Je, ABC bank wanatoa mikopo Kausha damu? Nimestaajabu sana

Je, ABC bank wanatoa mikopo Kausha damu? Nimestaajabu sana

muafi

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2015
Posts
2,557
Reaction score
6,128
Nimewasiliana na wakala wa Bank ABC juu ya mkopo
Tazameni wenyewe, naomba ABC bank mtolee ufafanuzi huu ni mkopo au kausha damu?

Hivi mtu ukope milionin14 urushe 39 huu si wizi kabisa?

Ndugu watumishi wa umma pamoja na walimu epukeni mikopo

Najuta sitarudia tena!
 
Sasa ndugu yangu Kwa miezi 96 , wao wanapata faida gan mkuu Kwa miez yote hyo , wakat kiuhalisia bank wanatengeneza faida kupitia mikopo , yani mtu akupe mkopo wa mil 14, alafu ilalie upande wake?? Kopa ndani ya miezi 12 uone interest rate yake
 
Sasa ndugu yangu Kwa miezi 96 , wao wanapata faida gan mkuu Kwa miez yote hyo , wakat kiuhalisia bank wanatengeneza faida kupitia mikopo , yani mtu akupe mkopo wa mil 14, alafu ilalie upande wake?? Kopa ndani ya miezi 12 uone interest rate yake
Je ni sahihi mtu mwenye basic ya 1.5M. Ukomo wake wa mkopo uwe ni 14 milion tu?
 
Kwa take home ya mtoa mada, akienda CRDB bank hakosi Mkopo wa milioni 26 kwa miezi hiyo 84
 
Kwani kukopa lazima? Ukiona mtu analalamikia mkopo basi anakopa akajenge ambapo ni ujinga wa kiwango cha lami
 
Nimewasiliana na wakala wa Bank ABC juu ya mkopo
Tazameni wenyewe, naomba ABC bank mtolee ufafanuzi huu ni mkopo au kausha damu?

Hivi mtu ukope milionin14 urushe 39 huu si wizi kabisa?

Ndugu watumishi wa umma pamoja na walimu epukeni mikopo

Najuta sitarudia tena!

View attachment 2753145
Easy loan
What are the Benefits?
· Interest rate as low as 1.6% per month
· You can get up to a maximum of TZS 40 million
· A longer repayment period of up to 72 months ( 6 years)
Kutokea hapo juu hilo ni tangazo la bancABC sasa kwa riba ya 1.6% kwa mwezi ambapo kwa mwaka ni 19.2% halafu unakupa kwa miaka nane unategemea nini? Kopa kwa mwaka urudishe principal + interest ya 19.2. na hii ndo akili.
Ila why pia usiende PBZ wao ni 13% kwa mwaka wajaribu pia.
All in all hakuna mkopo wa bei nafuu Tanzania kwenye bank/microfinance ambao mkopaji hatofeel mzigo.
Ukitaka riba nafuu benda saccos, au vicoba huko ndo labda utapata asilimia 10% kwa mwaka.
 
Kwa mujibu wa riba na limits zake walizoelekezwa na B.O.T wako sawa.

Chukua mikopo ya muda mfupi usizidi miaka miwili kulingana na lengo unaloliendea, usikope hiyo 14 milioni ili ukaanze ujenzi. Utatesa familia.

Kwa nchi yetu ilivyo fanya na penda kutegemea savings katika masuala ambayo sio ya uzalishaji kama vile ujenzi wa makazi binafsi,gari la matumizi binafsi. Kuanza biashara ndogo-ndogo(micro SME) na biashara ndogo (SME)

Kopa kwa kwa ajili ya biashara ambayo imeshaanza na ina consistency ya faida mkuu na kuna uhitaji wa mkopo ili kutanua operations n.k

Msome huyu jamaa kaandika vizuri sana


Unaweza mix strategy uka save for two years,then ukachukua mkopo wa two years, ukafanya jambo lako taratibu tu.
 
Nitangulize pole kwa watumishi wenzangu ambao wameomba mkopo kupitia bank hii kuanzia june 2024 kwasababu nina imani mpaka napoandika uzi huu leo august hawajapewa mikopo hiyo na pesa zao za mishahara zinakatwa. Banc abc mjue mtu anapoomba mkopo ana malengo yake thabiti hajaomba tu kama mchezo tunajua maumivu ya makato tunachukua mikopo ili kutatua changamoto mbalimbali kama vile ugonjwa,misiba,ada ,ujenzi na n.k lakini bank hii ni takataka ambayo inalaghai wateja kuchukua mikopo baadaye wewe unageula kuidai. Watumishi wenzangu na wafanyabiashara msithubutu kuisogelea hii bank mtateseka
Niende moja kwa moja
1.Wanaanza makato kwenye mshahara kabla ya kukupatia mkopo ulioomba
2.Bank inajinadi mkopo ni ndani saa 48 lakini ni mwezi na zaidi
3.Huduma kwa wateja ni idara ya uongo wanatoa promise hewa na wakati mwingine hawapokei simu
Ombi langu kwa BOT mwenye dhamana ya kutoa leseni iziangalie hizi bank uchwala ambazo zinajinadi na vipeperushi mitaani mpaka maofisini kuwa zina uwezo wa kukopesha lakini si kweli bali zipo kuwanyanyasa watanzania na kujipatia fedha ya njia ya kulaghai.
 
Tuliza mshono ndugu mwalimu. Ile benk yenu bado IPO? Si ungeenda huko au shobo?
 
Back
Top Bottom