"Ilinisikitisha sana kuona mwanaume akipigwa makofi na kudhalilishwa namna hiyo tena na Mwanaume mwenzake. Taswira hiyo imeumiza sana nafsi yangu. Ilinikasirisha sana. Naumia sana kuona mtu anateseka namna hiyo, haswa kwenye mazingira ya watu kama haya."
Nakumbuka
Jazzy Jeff alifanya mahojiano hivi karibuni ambapo alisema kama
Mike Tyson angekuwa kwenye jukwaa,
Will Smith angefanya hivyo hivyo. Na siamini kwamba angeweza.
Je ikiwa
The Rock ndo yupo nafasi ya
Chris Rock, ni wazi hakuna kitu ambacho kingetokea pale, wala
Will Smith asingeweza kwenda kumpiga kibao. Will alimuona
Chris Rock ni mnyonge hivyo kutumia nafasi ile kuonesha hilo.
Mke wako alitoka nje ya ndoa na kijana mdogo sawa na mtoto wako na ukakubali kuwa amekosea na kumsamehe. Dunia inafahamu kuwa tayari wewe upo kundi la
Simps. Watoto wako wanasimuliana habari ya Marehemu
Tupac na vile Mama yao ameishi na huzuni ya kifo cha
Tupac na wewe kama Baba umelibeba hilo na kulitunza.
Dunia inakuonea huruma kwa sababu
August Alsina ameshafachua upekee wa mke wako ila ukaamua kupunguza machungu yako kwa mwanaume mwenzako.
Maneno ya Michael Jai White alipokuwa akihojiwa na Supreme Fitness.