Jaydee anastahili heshima lakini asipewe sifa za uongo

Kwenye wimbo wa Zuchu mwambieni mwabieni mali yake yaliwa kuna mstari unasema "wape salamu za Betty Mkwasa" ,nilivyosikia tu hapo nikasema 100% huyu Chuchu anaandikiwa nyimbo zake.
Zuchu yupo 30's kumjua betty mkwasa ni kawaida Ila mimi siamini hadi leo kile kiswahili deep cha nyimbo zake anakiandika yeye maana nikiskia kiswanglish chake kwenye interviews, ni ngumu kuamini hilo.

Hata Ali Kiba pamoja na kukua kwa waswahili kariakoo Ila kiswahili cha dushelele alikiri kuandikiwa na mjomba wake. Mwasiti naye kwenye nalivua pendo, ule ushairi wa zamani alikiri kuandikiwa

Sasa hiki kiswahili deep cha Zuchu ambacho hata mzee Yusuph hawezi kukiandika. Kuna namna ni ngumu kuamini anakiandika yeye
 
Zuchu ngumu sana kumjua Betty Mkwasa ,wakati Betty Mkwasa anatamba(on her prime) Zuchu alikuwa anapenga makamasi kwa mkono ,Si Betty Mkwasa wa Bahi ,nazungumzia Betty Mkwasa wa ITV/RTD ambaye Zuchu ndiyo aliyempa sifa/Aliyemzungumzia.

Najua Zuchu anaandikiwa ila hapo ndiyo nika-confirm na inaonekana WCB wanaandikiwa na mtu mmoja maana miandiko yao inafanana.

Kuna msemo wa babu juma - naona Rayvann , Diamond ,Zuchu wameutumia kwenye nyimbo zao tofauti.
 
Wapo wasanii kwa uchache wa wanawake kwenye Sanaa walijitoa na kukubalika haraka na sasa tunawatazama kama "icons" kwenye Sanaa ya muziki, mmojawapo ni Lady Jaydee anastahili heshima Sana...

Lakini hata hivyo tusianze kabisa kuwapa wasanii wakongwe sifa za uongo kuwa ni wakali Sana kuzidi wasanii wa sasa. Wakati Sanaa imekuwa sana na sasa hakuna tena ubabaishaji kama wa zamani ...kama kipaji kipo kinaonekana na kama sauti ipo inaonekana.

Nampa Lady Jaydee heshima kuliko Zuchu au Maua Sama lakini kulazimisha kuwa lady Jaydee ni mkali kisanaa kuliko Zuchu na Maua Sama sio kweli.

Wasanii wakongwe wanastahili heshima lakini tusiwape sifa za Uongo.

Lady Jaydee hata Ray C kwenye ubora wake alikuwa hamfikii kabisa, tuwape heshima lakini sio sifa za Uongo..
Upo sahihi, nakubaliana nawewe, Binafsi hata Sugu nampa heshima kubwa sana kwa kupambania Muziki wa Bongo hasa HIP HOP & RAP lakini kwa kipaji nampa Ngwair na Professor Jay kuliko Sugu...pia wapo wengine wanaomzidi
 
Zuchu ngumu sana kumjua Betty Mkwasa ,wakati Betty Mkwasa anatamba(on her prime) Zuchu alikuwa anapenga makamasi kwa mkono ,Si Betty Mkwasa wa Bahi ,nazungumzia Betty Mkwasa wa ITV/RTD ambaye Zuchu ndiyo aliyempa sifa/Aliyemzungumzia.

Najua Zuchu anaandikiwa ila hapo ndiyo nika-confirm na inaonekana WCB wanaandikiwa na mtu mmoja maana miandiko yao inafanana.

Kuna msemo wa babu juma - naona Rayvann , Diamond ,Zuchu wameutumia kwenye nyimbo zao tofauti.

Mimi na Zuchu nahisi ni age mate, kipindi betty mkwasa ya anachukua tuzo ya utangazaji na makala Africa, aliongelewa sana na iliposemekana ana undugu na Ray C. Jina likazidi kuwa midomoni mwa watu

Kwa hiyo japo hata mimi sikuwa mkubwa Ila nilimjua Ila yawezekana ukawa na mantiki maana mtu wa sasa akiandika nyimbo pengine ataongelea watangazaji wa sasa kuliko waliovuma maybe miaka almost 20 nyuma

Kuhusu labels kuchukua ghost writers au msanii mwenye uwezo wa kutunga zaidi kuandikia wasanii wengine. Hiyo sio habari Ila tatizo bongo wanaficha. At least Ali kiba huwa anasema ukweli mfano kwenye utu, ilikuwa mega hit Ila alikiri iliandikwa na tommy
 
Wapo wasanii kwa uchache wa wanawake kwenye Sanaa walijitoa na kukubalika haraka na sasa tunawatazama kama "icons" kwenye Sanaa ya muziki, mmojawapo ni Lady Jaydee anastahili heshima Sana...

Lakini hata hivyo tusianze kabisa kuwapa wasanii wakongwe sifa za uongo kuwa ni wakali Sana kuzidi wasanii wa sasa. Wakati Sanaa imekuwa sana na sasa hakuna tena ubabaishaji kama wa zamani ...kama kipaji kipo kinaonekana na kama sauti ipo inaonekana.

Nampa Lady Jaydee heshima kuliko Zuchu au Maua Sama lakini kulazimisha kuwa lady Jaydee ni mkali kisanaa kuliko Zuchu na Maua Sama sio kweli.

Wasanii wakongwe wanastahili heshima lakini tusiwape sifa za Uongo.

Lady Jaydee hata Ray C kwenye ubora wake alikuwa hamfikii kabisa, tuwape heshima lakini sio sifa za Uongo..
ngoja kwanza jaydee alikua hamfikii ray c kwenye sekta ipi???
 
Haya huyo Zuchu anamzidi wapi Lady jaydee kwenye sanaa?

1. Tungo
2. Albamu
3. pesa
4. uwezo binafsi wa kuimba(acapela)
5. uwezo wa kutumia jukwaa

labda hapo tunaweza kuwapima vizuri, ili mtu asionewe
JAY DEE alijiaribia alipoanza kuimba MASIMANGO.
ndi ndi ndi
Mabinti
n.k
 
Msimshambulie mtu kwa kutoa mtazamo wake. Swala analoongea kuhusu Jide lilikuwa wazi kabla ya ujio wa hawa wasanii wengi. Jide sio open singer, vile alivyoimba ndio kamaliza, sisemi anaimba flat lakini ukweli usiopingika kwamba Jide hana uwezo wa kucheza na sauti
 
Kila mtu alikuwa na nyakati zake bora kabisaa, Zuchu hata miaka yake kwenye kuimba ni michache sana wakati Lady Jdee ana miaka zaidi ya 15 , huu ni wakati wa Zuchu
 
Zuchu ana kiswahili kitamu kama wali Nazi samaki Nazi..... Ila uchorwe mstari wasilinganishwe mbona ligi Ina wengi tu... Kina Nandi.... Wao walishafunika ilikuwa jaydee vs ray c
 
Potential atakuwa nayo kama atakomaa, lazima uangalie mazingira, Jide alikuwa katika mazingira magumu na akasurvive, huyo Zuchu angeweza kurvive katika mazingira yale? Zuchu yuko katika kipindi ambacho muziki umekuwa sana, lakini jamani kweli ufananishe wimbo wa Honey Vs Joto hasira, ft Prof J, au Faraja uko wapi faraja, wanaume kama mabinti
Kifanananisha nyimbo mmoja mmoja tena unayoichagua kwenye mada ya kulinganisha wasanii ni kukosa hoja, hao wasanii wana nuimbo zaidi ya 20 kilammoja kwanini uwe selective pia jua Zuchu ni msanii wa kisasa ana aina mbili za nyimbo wengi munakimbilia aina fulani ya nyimbo.
 
nimekupa mfano, basi fananisha wewe nyimbo za Zuchu na Jay dee uone kama zinakaa kwenye mizani moja, unavyosema muziki wa kisasa unamaanisha nini?
 
Mziki wa kisasa ni kuimba ili nyimbo i trend au kuwa hit song ila sio kwakusudi iwe nzuri kitungo mfano chapati, siji, Honey kwa Mond mfano Komasava, SHU.

Sijui nyimbo nyingi za Zuchu na Jaydee kwa majina ila najua msanii mzuri kwakusikiliza uimbaji mfano ukitaka kumjua Zuchu sikiliza ile nyimbo kaimbana Rayvanny utajua uwezo wake.
 
Back
Top Bottom