Je, ajali Iliyosababisha kifo cha Shujaa wetu, Deo Filikunjombe, ni ajali ya Mungu au ya shetani?

Je, ajali Iliyosababisha kifo cha Shujaa wetu, Deo Filikunjombe, ni ajali ya Mungu au ya shetani?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Preamble!

Japo ajali ni ajali tuu, huweza kutokea, popote kwa yeyote kwa sababu au bila sababu!
Ajali yoyote ambayo inapotokea na kusababishwa na natural causes, ambapo ilikuwa itokee tuu, no one can do anything to prevent it, or could have done anything to prevent it, inaelezwa kuwa ni ajali ya Mungu!

Lakini ajali inayosababishwa na uzembe au human mistakes, ni ajali za shetani!.

Pasco wa JF!

Kifo chochote kinapotokea, tumekuwa na tabia ya kujifariji kuwa kila kifo kimepangwa na Mungu, na kilikuwa kitokee tuu hivyo hivyo kilivyotokea, na ile siku binadamu ameumbwa, maisha yake yote yaliisha pangwa, hadi saa yake ya kufa, na atakufa kifo gani, hivyo hiyo saa ya mtu yoyote kufa, ikifika, mtu huyo atakutwa na umauti, jinsi ile ile alivyoandikiwa, ndio maana sote tunaaminishwa kuwa kifo ni kazi ya Mungu, hivyo vifo vilivyowakuta mashujaa wetu hawa wawili, Deo Filikunjombe na Capt. Wiliam Slaa, na hao watu wengine wawili, tunajifariji kwa kusema ni kazi ya Mungu, ili tuvipokee vifo hivyo na kuvikubali jinsi hiyo hiyo ilivyo kwa sababu no one can do anything to change anything, limetokea, limetokea, ni kazi ya Mungu, tulikubali na tuendelee na maisha!

Pia kuna wengi wetu, wanamfahamu shetani, na wanajua jinsi shetani anavyooparate, ndie source of all evils, majanga, ajali, na mambo mengine yoyote maovu yanayomkuta binadamu, yanasababishwa na shetani, hayasababishwi na Mungu!, ila ila yatokee, lazima kwanza Mungu aridhie, kwa sababu Mungu ana uwezo wa kuzuia kila kitu, ikiwemo mipango yoyote ya shetani!, kitendo cha Mungu kuiacha mipango ya shetani kutimia ndiko kumepelekea kumtwisha Mungu responsibility ya kila kifo, kunakopelekea kutojiuliza lolote kuhusu sababu iliyopelekea hadi vifo kama hivi kutokea!, kizungu wanaitwa the underlying factors, causes na causative factors.

Hivyo wakati wengi wetu tukihuzunika tuu na kuwalilia wapendwa wetu, sisi ma deep thinkers tunazama deeper zaidi sio kujua chanzo cha kifo, ni ajali, jee chanzo cha ajali hiyo ni nini?!, hitilafu ya chombo?, mabadiliko ya hali ya hewa?, natural causes?, human errors?, or what exactly!

Wenzetu ambao ni wataalamu wa aeronautics kutoka TCAA watakuwa bussy kurecover the black box, sisi ambao sio wataalamu wa kihivyo, tuna maswali ya kawaida ya kujiuliza.

Kwanza jee hiyo Chopper ni ya nani?!

Kama Chopper yenyewe ni hii

Wakati Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari akisema anashindwa kuamini kilichotokea na kunusurika katika ajali ya helikopta, mmiliki wa chopa hiyo, Philemon Ndesamburo amesema atanunua nyingine haraka kabla ya kuanza kampeni za Uchaguzi Mkuu.

helikopta hiyo inayomilikiwa na Ndesamburo kupitia kampuni yake ya Keys Aviation kupata ajali. Wakati ikipata ajali, ilikuwa imekodishwa na Kampuni ya General Aviation Services (T) Ltd inayomilikiwa na Kapteni William Silaa.

Lema alisema rubani aliyekuwa akiendesha helikopta hiyo alifanikiwa kuielekeza juu ya miti alioutumia kupunguza kasi ya kushuka chini na kusaidia abiria kutoka salama.

"Imeharibika lakini abiria wote ni wazima. Walikuwamo wanne" alisema na kuongeza kuwa helikopta hiyo ndiyo iliyotumiwa na CHADEMA katika Uchaguzi Mkuu wa 2010 na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka jana na chama hicho kilitegemea kuitumia katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Pia, imewahi kutumiwa na makada mbalimbali wa CCM akiwamo Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba na kada maarufu wa Moshi mjini, Buni Ramole.

Nassari alisema waliporuka kutoka Leguruki, hakukuwa na dalili zozote za kuchafuka kwa hali ya hewa, lakini dakika chache baada ya kuruka angani wingu zito lililoambatanana upepo mkali liliwafunika ghafla.

"Wingu lile na upepo ule sijawahi kuona katika maisha yangu yote zaidi ya kusoma kwenye vitabu vya simulizi vya mambo ya ushirikina.

Mbunge huyo alimwagia sifa rubani Silaa kwa uwezo na ustadi aliouonyesha hadi wakanusurika.

"Kama siyo ustadi wake, naamini watu wangeokota vipande vya nyama tu kwenye eneo la ajali, ila Mungu ni mkuu leo tuko hai wote licha ya madhara madogo," alisema.

Nassari alisema muda mfupi kabla ya kuruka saa kumi na moja jioni, wakati akihutubia mkutano huko Leguruki, alipokea simu kutoka kwa mchungaji mmoja akimtaarifu kupata maono kuwa anakabiliwa na hatari ya kukutwa na jambo kubwa na baya akimtaka adumu katika sala.

"Dakika 15 baadaye nikaruka na kupata ajali.

Naamini kilichotuokoa ni nguvu yasala niliyosali baada ya kupokea ujumbe wa mchungaji na maombi ya wachungaji wangu wanaoniombea kila siku," alidai Nassari.

Rubani Slaa alisema alishangaa lilipotokea wingu na upepo uliosababisha ndege kuanguka ikiwa njiani kuelekea Ndoombo na Ngureserosambu.

"Kabla ya kurusha ndege nilijiridhisha na hali ya hewa.

Chanzo: Mwananchi

Jee helcopter hiyo ndio hii?!, then hii ajali sio ajali ya Mungu!, ni ajali ya shetani! iliyosababishwa na human mistakes!.

kama ndio hii, imewahi kupata ajali zaidi ya mara 3!, jee kabla ya kuruka, ilifanyiwa ukaguzi wa 'airworthness survey' na kupewa go ahead iendelee kuruka? Hapa tunapaswa kuyasubiri maelezo ya wataalamu wa TCAA, ila mashuhuda wa wakati inaruka, wameeleza iligoma, ila kwa kutumia uzoefu wa rubani bingwa, ililazimishwa hadi ikaruka!

Kama ajali hii ulikuwa ni mpango wa Mungu, then Mungu atawafariji wafiwa na wahanga wote wote wa ajali hii kwa namna ambayo ni Mungu mwenyewe ataona inafaa, ila kama ajali hiyo imetokana na negligence ya human mistakes, kwa binadamu fulani kutomiza wajibu wake, kama ilivyo TCAA, na hii TCAA ni taasisi ya kiserikali, na serikali yenyewe ni serikali ya CCM!, hii inamaanisha serikali ya CCM, imeendelea tena kuchezea maisha ya watu wake, kwa kisingizio chochote!, hili halikubaliki liendelee, ajali ya MV Bukoba was a human mistakes, CCM ilichezea maisha ya watu!. Ajali nyingi zinazosababishwa na ubovu wa barabara ni human mistakes ya CCM kuchezea maisha ya watu!.

Pamoja na madhila yote haya ambayo serikali ya CCM imelifanyia taifa hili, bado sishauri tarehe 25 October, tusiipigie kura CCM kwa hasira ili kuiadhibu isirudi madarakani, kwa sababu mwenye jukumu la kutoa hukumu ya haki ni Mungu tuu mwenyewe!.

Wito wangu ni kuwatasisitiza wapiga kura wa Tanzania, kuisikiliza sauti ya Mungu ndani ya mioyo yao ikiwaelekeza the right thing to do hiyo tarehe 25 October!, ukisikia sauti inakuambia "Mchague Magufuli", despite all the odds kwenye CCM yake, wewe mchague tuu Magufuli, hivyo ndivyo Mungu atakuwa emetaka hivyo Magufuli atakuwa ni chaguo la Mungu kwa Tanzania.

Ila pia ukiisikia sauti inakuamba mchague Lowassa, wewe hata kama ni mwana CCM, mchague tuu Lowassa ili utumize mapenzi ya Mungu! na mapenzi ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliyesema upinzani wa kweli utatoka CCM na rais bora atatoka CCM, Edward Lowassa ni mwana CCM aliyekwenda upinzani ili kutimiza unabii huu, na hata kitabu kitakatifu cha Bible kuna mahali kimesema "Jiwe wallolikataa waashi, litafanywa kuwa jiwe kuu la pembeni"

RIP Shujaa Wangu, Deo Filikunjombe, sisi tulikupenda, ila Mungu amekupenda zaidi!.

Pasco
La Deo Filikunjombe, Capt Slaa ni sababu nyingine ya kwanini sitaichagua CCM kabisa

 
Hahaha hizi thread hata Pasco, hapendi kuziona sasa, enzi hizo alikuwa anonymous leo ni verified user.
Kwa jinsi mnavyosoma kiswahili kinyumenyume kama yale maandishi ya kiarabu, hamkawii kusema Pasco ndiye alimuua Deo Filikunjombe
 
Kaburi lafukuliwa?
What for any way......! SOMA HII THREAD YOTE HAPA CHINI UTAPATA MWANGA
 
deep thinker ni hatari mkuu pasco upo vizuri...
tehteh nifanyaje na mimi niwe deep thinker.......
 
Hahaha hizi thread hata Pasco, hapendi kuziona sasa, enzi hizo alikuwa anonymous leo ni verified user.
Kwa jinsi mnavyosoma kiswahili kinyumenyume kama yale maandishi ya kiarabu, hamkawii kusema Pasco ndiye alimuua Deo Filikunjombe
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]amekuwa muoga sana siku hizi
 
Back
Top Bottom