipiki akakubali japo roho ilimdunda.

Polisi hakuzoeleki!!


*****

Solomoni Bukaba alirudi ndani kwa Sundi na kuvua yale mavazi kisha akaenda kuyarudisha kama alivyoyakuta na kurudi kule chumbani alikokuwa amelala.

Akalala kama alivyoachwa.

****

Mtega nyoka alikuwa ameona Malima alivyotekwa pamoja na Remi.

Hivyo akapanga kurudi hadi nyumbani kwa Mwasu ili ambane Mwasu.

Hakuchukua zaidi ya saa mbili akawa yupo mlangoni kwa Mwasu.

Akagonga na kutulia.

Punde mlango ukafunguliwa akachomoza binti mrembo mwenye asili ya watu wa Rwanda ama Burundi.


"Nikusaidie nini!" Alisema Mwasu huku akimtizama Mtega nyoka usoni kwa makini.


Mtega nyoka alitabasamu.


"Nikaribishe ndani tuzungumze kidogo," alisema Mtega nyoka.

"Nakuingizaje ndani sikufahamu? Alisema Mwasu.

Mtega nyoka alikaa kimya kisha akatazama kushoto na kulia,alipoona kupo shwari Hakuna mtu akafanya kitendo cha haraka na kasi ya ajabu.

Akamsukuma Mwasu ndani kwa kasi kisha akatulia na kufunga mlango kwa nyuma.

Mwasu alijinyanyua chini huku akishangaa kasi alionayo bwana yule ambae alikuwa amesimama akimwangalia tu.

"unataka nini kwangu?" aliuliza Mwasu huku akijifuta kitu asichokiona mwilini mwake.

"naomba kufahamu alipo Malima" alisema Mtega nyoka.

Mwasu alishangaa!

"Malima?; mbona simjui!" alisema Mwasu.

Mtega nyoka akacheka kisha akatazama juu ukutani.


"Huyo uliebandika picha yake hapo ukutani ndie ninae mtaka" alisema Mtega nyoka huku akisonta kwa kidole picha kubwa iliokua imebandikwa ukutani.

Mwasu akagwaya huku akijutia uongo wake alioutoa bila kufikiria.

Mwasu alijua yupo matatani hivyo lazima afanye jihada za kujinasua kisha aombe usaidizi kama atashindwa kumdhibiti Mtega nyoka.

"Mi sujui alipo!" alisema Mwasu huku akimtizama usoni Mtega nyoka.

"Na Remi je!" aliuliza tena Mtega nyoka.

Mwasu alikodoa macho huku akishindwa kuelewa dhamira ya mgeni wake huyo.

"Hebu sema shinda yako bwana mana naona sikwelewi; Malima; Remi tuelewe lipi sasa" alikoroma Mwasu.

"Ukinijibu wote kwa pamoja itakuwa vizuri sana" alisema Mtega nyoka.

"watafute mwenyewe utajua walipo" alisema Mwasu.

Mtega nyoka alitulia kimya akimtizama Mwasu.

"Vipi kuna nini pale Makanisa matatu?" lilikuwa swali la mtego ambalo Mwasu hakulitarajia.


Akaingiwa na ubaridi wa gafla.

"Sasa mbona wafahamu mengi, kwanini waniuliza?"


"Kwa sababu na..." Mtega nyoka hakumaliza kauli yake alijiukuta akirudi nyuma kwa kasi na kujipigiza kwenye mlango na kusambaratika chini.


Mwasu alikuwa amemfanyia shambulizi la kushitukiza.

Mtega nyoka aliharakisha kunyanyuka ila alijikuta akienda chini tena baada ya kupigwa teke ubavuni.

Mwasu hakutaka kucheza na mtu kama yule.

Akapaa juu na kurudi na pigo la kifo.

Mtega nyoka aliliona akakwepa kisha akaachia konde zito lililompata Mwasu tumboni.

Mwasu akaenda chini huku akitoa kilio kama cha mwanamke anaebakwa.

Mwasu akasimama ila akajikuta anaingia kwenye wakati mgumu kujiokoa na makaonde mfululizo kutoka kwa Mtega nyoka.

Yapo aliopangua na mengine yalijaa mwilini mwake.


Mwasu akaona akifanya uzembe atakuwa mateka ili aseme anachokijua.

Hakutaka hilo litokee.

Akajifanya kama anaenda chini ila hakufika badala yake alifyatuka kichwa kikali kilichotua tumboni kwa Mtega nyoka na kumpeleka chini. Kisha yeye akasimama haraka na kujirusha mzimamzima na kwenda kulikumba dirisha la vioo lililokuwa sebuleni pale na kusambaratika nalo nje kisha bila kujiuliza akasimama na kutimua mbio za mbwa mwizi.

Mtega nyoka nae aliharakisha kutoka kwa kupitia pale pale dirishani baada ya kuwa wazi kwa kuvunjwa.

Alipotua nje hakuona hata unyayo wa Mwasu.

Alikwama tena.
 


Aisee hii kama muvi kabisa..
Inanikumbusha Enzi za akina Joram Kiango,Sargent vata,.


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Mwasu kakichafua
Sent using Jamii Forums mobile app
 


Hili ni zaidi ya stori


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Safi sana, mambo yazidi kunoga. Kitendawili kinaanza kuteguliwa taratibu
 
Wangap mpo active nishushe vipande vingine vitatu chap kidogo

Sent using my iPhone using jamiiforum app
We jamaa toka juzi unatudanganya, hivyo vipande hata hauna wenye navyo wanashusha tuu bila kuuliza wangapi wapo
 
Aisee hatari sana asije akaenda kule aliko Solomon Hahaha kitumbua kimeingia,mchanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…