JBL Sound Bar 9.1 detachable Watts 820

The Evil Genius

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2014
Posts
6,017
Reaction score
19,506
Wakuu habari?

Nataka kupendezesha kasebule kangu, nakosa mdundo mzuri tu sebuleni. Wadau wanashauri ninunue Sound Bar za JBL.

Nimefanya ununuzi wa madirishani kwenye baadhi ya maduka yanazouza hizo Sound Bars naambiwa ni wastani wa milioni 2 hadi milioni 2.6.

Naomba kuuliza kwa wazoefu, hii kitu ina value for money, yaani hiyo bei yake ni sahihi ama napigwa?

Ahsante sana.

Updates 10th October 2022
Nimenunua mzigo wa JBL 9.1.

Juzi baada ya kuununua huu mzigo nikawa naitumia kupitia Blue tooth ila sikufeel ile music niliyokua naitaka room.

Kwa bahati nzuri leo nikaingia you tube kuangalia jinsi ya kutumia hii sound bar ndio nikaona kua ukitaka kufurahia tumia HDMI eARC port.

Nilipofanikiwa kutumia hiyo port aisee hii kitu ni hatari, base lake sio la kitoto.

Nimekubali JBL ni noma na nusu.
 
Matumizi ya nyumbani yapi specifically?

Unanunua kwa ajili ya Kusikiliza Music au Kuangalia Movie au kitu gani specifically?

Inabidi uspecify matumizi ya unachonunua, ili baadae usianze tena kulalamika kuwa kina perform chini ya expectations zako.
Anayenunua kwa matumizi ya nyumbani maana yake ni kwamba
Atatumia kusikiliza muziki
Atatumia kuangalia muvi
Atacnnect na kifaa kingine wakati akicheza gemu
Kifupi atatumia kwa matumizi ya nyumbani unayoyajua wewe.
 
Anayenunua kwa matumizi ya nyumbani maana yake ni kwamba
Atatumia kusikiliza muziki
Atatumia kuangalia muvi
Atacnnect na kifaa kingine wakati akicheza gemu
Kifupi atatumia kwa matumizi ya nyumbani unayoyajua wewe.
Umeelezea vizuri.

Huhitaji elimu ya sekondari kujua matumizi ya nyumbani ni yapi hadi utake maelezo marefu.
 
Asante sana mkuu..

Mimi kama mpenda haya mambo umeniinua sana sana..
 
Anayenunua kwa matumizi ya nyumbani maana yake ni kwamba
Atatumia kusikiliza muziki
Atatumia kuangalia muvi
Atacnnect na kifaa kingine wakati akicheza gemu
Kifupi atatumia kwa matumizi ya nyumbani unayoyajua wewe.
Unachopaswa kufahamu ni kwamba hakuna sound system Inayoweza kukupa hayo yote(music & movies) kwa ubora wake wote kwa 100%.

Kuna system ambazo ni "music first", hizi zimetengenezwa ajili ya Music ila zinaweza pia kutumika kwa matumizi mengine kama movies (huko kwenye movies zitakuwa za kawaida)

Kuna system kwa ajili ya movies, kwenye mziki zitaperform ila zitakuwa za kawaida sana kwa upande huo.

etc..etc...

So, mtu anaponunua sound lazima ajue yeye anapendelea nini kwanza. (Yeye ni "music first", "movie first " etc..)

Mtu akishajijua then sasa atachagua sound system kulingana na mahitaji yake
 
Ndio uweke details hapa kwasababu mtu hawezi nunua jbl systm mbili ili apate fleva kamili ya muziki akitaka kuangalia muvi azime jbl anayotumia kwenye muziki awashe nyingine
 
Mkuu, Ulichoongea SIO KWELI na naona unawapeleka watu chaka hapa.

Kwanza 2.1 SIO mahususi kwa ajili ya movies. Unaelewa hasa hiyo 2 inamaanisha nini hapo?


5.1 na 9.1 SIO kwa ajili ya mziki mnene kama unavyosema.

Elewa kwanza ni kwanini inaitwa 5.1 na 9.1

Hiyo 5 na hiyo 9 unajua inasimama kwa ajili ya nini?
 
Hongera mkuu umemaliza Kila kitu. JBL. Nina uzoefu nazo. Hakuna haja yakuongezea neno kazi kwake πŸ‘πŸ‘πŸ‘
 
Ndio uweke details hapa kwasababu mgu hawezi nunua jbl systm mbili ili apate fleva kamili ya muziki akitaka kuangalia muvi azime jbl anayotumia kwenye muziki awashe nyingine
Mkuu, Elewa kwanza nilichosema kwenye comment yangu.

Yeye Anataka Movies na Music na Games ILA, Swali ni kwamba, Priority yake ni nini zaidi kati ya hivyo vitatu hapo?

Yaani yeye ni mpenzi wa nini zaidi kati ya hivyo vitatu hapo?

Hilo ndio linatakiwa liwe swali la kwanza kujibiwa, ili litoe mwanga wa aina ya kitu anachokihitaji
 
Hongera mkuu umemaliza Kila kitu. JBL. Nina uzoefu nazo. Hakuna haja yakuongezea neno kazi kwake [emoji106][emoji106][emoji106]
[emoji3][emoji3][emoji3]
Kwamba 2.1 imetengenezwa kwa ajili ya Movies halafu 5.1 na 9.1 inetengenezwa kwa ajili ya Mziki mnene?

Hivi mnafahamu hata ni kwa nini hizo speakers ndogo nyingine kwenye 5.1 na 9.1 zinachomolewa?

You people can't be serious.
 
Hakyanani wabongo bana. Extrovert njoo utue muongozo huku kuna mtu anajua mengi ila hataki kuyasema
 
Si bora ameandika anachokijua? We unapiga siasa tu hata huelezi ujuacho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…