Je, App ya Biashara ya Vipuri Kama BeForward kwa Soko la Tanzania Itafanikiwa au ni Kupoteza Muda?

KENGE 01

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2021
Posts
1,705
Reaction score
4,217
Nina wazo la kuanzisha App ya B2B Multivendor ambayo itawaunganisha wauzaji wa vipuri vya magari na wanunuzi nchini Tanzania, kama vile BeForward, lakini kwa soko letu la ndani. App hii itawawezesha wafanyabiashara wa vipuri kuorodhesha bidhaa zao, na wanunuzi wataweza kutafuta vipuri kulingana na aina ya gari, bei, na eneo. Pia, itakuwa na huduma za malipo mtandaoni, mfumo wa ujumbe wa papo kwa papo, na usafirishaji wa vipuri moja kwa moja kwa wateja.

Mfano wa Jinsi App Inavyofanya Kazi

Mfano 1: Juma ana gari lake aina ya Toyota Noah na anahitaji shock absorbers. Badala ya kupoteza muda akizunguka maduka tofauti, anaingia kwenye App, anatafuta "Shock Absorber Toyota Noah", anachagua ofa nzuri zaidi kutoka kwa wauzaji tofauti, anafanya malipo moja kwa moja kwenye App, na anasubiri vipuri vifikishwe kwake.

Mfano 2: Duka la vipuri la Mama Asha lipo Kariakoo, lakini anataka wateja wa mikoa mingine pia wanunue kwake. Anatumia App hii kupakia picha za vipuri, bei, na maelezo, kisha wanunuzi kutoka Mwanza, Arusha, au Mbeya wanaweza kuona bidhaa zake, kununua, na kusafirishiwa.

Mfano 3: Mohamed ni fundi wa magari na mteja wake anahitaji alternator ya Mercedes-Benz. Badala ya kupoteza muda akizunguka maduka, Mohamed anaingia kwenye App, anawasiliana na muuzaji moja kwa moja kwa njia ya chat ya papo kwa papo, anafanya malipo, na anapokea bidhaa haraka.


Maswali kwa Wataalamu na Wajasiriamali wa Teknolojia na Biashara:

1. Je, kuna uhitaji mkubwa wa soko la kidigitali la vipuri vya magari Tanzania?


2. Wauzaji wa vipuri nchini wako tayari kuhamia kwenye mifumo ya kidigitali au bado wanategemea maduka ya kawaida?


3. Changamoto gani kubwa zinaweza kujitokeza, kama malipo, uaminifu kati ya wauzaji na wanunuzi, au usafirishaji wa vipuri?


4. Je, kuna mifano ya biashara kama hii ambayo imejaribu Tanzania na imefanikiwa au kushindwa?


5. Je, ni vyema kuanza na jiji fulani kama Dar es Salaam kwanza, au ni bora kwenda kitaifa moja kwa moja?


6. Ni njia gani nzuri za kuhamasisha wauzaji wa vipuri waingie kwenye mfumo huu na kuona manufaa yake?



Nawakaribisha wataalamu wa IT, biashara, na sekta ya magari kutoa maoni yenu ili kujua kama hii ni fursa nzuri au ni kupoteza muda. Je, Tanzania iko tayari kwa biashara hii ya kidigitali, au bado ni mapema?

CC
Mad Max JituMirabaMinne
 
Anza haujachelewa, pia wanunuzi wakubwa ni mafundi hao ndio itabidi uwaweke karibu.
 
Wazo zuri mkuu anza chap. Ingawa itachukua muda mrefu ila itakuja kushika moto tu.

Kuna duka Arusha wana website yao (sio App) nilikua naitumia zamani ilikua na filters nzuri sana.

Challenge kubwa sio wateja, ila wauzaji maana tunajua dealers wengi wa spare watu flani mashefa wameridhika, hawa Middle men ndio watu wa mitandao.
 
Nishaanza Chap...ila shida ndio hiyo..Wanunuzi wengi ni mafundi na mafundi nao hawana Time ya kuanza kununua Spea mtandaoni...Ila ngoja tuweke shillingi kichwa au Mwenge tujaribu bahati🙏🏾
 
Mkuu anza, nafikri wazo lako ni zuri uhitqji wa kutafuta spea ni mkubwa sana, mtu anazunguka kutwa kucha huku na huko kutafuta spear.
Nashauri pia unapoweka spear uweke na model ya gari ikiambatana na engine no, manufacturing year, habari za kuuliza spear unaambiwa uje na sample dukani ni usumbufu na mambo ya kizamani. Kila heri mkuu.
 
Umejiandaa vipi kuhusu quality control?
Maana wabongo unatujua kwa kuuza fake bei ya original
 
Umejiandaa vipi kuhusu quality control?
Maana wabongo unatujua kwa kuuza fake bei ya original
Hapo itabidi unisaidie wazo aisee ila nitasajili Maduka yaliyosajiliwa kisheria
 


Aisee ni kama hii comment imenipa nguvu zaidi kwasababu nilikua napita humohumoo nishaandaa List mtu anaweza kutafta spea kwa Car Make, Car Model na mwaka ila injini ndio kipengele
 
View attachment 3230651

Aisee ni kama hii comment imenipa nguvu zaidi kwasababu nilikua napita humohumoo nishaandaa List mtu anaweza kutafta spea kwa Car Make, Car Model na mwaka ila injini ndio kipengele
Inakuwaje kipengele wakati gari zote zina injini number mkuu? Unajua wakati mwingine unaweza kutakankufanya service ya gari ikiwa bado inatembea sema tu ufanisi wake ndo sio mzuri! Sasa hii ya kuambiwa ulete sample maana yake kwamba ufungue hiyo part, gari ikae ukaoneshe tu dukani, je kisipokuwa chenyewe? huoni kama nimepoteza muda wa kufanya mambo mengine? Ukiweza fanya mkuu kama itakuwa ngumu basi nenda hivyo hivyo.
 
Sio ngumu kabisa na nimetoka kuongeza ni kikazi kidogo sana Ahsante sana kwa ushauri🙏🏾
 
Sio ngumu kabisa na nimetoka kuongeza ni kikazi kidogo sana Ahsante sana kwa ushauri🙏🏾
App ishaenda hewani? Inaitwaje? Nililua natafuta Spark Plug namba SK16HR11 basi nilitembea maduka kibao nikaikosa, wengi walikuwa na FK16HR11 au SC20HR11, mpaka nakuja kupewa namba ya wakala wa Toyota, nao bei ikawa kali, Tshs. 59,000/= kwa plug moja, nikaona isiwe kesi, nikaagiza aliexpress kwa Tshs. 112,000/= tu zote 4 pamoja na usafiri na mzigo ulisafiri siku 8 tu. Na hapo zilikuwepo pia za bei ya chini (Tshs. 36,000/= zote 4)
 

Attachments

  • IMG_20250122_083625.jpg
    388.2 KB · Views: 1
Kumbe Tatizo ni kubwa sana aisee..

App bado ipo jikoni naendelea kuongeza feature ikiwa Tayari Lazima niweke Uzi hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…