Je Alicho Fanya Eric Omondi Ni sahihi?

Je Alicho Fanya Eric Omondi Ni sahihi?

Tofautisheni kejeli na kuigiza, huyo amekejeli dini ya watu, sema wa kristo huwa tunakuwaga na mazoea ya ajab ajab kwenye dini yetu, wakati wenzetu waislam jaribu hata kuwa tania kidogo kuhusu dini yao uone, na kwa hilo nawapongeza, we must respect our entity tuache jokes na Yesu Kristo hebu tujifunze kwa wenzetu kuheshim tunacho kiamini.
Omondi alikosea sana


Lakini Mungu haruhusu kuhukumu hivyo Kikristo kabisa wewe ndo umefanya dhambi kwa kuhukumu klk huyo Muigizaji!
 
HABARINI! TOKA jana kwenye mitandao ya kijamii Mchekeshaji Erick Omond amejiwa juu na baadhi ya watu kwa kile Alicho Fanya na kuleta mvutano mkubwa sana katika Imani!

Mimi ni mkristo,Lakini sijaona Kosa kwa kile Alichokifanya Erick Omondi! kabla ya Kuja kumuhukumu Erick Omond .....Tujiulize Je Erick Omond ni nani na anafanya nini? ERICK ni Mchekeshaji na anafikisha ujumbe kwa njia ya kuchekesha na kuimba!

Sasa kile alichokifanya ni moja ya uigizaji wake na Lengo lake ni kufikisha ujumbe! Jumbe ulifika tatizo liko wapi? Tujiulize Je mtu akiigiza kama Rais ni kweli anakuwa Rais? au mtu akiigiza Ana maambukizi je kweli anakuwa mayo?

Moja ya watu walio Kuja juu ni baraka De prince Lakini mm sioni kama ni sawa kumuhukumu Eric kwa Alicho fanya

Sasa Tujiulize wote Je Alicho Fanya Eric ni Sahihi? Kwangu mimi yupo sahihi
Huyo Baraka ni kichwa maji kama walivyo mamilioni ya watanzania. Muweni mnasoma basi kabla hamjaropoka chuki.

Luka 23:32-43
32 Wakapelekwa na wawili wengine, wahalifu, wauawe pamoja naye.
33 Na walipofika mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, ndipo walipomsulibisha yeye, na wale wahalifu, mmoja upande wa kuume, na mmoja upande wa kushoto.
34 Yesu akasema, Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo. Wakagawa mavazi yake, wakipiga kura.
35 Watu wakasimama wakitazama. Wale wakuu nao walikuwa wakimfanyia mzaha, wakisema, Aliokoa wengine; na ajiokoe mwenyewe, kama ndiye Kristo wa Mungu, mteule wake.
36 Wale askari nao wakamfanyia dhihaka, wakimwendea na kumletea siki,
37 huku wakisema, Kama wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi, ujiokoe mwenyewe.
38 Na juu yake palikuwa na anwani; HUYU NDIYE MFALME WA WAYAHUDI.
39 Na mmoja wa wale wahalifu waliotungikwa alimtukana, akisema, Je! Wewe si Kristo? Jiokoe nafsi yako na sisi.
40 Lakini yule wa pili akamjibu akamkemea, akisema, Wewe humwogopi hata Mungu, nawe u katika hukumu iyo hiyo?
41 Nayo ni haki kwetu sisi, kwa kuwa tunapokea malipo tuliyostahili kwa matendo yetu; bali huyu hakutenda lo lote lisilofaa.
42 Kisha akasema, Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako.
43 Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi.
 
Msiwahukumu wengine nanyi hamtahukumiwa! Watendeeni wengine yale mnayopenda ninyi pia kutendewa! Naipenda sana imani yangu. Msamehe kwakua hajui atendalo.
 
Mmmm niliona ila sikufatilia ngoja niungetela nione
 
Msalabani walikuwepo watu watatu na Erick kachukua ya Mwizi alie samehewa
 
Sunday school siku ya pasaka ilikuwa lazima tufanye igizo na mtu lazima aigize ametundikwa msalabani.

Nadhani mkitazama video yote ya hii scene ya Omondi mtapunguza hili povu mnalolitoa kwa kutazama tu hiyo picha iliyochukuliwa kwenye hiyo video.

Pia kuna huyu Masanja Mkandazimaji anakejeli hizo dini zenu tena anajiita mchungaji ila mnamchekea hadi akawakejeli wale marehemu walioimba Kwetu pazuri na bado mnampongeza eti anakipaji, anzeni naye huyu wa Tanzania tuache unafiki.
 
Ndugu, umesahau kuwa Yesu alisulubiwa pamoja na watu wawili.. Yule wa mkono wa kuume ndio huyo Omondi amemuigiza..

Pitieni vizuri biblia zenu kabla ya kumlaumu Omondi..

Dhana ya kusulubiwa haikuwa kwa yesu pekee..

Omondi amemaanisha yule mwizi wa mkono wa kuume wa Yesu aliyenena maneno ya hekima kwa yesu na akasamehewa kabla yesu hajakata roho..
Mzee bahati mbaya sijaishika sana biblia. Nilikuwa naisoma niingiapo katika kipindi dini. Na nilikuwa naingia kwa sababu maalum. Utanisamehe sana. Nilichokiona kwa Bwana Erick ndicho nilichofkiri, kumbe yeye alimaanisha mengine.
 
Hata kanisani kuna maigizo ya YESU. Pale Azania Front Cathedral kina Jeremiah Mwakipesile wanaigiza kila mwaka
Mkuu wangu,zisingekuwepo kelele kama asingeweka kibao chenye hayo maandishi tunayoyasoma hapo!“MWIZI FORGIVEN"...nani sasa!Kristo Yesu au nani?angeweza kufanya hivyo kama angewaweka wengine wawili mmoja wao akamuwekea hiko kibao ingeleta maana ya Kibiblia zaidi sio ujinga huu.hawa comedian wanatafuta ubunifu kwa vitu wasivyokuwa na ufahamu navyo ingekuwa upande wa pili wangeondoka na kichwa chake na nashangaa kusikia kwamba huyu mtu ni mkristo.
 
Kwahiyo hawa hapa wako sahihi ...........???

IMG_9619.JPG

images

Crucifixion.jpg
Tatizo lipo hapo kwenye hiko kibao yeyote anaweza'fanya hivyo hata wewe unaweza ila hayo maandishi hapo yanakwaza...anamzungumzia nani wakristo tunajua aliyesulubiwa hivyo ni Yesu Kristo na hakuwekewa maandishi yenye maana hiyo huyo hayo kayatoa wapi au kayaweka kama nani?
 
Sijaona tatizo lolote..mbona Brian Deacon alipoigiza movie ya yesu hakuna aliyelalamika? au kwakuwa ni mzungu?
Bonge moja la point mkuu!sisi ngoz nyeusi majungu sana....ok kama alichokifanya ni kosa kwann makanisan mkesha wa pasaka huwa wanaigiza kanisan!!!,
 
Mungu wetu anajipigania mwenyewe, huyu jamaa asipoomba toba kwa kitendo hiki, yatakayomsibu asilie na mtu.
Kafanya kosa gani? kwani pale msalabani hakukuwa na mwizi? wagalatia mbona mnapoteza kumbu kumbu?
 
Tofautisheni kejeli na kuigiza, huyo amekejeli dini ya watu, sema wa kristo huwa tunakuwaga na mazoea ya ajab ajab kwenye dini yetu, wakati wenzetu waislam jaribu hata kuwa tania kidogo kuhusu dini yao uone, na kwa hilo nawapongeza, we must respect our entity tuache jokes na Yesu Kristo hebu tujifunze kwa wenzetu kuheshim tunacho kiamini.
Omondi alikosea sana
Kejeli hapo ikoje Mkuu... Hyo ni kazi ya sanaa.. Tupe uchambuzi wa kuthibitsha kuwa hyo ni Kejeli..
Icje kuwa unaongea out of emotions..
 
Hao ni wana uelewa mdogo ni kwamba kwani kuna mtu kamgusa au?
 
Huyu Baraka anapenda sana kukurupuka aiseee yeye kila kitu yumo anapenda kweli kuwa midomoni mwa watu.

Yeye anazini anakaa na mwanamke ambae sio mkewe hivyo ndio dini yenye mafundisho anayofata ndio inavyotaka?!
 
Sasa hapo tatizo lipo wapiii mbona watu huigiza sana tu ,,mnajifanya kuzijua diniii
dini hawaijui kabisa sijui tupojee naKumbuka kwenye biblia Yesu alivyokuwa akihukumiwa alihukumiwa na wale wezi wawili pale msaLabani kuna mwizi mmoja alimdhihaki Yesu kwa kumwambia ajiokoe na awaokoe na wao kama ni Mungu kweli then yule mwizi mwingine akamwambia Yesu amkumbuke kwenye ufalme wake na Yesu akamjibu umesamehewa dhambi zako na jioni hii tutakuwa wote kwa baba,sasa mijitu isiyosoma bibliA WALA KWENDA KANISANI MIPOVU KIBAOOOO
 
Back
Top Bottom