Jawabu kwa Lord Denning: Mikataba mithili ya IGA inayotaja gharama halisi za miradi ipo hapa Tanzania



Siitaji technicality yeyote au kuwa Mwanasheria, sijui, IGA, HGA or anything....

Mkataba huu mwenye common sense akisoma anajua hizi ni hamnazo kabisa.
 
Jibu mujarabu
 
Siitaji technicality yeyote au kuwa Mwanasheria, sijui, IGA, HGA or anything....

Mkataba huu mwenye common sense akisoma anajua hizi ni hamnazo kabisa.
Kitu kama hiki ndicho anakitumia huyu tapeli Lord denning ili kuulinda ule mkataba wa hovyo.

Ameshindwa kujua mazingira yetu kisiasa kati yetu na wenzetu hayafanani, wenzetu wapo accountable kisheria, wa kwetu wako huru hata wakikosea..

Licha ya vifungu vingine vyote vibovu kwenye ule mkataba, huyu tapeli ameokota hicho kimoja tu aje kujiliwaza nacho hapa, akiamini atatudanganya.
 
Jifunze kusikia na yale usiyopenda kusikia.

Jifunze pia kuwa sio kila jambo unalosimamia liko sahihi.

Ukishajua haya utaishi vizuri sana!
 
Jifunze kusikia na yale usiyopenda kusikia.

Jifunze pia kuwa sio kila jambo unalosimamia liko sahihi.

Ukishajua haya utaishi vizuri sana!
Nijibu tu kile nilichokuuliza, hayo mafunzo unayonipa naona hata nawe yanakuhusu zaidi.

Huwezi kuuliza swali mtu mwenye akili timamu, asitake kujua your motive behind, na hilo sio kosa.

Wewe wakati unatengeneza hilo swali lako, ulifanya utafiti kidogo kuona tofauti ya kimazingira, na kiuwajibikaji, iliyopo kati ya viongozi wetu na hao wengine?
 

IGA ni makubaliano ya uwekezaji katika bandari zetu.

Katika IGA nchi zimekubaliana DP World ndio kampuni itakayowekeza ikiwakilisha Dubai na TPA kampuni pokezi ya uwekezaji huo ikiwakilisha JMT.

Mikataba ya utekelezaji miradi (HGAs) itaandaliwa kwa misingi ya makubaliano (IGA) na si vingenevyo. Kama kutakuwa na vifungu nje ya hayo makubaliano, hakuna shaka kutazuka mgogoro. Kumbuka baadhi ya vifungu neno shall limetumika ambalo kisheria ni "ulazima" wa kutimiza kilichokusudiwa. Kwa kuwa shauri liko mahakamani tusubiri hatima yake ila natoa mfano wa nguvu ya IGA wakati wa kuandaa HGAs

Article 8: Land Rights
1. The Government of Tanzania
(na siyo Union Republic of Tanzania) shall take all necessary actions to ensure the acqusition and grant of rights to DPW or the relevant project company. Kitakachofuata hapo ni kuamini kuwa DPW hawataomba ardhi yenye maslahi mapana kitaifa kwa ajili ya shughuli zao.
 

Hoja ya mleta mada hii hapa:

 

Nimelijibu swali hilo kama ifuatavyo:

 

Asante kwa angalizo. Kwa uelewa zaidi somma aya hizi hapa:

 
IGA ya Italia na Algeria mwaka 2022 kwenye masuala ya nishati iliwekwa wazi kwamba Italia wangwekeza $4billions kwenye mashirikiano hayo.

Unauliza swali la kitoto sana, hata watu kukujibu wanaona uvivu. Kuna malaki ya IGA dunia na wewe sio ajabu hujawahi kuona hata zaidi ya tatu, halafu IGA za uwekezaji haziwezi kuwa sawa na za utamaduni, sheria, mazingira n.k
 
Daa! Kila nikikaribia kuelewa najikuta tena Chali! "Katika IGA nchi zimekubaliana DP World ndio kampuni itakayowekeza ikiwakilisha Dubai na TPA kampuni pokezi ya uwekezaji huo ikiwakilisha JMT." Ni nchi gani hizi tena? Mi mbona naona IGA ni kati ya Tanzania na DP WORLD!? Ngoja niisubirie mahakama tu. Ila mleta bandiko kwangu upande wangu ni moja ya watu waliolieleza jambo hili kwa rugha rahisi sana kueleweka (kwa anayetaka kujifubza)
1. Hakukuwa na haja ya IGA katika issue hii.
2. Kinachotafutwa kwenye IGA na HGA kipo kwenye framework contract na project contracts
3. IGA hii inatengeneza hatari kwa Tanzania
4. Mkataba ulipaswa uwe kati ya TPA na DPW na si vinginevyo.
5. Swali la Lord denning linatafuta UBISHI zaidi kuliko kuleta weredi kwa wadau.
 
Iweke hapa

Tuone kama ilisema kutakuwa na HGA na ikasema hayo
 
Hakuna ulichojibu

Jibu ni kuweka IGA au BIT inayoeleza kutakuwa na HGA alafu still ikaweka mgawanyo wa mapato. Ni bora ungesema tu sina jibu

Naona kanuni ya REASONING BY ANALOGY inakupiga chenga.
Recap:

The process of analogical inference involves noting the shared properties of two or more things, and from this basis concluding that they also share some further property. The structure or form may be generalised like so:

1. P and Q are similar in respect to properties a, b, and c.
2. P has been observed to have further property x.
3. Therefore, Q probably has property x also.

Source: Argument from analogy - Wikipedia
 
N Nimetengeneza swali langu purposely kuelimisha watu juu ya upotoshaji unaofanyika.

IGA yetu imeweka nafasi ya kuingiwa kwa HGA zitakazoweka rights za kila upande. ikiwemo masuala ya uwekezaji na mgawanyo wa mapato.

Unaposema mkataba mbovu eti haujaonesha mgawanyo wa mapato ndo hapo unaulizwa ili uweke ushahidi wako wa kuleta mkataba uliosema kutakuwa na HGA na bado ukaelezea mgawanyo wa mapato.

Alichofanya mjibu hoja ni kupuyanga sio kutoa jibu la kilichoulizwa.
 
Huku ndo kupuyanga kwenyewe sasa. Kama huna jibu sema sina jibu sio unapuyanga. Kwenye taaluma yetu jibu unachoulizwa ukujibu vingine ni kupuyanga tu
 

Swali lako linafutika kwa sababu ya mantiki kwammba hakuna haja ya IGA katika uwekezaji wa bandari. TICTS hawakusaini IGA na walisonga mbele. Kwa nini IGA leo?
 
Huku ndo kupuyanga kwenyewe sasa. Kama huna jibu sema sina jibu sio unapuyanga. Kwenye taaluma yetu jibu unachoulizwa ukujibu vingine ni kupuyanga tu

Ungetuliza akli yako ungegundua kuwa swali lako linafutika kutokana na jibu la swali hili: IGA inahitaji kwa ajili gani katika uwekezaji wa bandari?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…