Jay Moe vs Chid Benz

Niko na muda acha nitie neno!

Kila MC huwa wanakua na kitu fulani anachokiwezea zaidi. Kuna wanoweza kufreestyle sana, kuna wanaoandika lyrics kuntu zenye kuelimisha (edutainment), kuna wazee wa punchlines, alafu kuna wababe wa flow and delivery!

J Moe ni moja kati ya MC's wa kibongo wenye uwezo mkubwa sana wa kuandika mashairi yenye ujumbe. Ni rapper anaeweza kuijadili mada moja kwenye wimbo mzima kwa mvuto wa aina yake. Kasikilize story tatu, kasikilize kimyakimya, au kasikilize money na famous.

Chidi Benzino a.k.a King Kong, ni rapper mwenye flow na delivery kali zaidi kuwahi kutokea kwenye bongo hip hop. Nadhani Ulamaa Solo Thang ndio anaweza kushindana nae kwenye suala la flow and delivery. Sauti yake nzito, uwezo wa kunata na beat, vitakufanya uendelee kumsikiliza Chidi bila kujali anachokiimba kina mantiki au hakina!

Nikirudi kwenye hoja kuu ya mleta mada, Yes mimi pia naamini J Moe is a better MC than Chidi Benz. J Moe sio mnyonge pia kwenye flow, ila kwenye mashairi anamuacha Chid benz pakubwa. Pia J Moe anaweza kubadilika badilika kuendana na theme ya wimbo husika. Akiimba mambo ya starehe anafanya poa, na akiamua kuielimisha jamii pia anafanya poa bila shida. Chidi benz anabamba zaidi kwenye nyimbo za starehe pekee!

Mwisho kabisa, mifano ya nyimbo ulizozitaja hazina uhalisia. Nadhani kwakua unamkubali sana J Moe ndio maana ukatumia hisia zaidi kusema J Moe alifunika kwenye hizo ngoma.

Ukisikia paah (remix), walifunika zaidi JCB na Fid Q. Walielewa mada husika na nashairi yao yakabeba matukio yanayoendana na theme ya wimbo. J Moe alifanya kawaida tu. Kwa upande wa Chid benz, alienda chaka. Nadhani hakuelewa mada husika. Alichokiimba hakikuendana na wenzie kabisa

Mchizi wangu (remix), wengi walifanya poa hasa Fid Q na Lord Eyez. Alizingua Mh Temba tu na kisauti chake (ni maoni yangu), sijui nani alimuita. Pia kwenye hii ngoma, naona Chid benz alimfunika J Moe. Verse ya Benzino ilikua moto sana.

Mimi ya Geez Mabovu, naona kama ilikua 50/50. Verse ya J Moe ilikua na mistari kuliko ya Chidi, ila verse ya Chidi ikawa na flow kali kuliko ya J Moe.

Mwisho kabisa, kuna kitu kinaitwa Longevity. J Moe amekaa kwenye game kwa muda mrefu na kutoa hit songs nyingi kumzidi Chidi benz. Consistency ya J Moe inafanya nimpe nafasi mbele ya Chidi benz!

Adiós.
 
Ukishakuwa maarufu lazima ukubali skendo,sio kila siku watasifu lazima watabiga dongo,kuna wengine wakiona hawasikik basi hujifanya wana skendo,juma ndo yule yule umaarufu haujanibadilisha ni upara hakuna nywere style kiduku itapita........
....
 
Kuna hii ya
Jay melody na billnass
Kuna hii ya
Marioo na lony music..

Zipo Collabo kibao ambazo Chid Benz angeshilikishwa angefunika sana
 
You hit the target
 
Umesahau Ngoma Yao wenyewe wawili walifanyia mwanza kipindi producer Q Bado yupo mwanza ...inaitwa TWENZETU TUSONGE ... Chid alifunikwa Tena na Mbakiaji X-Man Jay Moe Mo-tech..... Jamaa ni underrated sana lakini ni Moja ya mamcee wakali kutokea bongo.
 
mchizi wangu remix Mwana FA na Maujanja walinibamba

Kwa kuflow Babu Wa Kitaa umemsahau mkuu
 
Ukishakuwa maarufu lazima ukubali skendo,sio kila siku watasifu lazima watabiga dongo,kuna wengine wakiona hawasikik basi hujifanya wana skendo,juma ndo yule yule umaarufu haujanibadilisha ni upara hakuna nywere style kiduku itapita........
....
famous ngoma yenye beat kali
 
Mo tech ni moja Kati ya M cee ambae anaudai hela nyingi muziki hii, Ana hits nyingi sana in short ni moja Kati ya Mcee wangu wa3 wakali kubless bongo fleva
 
Mchizi wangu remix, Mansulee killed it, flow and message, wengine wanafuata
 
Rapa pekee aliyekuwa anakaribiana uwezo na chid ni ngwair peke yake ,wengine wote wanafata baada ya chid.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…