Nadhani Jide toka anaanza muziki alikuwa akiimbia matured audience ndio maana catalogue yake ya muziki ipo clean. Kuanzia machozi, usiusemee moyo hadi Mambo matano.
Zuchu alianza na EP lakini pia ana classics ambazo hazitochuja kama Raha, mwambieni, utaniua, nisamehe, wana, Naringa etc
Lakini pia Zuchu yupo katika Era ya Muziki wa club bangers na miziki rahisi rahisi ya matusi. Na WCB kama label inayoneemeka kwa strategy hiyo ya biashara, lazma Zuchu aimbe nyimbo za aina hiyo ili avume kama ilivyo sasa
Sema kitu kimoja ulichosema ni muhim, Lady Jay Dee alikuwa anaimba bongo flava ya kuasisi, yaani ndo wanaifuma ala na uandishi katika kipindi ambacho bongo flava ilionekana ni muziki wa kihuni, mauzo ni shows na albums lakini pia media ndo platforms pekee zinaendesha promotion ya muziki. Hivyo, hata kama smooth vibes chini ya ruge na clouds ndo ilinsimamia, lakini nazoo ndo zilikuwa zinaanza
kwa hiyo huwezi kulinganisha na Zuchu ambae kakulia familia ya muziki, kakabidhiwa kwenye Music empire ambayo ipo established kifedha, kiuandishi, kimuziki, kipromotion na kila kitu lakini bado akapikwa miaka mitano ili tu aje atoke. So hapo unaona kabisa kufanikiwa kwa Jide na Zuchu ni mbingu na Ardhi
Kwa hiyo kumuweka Zuchu na Lady Jay Dee kwenye sentensi moja ni kumkosea heshima Lady Jay Dee japo, kama Zuchu anaandika nyimbo zake Mwenyewe, ni kweli ana tungo nzuri za kiswahili pengine kuliko hata wasanii wa kiume tulionao