Je! Ardhi Inapokunywa Damu ya Kutosha ni Kitu Gani kinachotokea?* 💫💫💫💫💫

Je! Ardhi Inapokunywa Damu ya Kutosha ni Kitu Gani kinachotokea?* 💫💫💫💫💫

Mtanzania2020

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2020
Posts
1,033
Reaction score
2,307
Kwanza kabisa ndugu mpendwa ni vyema ukatambua kuwa, damu imebeba uhai wa mtu. Maana Biblia inasema " Linda sana moyo wako maana humo ndimo zitokamo chemchemi za uzima". Lakini Biblia inaendelea kusema, "kuleni wanyama lakini msile damu zao, maana damu zimebeba uhai wao".

Kisa cha Henoko na Habili watoto wa Adamu kinatufundisha ni jinsi gani tukio / dhambi ya kumwaga damu ya mtu asiyekuwa na hatia linavyoweza kuleta madhara baadae.

Kaini alimwaga damu ya ndugu yake Habili. Na ardhi ikafungua kinywa chake ikainywa damu. Je! Nini kilitokea?

Yapo mambo makubwa manne ya kiroho hutokea pale ardhi inapokunywa damu ya watu wasiokuwa na hatia.

1. Damu inalia;
Damu inayomwagika ardhini huwa imebeba uhai/ roho ndani yake. Ule uhai huwa unapaza sauti unamlilia Mungu toka katika ile ardhi ili aje ahukumu kwa haki.

Mungu anamwambia Kaini, " damu ya ndugu yako inanililia toka katika ardhi".

Kwahiyo damu zinapomwagika mahali, ardhi ya mahali hapo inameza uhai wa watu, wale nao wanaanza kulia toka katika ile ardhi. Sauti zao Mungu huzisikia. Sauti zao haziendi wala hazipotei bure.

Katika ulimwengu wa mwili itaonekana ni kama vita kati yenu imeisha, lakini katika ulimwengu wa roho vita bado inaendelea.

2. Ardhi iliyokunywa damu inalaaniwa;
Hapa huwa kuna laana za aina mbili na moja wapo kati ya hizo mbili inaweza kutokea.

Inaweza ikalaaniwa ardhi kwaajili yako. Au ukalaaniwa wewe juu ya ardhi.

Ni vitu viwili tofauti vinavyoendana lakini vinafanya kazi kitofauti.

Adamu alipoasi ililaaniwa ardhi kwaajili yake. Lakini kaini alipomwaga damu , alilaaniwa yeye juu ya ardhi.

Inapolaaniwa ardhi kwaajili yako, laana hiyo inawagusa na watu wengine wengi walio juu ya hiyo ardhi, wenye mahusiano na wewe na wasio na mahusiano na wewe.

Atakayehama toka kwenye hiyo ardhi iliyolaaniwa kuna uwezekano akapata unafuu.

Unapolaaniwa wewe juu ya ardhi, laana hiyo inatembea na wewe na kizazi chako tu katika shughuli zinazohusiana na mazao ya ardhi. Popote pale utakapokwenda, hata ukihama ukaondoka kwenye hilo eneo, ukiilima ardhi haitakuzalia mazao.

Ikumbukwe kuwa ardhi inafungwa na mipaka katika ulimwengu wa mwili na katika ulimwengu wa roho.
Kwahiyo tunaposema imelaaniwa ardhi, tunamaanisha ni ardhi ile iliyokunywa damu. Kwahiyo kama ardhi iliyokunywa damu ni ya Mwanza, laana hiyo haihusiani na ardhi ya Bukoba.

Mungu anamwambia Kaini "Umelaaniwa wewe juu ya ardhi iliyofungua kinywa chake kuimeza damu ya Habili".

3. Aliyeimwaga damu analaaniwa;
Baada ya kulaaniwa ardhi, mtu aliyeimwaga damu pia analaaniwa.
Mungu anamfukuza Kaini na anamwambia "utakuwa mtu usiyekuwa na kikao duniani". Yaani mtu usiyekuwa na makazi maalumu, mtu wa kuhamahama na kukataliwa.

Hili wala halihitaji akili nyingi kuligundua. Nchi zinazomwaga damu raia wao/ vizazi vyao hugeuka kuwa wakimbizi kwenye mataifa mengine. Na viongozi wao huishi kwa kujifichaficha na kuogopa kukamatwa kushitakiwa au kuuwawa na mahasimu wao.

Hata wale wanaomwaga damu za mtu mmoja mmoja huwa wanakimbia na kuishi maisha ya kujifichaficha na hofu.

Katika laana hii, kinaguswa pia kizazi cha mtu aliyemwaga damu. Laana itatembea na kizazi chake hata kizazi cha tatu na nne.

4. Damu inadai kisasi;
Hapa ndiyo patamu au pabaya zaidi. Ile damu iliyomwagika ikamezwa na ardhi huwa inadai kisasi kilipwe.

Waswahili huwa wanasema"ukimwaga damu ya mtu, ile damu itakusumbua sana". Katika ulimwengu wa roho tunasema ile damu imeanza kudai kisasi.

Jambo la kwanza kabisa; damu ile toka ardhini huwa inadai damu nyingine imwagike palepale. Yaani kilio cha damu kinazimwa kwa kumwaga damu.

Ndiyo maana kwa Wayahudi, ilikuwa mtu akiuwawa kwenye ardhi ya nyumbani kwako, ilikuwa ni lazima mtoe sadaka ya kumwaga damu ya ng' ombe ili mjisafishe na unajisi na ardhi itakaswe.

Kwahiyo mkichelewa kuitakasa ardhi ile, basi ule unajisi utasababisha patamwagika damu nyingine tena maeneo hayo.

Ndiyo maana ukifatilia kwa kina, mataifa mengi yaliyomwaga damu huendelea kumwaga damu tena na tena.

Jambo la pili; ile damu itamtaka aliyeimwaga amwage tena damu ya mtu mwingine kwa mkono wake au kwa amri yake yeye mwenyewe.

Ndiyo maana waswahili huwa wanasema "ukimwaga damu au ukila nyama ya mtu huwezi kuacha, utatamani umwage tena".
Kimsingi siyo wewe unayetaka kufanya hivyo, bali unaanza kuendeshwa na roho zilizo kwenye ulimwengu wa roho.

Ndiyo maana wauaji mara nyingi huwa ni walewale na huwa wanamzuka wa kuua tena na tena. Ukiwazingua kidogo tu hawaoni hatari kukuua au kutoa amri uuwawe.

Jambo la tatu; damu iliyomwagika hupandikiza chuki na roho ya kisasi kwa watu walioumizwa na kifo chake. Kwahiyo kama wewe muuaji usipoua tena, wao watakutafuta wakuue kulipia kisasi cha ndugu/ jamaa yao.

Jambo la nne; mambo hayo matatu juu yasipofanyika, basi viumbe wa ulimwengu wa roho (hasa wa giza) hushirikiana
Kwa ridhaa ya damu iliyomwagika ili kusababisha damu nyingine imwagike. Visipokuja vyenyewe ( majini na mapepo wachafu), basi vitatumia wachawi. Ndiyo maana ajali nyingi hutokea mara kwa mara kwenye eneo moja.

Nimesema viumbe wa ulimwengu wa roho hasa wa giza. Hii ni kwa nyakati hizi. Lakini katika nyakati za agano la kale, msipojitakasa, hadi viumbe wa ulimwengu wa roho wa Nuru, walihusika kufanya malipizi ya kumwaga damu katika jamii au familia iliyomwaga damu. Na ikibidi alishuka Mungu mwenyewe.

Wamisri walimwaga damu za Waisrael wengi sana kipindi cha kuwatumikisha kama watumwa. Walifikia hatua mpaka ya kuua watoto wachanga wa kiume wote wanaozaliwa.

Unadhani ile damu ingepotea bure bila kudai kisasi? Kamwe. Kanuni ya kiroho iko pale pale na Mungu alijua ipo siku itafika kisasi cha zile damu zilizomwagika kitafika.

Baadae tunakuja kuona Mungu anaua wazaliwa wa kwanza wote wa binadamu na wanyama wa kimisri kwa usiku mmoja. Malipizi ya kumwaga damu. Ilikuwa ni lazima Damu imwagike ili kufuta vilio vya damu.

Damu iliitakasa najisi ya damu. Ili wana wa Israel wasiguswe na malipizi ya kumwaga damu aliyoyafanya Mungu huo usiku, iliwabidi wao wajitakase kwanza kwa kumwaga damu za kondoo katika kila familia na kuzipaka milangoni. Ilikuwa ni sadaka ya kafara ya mnyama kwa Mungu. Kipindi hicho Mungu alikuwa anapenda sadaka ya damu.

Malipizi mengine ya damu kwa wamisri aliyoyafanya Mungu mwenyewe yalikuwa katika bahari ya Shamu.

Kwanini Mungu aliua wazaliwa wa kwanza wa Misri na siyo wa pili, wa katikati, wala wa mwisho?
 
Ndio maana kwa sasa kila mmoja wetu mwenye kujua athari za tukio hilo ameingia magotibi kuomba Rehema kwa Mungu na pia kwa ile damu takatifu ya bwana Yesu kristo ifute haitia , laana , malilio na kisasi.

Pole nyingi kwa walio athirika na hili po ia Mungu mwenye mwenyezi awajalie pumziko jema la amani ndugu zetu walio poteza maisha yao.
 
Hakuna uhusiano wowote wa Damu, ardhi na Mungu.

Huyo Mungu alishindwa kusikia sauti za maelfu ya mababu zetu waliomwaga damu zao na kufa kipindi cha utumwa na hakuna kilichotokea.

Unategemea ndio atasikia sauti leo hii?

Hakuna Mungu.

Hizo hekaya za Biblia ni danganya toto..!!

Mungu hayupo, Usipolinda uhai wako wewe mwenyewe usifikiri kuna Mungu wa kukulinda.
 
Back
Top Bottom