Daudi1
JF-Expert Member
- Dec 14, 2013
- 12,444
- 18,741
Mtwanga mbele si alikumbana naye pale kituo cha polisi lazima atamfuatilia
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mtwanga mbele si alikumbana naye pale kituo cha polisi lazima atamfuatilia
Ngoja tuone.Mtwanga mbele si alikumbana naye pale kituo cha polisi lazima atamfuatilia
Wamfanye wamfanyavyo lakini atabaki hai maana starring hauwawiHahahahaha Kojo si atatoa kimba kabisa badala la kojo kizibo kitazibuliwa
Hii leo umetunyoosha hak ya naniRIWAYA : MPANGO WA CONGO.
SEHEMU YA 15
Sajini kebu akageuza macho yake kushoto kwake akakutana na jicho la Kojo ambae waliunganishwa pamoja baada ya vijana wa Kebu kuadhibiwa na Honda; hivyo sasa alikuwa ameungana na kundi la Kizibo na Kojo.
Aliona jinsi uso wa Kojo ulivyopasuka bila mpangilio.
“Umesema hii kazi ya yule bwege sio!!” aliuliza Sajini Kebu.
Swali lile lilionekana kumkera Kojo ila hakujibu akabaki kutazama pembeni.
“Bwana yule ananitesea rafiki yangu aisee” alidakia Kizibo aliekuwa amekaa kwenye kiti cha dereva.
“Hebu nipelekeni nikapumzike kwa mrembo wangu nikitoka huko risasi za kichwa zitammaliza Honda!!” alisema Sajini Kebu huku akiegemea kiti cha abiria alichokuwa amekalia.
Gari ikawashwa na kuondoka kuelekea viunga vya mji wa Gombe pembeni kidogo ya mji wa Kinshasa.
Ni kwa kuwa hawakujua lijalo halijawahi kujulikana kamwe.
Na kama walidhani wanaenda kupumzika walikosea sana.
****
Simbi Musinza alikuwa ni mshindi wa mashindano ya ulimbwende katika mji wa Kishansa kisha akaenda kushiriki mashindano ya urembo yaliokutanisha warembo kadhaa kutoka maeneo mbalimbali ya nchini Congo.
Bahati mbaya kwake, hakufanikiwa kufanya vizuri sana hasa baada ya wandaaji kugundua Simbi alikuwa akitumia zaidi mwili wake kushawishi wandaaji wamchague.
Ukizungumizia warembo waliotikisa katika mashindano hayo basi huwezi kumsahau Simbi ila tabia yake ya kupenda rushwa kwa kutumia mwili wake ilisababisha aangukie pua.
Licha ya kushindwa katika mashindano hayo,lakini bado jina lake na uzuri wake uliendelea kutikisa kurasa za magazeti jijini Kinshasa.
Simbi alikuwa na maisha ya kupenda anasa, kila siku lazima avinjari viwanja kadhaa waliokuwa wanapapatika na uzuri wake na umaarufu wake.
Hakuna sehemu yoyote ya anasa ambayo Simbi hakufahamika.
Katika sehemu moja ya chumba cha watu maalumu(VIP) kulikuwa kuna watu wawili wamekaa huku wakisikiliza muziki uliokuwa utoka kwenye sipika zilizokuwa zimefungwa kila kona ya chumba kile.
Mwanaume mmoja wa kizungu alikuwa amekaa huku amenyoosha miguu yake na usawa wa tumbo lake kulikuwa kuna kichwa cha mwanamke kilichokuwa kimejaa nywele bandia za gharama kubwa.
Mwanamke yule alikuwa akiperuzi mtandaoni huku mara kwa mara akicheka peke yake na mara zingine alicheka huku akimtizama usoni mwanaume wake wa kizungu.
Alikuwa ni Simbi!!
Mzungu aliendelea kumpapasa Simbi kuanzia kifuani hadi kichwani.
Ni kama Simbi hakusikia mguso wowote kutoka kwa mtu wake huyo, yeye alikuwa bize tu na kuperuzi kwenye mtandao.
Kama si upofu wa mapenzi basi Mzungu yule angekasirika kwa kutokupewa muda na Simbi.
Ila hakujali!!
Simbi akiwa bado anaperuzi, mara akaona ujumbe kwenye simu yake.
“Uko wapi!!” ulisomeka hivyo huo ujumbe kutoka kwa mtu aliekuwa amehifadhi jina lake kwa SAJINI.
Akanyanyuka gafla kisha akamtazama mzungu ambae wala hakujali yeye aliendelea kuvuta shisha tu.
Simbi alibaki ameganda bila kufanya lolote huku akijua kabisa ni nadra sana kuona lile jina linamtafuta.
Na likimtafuta basi siku hiyo anajua lazima avuliwe chupi.
Kilichomfikirisha sio kuvuliwa chupi na mmiliki wa jina lile.
la hasha!
Yeye aliwaza dau la pesa ambalo angeachiwa ahsubuhi na bwana huyo.
Dau la bwana yule huwa ni kubwa kuliko analoachiwa na mzungu.
Akawaza jibu.
“Nipo njiani naenda home” alijibu kisha akamsogelea mzungu.
“Leo unatoa ngapi kwani!!” aliuliza kwa sauti kavu huku mkono akiwa ameshika kiunoni.
Mzungu alishangaa mabadiliko ya mwenzi wake huyo.
“Kama kawaida dola mia!!” alisema Mzungu.
“Ooh ok!!” alisema Simbi.
“Kwani vipi!!” Mzungu alionesha mashaka yake.
“Hapana mpenzi, ila nimeingia kwenye mzunguko wa hedhi sasa hivi!!”
Mzungu alinywea kama kapigwa denda na kichaa.
Wakati bado Simbi anangojea kauli nyingine kutoka kwa Mzungu; mara akasikia ujumbe mwingine ukiingia kwenye simu yake.
Akaufungua!!
Aisee!
Alitamani kuivunja simu wakati huohuo na asipatikane kabisa.
Akaurudia kuusoma ujumbe ule na kuhakikisha jina la mtumaji.
Halikubadilika lilikuwa ni lile lile na ujumbe ni ule ule na ulisomeka vile vile.
“Nipo nakuja kwako Chimamy” ulisomeka hivyo na mtumaji mtu aliekuwa amemhifadhi kwa jina la CHIBABY.
Simbi alihisi kubanwa na tumbo la kuhara,haraka akakimbilia chooni.
Huko wala alichotarajia kitoke hakikutoka, isipokuwa aliongeza joto mwilini kwa mbio zilizomfikisha huko maliwatoni.
Mapigo yake ya moyo yalitaka kuzidi kipimo cha kawaida cha udundaji wake.
Akatoka maliwatoni bila kufanya lolote huko na alipomtazama mzungu wake akamwona alivyosawajika na midomo kumuanguka kama rasi alienyolewa usingizini.
Hakumjali!!
Yeye alikuwa anawaza tu namna ya kutatua fumanizi huko kwake na ukizingatia wanaume wote aliwahitaji mana mmoja alikuwa anamhonga vizuri na mwingine ndie mwanaume aliempenda sana.
Nani alisema wapenda pesa hawana moyo wa kupenda!!
Simbi hakutaka kumpoteza kabisa chibaby wake, mwanaume wa kitanzania alietokea kumgusa kila kona ya mwili wake nae akagusika,mwanaume aliejua kumwacha hoi kila walipokutana,mwanaume aliejaliwa mwili mzuri wa kiume.
Hata!!
Wote aliwahitaji.
Mwanaume mwenye pesa na mwanaume wa moyo wake.
Lazima aue fumanizi hilo kivyovyote.
Haraka akakimbilia mkoba wake na kutoka nje ya chumba kile kilichokuwa kwenye jumba kubwa la anasa ndani ya mji wa Gombe.
****
Nje ya nyumba ya Simbi kulikuwa kuna gari moja jeupe limesimama huku ndani yake kukiwa na watu watatu.
Sajini Kebu;Kizibo na Kojo.
“Komredi mi naingia kupiga pumzi kidogo,nitakaa saa tatu!!”
Alisema Sajini Kebu huku akifanya jitihada za kushuka ndani ya gari.
“Kwa hiyo sisi tunabaki kuwa walinzi wako? Aliuliza Kizibo.
“Hapana! Kama kuna anaetaka kuingia nae akapumzike kidogo twenzetuni jama” Sajini aliwaelekeza wenzie.
Kizibo na Kojo walitazamana, kisha Kizibo akazima gari na kushuka huku akimwacha Kojo akijilaza kwenye viti kumaanisha yeye atapumzika ndani ya gari.
“Unalala tena kwenye gari yule bwege atakuotea tena aisee!!” alitahadharisha Kizibo na Kojo akanyoosha bastola juu kumaanisha akitokea tu anamlipua kwa risasi kadhaa.
Kizibo na Sajini Kebu wakatasamu huku wakiliendea geti.
Kitu ambacho hawakujua ni kuwa Simbi alikuwa ndani na mwanaume mwingine na mwanaume aliekuwa ndani nae hakujua kuna mwanaume mwingine nae anakuja hapo ndani.
Wao walikuwa hawajui ila Simbi alijua na alipanga kucheza nao wote usiku mmoja.
Tatizo hakuwahi kujua wanaume wanaonenda kukutana ndani ni wanaumeume wa aina gani!!
Patamu
******
Ni fupi leo, ila heri kidogo kuliko kukosa kabisa
Tuvumiliane kwa leo
Akikujibu nitagNdugu mwandishi Leo ndo tunapiga pass ndefu au tukae mkao wa kula?
SawaAkikujibu nitag
Basi hiyo asubh weka hata 4 za siku nzimaShemeji leo nimetingwa kidogo nadhani naeza ibuka usiku sana na ahsubuh mkaikuta ama la basi kesho
Mtanisamehe kwa usumbufu wa kuchungulia chungulia kila mara
Poleni
ItapendezaBasi hiyo asubh weka hata 4 za siku nzima
Riwaya :Mpango wa Congo
Sehemu ya tano
Mtega Nyoka!!
Ndio alikuwa ni Mtega Nyoka, Nyoka wanaomwinda Mzee Kinyonga!!
Ila kama alijua ni kazi rahisi kumlinda Kinyonga mbele ya nyoka wakaao pangoni, yaezekana alikosea kufikiri vema.
****
Katika mitaa ya Igoma, jirani na Ndama Hotel, msichana wa kadri ya miaka minne alikuwa amesimama kwenye kituo cha kungojea daladala.
Hakuna aliejua safari yake ilikuwa ni kuelekea Kishiri ama aliamua tu kupumzika pale huku akishuhudia magari ya upande wa pili yanayotoka Kishiri na Igoma yakielekea katikati ya mji, na pia akishuhudia magari ya upande wake yakishusha abiria zaidi kuliko kuwabeba.
Alivaa mawani ya jua,na hakuna aliejua kama anatazama kitu ama alikuwa anahamsini zake.
Kama angekuwa ameamkia sehemu safi na yenye hadhi, basi wakati huu angelikuwa ananukia uturi wa kisasa.
Lakini kama ungelimtizama kwa makini basi ungeligundua huyu binti hajapata lau hata nusu maji katika mwili wake kwa siku kadhaa.
Nae hakuonekana kujali uchafu wa mwili wake, pengine kwa kuwa alikuwa mweusi wa ngozi na uchafu haukuwa kigezo kwake tena.
Macho yake yakiwa yamefichwa nyuma ya mawani ila bado yalipepesa eneo lile alilokuwa amesimama na kuna kitu alikuwa anahakikisha upande wa pili wa barabara, kulikokuwa na kituo cha kuoshea magari na pikipiki.
Akatabasamu huku akitaka kuvuta hatua ili avuke barabara.
Akasita gafla huku tabasamu lake likififia na hofu ikauvaa mwili wake.
Haraka akatoa kofia aliokuwa ameishika kwenye mkono wake wa kulia na kupachika kichwani, kisha kama anaekimbia na nusu kutembea kutoka mbali na eneo lile.
Mtega nyoka nae alikuwa pale amekaa huku akiwa na mawazo lukuki, hasa baada ya kulala na kuamka bila kupiga hatua yoyote ile.
Akiwa ametulia tu, huku akiwaza wapi pa kuanzia ahsubuh ile, mara macho yake yakatua kwa mwanadada mrefu mweusi mwenye asili ya kitutsi akiwa amevaa miwani na kofia mkononi huku mgongoni akiwa na kibegi kidogo ambacho hakikuonekana kubeba nguo yoyote.
Kama ilivyo kwa wanaume wengi;nae Akaanz kumthaminisha binti yule huku akisahau mawazo yaliomfikisha pale.
Mbali ya tathimini yake, ila hakukawia kujua uchafu uliokuwa kwenye mavazi ya binti yule ambae hadi wakati huo hakuwa amefanya tashititi yoyote ile kumuangalia yeye ama yeyote aliekuwa nyuma yake.
Ilikuwa ni rahisi kwa mtu wa kawaida kuhisi binti yule anamatatizo ya akili ama kaibiwa siku chache nyuma, ama katoroka kwao na kafika mjini pasi na ramani ya kumfanya uzuri wake ubaki katika thamani yake. Lakini ilikuwa tofauti kidogo kwa Mtega nyoka ambae aligundua kitu kingine kabisa.
Kwa mtazamo wa haraka kulingana wajihi wa binti yule, aligundua yaezakuwa si mkazi wa jiji la Mwanza na Tanzania kiujumla.
“Mnyarwanda huyu binti” alijisemea Mtega nyoka huku akiamua kuacha kumtazama binti yule ambae aliamini tayari amekutana na wajanja wa mjini kulingana na hali aliokuwa nayo binti yule.
Mtega nyoka aliamua kuendelea kuwaza hili na lile na sasa alipata wazo moja tu,nalo ni kumtafuta msanifu wa majengo aliekuwa anafanya kazi binafsi.
Mbali ya kupata orodha kamili ya watu wanaofanya kazi na msanifu huyo; lakini pia angepata mwanga kidogo ni kwanini wafanyakazi wa msanifu huyo wa majengo walikuwa wanakufa vifo vya ajabu kiasi kile huku yeye akiwa nae akiwa amepewa kazi na serikali yake kuhakikisha wasaidizi wa msanifu mkuu wanafanywa ilivyotakiwa kufanywa ili kulinda itifaki.
Ni wakati akianza kujiinua kutoka alipokuwa amekaa, ndipo alipoona jambo lingine lililomsitua zaidi,yule binti alikuwa anaharakisha kuondoka pale kwa mwendo wa nusu kukimbia na nusu kutembea.
Ingelikuwa macho ya kawaida ungeona ni haraka tu za yule dada,lakini macho ya Mtega nyoka, yaligundua hofu na mashaka kwenye mwendo wa binti yule.
Kwa nini!! Hakujua.
Mawazo yake yakamtuma amfuate yule binti lakini akajikuta hana sababu ya kumfuata.
Akapuuza.
Yule binti alizidi kukata mitaa kuelekea Igoma katikati huku kila mara akigeuka na kuhakikisha usalama wake,alikokuwa akielekea hakupajua, japo aliamini aelekeako atapata mawazo mapya kuhusu maswahibu yanayompata na namna ya kukabiliana nayo japo aliamini kupona ni miujiza ya mwenyezi Mungu.
Roho mkononi!
Lakini kuna kitu kilichomchanganya akili zaidi ni kile alichokiona.
Aliemhitaji alimwona ni baada ya kumtafuta ndani ya mji wa Mwanza karibuni siku tatu. Lakini aliekuwa anamkimbia alimwona pale kwa mtu aliekuwa anamtafuta kwa udi na uvumba.
“alijuaje nitafika kwa Mwasu?” alijisemea binti yule.
“mh” akaguna na kusita kuendelea kupiga hatua zaidi.
“Mungu wangu!!” akasema kwa hamaki baada ya kuhisi jambo baya linaweza kumtokea Mwasu, au Mama Ujazo kama walivyopenda kumuita wateja wa chakula chake.
Binti yule akapiga hatua ndefu zaidi kurudi kule alikomwona Mwasu,huku dhahiri shahiri akionekana kupagawa kwa alilokuwa ameliwaza.
Dakika sita baadae alikuwa anatazamana na binti wa miaka kama kumi na sita hivi; aliekuwa anahudumia wateja kwenye mgahawa ule wa maturubai.
“kuna wali maharage;ugali dagaa..” alitaja vyakula vilivyokuwa vinapatikana pale mgahawani kwake.
“sihitaji chakula mdogo wangu” alijibu binti aliefika pale.
Ikawa mshangao kwa binti anaehudumia.
Lafudhi!!
Msukuma yule anaehudumia kwenye mgahawa wa Mama ujazo,alibaki anashangaa lafudhi ya mgeni wake yule,haikuwa lafudhi ya Kitanzania,lakini kubwa lafudhi ile inaufanano kwa mbali na lafudhi ya Mwasu.
Akashangaa!!
Licha ya kushangaa, ila hakutaka fikira zake zimuibulie maswali.
Akabaki kimya kumsikiliza msichana mwenzie alimzidi kimo cha urefu na weusi wa kung’aa.
“Namuulizia Mwasu!” alisema binti mweusi huku akimtizama Msukuma wa Bariadi.
Msukuma wa Bariadi akagundua kitu kingine tena.
Ustarabu!
Binti aliekuwa mbele yake, hakuwa na ustarabu wa Kitanzania,Mtanzania yeyote akitaka kuuliza lazima aanze na neno ‘Samahani’ila huyu huo ustarabu hakua nao kabisa.
“Sio Mtanzania huyu” alijiwazia Msukuma.
“mmh hilo jina silifahamu dada” Binti wa kisukuma akajibu huku bado akiwa amemkodolea macho binti mgeni.
Binti mgeni akalikumbuka jina maarufu aliloambiwa na Mwasu siku kadhaa nyuma, jina hilo lilimeza jina lake la kuzaliwa.
Mama ujazo!!
“mh nimekumbuka, anaitwa Mama ujazo” alisema binti mgeni huku akitabasamu ili kumtoa kwenye udadisi mwenyeji wake.
“aah sawa;katoka hapa punde tu na Kaka yake!”
“kaka yake!!?”
“ndio amesema ni kaka yake, na wameenda kwake”
Akili ya binti mgeni ikapiga kite cha hofu baada ya kuhisi huyo kaka alieondoka na Mwasu ni yule aliemkimbia dakika chache zilizopita.
Binti mgeni akasikia tumbo likiunguruma kwa woga,akaangaza kushoto na kulia kuona kama kuna choo maeneo yale,hakukiona.
Jasho la hofu likatanda mwilini mwake,kichwa kikamwasha mithili ya mtu mwenye mba sugu.
“my God! Mwasu hastahili kufa” akajiwazia haraka akataka kutoka mle mgahawani.
Akakumbuka cha muhimu.
“aah anaishi wapi kwani” aliuliza.
“anapoishi sipafahamu; ila ni huko Nyakato Meko” alijibu binti wa kisukuma.
“shiiit” akang’aka kwa fadhaa.
Binti mgeni akaanza kutoka kwa pupa akadakwa mkono.
“Hebu ngoja kwanza; kwani wewe ni nani yake?” aliuliza Msukuma.
“mdogo wake” alijibu Binti mgeni.
“unaitwa nani?”
Binti mgeni akafikiria kidogo kisha akajibu.
“Naitwa Remi”
“ooh, sasa nenda Buzuruga plaza,pale kuna ofisi za Kasuku contractors,hapo kuna mchumba wake anaitwa Malima,yeye anaeza kukufikisha kwake kirahisi,mana hapa harudi tena na mimi sina simu dada angu” alieleza kwa kirefu binti Msukuma.
Remi alishukuru kwa ukarimu wa aina ile kutoka kwa Msukuma. Akaaga na kuondoka kwa haraka ya ajabu huku akimwacha Msukuma akimwangalia bila kujiuliza haraka zile za nini.
Watanzania hatuna udadisi,amani imetujaa!!
***
Nusu saa badae,Remi alikuwa anashuka kwenye daladala huku tumbo la kukata lilomkumba gafla kule mgahawani kwa Mwasu,lilianza tena kukata huku jasho likianza kutoka tena.
Hali ile ilimkuta kwa sababu hakuwa na hakika na kumpata Mwasu.
Akatazama jengo lile lilivyopendeza huku watu wakiendelea na shughuli zao kama kawaida. Macho yake yalikuwa yanapepesa kila kona ili apate kuona kibao cha Kasuku Contractors.
Alikiona.
Akapiga hatua za tahadhari huku mapigo ya moyo yakiongezeka kama ya mkimbia marathon.
Alizidi kufuata ulekeo kama kibao kilivyoelekeza.
Alibaki akitazamana mlango wa mapokezi. Mapigo ya moyo yalizidi kwenda kasi ya zaidi.
Akapumua kwa nguvu kujipa ahueni kidogo.
Hatimae akausukuma mlango na kuingia ndani.
Akakaribishwa na mandhari nzuri za ofisi ile ya ujenzi na uhandisi wa majengo,lakini pia ilikuwa na watalaamu wa kusanifu majengo.
Ilimchukua dakika nzima kushangaa na kujaribu kuyazoea mazingira ya ofisi ile.
“Karibu dada!” ilisema sauti ya kike.
Remi alipiga hatua za woga kusogea pale alipokuwa dada aliemkaribisha,ambae hakuwa peke yake,kulikuwa na mtu mwingine mwenye jinsia ya kiume na kimtazamo tu nae alionekana kuwa ni mgeni ofisini pale.
Alieyekuwa pale mapokezi alikuwa ni Mtega nyoka.alifika pale kumuulizia Msanifu mkuu wa majengo wa kampuni ile inayomilikiwa na vijana wa kitanzania.
Akiwa ndo kwanza ameanza kusikilizwa mara akaingia mwanadada ambae yule yule ambae alimwona pale Igoma saa moja iliopita.
Akapigwa butwaa!
Remi hakujali uwepo wa mtu mwingine pale. Alikuwa anataka kuwahi kuonana na Mwasu.
“Nauliza ilipo ofisi ya Malima” aliuliza Remi.
Dada aliekuwa mapokezi akamtazama kisha akainama chini na alipoinuka alikuwa anadaftari na kalamu.
“Andika hapo majina yako na namba yako ya simu” akaeleza dada wa mapokezi.
“Sijui kuandika wala kusoma”
Ajabu hii.
Si dada wa mapokezi alieshangaa jibu la Remi; hata Mtega nyoka hakutaka kuamini kirahisi vile eti katika Dunia hii kuna mtu mwenye uzuri na sura ile hajui kusoma.
Hata!!
“Basi kama ndivyo hutaweza kusikilizwa” alisema dada wa mapokezi huku akionekana kukereka baada ya kuhisi amedharauliwa na mwanamke mwenzie.
“Ni muhimu,tafadhali nielekeze” alisema Remi.
Huku akibinua midomo na kuendelea kuwa bize na Tarakilishi iliokuwa mezani kwake akasema.
“Binafsi au kikazi?”
“Binafsi dada” Remi alijibu.
Muda wote huo Mtega nyoka alikuwa kimya kabisa.
“kwa hiyo Malima ndo huwa anakutana na wasiojua kusoma?” aliuliza dada wa mapokezi.
Tofauti na mawazo yao kwamba yule mgeni asiejua kusoma na kuandika ataendelea kubembeleza; haikuwa hivyo.
Remi akapiga hatua ndefu na kuanza kuondoka ofisini pale huku dhahiri akionekana kupagawa.
Dada wa mapokezi alimwita ila Remi hakugeuka wala kusimama aliendelea kuendea mlango.
“kwani huyo Malima yupo?” Hatimae Mtega nyoka akauliza,na kwa gadhabu dada wa mapokezi akajibu.
“Wameenda kuzika wahandisi wa kampuni waliokufa juzi”
Mtega nyoka hakustuka kwa vifo vya wahandisi hao mana alishuhudia miili yao ikiwa haina uhai usiku wa jana japo akiefanya vile hakumjua.
Mtega nyoka akaona kuna kitu kipo kati ya dada asiejua kusoma na huyo Malima ambae nae alikuwa na shida nae. Mtega nyoka akapiga hatua kumwahi yule dada kabla hajatoka kwenye viunga vya Buzuruga Plaza.
Remi hakuwa mjinga wa kutoka pale bila kujua au kuonana na Malima.
Kabla hajaingia pale ofisini ,pembeni yake aliona saluni ya kike kubwa na kwa tabia za wanaume na wanawake alijua kabisa mmoja ya wahudumu pale saluni atakuwa anajuana na Malima ama la anamawasiliano yake.
Akauendea ule mlango wa saluni.
***
Mtega nyoka alibaki amezubaa kwenye valanda pana iliotenganisha milango ya ofisi zilizokuwa pale.
Hakumuona aliemtaka.
.haraka akakimbia nje ya lango la kuingilia pale Plaza huko nako hakumuona.
Akili yake haikukubali yule dada ametoka ndani kwa haraka kiasi kile.
Akarudi tena kule ndani.
Wakati yeye anaingia akapishana na Remi akitoka huku akiweka kitu kwenye matiti yake.
Mtega nyoka akamwacha apite kisha awe nyuma yake.
Mtega nyoka hakujua sababu gani aliamua kumfuatilia yule dada, ila alijikuta tu anamfuatilia.
Remi aliendelea na safari yake huku akiwa na jambo moja tu,kutafuta simu na kuzipiga namba za Malima alizopewa na mmoja ya wahudumu wa saluni.
Kitu kimoja ambacho hakujua ni kuwa wakati wote wa harakati zake kulikuwa na mtu mmoja zaidi aliyekuwa nae bega kwa bega na sasa alikuwa amepokea amri ya kumchukua mzima ama mfu na kumpeleka kusiko julikana na kazi hiyo ilitakiwa kufanywa wakati Remi akitoka Buzuruga Plaza.
Remi hakujua hesabu anazopogiwa na watu wawili kwa wakati mmoja huku miongoni mwao akiwepo mwenye nia ya kujua sababu ya kumtafuta Malima na mwingine akiwa na sababu ya zaidi kuua.
Hatimae Remi akaanza kuambaa na kuifuata Barabara mara mbele yake akakutana na mtu ambae hakutarajia kumuona pale.
Mtekaji!!
Remi akataka kugeuka na kurudi alikotoka.
Alichelewa!
Mikono imara ikamdaka bega lake na kumvuta kwa nguvu,kisha kikafuatia kibao kikali kilichotua sawia mgongoni mwa Remi huku kikimtoa kelele ya uchungu.
Remi alipepesuka na kutaka kuanguka chini,lakini akajikuta akijaa mikononi mwa mtu mwingine aliekuwa nyuma yake.
Alinguka mikononi mwa Mtega nyoka!
Mtekaji akabaha baada ya kuona kasi iliotumika kumdaka Remi.
“ugomvi huu haukuhusu braza, nipe huyo binti niende nae zangu” alisema mtekaji.
Mtega nyoka alikuwa akitazamana na mtu mrefu mwembamba lakini alionekana kuwa imara sana.
Mbali na mwonekano huo, lakini pia Mtega nyoka aligundua lafudhi ya mtekaji na mtekwaji zinafanana lakini pia hata sura na mwonekano ni watu wa jamii moja.
Kuna nini! Hakujua na la muhimu zaidi ni kuomukoa kwanza binti kisha mengine yatajulikana badae.
Akamvutia nyuma na kuwa kinga yake.
Mchoro ukachorwa huku raia wakianza kujaa kushuhudia linalojiri.
****
KINSHASA CONGO
…kutoka pale alipokuwa Honda alibakiza hatua mbili tu afike kwenye ukingo wa daraja lililokuwa linapitisha maji kwa chini.
Na bado alikuwa amemkaba barabara Sajini Kebu.
Wale askari wengine walikuwa bado wanapiga hesabu za kumwokoa Sajini Kebu kwa kusuburi Honda afanye kosa lolote ambalo hadi wakati huo halikuwa limefanywa nae hivyo wakakosa la kufanya.
Lakini Honda mbali ya kuwa na hesabu za kutoroka bado alikuwa anawazia namna ya kuwatoroka ama kuzua varangati litakalo wafanya wasahau kuhusu mkoba na kile kidole pale chini.
Pale walipokuwa ilikuwa ni barabara isiopitisha magari kwa wingi.
Lakini kwa mbali masikio ya wote yalinasa sauti ya kuja kwa gari kubwa.
Honda alitabasamu huku watekaji wake wakiingiwa na mchecheto wa namna ya kumuokoa sajini Kebu kabla gari hakijafika.
Hesabu zilipigwa pande zote.
Dereva wa lori aliona tukio lililokuwa mbele yake. Kurudi nyuma akaona haiwezekani hivyo akaamua kuongeza mwendo ili avuke pale darajani kwa kasi huku woga ukiwa umemtamalaki na mkojo ukikaribia kugonga hodi kwenye kipamchulio.
Lori lilizidi kukaribia na Honda nae alizidi kujisogeza kwenye ukingo wa daraja huku akiwa bado amemtundika kabali matata Sajini Kebu.
Hatimae lori likafika na hapo ndipo lilitokea tukio ambalo yaezekana Sajini Kebu na wenzie hawatakuja kuliona likijirudia tena katika himaya za macho yao iwe akhera ama Duniani.