PakaJimmy
JF-Expert Member
- Apr 29, 2009
- 16,199
- 8,761
I beg to differ........HATUSHAMBULIANI........ BALI TUNAWEKANA SAWA....... KUHESHIMU MAWAZO YA WATU HAIMAANISHI KUWA LAZIMA UKUBALIANE NA ANACHOKISEMA MTU HUYO........ HATA KUPINGANA NA MAWAZO HAYO KUNAWEZA KUWA NA MAANA YA KUYAHESHIMU......... IT ONLY DEPENDS ON HOW YOU PRESENT YOUR MTAZAMO......
Mkuu Ngalikihinja.
Uko sawa kabisa...
Labda niwapeni kisa kimoja cha mambo haya, na ni kisa cha ukweli nilichoona mwanzo mwisho...
Kuna jamaa ambaye amekuwa pilot wa siku nyingi sana, na ana rating za ndege kibao...Maisha yake yote ya u'pilot alikuwa anawekeza ili aanzishe kampuni ya ndege, na kweli coming of 2006 jamaa akasaidiwa na wazazi wake ambao wako huko majuu, na wako njema, akaanzisha kampuni iliyojulikana kama SAFARI EXPRESS, akaanza na kukodisha ndege ndogo za abiria 12, lakini baadaye akakodisha ndege 2 nzuri sana aina ya Beechcraft-19 (BE19) na BE20 KUTOKA kwa rafiki zake wa South Africa, zikawa zinapiga tenda za mgodini NORTH-MARA na Sasakwa(Hoteli ya Mmarekani tajiri sana huko Serengeti). ..
Ndani ya mwaka 1 wa kuendesha biashara hiyo, aliangukia pua...! Pamoja na uzoefu mwingi wa ndege aliokuwa nao, madeni yakamzidi...Alikuwa anadaiwa mafuta, hadi jamaa wa Air-BP wakagoma kumpa mafuta kwa utaratibu wa kawaida wa cannet, wakamtaka alipe cash!.. .
MADENI YALIPOMZIDI aliamua kiume:
Aliamua kukimbia nchi hii, na mpaka wa leo hapa naandika hajatokea, wengi wakisema alienda kubadilisha sura ili kuwakwepa wadeni wake...
Aliacha ofisi yake ya quality ya juu ikiwa full-furnished,gari, Hiace custom, Macompyuta kibao, jikoni kukiwa na majiko ya kisasa, mafriji ya kisasa, pamoja na mashine ya bei mbaya ya kutengenezea kahawa(kwa wale wanaojua ma'cappuchino, ma'cafe-late, ma'chocochino etc)...
Waliokuwa wafanyakazi hawakuwa na jinsi zaidi ya kuanza kujisevia kila mtu alivyoweza...Mhasibu alikuwa anacheka, maana aliachwa na account ya kampuni...
Kwahiyo tunaongea vitu hivi kwa kuvifahamu sana, na SI KWA KUMDHARAU MTU!...Nawsilisha!