Je, 500,000 inatosha kuanzisha ufugaji wa mbuzi wa kienyeji?

Je, 500,000 inatosha kuanzisha ufugaji wa mbuzi wa kienyeji?

Habari wadau! Naomba kufahamu pesa tajwa hapo juu kama inatosha kufuga mbuzi. Sins hata banda nina kiwanja tu!

Maoni yenu ndiyo mafanikio yangu
Inatosha kabisa kikubwa ni ujue mbegu unazochukuwa na uanze na majike wanao zaa mapacha na uchukue waio pandwa kabisa. kila la kheri ktk hilo mimi nimeanza mwaka huu nasonga taratibu.
 
Kila la kher mkuu.. ila kuna changamoto moja hv ya mbuzi kuwakataa watoto pindi akishazaa. Je, huwa unaikabili vipi?
Sijaanza kukumbana nayo ila naamini nitajaribu kuwauliza wenzangu amabao wamenitangulia ktk ufugaji nikipata taarifa nitaleta mrejesho kwenye Mbwa niliweza kukabiliana nayo pamoja yakuwa ilinigarimu sana ila nilipambana.
 
Kama hauna banda..
Anza na mtaji wa kabanda kadogo chenye bati 3 hivi + kuna mabanzi yanauzwa hadi 3000 nunu hata 30 hivi utapata punguzo then ongea na fundi mshirikiane kujenga hilo banda


Sasa baada ya hapo cost ya bati na mabanzi itagharimu kama 160000 hivi so ukifanya na fundi jumla kama 180,000 sasa kwa kipimo cha kawaida jumlisha na misumari ni kama 200,000 kwa makadirio



Turudi makadirio ya kijumla tufanye sasa 250,000 nikimaanisha usafiri na vibarua,iliyobaki nunua mbuzi jike wawili WALIOSHIBA WENYE AFYA + kadume kadogo.


Then pandisha hayo majike baada ya muda,utarudisha mrejesho hapa.


Ila kama huna banda na unataka wa kuwekwa eneo tuu,utanunua hadi mbuzi 10 hadi 12 za kutosha kabisa

Kila la kheri!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom