Jaydee anastahili heshima lakini asipewe sifa za uongo

Sifa hizo za uongo ni zipi?
 
Soma comments za wadau utaona ni namna gani umeandika uchafu wa kutosha
 
I am a music producer, sound engineer, and vocalist.

Waimbaji wa zamani watabaki kuwa bora wakati wote. Nasema hivo kwa sababu;
1. Waimbaji wa zamani hawakuwa wanategemea sana effects za studio kwa ajili ya ku-tune sauti zao. Sauti zao zilikiwa ni hivo hivo zilivyo.

2. Waimbaji wa sasa hivi ukiwavua "Autotune" sauti zao ni mbaya mbaya tukizitoa huko kwenye platforms mtawachukia. Hata baadhi yao huwa wanajistukia. Ukimaliza tu kumrecord anakuambia niwekee Autotune.

3. Waimbaji wa zamani walikuwa sio wavivu kiuandishi, na walikuwa wakiandika kwa kufuata sheria za uandishi wa nyimbo.

Of course wapo waimbaji wa kike wazuri ila ni wale waliopita THT au waliotokea makanisani au waliokuwa wanaimba Kaswida.

4. Wasanii wa hivi sasa hata ukimuuliza Bridge/daraja katika music ni nini? Hajui.

Mi ni hayo tu machache, sitaki nimfukuze Zuchu bado sijaruka naye duniani. 😂
 
Zuchu kuna namna akiimba huwa anaimba haswa nyimbo kama ,Raha, Naringa, Utaniua ni nyimbo ameimba kweli kweli .
Ila sasa tatzo kwenye hizi zingine zipo kibiashara zaidi
Sijui sukari
Hanii
Siji
Shika etc kwa kweli huwez zisikiliza
 
Alivyopewa jina Commando na Dada Mkuu/Mkubwa walikuwa sawa kabisa..
Kwa changamoto alizokutana nazo...sioni Mwanamziki wa Kike angeyeweza kuvuka...

Pongezi kwako Jide....kukulinganisha na hao wengine wote ni kukosea heshima..
ni kumkosea heshima kabisa, Zuchu ashinde mechi zake, aendelee kugawa sugar sukari
 
Mi siwezi nikakaa eti naskiliza mziki wa msanii anaitwa Zuchu.

Hizi ni nyimbo ambazo maudhui yake yapo dedicated kwa ajili ya watoto au mtu yeyote ambaye ni mvivu wa kufikiri.

Sina maana kama wanaopenda hizi nyimbo za aina hiyo ni wajinga. Hapana

Kitu ambacho watu wengi wanashindwa kupima na kujikuta wakimpa minyama huyo artist ni kutokana na lebel ambayo inamsimamia.

Watanzania wengi hususan hii new generation wamejikuta wameanza kupenda lebel kwanza kabla ya kuupenda na kuujua mziki.

Mwisho wa siku kinachotokea ni kwamba ubunifu kwenye sanaa kuhusiana na ubora wa mashairi unapungua kwasababu wasanii wamejihakikishia kuwa mziki wao lazima tu utasikilizwa hata uweje.

Kwa hiyo

Sio kweli kama Zuchu ni msanii mkali, Zuchu ni msanii maarufu. Umaarufu uliokuja kupitia lebel ambayo ina fan base kubwa.

Ni ukweli kuwa hiki anachokiimba saizi Zuchu angekiimba nje ya hiyo lebel hakuna mtu ambaye angemjua na wala huu mjadala leo usingekuwepo.

Ni ukweli usiopingika kwamba Zuchu hata akiingia booth na kukohoa kwenye mic kwa dakika 3 then hicho kikohozi kikafanyiwa mixing na auto tunes kisha ikafanywa kuwa ndio ngoma official. Watu wataipenda na sio ajabu kuona ikisumbua sana kwenye top 10 za media zetu.
 
Zuchu ana lipi sasa aliloliimba mkuu?Binafsi Zuchu namuona kama kituko tu
 
Umemaliza kila kitu. Mjadala ufungwe. Binafsi nimefanya muziki wa Hip Hop. Nimerekodi kwa Amba AB Records na Lamar lakini ilikuwa nikiwasikiliza Wasanii wa zamani naona kabisa siwezi kupenya. Sasa hivi ningesema niwekewe autotune na Beat nzuri, basi nimemaliza.
 
Kweli nyimbo ya "honey" na " chapati" zimekuchanganya
Ebu elezea ukali wa zuhura
KWa kuimba lugha za matusi kweli zuchu fundi
 
Hapa kapendeza na anafaa kuliwa bila hata kachumbari na chumvi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…