Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
NBC pia wana tabia hii. mwezi lzm ufike na kupitaNitangulize pole kwa watumishi wenzangu ambao wameomba mkopo kupitia bank hii kuanzia june 2024 kwasababu nina imani mpaka napoandika uzi huu leo august hawajapewa mikopo hiyo na pesa zao za mishahara zinakatwa. Banc abc mjue mtu anapoomba mkopo ana malengo yake thabiti hajaomba tu kama mchezo tunajua maumivu ya makato tunachukua mikopo ili kutatua changamoto mbalimbali kama vile ugonjwa,misiba,ada ,ujenzi na n.k lakini bank hii ni takataka ambayo inalaghai wateja kuchukua mikopo baadaye wewe unageula kuidai. Watumishi wenzangu na wafanyabiashara msithubutu kuisogelea hii bank mtateseka
Niende moja kwa moja
1.Wanaanza makato kwenye mshahara kabla ya kukupatia mkopo ulioomba
2.Bank inajinadi mkopo ni ndani saa 48 lakini ni mwezi na zaidi
3.Huduma kwa wateja ni idara ya uongo wanatoa promise hewa na wakati mwingine hawapokei simu
Ombi langu kwa BOT mwenye dhamana ya kutoa leseni iziangalie hizi bank uchwala ambazo zinajinadi na vipeperushi mitaani mpaka maofisini kuwa zina uwezo wa kukopesha lakini si kweli bali zipo kuwanyanyasa watanzania na kujipatia fedha ya njia ya kulaghai.