Je, ajali Iliyosababisha kifo cha Shujaa wetu, Deo Filikunjombe, ni ajali ya Mungu au ya shetani?

Je, ajali Iliyosababisha kifo cha Shujaa wetu, Deo Filikunjombe, ni ajali ya Mungu au ya shetani?

Hizi nyuzi hizi! naona mkakati wa kumchafua Marope unashika kasi!
Anyway,safari hii namtetea Paskali,hajamtaja mtu hapo juu,ila mmeufufua muutumie kwa mambo yenu mnayowaza kichwani.
 

huu uzi umefukuliwa ili atleast mazuzu wapate ualau wa decryption ya uzi mpya...

ingekuwa vizuri kwenye huu uzi mpya wadau watafute mtu wa kuutafsiri maana umekuwa more coded then mfupi umekuwa kama ‘kitendawili’
 
Mrope hana hamu 😂😂😂

Naona mnamuiga kigogo wa Twitani kutimiza mkakati wenu kuja na habari kinzani.

Nipo pamoja na mtawala wa sasa, ILA yale maneno ya jasusi bobezi ya "niguse ninuke" yana mashiko sana, jamaa aliona mbele.

Chema chajiuza, kibaya chajitembeza.
 
Wanabodi,

Preamble!.

Kifo chochote kinapotokea, tumekuwa na tabia ya kujifariji kuwa kila kifo kimepangwa na Mungu, na kilikuwa kitokee tuu hivyo hivyo kilivyotokea, na ile siku binadamu ameumbwa, maisha yake yote yaliisha pangwa, hadi saa yake ya kufa, na atakufa kifo gani, hivyo hiyo saa ya mtu yoyote kufa, ikifika, mtu huyo atakutwa na umauti, jinsi ile ile alivyoandikiwa, ndio maana sote tunaaminishwa kuwa kifo ni kazi ya Mungu, hivyo vifo vilivyowakuta mashujaa wetu hawa wawili, Deo Filikunjombe na Capt. Wiliam Slaa, na hao watu wengine wawili, tunajifariji kwa kusema ni kazi ya Mungu, ili tuvipokee vifo hivyo na kuvikubali jinsi hiyo hiyo ilivyo kwa sababu no one can do anything to change anything, limetokea, limetokea, ni kazi ya Mungu, tulikubali na tuendelee na maisha!.

Pia kuna wengi wetu, wanamfahamu shetani, na wanajua jinsi shetani anavyooparate, ndie source of all evils, majanga, ajali, na mambo mengine yoyote maovu yanayomkuta binadamu, yanasababishwa na shetani!, hayasababishwi na Mungu!, ila ila yatokee, lazima kwanza Mungu aridhie, kwa sababu Mungu ana uwezo wa kuzuia kila kitu, ikiwemo mipango yoyote ya shetani!, kitendo cha Mungu kuiacha mipango ya shetani kutimia ndiko kumepelekea kumtwisha Mungu responsibility ya kila kifo, kunakopelekea kutojiuliza lolote kuhusu sababu iliyopelekea hadi vifo kama hivi kutokea!, kizungu wanaitwa the underlying factors, causes na causative factors.

Hivyo wakati wengi wetu tukihuzunika tuu na kuwalilia wapendwa wetu, sisi ma deep thinkers tunazama deeper zaidi sio kujua chanzo cha kifo, ni ajali, jee chanzo cha ajali hiyo ni nini?!, hitilafu ya chombo?, mabadiliko ya hali ya hewa?, natural causes?, human errors?, or what exactly!.

Wenzetu ambao ni wataalamu wa aeronautics kutoka TCAA watakuwa bussy kurecover the black box, sisi ambao sio wataalamu wa kihivyo, tuna maswali ya kawaida ya kujiuliza.

Kwanza jee hiyo Chopper ni ya nani?!.

Kama Chopper yenyewe ni hii



Jee helcopter hiyo ndio hii?!, then hii ajali sio ajali ya Mungu!, ni ajali ya shetani! iliyosababishwa na human mistakes!.

kama ndio hii, imewahi kupata ajali zaidi ya mara 3!, jee kabla ya kuruka, ilifanyiwa ukaguzi wa 'airworthness survey' na kupewa go ahead iendelee kuruka?!. Hapa tunapaswa kuyasubiri maelezo ya wataalamu wa TCAA, ila mashuhuda wa wakati inaruka, wameeleza iligoma, ila kwa kutumia uzoefu wa rubani bingwa, ililazimishwa hadi ikaruka!.

Kama ajali hii ulikuwa ni mpango wa Mungu, then Mungu atawafariji wafiwa na wahanga wote wote wa ajali hii kwa namna ambayo ni Mungu mwenyewe ataona inafaa, ila kama ajali hiyo imetokana na negligence ya human mistakes, kwa binadamu fulani kutomiza wajibu wake, kama ilivyo TCAA, na hii TCAA ni taasisi ya kiserikali, na serikali yenyewe ni serikali ya CCM!, hii inamaanisha serikali ya CCM, imeendelea tena kuchezea maisha ya watu wake, kwa kisingizio chochote!, hili halikubaliki liendelee, ajali ya MV Bukoba was a human mistakes, CCM ilichezea maisha ya watu!. Ajali nyingi zinazosababishwa na ubovu wa barabara ni human mistakes ya CCM kuchezea maisha ya watu!.

Pamoja na madhila yote haya ambayo serikali ya CCM imelifanyia taifa hili, bado sishauri tarehe 25 October, tusiipigie kura CCM kwa hasira ili kuiadhibu isirudi madarakani, kwa sababu mwenye jukumu la kutoa hukumu ya haki ni Mungu tuu mwenyewe!.

Wito wangu ni kuwatasisitiza wapiga kura wa Tanzania, kuisikiliza sauti ya Mungu ndani ya mioyo yao ikiwaelekeza the right thing to do hiyo tarehe 25 October!, ukisikia sauti inakuambia "Mchague Magufuli", despite all the odds kwenye CCM yake, wewe mchague tuu Magufuli, hivyo ndivyo Mungu atakuwa emetaka hivyo Magufuli atakuwa ni chaguo la Mungu kwa Tanzania.

Ila pia ukiisikia sauti inakuamba mchague Lowassa, wewe hata kama ni mwana CCM, mchague tuu Lowassa ili utumize mapenzi ya Mungu! na mapenzi ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliyesema upinzani wa kweli utatoka CCM na rais bora atatoka CCM, Edward Lowassa ni mwana CCM aliyekwenda upinzani ili kutimiza unabii huu, na hata kitabu kitakatifu cha Bible kuna mahali kimesema "Jiwe wallolikataa waashi, litafanywa kuwa jiwe kuu la pembeni"

RIP Shujaa Wangu, Deo Filikunjombe, sisi tulikupenda, ila Mungu amekupenda zaidi!.

Pasco
La Deo Filikunjombe, Capt Slaa ni sababu nyingine ya kwanini sitaichagua CCM kabisa





Iko siku nitamwaga vyote (ugali na mboga) kuhusiana na kifo Cha deo,kuanzia mawasiliano ya mpango huo mpaka utekelezaji wa ushetani huu,kila kitu kipo clear,tuna nyamazaga tu mambo mengine
 
Iko siku nitamwaga vyote (ugali na mboga) kuhusiana na kifo Cha deo,kuanzia mawasiliano ya mpango huo mpaka utekelezaji wa ushetani huu,kila kitu kipo clear,tuna nyamazaga tu mambo mengine
Imeshapita miaka 12 sasa its no more classfied issue. Mwaga upupu watu wajifunze mambo yanavyoenda. Tena fungulia uzi wake kabisa mods hawataufunga coz haina madhara yoyote kwa sasa.
 
Kitaani wanasema kina Deo waliku,wa na pesa nyingi walikuwa wanasafiri nazo,rubani mzee Slaa (babake mbunge wa Ukonga) akaingia tamaa,akataka awatose kwa ku crush ndege asepe na kipunda,jamaa wakastukia chezo wakawa wanagombea fuko la minoti,matokeo yake ndiyo hayo...R.I.P.
 
Kitaani wanasema kina Deo waliku,wa na pesa nyingi walikuwa wanasafiri nazo,rubani mzee Slaa (babake mbunge wa Ukonga) akaingia tamaa,akataka awatose kwa ku crush ndege asepe na kipunda,jamaa wakastukia chezo wakawa wanagombea fuko la minoti,matokeo yake ndiyo hayo...R.I.P.
Wewe jamaa kwahiyo marehemu ndio walishudia hilo maana wote walikufa mule
 
Back
Top Bottom