bless on
JF-Expert Member
- May 22, 2026
- 1,213
- 2,938
Ilikuwa ni miaka ya 90 kuelekea 2000. Pale Liberia kulikuwa na Rais mmoja mbabe sana, anaitwa Charles Taylor. Huyu jamaa alikuwa haambiliki, alikuwa anafadhili vita vya Sierra Leone wapigane wenyewe kwa wenyewe..
CIA walikuwa wanamtamani sana, lakini walikosa njia ya kuingia Ikulu kwake.
Sasa, CIA wakapiga hesabu Huyu mwanaume anapenda sana warembo. Hapo ndipo wakamvuta binti mmoja fundi, mrembo balaa na kichwa chake nihatari, anaitwa Alicia Macy.
Alicia aliingia nchini kama mfanyakazi wa kutoa misaada . Alijua kuvaa, alijua kuongea, na alijua namna ya kumfanya mwanaume yeyote ageuke shingo.
Haikuchukua muda, akajisogeza kwenye duru za karibu na Rais. Siku moja kwenye bonge la party, Charles Taylor akatupa jicho kwa Alicia. Akatupa tabasamu moja la gharama. Taylor akaingia kingi, hakujua kuwa huyo mwanamke ni "sumu" iliyotumwa na Washington.
Alicia akawa mpenzi wa Rais. Alikuwa anakaa naye Ikulu, wanalala kitanda kimoja, na wanakula meza moja. Wakati Taylor anadhani amepata "tunda" la roho yake, Alicia alikuwa anapiga kazi.
Wakati Rais amelala fofofo, Alicia alikuwa anachukua muda huo kupekua makaratasi ya siri, kusikiliza mazungumzo ya siri ya biashara za silaha, na kujua ramani nzima ya jinsi almasi zinavyochimbwa na kuuzwa nje ya nchi. Kila kitu alichokiona usiku, asubuhi kilikuwa mezani kwa mabosi wa CIA.
Lakini unajua maisha ya kijasusi ni kama kutembea kwenye kamba? Baada ya muda, walinzi wa Taylor wakaanza kujiuliza "Huyu mzungu mbona anauliza sana maswali?" Hali ikawa tete.
Alicia akaanza kuhisi kuwa Charles Taylor anaanza kumshtukia. Siku moja usiku, akapokea ujumbe wa dharura kutoka kwa mabosi wake.
"Ondoka hapo mara moja, mchezo umegundulika!"
Ilibidi atumie mbinu za hatari kutoroka Liberia usiku wa manane kabla ya makomando wa Taylor hawajamkamata. Alirudi Marekani akiwa na siri zote ambazo baadaye zilitumika kumfunga Charles Taylor maisha kule mahakama ya The Hague kwa makosa ya kivita.